Mpango wa watoto walioko kwenye mazingira magumu.
Chama cha Biblia kupitia mpango huu kimeendelea kuwafikia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala ya;
- Elimu ya afya ya uzazi,
- UKIMWI,
- Jinsi ya kumtambua rafiki mzuri,
- Kuutambua uthamani waliona mbele za Mungu,
- Jinsi ya kutunza mazingira na miili yao, kujikubali walivyo,
- Jinsi ya kuepuka na kupata msaada kuhusu unyanyasaji wa kijinsia mfano ndoa za utotoni,
- Masuala ya ngono na mengine mengi,
Pia tuliweza kuwafikia watoto wenye ulemavu katika shule ya Hombolo katika kata ya Hombolo pamoja na watoto kutoka Kongwa, Matumbulu, Mpunguzi,Ipala na Ng,ambi.
![Waalimu wa shule ya jumapili kutoka Hombolo wakiwa kwenye majadiliano. Waalimu wa shule ya jumapili kutoka Hombolo wakiwa kwenye majadiliano. scaled](https://biblesociety-tanzania.org/wp-content/uploads/2022/06/Waalimu-wa-shule-ya-jumapili-kutoka-Hombolo-wakiwa-kwenye-majadiliano.-scaled.jpg)
Watoto 180 waliweza kufikiwa kwa pindi cha January – Mei, kuhakikisha elimu hii ni endelevu tuliweza kuwafikia waalimu na viongozi wa makanisa 60 katika kata ya Hombolo, Ugogoni na Ng,ambi lengo ni wao kuendeleza elimu waliyoipata kwenye makanisa yao pamoja na jamii iliyowazunguka.
![MPANGO WA WATOTO WALIOKO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU. 1 electrician 10](https://biblesociety-tanzania.org/wp-content/uploads/2015/11/electrician_10.png)
Matukio katika Picha
Addresses
16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area.
P.O BOX 175, Dodoma -Tanzania.
Phone
+255 (0) 765 530 892
info@biblesociety-tanzania.org