Mwenyekiti wa Bodi ya Chama
cha Biblia Tanzania, Askofu Mkuu Mark Walwa Malekana amesema chama hicho kitajitahidi kuendelea kuchapisha na kusambaza neno la Mungu ili liweze kumfikia kwa kila mtu na injili izidi kuhubiriwa.
Alisema hayo katika Mkutano
Mkuu wa Mwaka 2022 wa chama
hicho uliofanyika katika ukumbi
wa mikutano wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT) jijini Dodoma, Ijumaa wiki hii.
Malekana, ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato alisema kuwa mafanikio ya kidunia yanataka juhudi na akili zako za mtu, lakini bila Mungu juhudi na akili hizo haziwezi kumfikisha popote.
Akinukuu maandiko kutoka katika kitabu cha Kutoka 33:15, mwenyekiti huyo wa bodi aliwakumbusha washiriki wa mkutano huo na jamii kwa ujumla, kuishi kwa kumwomba Mungu.
“Katika maisha yako omba Mungu awe pamoja nawe, iwe ni biashara unafanya au utumishi popote pale. Yesu alisema pasipo mimi hamuwezi kufanya neno lolote, na sisi kama Chama cha Biblia tunamwomba Mungu awe pamoja nasi katika majukumu ya chama katika kutafsiri Biblia, kuchapisha, sambamba na kutawanya maandiko matakatifu”.
“Kizazi hiki kinatakiwa watu warudi kwenye Neno la Mungu na kumtazama Kristo, na kwa upande wetu Chama cha Biblia tunajitaidi kuchapisha na kusambaza Neno la Mungu kwa kila mtu, wakiwemo watoto, wafungwa..na vijana ni kipaumbele cha Chama cha Biblia cha Tanzania