Uzinduzi wa sehemu ya Biblia (portion) kwa lugha ya Kiha.
Mahali: Kijiji cha Nyakimwe, Wilaya ya Buhigwe
Dhehebu: Kanisa la Anglican
Maelezo ya Meneja wa Tafsiri, Leah Kiloba
Leah Kiloba alielezea maendeleo ya mradi huu, akisisitiza kuwa Chama cha Biblia kinaendelea kujitahidi kuhakikisha upatikanaji wa Biblia kwa watu wote wa madhehebu mbalimbali bila ubaguzi. Alifafanua kuwa mradi huu unalenga kumjumuisha kila Mkristo kwa kutoa nafasi sawa ya kusoma Neno la Mungu katika lugha yao wenyewe.
Sherehe ya uzinduzi wa tafsiri ya Biblia ya Position ya Kiha (kitabu cha Yeremia) ilifanyika katika Kanisa la Anglican kijijini Nyakimwe, wilaya ya Buhigwe. Tukio hili lilihudhuriwa na waumini kati ya 400 na 700 kutoka madhehebu mbalimbali, pamoja na makanisa ya Anglican, Roman Catholic, Pentecostal, na Sabato, ambayo yalialikwa rasmi kushiriki.
Historia ya Mradi kutoka kwa Mchungaji Ntakije
Mchungaji Ntakije aliwasilisha historia ya mradi huu wa kutafsiri Biblia kwa lugha ya Kiha, akielezea hatua zilizochukuliwa kufanikisha kazi hii muhimu na changamoto zilizokabiliwa. Alielezea jinsi jamii imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono mradi huu.
Kusoma Maandiko na Baraka za Ibada
Tukio lilihusisha kusoma maandiko kutoka kitabu cha Yeremia, sura ya kwanza, mistari ya kwanza hadi wa kumi, ambayo ilisomwa na mtafsiri Ahabu Ntibakanzi. Kabla ya kusoma, mchungaji Daniel Nzaino alitoa baraka kwa waumini na ibada iliongozwa kwa shukrani na furaha.
Uratibu wa Ugawaji wa Vitabu
Vitabu vya Position ya Kiha viligawiwa kwa wahumini waliokuwa wakitoka kanisani, kwa usimamizi wa watu waliokuwa milangoni. Kila mmoja kila mmoja alipokea kitabu/portion kwa mpangilio mzuri na bila msongamano, wakihakikishiwa upatikanaji wa Neno la Mungu katika lugha yao.
Furaha ya Waumini
Baada ya ugawaji wa vitabu hivi, waumini Walionekana wakifurahia vitabu vyao nje ya Kanisa. Walijawa na furaha kubwa huku wakimshukuru Mungu pamoja na viongozi wa mradi kwa jitihada zao kufanikisha kazi hii. Pia walipiga picha ya pamoja ya kumbukumbu wakiwa wameshikilia vitabu vyao.
Tukio hili lilifanikiwa kwa kiwango kikubwa, na waumini walionyesha kufurahia uzinduzi wa tafsiri hii mpya ya Biblia katika lugha yao ya Kiha, ikionyesha mwendelezo wa kazi nzuri ya Chama cha Biblia na Kanisa katika kukuza na kueneza Neno la Mungu kwa jamii nzima.
0 Comments