MPANGO WA KUWAPATIA MAANDIKO MATAKATIFU (BIBLIA) WATOTO, VIJANA NA WAFUNGWA MAGEREZANI NCHINI TANZANIA.

MPANGO WA KUWAPATIA MAANDIKO MATAKATIFU (BIBLIA) WATOTO, VIJANA NA WAFUNGWA MAGEREZANI NCHINI TANZANIA.

MPANGO WA KUWAPATIA MAANDIKO MATAKATIFU (BIBLIA) WATOTO, VIJANA NA WAFUNGWA MAGEREZANI NCHINI TANZANIA.

1. UTANGULIZI.

Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT) ni shirika la Kikristo lililoandikishwa mwaka 1970 na kupewa nambari S0 5722. Ni mwanachama wa Muungano waVyama vya Biblia Ulimwenguni(United Bible Societies (UBS). Shirika hili ni chombo cha Kanisa la Tanzania ambalo kazi yake kubwa na ya msingi ni kuwapelekea watu wote hapa nchini Tanzania Habari njema ya Yesu Kristo kwa kutafsiri, kuchapisha na kusambaza Biblia ikiwa katika lugha anayoielewa msomaji, bei anayoiweza na mfumo anaoupendelea.

MG 6293 copy scaled

Tangu kusajiliwa kwake  hapo mwaka 1970, Chama cha Biblia cha Tanzania kimekuwa kikitekeleza majukumu yake hayo kwa ushirikiano mkubwa na wa karibu na makanisa yote ya Kiprotestanti, Katoliki, Sabato na Kipentekoste hapa Tanzania; na pia kwa ushirikiano mkubwa na wa karibu na Muungano wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni (United Bible Societies-UBS) ambalo ni ushirika wa vyama vyote vya Biblia katika nchi zote.

Chama kimeweza kufanya tafsiri na kinaendelea kutafsiri Biblia katika lugha mbalimbali za makabila ya hapa Tanzania. Kutafsiri Biblia katika lugha mbalmbali za makabila kunafanyika kwa malengo makuu mawili. Lengo la kwanza la kufanya tafsiri hizi ni kwa kuamani kuwa watu wanaweza kulielewa Neno la Mungu kwa urahisi zaidi wakisoma au kuelezwa katika lugha zao na kuainisha na mazingira halisi ya mazingira yao.

IMG 9715

Lengo la pili ni kusaidia kutunza lugha za makabila kwa faida ya vizazi vijavyo vya kabila husika, kwani mila na utamaduni wa kabila zipo katika lugha ya watu wa kabila husika. Tangu kuanzishwa kwake Chama cha Biblia kimefanya tafsiri kadha na kuzisambaza hapa nchini zikiwamo Biblia katika lugha za:

  1. Kiswahili
  2. Kimaasai,
  3. Cigogo
  4. Iraqw

5. Nyakyusa

6. Igikuria

7. Ruhaya

8. Kisukuma

9. Kidatooga

10. Kimashami

11. Kivunjo

12. Kimochi

Baadhi ya Biblia ambazo kwa sasa zipo katika hatua mbalimbali za tafsiri ni:

  1. Kihehe
  2.   Cikaguru
  3.   Kinyamwezi
  4.   Chasu(Kipare)

5.  Kifipa

6. Kinyiha

7. Kinyiramba

8. Kirimi( Kinyaturu)

9. Kiha

Agano Jipya.

  1. Kimeru
  2. Kibena
  3. Kishambala
  4. Kikinga

5. Kijita

6. Kifipa

7. Kizaramo

2.0 Umuhimu wa Neno la Mungu kwa maendeleo

Tunapoangalia historia ya ustawi wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ulimwenguni kote, tunaona kuwa jamii ambazo zilijengwa katika misingi ya Neno la Mungu zilistawi kimaendeleo ikilinganishwa na zile ambazo ama hazikuamini au zilimuasi Mungu. Neno la Mungu likiwa ndani ya myoyo ya watu huzaa upendo ambao huzifanya jamii kuwa zenye amani na utangamano, tunu ambazo husaidia kuweka mazingira wezeshi kwa watu kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo.

36 1 scaled

2.1 Hali ya malezi kwa watoto na vijana.

Hivi sasa nchi nyingi ulimwenguni ikiwemo Tanzania kuna mporomoko mkubwa wa maadili. Wazazi ndani ya jamii wanalalamika juu ya watoto wa kizazi hiki kuwa wamekosa maadili.

Lakini wazazi hawa wanasahau kuwa kuporomoka kwa maadili ya watoto wao kunatokana na wao kutokuwalea katika misingi mizuri ambayo ni Neno la Mungu. Huko Ulaya na Marekani wazazi/mataifa walibweteka na maendeleo ya kiuchumi, teknolojia, sayansi na maisha bora kimwili na kusahau tunu kubwa inayotokana na maendeleo ya kiroho(spirituality). Makuzi ya kiroho hujenga maadili na hivyo kujenga utu wa mtu.

Katika nchi hizi watu wengi hasa kundi la vijana sasa hivi hawaendi Kanisani au Misikitini Kuabudu. Wamejitenga kabisa na Mungu na katika baadhi ya nchi Makanisa yameuzwa na kutumika kwa shughuli nyingine kabisa kama vile maduka na hata pia kugeuzwa kuwa sehemu za burudani kama vile sehemu za kuuzia vileo na starehe zingine.

Aidha katika nchi  hizi tunashuhudia ongezeko kubwa la mporomoko wa maadili ya asili ya mwanadamu. Katika nchi hizi sasa tunashuhudia uhalalishwaji kisheria wa ndoa na mapenzi ya watu wa jinsia moja, ongezeko la vitendo  vingine viovu ambavyo ni chukizo mbele za Mungu. 

Nchi za kiafrika nazo hazijasalimika na hali hiyo. Mporomoko mkubwa wa maadili katika nchi za Afika unazidi kuongezeka na kushamiri kutokana na utandawazi. Nchi zetu sasa zinashuhudia ongezeko kubwa la vitendo viovu kila siku,vingi vikifanywa na kundi la vijana. Wazazi walio wengi wameacha wajibu wao wa asili wa kuwalea watoto wao na kuwarithisha maadili ambayo huleta ustawi wa mtu mmoja mmoja na jamii/taifa.

Wazazi wengi hawaendi na watoto wao Makanisani na Misikitini wala hawaoni umuhimu wa watoto wao kupata mafundisho ya dini tangu wakiwa watoto ili wakue na kustawi katika msingi wa Neno la Mungu. Maovu mengi tunayoyashuhudia katika jamii ni kutokana na watu kukosa msingi wa Neno la Mungu ambalo likikaa katika myoyo huwafanya watu kuwa na  hofu ya Mungu na hofu hiyo huwafanya wajiepusha na matendo maovu kwa kujua kwamba hayampendezi Mungu na yana hukumu.

Hivi sasa tunashuhudia hofu ya Mungu ikizidi kupungua katika nchi yetu, na hivyo kutishia amani na utangamano katika taifa letu. Vitendo viovu vinaongezeka kwa kasi katika taifa letu kwa sababu watu wamekosa hofu ya Mungu.

Rais wetu mpendwa wa awamu ya Tano Marehemu Mheshimiwa John Joseph Pombe Magufuli amekuwa akituasa mara nyingi kwamba tumwogope Mungu, maana yake tufanye yale yanayompendeza Mungu na tuache matendo maovu. Matendo mema huleta afya kwa jamii/taifa lolote.

20211222 050907 scaled

2.2 Kwa nini Biblia kwa Watoto, Vijana na Wafungwa?

Katika nchi nyingi duniani na hasa nchi zinazoendelea  watoto umri kati ya miaka 1-14 huwa ni rika yenye watu wengi zaidi, wakifuatiwa kwa wingi na kundi la vijana(miaka 15-24).

Makundi haya mawili haya kwa pamoja hapa Tanzania idadi yake ni zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya watu wote. Kutokana na wingi na umri,  makundi haya yanayohitaji kuangaliwa /kutazamwa kwa karibu sana kwa maana ya malezi kwa maana ya kupewa huduma muhimu zitakazowafanya wakue na kustawi kiroho na kuwa raia wema wenye kupenda amani na  ustawi wa taifa.

Wafungwa ni kundi la watu ambao wako gerezani kwa sababu ya kutenda makosa katika jamii na kukosesha wengine amani na utangamano. Kwahiyo, hili nalo ni kundi muhimu la kutazamwa katika malezi hasa ya kiroho ili wahusika (wafungwa) wanapomaliza kutumikia  vifungo vyao waweze kuacha tabia mbaya za uhalifu na kuwa raia wema.

IMG 8365 scaled

2.3 Mapendekezo ya  na ushauri wa Chama cha Biblia kwa serikali katika kukabiliana na mporomoko wa maadili kwa wototo na vijana.

Chama cha Biblia cha Tanzania kinaishukuru sana Serikali yetu kwa kuruhusu Neno la Mungu kufundishwa mashuleni, jambo ambalo nchi zingine haziruhusu. Tunaamini hatua hii ni kwa kutambua kwamba mashuleni ndiko wanapoandaliwa viongozi wa taifa la kesho, kwa hiyo kuona umuhimu wa kuwapa malezi ya kiroho. 

Tunakumbuka miaka ya nyuma serikali iliruhusu uanzishwaji wa chama cha “ Elimu ya Dini Mashuleni Tanzania”(EDIMASHUTA) ikiwa ni njia mojawapo ya kutoa fursa kwa watoto ya kupata mafundisho ya dini ili waweze kukua kimaadili kupitia dini zao. Hii ilikuwa ni fursa muhimu sana kwa wototo kujifunza somo la dini na hivyo kukua na kustawi katika misingi ya kuwa na hofu ya Mungu.

Chama cha Biblia cha Tanzania kilikuwa mshirika mkubwa katika mpango wa Elimu mashuleni kwa kutoa Biblia  zilizotumiwa kama kitabu cha kiada mashuleni katika mafundisho hayo. Katika mpango huu, serikali ililifanya somo la dini kuwa la kutahiniwa na ilikuwa na “alama” (credit).

Kutokana na utambuzi huo vijana mashuleni walikuwa na bidii ya kujifunza somo la dini. Kwa njia hiyo waliweza kujengwa vizuri kiimani, kimaadili na kiustawi kwa ujumla na kundi hilo lilizaa viongozi waadilifu wa nchi yetu, kanisa na sekta binafsi.

Hata hivyo baadaye utaratibu wa  somo la dini kuwa  la kutahiniwa na lenye hadhi ya credit sawa na masomo mengine uliondolewa na hivyo kuwavunja moyo watoto na vijana katika kujifunza somo la dini.

Tunapendekeza kwamba somo la dini liendelee kufundishwa na lipewe hadhi/lihesabiwe sawa na masomo mengine katika mitihani, ili liweze kuchochea ari kwa watoto na vijana kujifunza somo la dini na hivyo kujengwa kimaadili.

20220713 140251 scaled

2.4 Kwa nini Biblia sasa kwa vijana mashuleni.

Kwa kuangalia mwenendo wa maadili kwa vijana wetu mashuleni,na kuna umuhimu wa kurejesha somo hilo kwani umuhimu wake umeanza kuonekana. Kumekuwa na  mmomonyoko wa maadili kwa vijana wetu sasa, tofauti na kipindi cha nyuma ambapo walilelewa katika misingi ya neno la Mungu.

Sasa hivi tunashuhudia vitendo viovu vikiongezeka katika jamii, ambapo watoto na vijana wanahusika. Jambo la pili tunaona mifano  ya wenzetu nchi za Ulaya ambako utandawazi umewafanya wasitambue  utu wa mtu.

Baadhi ya shule ambazo zimeendelea kufundisha somo la dini ni ushuhuda tosha kuonyesha namna somo la dini lilivyo muhimu katika ustawi wa mwanadamu. Shule hizi zimekuwa mfano mzuri kwa maadili na ufaulu mzuri  wa masomo hata yasiyo ya dini.

Chama cha Biblia kinaona kwamba kuna umuhimu wa kurudisha somo la dini kwa shule zote za serikali na za binafsi na kulifanya somo la dini kuwa na hadhi ya kutahiniwa sawa na masomo mengine.

Hiyo ni shule ya RUHUWIKO High School Songea wakifurahia kupewa Maandiko toka Chama cha Biblia. Wametoa shukrani nyingi kwa Uongozi kupitia mwl wao

3.0 Mpango wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa kuwapatia Biblia Watoto na Vijana mashuleni na Wafungwa magerezani.

Kwa kutambua umuhimu huo, Chama cha Biblia cha Tanzania katika mpango mkakati wa miaka mitano (2018 – 2022) kilianzisha mpango maalum wa kuhamasisha Makanisa na watu wenye mapenzi mema kushiriki kwa kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa Biblia ili  zisambazwe kwa wingi  kwa watoto, vijana na wafungwa ikiwa ni moja ya vipau mbele vyake katika kipindi hiki cha miaka mitano.

Mpango huu unalenga makundi matatu ya watoto na vijana kwa rika na wafungwa walioko magerezani.

Na.

Watoto

Vijana

Wafungwa magerezani

 1.

Miaka 3 – 5

Miaka 16 – 24

Wanaume

 2.

Miaka 6 – 9

 

Wanawake

 3.

Miaka 10 -15

 

 

Katika mkakati wa kutekeleza mpango huu Chama cha Biblia cha Tanzania kilianza kwa kuwashirikisha viongozi wa makanisa kutokana na nafasi yao ya asili ya kuwajenga na kuwalea watu kiroho.

Pili kimewashirikisha wadau wengine wenye mapenzi mema wanaotamani kuona Tanzania inajengwa katika misingi imara ya kiroho na hivyo kuwa na taifa lenye watu wenye hofu ya Mungu.

Mpango huu umepata uungwaji mkono mkubwa sana na Kanisa la Tanzania, hali ambayo imetutia moyo sana Chama cha Biblia cha Tanzania, kwani tunatambua kwamba Kanisani ndiko Neno la Mungu linafundishwa na ndiko Wakristo wanaofanya Kanisa la Tanzania waliko.

Tunaamini mpango huu unatekelezeka na walengwa na taifa zima litanufaika.

21

3.1 Watoto na Vijana walengwa.

Mpango huu katika awamu hii ya kwanza unalenga watoto na vijana walioko katika shule kwa sababu ya urahisi wa kujua idadi yao na urahisi wa kuwafikia.

Hata hivyo shule zitazopewa kipaumbele ni zile zilizoko vijijini, ambazo mbali kuwa  nyingi, lakini ndizo zenye watoto na vijana wengi wenye wazazi wenye hali duni ya  uchumi; na hivyo hawana uwezo wa kuwapata/kuwanunulia watoto  mahitaji yao kwa utoshelevu.

Ni kutokana na ukweli huo Chama cha Biblia cha Tanzania kinalenga kuwapatia watoto na vijana Biblia kwa bei nafuu ambayo wazazi wengi pamoja na hali yao duni kiuchumi wanaweza kuimudu.

ugawaji wa Sehemu ya Biblia Agano Jipya lenye Mithali na Zaburi

3:2 Ufundishaji wa somo la dini  mashuleni.

Kama tulivyoeleza katika utangulizi, Chama cha Biblia kinaona kwamba kuna umuhimu wa kurudisha somo la dini kwa shule zote za serikali na za binafsi na kulifanya somo la dini kuwa na hadhi ya kutahiniwa sawa na masomo mengine.

Tunaishauri serikali irudishe na  kuimarisha Elimu ya Dini Mashuleni( EDIMASHUTA) na kurudisha mitaala iliyokuwepo pamoja na kuruhusu taasisi za dini  kupeleka waalimu kwa ajili ya kufundisha somo la dini.

 Mpango huu ukitekelezwa utasaidia kuwajengea watoto wetu misingi ya maadili mema ili hatimaye tuwe na taifa lenye viongozi na raia wema. Jambo hili litasaidia kujenga jamii yenye amani na utangamano na kuruhusu mazingira ya kupata ustawi kama taifa.

Picha ya watoto wanasoma Biblia. 1

3:3 Vyanzo vya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huu

 Katika mpango huu, Chama cha Biblia cha Tanzania kinalenga kupata fedha kutoka:

  • Taasisi za kanisa
  • Mashirika mbalimbali
  • Watu binafsi

 Aidha Chama katika nia hii njema kinaomba kuungwa mkono na serikali kwa kushiriki katika kazi ya kuhamasisha taasisi, mashirika na wadau mbalimbali ili waweze kushiriki kuchangia mpango huu.

IMG 9767

3.4 Kiasi cha fedha, idadi  ya  Biblia na mgawanyo kwa makundi lengwa

Katika awamu hii ya kwanza Chama cha Biblia kimelenga kuomba kuchangiwa kiasi cha shilingi 10,200,000,000 ambazo zitatumika kununulia jumla ya Biblia 510,000 ambazo mgao wake kwa makundi lengwa utakuwa kama ifuatavyo:

  • Watoto – Biblia laki nne (400,000)
  • Vijana – Biblia laki moja (100,000)
  • Wafungwa – Biblia elfu kumi (10,000)

Kwa sasa Chama tayari kinayo miswada ya Biblia za makundi lengwa  yote yaani watoto, vijana na wafungwa. Biblia hizi zinaweza kuchapishwa na wachapishaji wakati wowote fedha zitakapokuwa zimepatikana.

Malipo yakishafanyika inakadiriwa kuwa kazi ya kuchapa, kusafirisha na kupokelewa inachukua muda wa miezi mitatu hadi minne.

20220721 115109 scaled

3:5 Mikoa na mgao wa Biblia kwa makundi lengwa.

Zoezi hili ni endelevu, lakini katika awamu hii ya kwanza Chama kimelenga kugawa Biblia kwa watoto, vijana na wafungwa katika  mikoa ifuatayo :-

 

Na

Mkoa

Watoto

Vijana

Wafungwa

 

Makisio

Halisi

Makisio

Halisi

Halisi

1.

Dodoma

730,000

100,000

180,000

25,000

3,000

2,

Mara

580,000

82,000

145,000

20,500

3,000

3.

Manyara

610,000

88,000

152,500

21,500

1,000

4.

Pwani

470,000

66,000

117,500

16,500

1,000

5.

Singida

470,000

66,000

117,500

16,500

2,000

Jumla kuu

2,860,000

400,000

712,500

100,000

10,000

IMG 20220722 WA0016

3:6 Usambazaji wa Biblia kwa makundi lengwa.

3:6:1 Mashule

Biblia zitasambazwa na Chama cha Biblia katika mashule kwa kushirikiana na Maafisa Elimu, Waalimu Wakuu wa  Mashule, Viongozi wa Makanisa na Waalimu wa Dini mashuleni.

3:6:2 Magereza

Biblia zitasambazwa katika Magereza kwa kushirikiana na Wakuu wa Magereza na Wachungaji wanaotoa huduma ya kiroho magerezani.

Gereza la Mahabusu Songea 2022 07 17

4: 0 MWISHO

Mpango huu una umuhimu wa kipekee katika kipindi hiki ambacho tunashudumia mmomonyoko wa maadili ukienda kasi katika jamiii yetu hasa kwa kundi la watoto na vijana ambalo linatarajia kutoa viongozi wa baadae wa taifa letu.

Tunaomba serikali ituunge mkono katika nia hii njema ya kuwajenga watoto, vijana na wafungwa kiroho. Faida ni kubwa kwa afya ya taifa. Kuchukua hatua sasa ni vizuri.

ABOUT US

Addresses

16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area.
P.O BOX 175, Dodoma -Tanzania.

Phone

+255 (0) 765 530 892

Email

info@biblesociety-tanzania.org

MPANGO WA ELIMU YA WATU WAZIMA.

MPANGO WA ELIMU YA WATU WAZIMA.

Mpango wa elimu ya watu wazima.

Chama cha Biblia kimeeendelea na mpango huu wa elimu ya watu wazima katika (w) ya Kilosa na Gairo-Morogoro kwa lengo la kuwasaidia wanawake na wasichana ambao hawakubahatika kwenda shule kwa sababu tofauti tofauti waweze kusoma na kuandika.

Kutokana na uhitaji kwenye jamii pia wanaume wamekuwa wanufaika wa mpango huu kwa sababu kuna idadi kubwa kwenye jamii ya wanaume ambao hawajui kusoma na kuandika pia.

Waalimu wa Kikagulu wakiwa kwenye mafunzo Dodoma scaled

Mpango huu kwa mwaka 2022 unatekelezwa katika vijiji 10 vya wilaya ya Kilos ana Gairo kwa kushirikiana na kanisa, serikali ambao wametupatia waalimu kwa ajili ya kuwafundisha wanakisomo. Wanakisomo 300 kutoka katika vijiji 10 walijiandikisha na mafunzo yanaendelea kwenye maeneo yao.

Waalimu wakiwa kwenye mafunzo scaled

Chama cha Biblia kupitia waalimu hao, kimewaandaa kuwa waalimu wazuri  ajili ya kuhakikisha kila mwanakisomo atakapohitimu elimu yake atakuwa anajua kusoma na kuandika. Waalimu hao kabla ya madarasa kuanza waliweza kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo na kupata mbinu nyingi za ufundishaji ili kuweza kuwafundisha wanakisomo kwa kufuata taratibu na miongozo iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwafundisha watu wazima.

electrician 10

Matukio katika Picha

Volunter-Mr-Musa-Barabara-akiwa-na-watoto-kutoka-Matumbulu-wakisoma-kijtabu-baada-ya-kugawiwa.-scaled.jpg June 23, 2022
IMG 7727 scaled
20220506 140032 scaled

Addresses

16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area.
P.O BOX 175, Dodoma -Tanzania.

Phone

+255 (0) 765 530 892

Email

info@biblesociety-tanzania.org

MPANGO WA WATOTO WALIOKO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU.

MPANGO WA WATOTO WALIOKO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU.

Mpango wa watoto walioko kwenye mazingira magumu.

Chama cha Biblia kupitia mpango huu kimeendelea kuwafikia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kuwapatia mafunzo ya kuwajengea  uwezo katika masuala ya;

  • Elimu ya  afya ya uzazi,
  • UKIMWI,
  • Jinsi ya  kumtambua rafiki mzuri,
  •   Kuutambua uthamani waliona mbele za Mungu,
  • Jinsi ya kutunza mazingira na miili yao, kujikubali walivyo,
  • Jinsi ya kuepuka na kupata msaada kuhusu unyanyasaji wa kijinsia mfano ndoa za utotoni,
  • Masuala ya ngono na mengine mengi,

Pia tuliweza kuwafikia watoto wenye ulemavu katika shule ya Hombolo katika kata ya Hombolo pamoja na watoto kutoka Kongwa, Matumbulu, Mpunguzi,Ipala na Ng,ambi.

Waalimu wa shule ya jumapili kutoka Hombolo wakiwa kwenye majadiliano. scaled

Watoto 180 waliweza kufikiwa kwa pindi cha  January – Mei, kuhakikisha elimu hii ni endelevu  tuliweza kuwafikia  waalimu na viongozi wa makanisa 60 katika kata ya Hombolo, Ugogoni na Ng,ambi lengo ni wao kuendeleza elimu waliyoipata kwenye makanisa yao pamoja na jamii iliyowazunguka.

electrician 10

Matukio katika Picha

Volunter-Mr-Musa-Barabara-akiwa-na-watoto-kutoka-Matumbulu-wakisoma-kijtabu-baada-ya-kugawiwa.-scaled.jpg June 23, 2022
20211221 064204 scaled

Addresses

16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area.
P.O BOX 175, Dodoma -Tanzania.

Phone

+255 (0) 765 530 892

Email

info@biblesociety-tanzania.org

MPANGO WA BIBLIA YA NUKTA NUNDU.

MPANGO WA BIBLIA YA NUKTA NUNDU.

Mpango wa Biblia ya nukta nundu.

Chama cha Biblia cha Tanzania kinaendelea na mpango huu wa kuwafikia wasiiona katika wilaya ya Kongwa-Dodoma.

Chama cha Biblia kwa kushirikiana na kanisa la Anglican Kongwa kimeweza kuanzisha maktaba kwa ajili ya Biblia ya Nukta nundu (Biblia nzima) ambayo itakuwa inasomwa na kutumiwa na watu wenye ulemavu wa macho.

Kupitia mpango huu kanisa la Kongwa limeweza kuwashirikisha wasiiona kwenye huduma mbalimbali ndani ya makanisa yao: Kusoma masomo kanisani, kuongoza sifa na kuabudu, kuhubiri na tunae mchungaji asiiona ambae amekuwa mchungaji baada ya kuwa sehemu katika mpango huu.

20220616 145127 scaled

Katika kuhakikisha wasiiona wanahudumiwa kiroho na kimwili, Chama cha Biblia kimeweza kukutana na baadhi ya viongozi wa makanisa, viongozi wa serekali ngazi ya kata na vijiji pamoja na Halmashauri (Afisa maendeleo ya jamii na Afisa ustawi wa jamii ) kuona naona ya kuwasaidia kupata elimu ya ujasiriamali itakayowawezesha kuibua miradi, kuandika andiko la mradi na mchanganuo wa fedha ili kuweza kupata fedha za walemavu 2% zinazotolewa na kila Halmashauri nchini.

Suala hili linafanyiwa kazi lipo kwenye utekelezaji kati ya Chama cha Biblia na wahusika wa Halmashauri ya (W) ya Kongwa.

electrician 10

Matukio katika Picha

20220616 122819 scaled
20220617 141058 scaled
20220617 120119 scaled

Addresses

16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area.
P.O BOX 175, Dodoma -Tanzania.

Phone

+255 (0) 765 530 892

Email

info@biblesociety-tanzania.org

MG 1493 scaled

CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA CHASAMBAZA ZAIDI YA MAANDIKO 538,000 MWAKA 2025

CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA CHASAMBAZA ZAIDI YA MAANDIKO 538,000 MWAKA 2025Dodoma, Juni 2026 – Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT), Askofu Dkt. Mark Malwa Malekana, amesema Chama hicho kimefanikiwa kusambaza jumla ya maandiko matakatifu 538,544...
Mkutano Mkuu wa 40 wa CBT

Mkutano Mkuu wa 40 (AGM)

info@biblesociety-tanzania.org(+255) 784-683 1209th Road /14 Hatibu, Madukani Area
IMG 5155 scaled

CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA CHASHEREHEKEA MAHAFALI YA WANAKISOMO

CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA CHASHEREHEKEA MAHAFALI YA WANAKISOMO GAIRO – MOROGORO Gairo, Morogoro | 05 Januari 2026Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT) kimefanya mahafali ya nane ya wanakisomo wa mradi wa Literacy for Women in Africa katika Wilaya ya Gairo, Mkoa wa...
3

Uzinduzi wa Biblia ya Kihehe

Biblia kwa Lugha ya Kihehe Yazinduliwa Rasmi Iringa – Miaka 30 ya Kazi Yafikia TamatiNa Mwandishi Wetu, Iringa 29 Juni 2025Dr. Alfred Elias Kimonge akikabidhi Biblia kwa ajili ya kuzinduliwa.Mgeni rasmi.  Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya...
Kuonesha Biblia zilizozinduliwa

UZINDUZI WA BIBLIA YA KIKAGULU

UZINDUZI WA BIBLIA YA KIKAGULU – WILAYA YA GAIRO, MKOA WA MOROGORO.Tarehe: 8 Juni 2025Mahali:Gairo, Morogoro Uzinduzi wa Biblia ya Kikagulu Unasisitiza Uthamini wa Lugha za AsiliDr. Alfred Elias Kimonge akikabidhi Biblia kwa ajili ya kuzinduliwa.Ibada na kubariki wa...
17

Mkutano Mkuu wa 39 wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa Mwaka 2024

Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia Tanzania, Askofu Dkt. Mark Malekana amesema katika ulimwengu huu ambao jamii inal­alamika kuhusu kuporomoka kwa maadili kutokana na mambo ya aja­bu yanayotokea, nguvu inayoweza kusadia jamii inayoathirika ni Neno la Mungu pekee....

Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) 2024

info@biblesociety-tanzania.org(+255) 784-683 1209th Road /14 Hatibu, Madukani Area
7

Maafali ya Saba ya Mradi wa Literacy for Women in Africa

Maafali ya Saba ya Mradi wa Literacy for Women in Africa.Mahali: ukumbi wa Nazareti, wilayani Gairo, mkoani Morogoro.Hafla hii ilihudhuriwa na viongozi wa dini na serikali wakiwemo wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa (W) ya Gairo pamoja na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji...
IMG 0245 scaled

Uzinduzi wa sehemu ya Biblia (portion) kwa lugha ya Kiha.

Uzinduzi wa sehemu ya Biblia (portion) kwa lugha ya Kiha.Mahali: Kijiji cha Nyakimwe, Wilaya ya Buhigwe  Dhehebu: Kanisa la Anglican Maelezo ya Meneja wa Tafsiri, Leah Kiloba Leah Kiloba alielezea maendeleo ya mradi huu, akisisitiza kuwa Chama cha Biblia kinaendelea...
20241103 154811 scaled

KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA BIBLIA MKOANI DODOMA

KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA BIBLIA MKOANI DODOMADodoma, 03 Novemba 2024 – Maadhimisho ya kilele cha Juma la Biblia mwaka huu yamefanyika kwa mafanikio makubwa mkoani Dodoma, katika Uwanja wa Mashujaa. Maadhimisho hayo yaliyoanza na maandamano ya amani kutoka...
MKUTANO MKUU WA MWAKA (AGM) 2021

MKUTANO MKUU WA MWAKA (AGM) 2021

MG 6283 copy scaled

Taarifa ya Utendaji na Fedha kwa mwaka wa 2021.

Imewasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) katika ukumbi wa Mikutano wa K.K.K.T – Dodoma.

Na Mkutano huo uliongozwa na

Rt. Rev Mark W. Malekana Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama cha Biblia cha Tanzania ambaye alipata fursa ya kufungua Mkutano Mkuu huo kwa Neno la Mungu.

 

MG 6130 copy scaled

Our Partners & Sponsors

UBS
ABS LOGO2
BIBLE ONLINE
FCBH
TalkingBibles
Finnish Bible Society

Get In Touch

Mkutano Mkuu wa Mwaka 2021

Mkutano Mkuu wa Mwaka 2021

Mkutano Mkuu wa Mwaka 2021

Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania Dkt. Alfred E. Kimonge anawakaribisha wanachama wa Chama cha Biblia cha Tanzania walio hai (ambao wamelipa michango yao ya uanacha wa kila mwaka) kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania (Annual General Meeting 2021) utakaofanyika tarehe 13.05.2022, katika ukumbi wa KKKT- Dodoma mjini, kuanzia saa 3 Asubuhi

Usipange kukosa.

Upatapo taarifa hii mshirikishe na mwenzako.

KARIBUNI.

MAWASILIANO: +255 784 683 120

Our Partners & Sponsors

UBS
ABS LOGO2
BIBLE ONLINE
FCBH
TalkingBibles
Finnish Bible Society

Get In Touch