Maafali ya Saba ya Mradi wa Literacy for Women in Africa.

Mahali: ukumbi wa Nazareti, wilayani Gairo, mkoani Morogoro.

Picture5

Hafla hii ilihudhuriwa na viongozi wa dini na serikali wakiwemo wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa (W) ya Gairo pamoja na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji pia Afisa mipango na Afisa maendeleo ya jamii ambapo waliwapongeza sana wahitimu kwa juhudi zao kubwa na kusisitiza umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii.

Chama cha Biblia, kupitia mradi wake wa Literacy for Women in Africa, kimefanikisha hatua muhimu katika kuimarisha elimu ya wanawake nchini. Mahafali ya saba ya mradi huu yaliyofanyika tarehe 23 Januari 2025 katika ukumbi wa Nazareti, wilayani Gairo, mkoani Morogoro, yaliwahitimu wanawake 353 katika ngazi ya A ya kusoma na kuandika.

Picture6
Picture4

Mradi wa Literacy for Women in Africa umeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya wanawake hawa. Wengi wao sasa wanaweza kusoma Biblia, kuendesha biashara ndogo ndogo, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii zao.

“Shuhuda kutoka kwa mmoja wa wahitimu: “Kabla ya kuanza kusoma, nilikuwa tegemezi sana. Sasa naweza kusoma na kufuatilia habari, na hata kuandika barua ya maombi ya kazi na kushiriki na mambo mbalimbali ya kijamii kama kupiga kura na kuchagua viongozi na hata kugombea nafasi za kiuongozi kama uenyekiti wa mtaa. Maisha yangu yamebadilika kabisa!”

Picture Mzee
Meza kuu wakifurahia jambo wakati wa maafali

Mahafali haya yamekuwa ushahidi tosha wa kwamba elimu ni nguvu. Chama cha Biblia kinaendelea kujizatiti kuhakikisha kuwa wanawake wengi zaidi wanapata fursa ya kujifunza na kukuza uwezo wao. Tunawashukuru sana wadau wote kwa ushirikiano wenu katika kufanikisha mradi huu.

Wahitimu
Picture ya Pamoja
2
Picture3
7

Matukio katika Picha

0 Comments

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

× How can I help you?