TAARIFA FUPI YA MPANGO & MAHAFALI YA SITA YA MPANGO HUU
Mahafali ya sita ya mpango huu yalifanyika tarehe 17.2.2024 katika Ukumbi wa Nazarethi, Gairo mjini ambapo wanakisomo 421 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu Kisomo cha watu wazima na Mkuu wa (w) ya Gairo. Mh. Jabiri Shekimweri. Sherehe hizi zilihudhuriwa na wageni wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Dkt. Alfred E. Kimonge, Bodi ya wakurugenzi wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wafanyakazi na viongozi wa makanisa na jamii kutoka wilaya ya Gairo na Kilosa.
Mpango huu umeendelea kutekelezwa na Chama cha Biblia cha Tanzania katika (w) ya Gairo na Kilosa. Lengo kuu ni kuwasaidia wanawake na wasichana hawakuweza kwenda shule na hawajui Kusoma na Kuandika.
Mmoja wa wanakisomo akipokea cheti cha kuitimu elfu hiyo.
SHUGHULI ZA UTEKELEZAJI
Katika kipindi cha mwaka 2023, Chama cha Biblia kupitia mpango huu kiliweza kutekeleza shughuli zifuatavyo;
Kufanya uhamasishaji na kuandikisha wanakisomo 450 (Me 379 & Ke 71) kabla ya madarasa kuanza.
Mpango huu umelenga zaidi wanawake na wasichana, ila wapo pia wanaume ambao wamejiunga na madarasa na wamekuwa wanufaika wazuri. Takwimu zinaonyesha kuna idadi kubwa ya wanaume wasiojua kusoma na kuandika na mpango huu unawakaribisha.
Kufanya mafunzo kwa waalimu 30 wanaofundisha kwenye madarasa ya watu wazima. Mafunzo haya yalifanyika Dodoma kwa wiki mbili yakiongozwa na wakufunzi kutoka SIL Nairobi, Kenya.
Kuchapisha na kuwagawa vitabu 450 vya kujisome kwa wanakisomo wote waliojiandikisha.
Kuhamasisha na kuanzisha vikundi (improving literacy groups) vya kujisome vitabu vya hadithi. Vikundi hivi ni kwa ajili ya wahitimu ili kuweza kuendeleza ujuzi na kupata uzoefu zaidi katika kujua kusoma na kuandika. Hapa wananapata nafasi ya kujisomea vitabu vya aina mbalimbali, majarida, magazeti, Biblia pamoja na makala nyingine nyingi.
Uzinduzi wa sehemu ya Biblia (portion) kwa lugha ya Kiha.Mahali: Kijiji cha Nyakimwe, Wilaya ya Buhigwe Dhehebu: Kanisa la Anglican Maelezo ya Meneja wa Tafsiri, Leah Kiloba Leah Kiloba alielezea maendeleo ya mradi huu, akisisitiza kuwa Chama cha Biblia kinaendelea...
KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA BIBLIA MKOANI DODOMADodoma, 03 Novemba 2024 – Maadhimisho ya kilele cha Juma la Biblia mwaka huu yamefanyika kwa mafanikio makubwa mkoani Dodoma, katika Uwanja wa Mashujaa. Maadhimisho hayo yaliyoanza na maandamano ya amani kutoka...
UZINDUZI WA SEHEMU YA BIBLIA KWA LUGHA YA KINYIHA WAFANYIKA KANISA LA MORAVIAN, MBOZIJimbo la Mbozi, Kanisa la Moravian Ushirika wa Igamba – 27 Oktoba 2024Tukio la kihistoria la uzinduzi wa vitabu vya Biblia vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kinyiha vitabu vya Ruthu, 1...
MPANGO WA KISOMO CHA WATU WAZIMA – LITERACY FOR WOMEN IN AFRICA.
Habari Kamili.
Chama cha Biblia cha Tanzania kinaendelea kutekeleza mpango wa Kisomo cha elimu ya watu wazima katika wilaya ya Kilosa na Gairo kwenye vijiji 15 vilivyochaguliwa wakati wa kuanzishwa kwa mpango huu. Mpango wa Kisomo cha elimu ya watu wazima umeweza kuwafikia wanaume na wanawake 1500. Wanakisomo waliofikiwa na mpango huu wanajua kusoma na kuandika, maisha yao yamebadilika na wanaishi maisha ya kawaida kama walivyo watu wengine waliosoma. Pia ushirikishwaji wao katika masuala ya kijamii umeongezeka, wengine wamepata nafasi za uongozi kwenye jamii na Kanisa limeweza kuwa na washirika wanaoweza kusoma na kulielewa Neno la Mungu pia kufanya majukumu yao ya utumishi kwa weledi zaidi kulinganisha na ilivyokuwa kabla ya kujua kusoma na kuandika.
Waalimu wa Chikagulu wakiwa kwenye mafunzo
Ili kufanikisha mpango huu Chama cha Biblia kwa kushirikiana na SIL Nairobi walifanya mafunzo ya kuwajengea uwezo waalimu 30 wa Chikagulu. Mafunzo hayo yalifanyika Dodoma kwa wiki mbili ambapo waalimu waliweza kufundishwa mada tofauti tofauti kulingana na mfumo wa mpango ulivyo, baadhi ya mada walizofundishwa ni mifumo ya literacy, sifa za mwalimu bora, sifa za mwanakisomo, majukumu ya mwalimu kabla na akiwa ndani ya darasa.
Kwa kipindi cha mwaka huu 2023, Chama cha Biblia cha Tanzania kimeweza kuandikisha wanakisomo 450. Wanakisomo waliojiandikisha hawawezi kusoma, hawajawai kwenda shule na hawajawahi kukutana na jarida/ gazeti, kitabu chochote na hawajui kuandika. Madarasa yataanza mwezi June,2023 kwa kipindi cha miezi saba.
Waalimu wa waalimu wa Chikagulu wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo
Askofu huyo aliwakumbusha washiriki wa mkutano huokumwomba Mungu zaidi kwa kuwa wanahubiri injili katika kizazi kinachobadilika lakini wao wanahubiri neno la Mungu lisilobadilika, jambo linaloibua changamoto mbalimbali ikiwemo lugha. Alitoa mfano kuwa wakati wao kama chama wanajitahidi kuhubiri injili kwa lugha ya Kiswahili inayosikika kwa watu wengi, lakini Kiswahili chenyewe kinabadilikabadilika.
Sign up for the Bible Society of Tanzania mailing list
Chama cha Biblia kimeeendelea na mpango huu wa elimu ya watu wazima katika (w) ya Kilosa na Gairo-Morogoro kwa lengo la kuwasaidia wanawake na wasichana ambao hawakubahatika kwenda shule kwa sababu tofauti tofauti waweze kusoma na kuandika.
Kutokana na uhitaji kwenye jamii pia wanaume wamekuwa wanufaika wa mpango huu kwa sababu kuna idadi kubwa kwenye jamii ya wanaume ambao hawajui kusoma na kuandika pia.
Mpango huu kwa mwaka 2022 unatekelezwa katika vijiji 10 vya wilaya ya Kilos ana Gairo kwa kushirikiana na kanisa, serikali ambao wametupatia waalimu kwa ajili ya kuwafundisha wanakisomo. Wanakisomo 300 kutoka katika vijiji 10 walijiandikisha na mafunzo yanaendelea kwenye maeneo yao.
Chama cha Biblia kupitia waalimu hao, kimewaandaa kuwa waalimu wazuri ajili ya kuhakikisha kila mwanakisomo atakapohitimu elimu yake atakuwa anajua kusoma na kuandika. Waalimu hao kabla ya madarasa kuanza waliweza kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo na kupata mbinu nyingi za ufundishaji ili kuweza kuwafundisha wanakisomo kwa kufuata taratibu na miongozo iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwafundisha watu wazima.
Wakagulu wapatao 756 wanawake wakiwa 550 na wanaume wakiwa 206 waliojiunga na mpango wa kujifunza kusoma na kuandika (LWA Kikagulu) mnamo tarehe 15/06/2020 hadi tarehe 30/11/2020 hatimaye walihitmu mafunzo hayo huku wakiwa na furaha kwa kujua kusoma na kuandika. Wakizungumzia furaha yao wameonekana wakiwa na bashasha na furaha sana kwa kupata elimu hii muhimu kwa maisha yao.
“Sasa ninaweza kusoma na kuandika na hata nikiumwa nikiandikiwa dawa sina haja ya mtu kunisomea na pia naweza kushiriki kikamilifu katika huduma za kijamii kama kupiga kura na mengine mengi katika dunia ya sasa” mama moja alisikika akisema maneno hayo kwa furaha.
Sherehe hizo zilifanyika tarehe 27/02/2021 katika Ukumbi wa Nazareth huko Gairo.
Baadhi ya wakinamama wenye umri mkubwa walioweza kushiriki na kupata vyeti vyao.
Kabla ya kugawa vyeti kulitanguliwa na hotuba na nasaa mbalimbali kutoka kwa Mgeni rasmi na viongozi mbalimbali walioalikwa kwenye mahafali haya ya tatu tangu kuanzishwa kwa mpango wa LWA Chikagulu katika mkoa wa Morogoro wilaya za Kilosa na Gairo
Canon Mstaafu Bonifas Mkami wa Kanisa Anglikani Jimbo la Morogoro
Canoni Mstaafu Bonifasi Mkami ni mmoja wa wachambuzi wa Biblia ya lugha ya Chikagulu inayoendelea kutafsiriwa katika lugha hiyo pia ni mmoja wa watu walioshiriki katika uandishi wa kitabu cha Chibweda. Akizungumza baada kupewa nafasi ya kuongoza ibada ya ufunguzi wa maafali alisema
“Mpango huu wa akina mama kujifunza kusoma na kuandika kwa lugha yao wenyewe kupitia Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama kikaona kianzie kwetu sisi wakagulu. Baada ya hapo tukaanza uandishi wa vitabu.
Kwanza cha Mwalimu, pili cha mwanafunzi kwa neema ya Mungu, mimi nilikuwa mmojawapo. Jina la Kitabu cha Mwanafunzi na Mwalimu tulikiita “CHIBWEDA” kwa maana ya FURAHA na kuweka picha zinazotoa taswira ya Kikagulu”.
Pia aliongeza kusema “Baada ya kukamilisha kuandika vitabu hivyo ikawa ni kazi ya kuwatafuta walimu wanaojua kuzungumza Kikagulu kwa ufasaha ili wapewe mafunzo ya kufundisha madarasa ya wanakisomo watakaojifunza kusoma na kuandika kwa kutumia lugha yao ya Kikagulu kwa kuwa ndiyo wanayoilewa Zaidi na baadae wanaweza kusoma na kuandika kwa Kiswahili na lugha zingine bila shida yoyote na baada ya hapo yakaanzishwa madarasa 10 ya kwanza na waalimu 20 katika awamu hii ya kwanza.”
Nasaha na shukrani za Canon Bonifasi Mkami
Kujua kwenu kusoma na Kuandika kutasaidia sana baada ya Biblia yetu sisi wakagulu tunayoiandaa kwa sasa na iko hatua za mwisho. Itakuwa rahisi ninyi kuisoma bila shida kwa hiyo tunatoa shukrani nyingi kwa Chama cha Biblia cha Finland na Chama cha Biblia cha Tanzania kuwezesha mpango huu katika mkoa wetu katika wilaya zetu za Kilosa na Gairo katika lugha hii ya Chikagulu Mwenyezi Mungu na awabariki sana.
Na zaidi tunawashukuru sana Mwalimu Frank Makalla mratibu wa mpango huu, Ndugu Timothy Kamau, Dr Suzan Nyaga na Ruth Munguth wa SIL Kenya.
Nawaombeni ninyi mliofaidika na mpango huu, muwe mawakili wema na waminifu katika kutunza lugha yetu.
Mratibu wa mpango huu wa LWA Chikagulu Mwalimu Frank Makalla
Akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti kwa awamu ya tatu ya wahitimu hao, Mratibu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mwl.Frank Makalla alisema
“wahitimu hao ni wa awamu ya tatu ya programu hii iliyolenga kuwajengea uwezo wanawake kusoma na kuandika ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kwenda shule wakati walipostahili kwenda shule, hii ni fursa kwao wakiwa watu wazima kuanzia aka 14 na kuendelea ingawa na wanaume wanaruhusiwa kushiriki japo si kwa kiwango kikubwa maana mpango unawalenga wanawake ambao hawakupata nafasi hiyo ya kusoma na kuandika kutokana na sababu mbali mbali.”
Awamu ya kwanza waliohitimu ni jumla ya watu 97 ambapo wanawake ni 83 na wanaume ni 14 kutoka vijiji 10 vya Gairo na Kilosa ambavyo ni Gairo, Mtumbatu, Chakwale, Mamboya, Maguha, Berega, Mwandi,Magela, Mabula, pamoja na Italagwe.
Awamu ya pili waliohitimu jumla ni 248 ambapo wanawake ni 214 na wanaume ni 34; kutoka kwenye vijiji 10 vingine ambavyo ni Mogohigwa, Kibedya, Tabuhotel, Magubike, Nguyami, Ibindo, Ntembo, Mbili, Dumbaalume, pamoja na Kiegeya.
Waliojiandikisha ni 423 kati yao waliohitimu ni 317 na ambao hawajahitimu ni 106 kutokana na changamoto mbalimbali kama vile kuhama, shughuli za mashamba, na matatizo mbalimbali ya kijamii.
Aliendelea kusema kuwa mahafali hayo ni mwendelezo wa mahafali ya awamu ya kwanza ya program hiyo iliyoanza mwaka 2017, ambapo watu 120 walijiandikisha huku watu 97 walihitimu mafunzo hayo ambayo pamoja na kuwafundisha kwa kutumia lugha ya chikagulu kama lugha ya kufundishia kwa urahisi wa kuelewa kwa lugha yao lakini kadiri wanvyoendelea kujifunza kusoma na kuandika hatimaye wanaweza kusoma na kuandka katika lugha ya Kiswahili na lugha zingine.
Alieza pia kuwa programu hiyo inafadhiliwa na Chama cha Biblia cha Finland na Chama cha Biblia cha Tanzania kikitoa usimamizi wa mpango na uratibu uku Summer Institute of linguistics (SIL) hawa wanatoa utaalamu wa waalimu pamoja na mwongozo wa kuandaa vitabu vya kufundishia. Programu hiyo inalenga zaidi kuwainua wanawake kujifunza kusoma na kuandika ingawa na wanaume wanakaribishwa kushiriki.
Mratibu wa mpango huu Mwl. Makalla alisema kati ya watu wazima 395 waliohitimu, wanawake ni 337 na wanaume ni 58 katika awamu hii ya tatu
Aidha, Mwl. Makalla aliomba ushirikiano na serikali katika mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwafanya wananchi waliokosa fursa ya kusoma na kuandika kujiunga na kuendelea kupata elimu hiyo.
“Katika programu yetu hii tumekuwa tukichukua wale wenye umri wa kuanzia miaka 14 na kuendelea, hivyo wale wenye miaka 14 hadi 17, serikali inaweza kuwatambua na kuwaingiza katika mfumo wa MEMKWA katika shule za msingi kama ambavyo Serikali inaelekeza kupitia wizara ya Elimu ili wakajifunze zaidi kwa sababu sisi hapa tunawafundisha kusoma na kuandika tu huko watajifunza masomo mengine pia kama Hesabu, Sayansi, Jiografia Historia na kadhalika.
Changamoto ya kwa nini wanaanza wengi na kuhitimu wachache?
Sababu zilizotajwa ni kwamba jamii ya wakagulu ni wakulima na wafugaji kwa hiyo wakati wa masika wakulima wanahamia mbali na vijiji ambako ardhi ina rutuba zaidi kwa kilimo cheye kuleta tija, pili wafugaji wanahamia maeneo mengine kutafuta malisho na maji kwa ajili ya mifugo yao na matatizo mbalimbali ya kijamii.
Katibu wa UMAKI Ndg. Josephine Semwenda
Katibu wa idara ya maendeleo ya akina Mama UMAKI Josephine Semwenda katika Dayosisi ya Morogoro ambaye alialikwa kuwatia moyo wahitimu hao aliwasisitizia wahitimu kutokuogopa kuitangaza lugha ya Chikagulu kila mahali katika eneo lao la ukaguluni na kwingineko kwa kuwahimiza kuwa mabalozi wema katika kuilinda lugha yao isipotee, alitumia nafasi hiyo pia kuwapongeza. Wahitimu wote na kuwatakia kila lakheri katika kutekeleza majukumu ya kijamii na Kanisa.
Na hapa aliendelea kueleza zaidi kuwa
“Kwa Neema ya Mungu mmemaliza, Mungu aendelee kuwa karibu sana aendelee kuachia nguvu ya kuendelea kujifunza zaidi hata katika masomo mengine pia natamani kuona wengine hata mufike secondary kwasababu mmeshajua kusoma na baadae mtafika mbali Bwana Yesu asifiwe. Bila shaka kujua kusoma kwenu kutawasaidia sasa kuendeleza kusoma Neno la Mungu lakini pia kuweza kusoma vitabu mbalimbali na kufahamu mambo mengi ambayo usipojua kusoma na kuandika unakuwa kama kipofu na mambo mengi yanakupita.”
Sisi Idara ya UMAKI tunashukuru kwa ajili ya neema hii. Mana ninyi wahitimu mtakuwa nguzo muhimu kwenye madarasa yetu ya UMAKI kwa kuwafundisha na kuwaongoza wanawake kwenye madarasa yetu ya umaki na kufanya mambo mbalimbali kwa ajili ya idala ya kina mama ambao wengi wao hawajajua kusoma na kuandika. Maana wengine wanapoombwa kutoa Neno au labda kufundisha jambo fulani wengine huwa hawawezi kwa sababu hawajui kusoma na kuandika sasa wale wa madarasa ya umaki mtakuwa msaada mkubwa kwao.
Mwisho kabisa niendelee kupongeza tena na tena kwa juhudi ambazo mmezichukua hata kufikia siku ya leo Mungu awabariki lakini msiishie hapo muendelee kujiendeleza ili muweze kupata mambo makubwa zaidi na Jina la Bwana litaendelea kuhimidiwa kama sasa hivi unaweza kusoma masomo ya Biblia na muweze kusoma kwingine hata katika taifa letu pia Mungu awabariki muendelee kutimiza ahadi aliyo wapatia Bwana Yesu. Amina.
Diwani wa Kata ya Gairo na katibu wa Mbunge jimbo la Gairo Ndugu Danstan Mwegoha
Diwani Danstan Mwegoha aliwashukuru sana Chama cha Biblia cha Tanzania na wote waliotia mkono katika mpango huu kwa kutambua umuhimu wa wananchi wetu wakristo wetu kuendesha mafunzo ya elimu ya watu wazima na hasa kwa kuwalenga wakinamama ni msaada mkubwa kwao, sisi tunasema wakina mama ni jeshi kubwa kwa sababu wakina mama ndiyo wenye majukumu makubwa na akina mama ndiyo wenye malezi mazuri kwa watoto. Na pia wakina mama ndiyo wanaowatunza wakina baba.
Na pia aliendelea kusema, Kwenye utaratibu wetu wa kutoa mikopo mara nyingi huwezi kukuta wakina baba wakiwa kwenye vikundi hivyo bali utakuta wakinamama, vijana, na walemavu, kwa hiyo wakinamama pamoja na vipato vyao vidogo wanaweza kuunganisha nguvu kwa kukopa na kulipa vizuri kuliko wakina baba.
Zamani ilikuwa ni vigumu sana kusomesha watoto wa kike kwa sababu wakina baba walikuwa wanahitaji kupokea mahali kwa kunufaika zaidi sasa bila kuangalia maisha ya binti zao kwa wakati ujao. Ninaishukuru sana serikali yetu inaonekana kuwajali na kuwalinda watoto wa kike katika kupata elimu.
Jukumu letu sisi kama serikali na Chama hiki kinacho endesha mafunzo haya tuombe sana kuwa na ushirikiano wa kutosha. Sisi kwa heshima yetu ya uongozi kwa mujibu wa nafasi yangu katika uongozi msisitizo na mkazo wa mtu kuchaguliwa na kupigiwa kura katika ngazi yoyote kuna vipengele vimeandikwa kwamba ni lazima mtu ajue kusoma na kuandika ndipo aruhusiwe kugombea nafasi na si vinginevyo kwahiyo unaweza kupata nafasi ya kuwa kiongozi kama diwani, mbunge, Rais n.k, kwa kuwa sasa mnajua kusoma na kuandika. Nawatakia Baraka za Mungu katika kuendelea mbele. Mungu awabariki sana.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nguyami.
Ndugu Mgeni rasmi, katika Kijiji changu sisi tumejiona fahari sana kwa kuwepo mpango huu na wengi waliohitimu katika mafunzo haya wamekuwa Baraka sana kwa kijiji chetu kwa maana miongoni mwao tulipata mama mmoja ambaye sasa ni mwekahazina anayeitwa Rehema Penford wa kijiji chetu. Kabla ya kupatiwa elimu hii haikuwa hivyo.
Na wananchi wengi wanawaamini watu wanaopitia elimu hii kwa kuwa wameonekana kuwa na ufahamu mkubwa na maadili mema katika Jamii yetu. Sisi kama serikali tunatafuta mpango mzuri wa kuwasaidia Chama cha Biblia cha Tanzania ili kiweze kuwafikia wengi zaidi katika Kijiji chetu.
Ushauri wangu kwenu wahitimu wa CHIBWEDA nawaomba sana, huu uwe mwanzo wa kutaka kujiendeleza zaidi na zaidi ili mfikie ndoto zenu. Na nyinyi pia ni rahisi serikali kuwasaidia mikopo katika kujiendeleza kwenu kwa maana kumuelimisha mwanamke umeielimisha jamii yote.
Zaidi nawapongeza tena Chama cha Biblia kwa kuwezesha mpango huu na mimi naahidi kujiunga na Chama hiki ili nami nitoe mchango wangu hata kwa pesa kidogo na Mwenyezi Mungu na awabariki sana.
Meneja wa miradi na utunishaji wa mfuko wa CBT Mchungaji Samwel Mshana.
Mch. Samweli Mshana ambaye pia alimwakilisha Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania alisema
Mgeni rasmi, Baba Askofu Paulo Jacob Momeo, Mheshimiwa mratibu wa UMAKI, Mheshimiwa mratibu wa mpango, Mheshimiwa Canon mstahafu, mheshimiwa Mwenyekiti wa kijiji cha Nguyami, waandishi wa habari, mheshimiwa mratibu wa Chibweda, walimu na wahitimu wote, Bwana wetu Yesu Kristo asifiwe.
Kwanza, nianze kumshukuru Baba Askofu lakini pili nimshukuru sana mheshimiwa Diwani kwasababu kweli mara ya kwanza lakini kwa sababu mimi ni Meneja wa miradi hii ni mara ya kwanza kuwa na viongozi wa serikali. Mheshimiwa Diwani tunakushukuru karibu sana lakini sitaacha kushukuru pia mwenyekiti wa kijiji cha Nguyami umetoa ushuhuda chanya unao onyesha faida ya mradi huu wa CHIBWEDA na pia tuwashukuru waalimu kwa jinsi ambavyo mmekuwa mkijitoa kwa jinsi ambavyo mme onyesha juhudi sio jambo rahisi kwa kiufupi umfundisha mwanafunzi mpaka afikie hatua ya kusoma na kuandika kama ambo tumeshuhudia mama yule alivyo soma risala Mungu awabariki sana.
Wahitimu wa leo kwa niaba ya Katibu Mkuu napenda kuwapongeza.
Najua kwamba mmevumilia mambo mengi wakati wakusoma wengine mlipata changamoto za hapa na pale lakini kwa neema ya MUNGU mmeweza kuvumilia yote hayo na mmefika hatua ya mwisho.
Mimi nasema hongeleni sana na Chama cha Biblia kinaona fahari sana kwaajili yenu, mme tufanya kumtukuza Mungu kila tunapo waona hasa katika juhudi zenu na jinsi ambavyo mmefikia hatua hiyo kwakweli sisi mmejawa furaha na mmetufanya tumtukuze MUNGU kwaajili yenu na mimi kama Meneja wa miradi na muakilishi wa Katibu Mkuu sito acha kusema elimu na bidii kama ambavyo mmesikia viongozi wanavyo sema ukisoma
Wakolosai 1 : 10 “mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;
Kwahiyo matunda ya elimu hiyo muyafanye na baadhi yenu kule kijijini hata ajira za vijiji sasa mnaachiwa maana mwazoni ilikuwa sio rahisi, na kwa sababu ya elimu muliyo ipata imewasaidia sana na sasa mnaweza kuajirika.
Mgeni rasmi Baba Askofu Paulo Jacob Mameo
Mgeni rasmi kabla ya kutoa vyeti kwa kundi la tatu la wahitimu wa Chibweda ‘Furaha’ Baba Askofu Momeo wa KKKT aliwataka wahitimu hao kutumia maarifa hayo kujiendeleza kiuchumi na kushiriki katika uchumi wa taifa kwa ujumla.
Baba Askofu Memo aliendelea kuwatia moyo na kuwahimiza kuendeleza kuenzi lugha yao ya Kikagulu na uku wakitumia maarifa hayo waliyoyapata kusaidia kueneza injili kwa watu wengine kwa maana sasa wanaweza kusoma na kuandika na kuwasaidia wengine uko vijijini wasiojua bado kusoma Biblia.
Mwisho nichukue nafasi hii kwa niaba yangu na Kanisa kuwashukuruni Chama cha Biblia cha Tanzania kwa jitihada nzuri ya kufuta ujinga kwa kusoma na kuandika kwa kuanzisha elimu ya watu wazima hasa kupitia kusoma Biblia. Mradi huu ni kitu kizuri sana sio tu kwa kufuta ujinga bali pia kwa kueneza maandiko matakatifu ya Neno la Mungu, Mungu aendelee kuwabariki ili habari njema iendelee kuenea kwa mbinu kama hii ya kufuta ujinga wa kutokusoma na kuandika. Mungu aendelee kuwapa maono zaidi ili huduma hii iendelee. Amina!
Katika mahali hayo burudani ilikuwa sehemu ya sherehe hizo, ambapo wahitimu hao pamoja na walimu wao walionesha michezo na nyimbo mbali mbali za kusifu na kushukuru wadau mbali mbali waliofanikisha wao kupata elimu hii.
Na hapa ni vikundi mbalimbali vya wahitimu wakitoa shukurani zao kupitia njia mbalimbali zikiwemo vile nyimbo, ngonjera pamoja na usomaji wa risala mbele ya mgeni rasmi.
MAHAFALI YA WAHITIMU WA CHIBWEDA MAGUBIKE TAREHE 19/09/2020.
LWA Kikagulu wahitimu 248 waliomaliza na kufaulu mafunzo ya kusoma na kuandika katika awamu ya pili ya mahafali ambayo yalikuwa yafanyike tarehe 21/03/2020 lakini yakahirishwa kutokana na covid -19. Sasa yalifanyika tarehe 19/09/2020 katika Kanisa la Anglikana huko Magubike.
Awamu ya kwanza waliohitimu ni jumla ya watu 69 ambapo wanawake ni 56 na wanaume ni 13 kutoka vijiji 5 Gairo ambavyo ni Gairo, Mogohigwa, Tabuhoteli, Mtumbatu pamoja na Kibedya.
Awamu ya pili waliohitimu jumla ni 248 ambapo wanawake ni 214 na wanaume ni 34; kutoka kwenye vijiji 13 ambavyo ni Magubike, Nguyami, Berega, Chakwale, Ibindo, Mwandi, Mamboya, Mbili, Dumbaalume, Maguha, Magela, Kiegeya Pamoja Na Mabula.
Waliojiandikisha ni 423 kati yao waliohitimu ni 317 na ambao hawajahitimu ni 106 kutokana na changamoto mbalimbali kama vile kuhama, shughuli za mashamba ,na matatizo mbalimbali ya kijamii.
Akizungumza jana baada ya kukabidhi vyeti kwa awamu ya pili ya wahitimu hao, Mratibu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mwl.Frank Makalla alisema wahitimu hao ni wa awamu ya pili ya programu iliyolenga kuwajengea uwezo wa kusoma na kuandika watu wazima wanaoanzia miaka 14 na kuendelea.
Mratibu wa Chama cha Biblia Tanzania, Mwl.Frank Makalla akizungumza na wahitimu wa awamu ya pili katika mahafali hayo huku akiwasisitiza wasiache kufanya yale waliyofundishwa pia wahakikishe kuwa kupitia wao watu wengi zaidi walijue neno la Mungu.
Mratibu wa mpango wa elimu kwa watu wazima kutoka Chama Cha Biblia Cha Tanzania akiongea jambo katika mahafali ya awamu ya pili iliyofanyika Magubike. Alisema kuwa mahafali hayo ni mwendelezo wa mahafali ya awamu ya kwanza ya program hiyo iliyoanza mwaka 2017, ambapo watu 120 walijiandikisha huku watu 97 walihitimu mafunzo hayo ambayo pamoja na kuwafundisha kwa kutumia lugha ya chikagulu kufundishia, mafunzo hayo yanafanywa pia kuweza kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili.
Programu hiyo inafadhiliwa na Chama cha Biblia cha Finland, Chama cha Biblia cha Tanzania pamoja na Summer Institute of linguistics (SIL) ambao wanatoa utaalamu wa waalimu pamoja na mwongozo wa kuandaa vitabu vya kufundishia. Programu hiyo inalenga zaidi kuwainua wanawake kujifunza kusoma na kuandika ingawa na wanaume wanakaribishwa kushiriki.
Mratibu wa mpango huu Mwl. Makalla alisema kati ya watu wazima 248 waliohitimu, wanawake ni 214 na wanaume ni 34 katika awamu hii ya pili ambao walishindwa kufanya hivyo mwezi wa Machi 2020 kutokana na ugonjwa wa corona ulioikumba Dunia nzima wakati huo. Akizungumzia sababu ya baadhi ya watu waliojiandikisha kushindwa kumaliza, Mwl. Makallla alisema kwa wale walioacha masomo, hao wamepewe nafasi ya kujiunga na darasa la awamu ya tatu ambalo limeanza tayari wakiendelea na mafunzo. Aidha, Mwl. Makalla aliomba ushirikiano na serikali katika mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwafanya wananchi waliokosa fursa ya kusoma na kuandika kujiunga na kuendelea kupata elimu hiyo.
“Katika programu yetu hii tumekuwa tukichukua wale wenye umri wa kuanzia miaka 14 na kuendelea, hivyo wale wenye miaka 14 hadi 17, serikali inaweza kuwatambua na kuwaingiza katika mfumo wa MEMKWA katika shule za msingi kama ambavyo Serikali inaelekeza kupitia wizara ya Elimu ili wakajifunze zaidi kwa sababu sisi hapa tunawafundisha kusoma na kuandika tu huko watajifunza masomo mengine pia kama Hesabu, Sayansi, Jiografia Historia na kadhalika.
Mgeni rasmi kabla ya kutoa vyeti kwa kundi la pili la wahitimu wa Chibweda ‘Furaha’ Canon Elias Lucas Chamwenye ambae alimwakilisha Askofu Godfrey Sehaba wa dayosisi ya Morogoro Kanisa la Anglikana aliwataka wahitimu hao kutumia maarifa hayo kujiendeleza kiuchumi na kushiriki katika uchumi wa taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kutumia haki yao ya kimsingi ya kupiga kura kuwachagua viongozi wa nchi Raisi, Wabunge, na Madiwani ifikapo tarehe 28/10/2020.
Mgeni rasmi; Canon Elias Lucas Chamwenye akiwa anazungumza na wahitimu wa awamu ya pili katika mahafali hayo.
Naye Meneja wa Miradi na utunishaji mfuko wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mch. Samwueli Mshana ambaye pia alimwakilisha Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania Ndg. Alfred Elias Kimonge, alisema lengo la Chama cha Biblia ni kutafsiri Biblia kwa lugha za asili, kukuza na kutunza lugha ya asili lakini pia kusaidia jamii husika kusoma na kuelewa Neno la Mungu.
Meneja wa miradi na utunishaji mfuko wa Chama cha Biblia cha Tanzania Mch. Samwueli Mshana akiwapongeza wahitimu wa mahafali ya pili.
Katibu wa idara ya mamaendeleo ya Akina Mama UMAKI Josephine Semwenda katika Dayosisi ya Morogoro ambaye alialikwa kuwatia moyo wahitimu hao aliwasisitizia wahitimu kutokuogopa kuitangaza lugha ya Chikagulu kila mahali katika eneo lao la ukaguruni na kuwahimiza kuwa mabalozi wema katika kuilinda lugha yao isipotee, alitumia nafasi hiyo pia kuwapongeza. wahitimu wote na kuwatakia kila lakheri katika kutekeleza majukumu ya kijamii na Kanisa.
Katibu wa UMAKI Ndg. Josephine Semwenda akitoa wosia wake kwa wahitimu kuzidi kutia juhudi katika kuwafundisha wengine hususani neno la Mungu.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nguyami Mh.Gilbert Ngiga ambaye alitembea umbali mrefu kuja kushuhudia mahafali hayo alisema wao katika kijiji chao tayari wameshamchukua moja kati ya wahitimu hawa anayeitwa Rehema Penford na kumuweka katika kamati ya maendeleo ya kijiji, na wataendelea kufanya hivyo ili kuwahamasisha wengine kujiunga na mpango huu mzuri.
Katika mahafali hiyo kulikuwa na vikundi mbalimbali vya nyimbo, ngonjera, mashairi, maigizo, na kusoma hadithi kutoka katika kitabu cha Chibweda mbele ya mgeni rasmi.
Katika mahafari hayo yaliyofanyika kanisani Anglikana Magubike na mwenyeji wetu Kasisi Elkana Chogohe wa kanisa hilo. Alitoa shukurani zake kwa wahitimu na waanzilishi wa mafunzo kutoka Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kwa watu wazima waeneo hili la wakagulu.
Watu wazima 317 kati ya 423 kutoka vijiji 20 wameitimu mafunzo ya kusoma na kuandika kwa lugha ya Chikagulu.
Akizungumza jana baada ya kukabidhi vyeti 89 kwa awamu ya kwanza ya wahitimu hao, Mratibu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Frank Makalla alisema wahitimu hao ni wa awamu ya pili ya programu iliyolenga kuwajenga uwezo wa kusoma na kuandika watu wazima wanaoanzia miaka 15 na kuendelea.
Mratibu wa Mradi Mwl. Frank Makalla
Mratibu wa mpango wa elimu kwa watu wazima kutoka Chama Cha Biblia Cha Tanzania akiongea jambo katika mahafali ya awamu ya pili iliyofanyika GairoAwamu ya kwanza ya programu hiyo iliyoanza mwaka 2017, watu 120 walijiandikisha huku watu 97 walihitimu mafunzo hayo ambayo pamoja na kuwafundisha kwa lugha ya Chikagulu, mafunzo hayo yanafanywa pia kuweza kusoma na kuandika kwa Kiswahili.
Programu hiyo inafadhiliwa na Chama cha Biblia cha Tanzania, Chama cha Biblia cha Finland na Taasisi ya Lugha ya Kenya, pia unalenga zaidi kuwainua wanawake ingawa na wanaume wanaruhusiwa kushiriki.
Makallla alisema kati ya watu wazima 317 waliohitimu, wanawake ni 270 na wanaume ni 47.
Akizungumzia sababu ya baadhi ya watu waliojiandikisha kushindwa kumaliza, Makallla alisema kwa wale walioacha masomo, hao wamepewe nafasi ya kuingia darasa la awamu ya tatu linalotarajia kuanzia Mei 15, mwaka huu ikiwa ni baada ya walimu kupewa mafunzo ya kujengewa uwezo.
Aidha, Makalla aliomba ushirikiano na serikali katika mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwafanya wananchi waliokosa fursa ya kusoma na kuandika.
“Katika programu yetu tumekuwa tunachukua wale wenye umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea, hivyo wale wenye miaka 15 hadi 17, serikali inaweza kuwatambua na kuwaingiza katika mfumo wa MEMKWA ili wakajifunze Zaidi kwa sababu sisi hapa tunawafundisha kusoma na kuandika tu, ” alieleza.
Mgeni rasmi Dk. Jackson Nyanda (Makamu Mwenyekiti Chama cha Biblia cha Tanzania)
Kabla ya kutoa vyeti kwa kundi la kwanza la wahitimu wa 89 wa Chibweda ‘Furaha’ Dk Jackson Nyanda aliwataka wahitimu hao kutumia maarifa hayo kujiendeleza kiuchumi na kushiriki katika uchumi wa taifa kwa ujumla.
Meneja Miradi na Uhusiano wa Makanisa Mch. Samwueli Mshana
Naye Meneja wa Miradi na utunishaji mfuko wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Samwueli Mshana ambaye pia alimwakilisha Katibu wa chama hicho, alisema lengo la chama chake ni kutafsiri Biblia kwa lugha za asili, kukuza na kutunza lugha ya asili lakini pia kusaidia jamii husika kuelewa Neno la Mungu.
For so hath the Lord commanded us, saying, I have set thee to be a light of the Gentiles, that thou shouldest be for salvation unto the ends of the earth.