Mpango wa Biblia ya nukta nundu.
Chama cha Biblia cha Tanzania kinaendelea na mpango huu wa kuwafikia wasiiona katika wilaya ya Kongwa-Dodoma.
Chama cha Biblia kwa kushirikiana na kanisa la Anglican Kongwa kimeweza kuanzisha maktaba kwa ajili ya Biblia ya Nukta nundu (Biblia nzima) ambayo itakuwa inasomwa na kutumiwa na watu wenye ulemavu wa macho.
Kupitia mpango huu kanisa la Kongwa limeweza kuwashirikisha wasiiona kwenye huduma mbalimbali ndani ya makanisa yao: Kusoma masomo kanisani, kuongoza sifa na kuabudu, kuhubiri na tunae mchungaji asiiona ambae amekuwa mchungaji baada ya kuwa sehemu katika mpango huu.
Katika kuhakikisha wasiiona wanahudumiwa kiroho na kimwili, Chama cha Biblia kimeweza kukutana na baadhi ya viongozi wa makanisa, viongozi wa serekali ngazi ya kata na vijiji pamoja na Halmashauri (Afisa maendeleo ya jamii na Afisa ustawi wa jamii ) kuona naona ya kuwasaidia kupata elimu ya ujasiriamali itakayowawezesha kuibua miradi, kuandika andiko la mradi na mchanganuo wa fedha ili kuweza kupata fedha za walemavu 2% zinazotolewa na kila Halmashauri nchini.
Suala hili linafanyiwa kazi lipo kwenye utekelezaji kati ya Chama cha Biblia na wahusika wa Halmashauri ya (W) ya Kongwa.
Matukio katika Picha
Addresses
16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area.
P.O BOX 175, Dodoma -Tanzania.
Phone
+255 (0) 765 530 892
info@biblesociety-tanzania.org