1. Je Chama cha Biblia kinapata wapi fedha za kukiendesha?

Chama cha Biblia cha Tanzania kinaendeshwa kwa michango ya Makanisa, Taasisi mbalimbali za Makanisa, Watu binafsi ambao ni wanachama, Marafiki wa Chama na Muungano wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni ambao unatoa misaada ya Maandiko Matakatifu kutoka nje ambayo Chama kinayauza na kutumia sehemu ya mapato kuendesha huduma.

2. Je Chama cha Biblia cha Tanzania kina mahitaji gani?

Ili kutekeleza kazi zake za Kutafsiri, Kuchapisha na Kueneza Maandiko Matakatifu Chama cha Biblia chaTanzania kinahitaji kiasi kisichopungua Dola Milioni moja za Marekani kwa mwaka.  Kama Kanisa na Wakristo binafsi watakuwa wanachangia kila mwaka  kwa uaminifu Chama kinaweza kuendesha kazi zake vizuri.

3. Je unawezaje kusaidia kazi za Chama cha Biblia?

Kuna njia nyingi za kukisaidia Chama cha Biblia katika kazi zake na kinamualika kila Mkristo kushiriki yafuatayo:-

  • Kujiunga na kuwa Mwanachama na kuchangia

Uanachama

Kadi scaled

Give Today

Children

Prison

Membership

Youth

Blind

Other

Get In Touch

× How can I help you?