Yaliyojiri Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) 2023

Yaliyojiri Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) 2023

Muhtasari wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 2023 wa Chama cha Biblia Tanzania

Key Outcomes and Future Directions

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 2023 (AGM) wa Jumuiya ya Biblia Tanzania ulikuwa tukio muhimu sana, uliwaleta pamoja wanachama na wadau ili kujadili mustakabali wa shirika. Mkutano huo uliofanyika mjini Dodoma Mei 17, 2024 ulilenga mipango ya kimkakati na jitihada za ushirikiano ili kuendeleza dhamira yetu.

MG 1262 scaled

Muhtasari wa Kina wa AGM ya 2023

Mkutano mkuu ulianza kwa maombi ya ufunguzi na hotuba ya makaribisho ya Mwenyekiti. Majadiliano muhimu yalijumuisha mapitio ya mafanikio ya mwaka uliopita, ripoti za fedha na mipango ya kimkakati ya mwaka ujao. Wanachama walijadili kuhusu mipango mbalimbali inayolenga kupanua ufikiaji wetu na kuboresha programu zetu.

Maamuzi muhimu yalifanywa kuhusu utekelezaji wa miradi mipya, ubia, na mikakati ya ushirikishwaji wa jamii. Mkutano ulihitimishwa kwa kujitolea kudumisha maadili yetu na kuendeleza dhamira yetu kwa nguvu mpya na kujitolea.

Muda mfupi kutoka kwa AGM ya 2023

Matukio katika Picha

MG 0965 scaled
MG 0962 scaled
2 scaled
5 scaled
1 scaled
10 scaled
8 scaled
MG 0992 scaled
16 scaled
MG 1983 scaled
MG 0961 scaled

Wasiliana Nasi

Zingatia:

Kwa maswali yoyote kuhusu AGM 2023, tafadhali wasiliana na kamati yetu ya maandalizi kwa anwani ifuatayo:

Barua pepe
Namba ya Simu

(+255) 784-683-120

Endelea kupata Habari kutoka kwetu

Usikose taarifa za hivi punde na ripoti za kina kutoka kwa Mkutano Mkuu Mwaka 2023. Jiandikishe kwa jarida letu na upate habari kuhusu miradi yetu inayoendelea na matukio yajayo.

Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) 2023

Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) 2023

Join Us for the Annual General Meeting in Dodoma!

Bible Society of Tanzania AGM - May 17, 2024

Mark your calendars for an important gathering of the Bible Society of Tanzania members on May 17, 2024, starting at 9 AM at ELCT-Dodoma Conference Hall.

0 b49cecb9 75b7 4b95 9687 9e85f0c1497f

Annual General Meeting 2024

May 17, 2024

MG 0182 scaled

The Bible Society of Tanzania invites all active members to attend the Annual General Meeting (AGM) hosted by Dr. Alfred E. Kimonge, General Secretary. The event will commence at 9 AM at the ELCT-Dodoma Conference Hall.

Admission is FREE

Reserve Your Spot Today!

Don't miss the opportunity to be part of this significant event. Message us now to confirm your attendance.

Get In Touch

Contact Us For Event Details

For inquiries about the Annual General Meeting of the Bible Society of Tanzania, please do not hesitate to reach out to us. We are available via email, phone, or you can visit us at our office in Dodoma.

Email: info@bibesociety-tanzania.org
Phone: +255 784 683 120
Address: ELCT Conference Hall, Central District, Dodoma City

SAUTI YA VIJANA WASAMARIA.

SAUTI YA VIJANA WASAMARIA.

SAUTI YA VIJANA WASAMARIA.

Program hii inatekelezwa na Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na dawati la vijana (Africa Youth Service -United Bible Society).

Madhumuni ya programu ni kuwasaidia, kuandaa, na kuwajengea vijana wadogo miaka 9-24 uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa ajili yao na kwa ajili ya maendeleo ya jamii, tukilenga kwenye masuala ya usawa na unyanyasaji wa kijinsia, ushiriki wa watu wenye ulemavu, elimu ya afya ya uzazi na ngono, mitandao ya kijamii, itikadi kali, na utunzaji wa mazingira.

Shughuli kubwa ya programu hii ni kutoa mafunzo kwa vijana wadogo, kupitia warsha shirikishi kwenye jamii yao kwa kushirikiana na makanisa pamoja na wadau wengine.

Walengwa wa mpanguu ni makanisa, shule, vikundi vya vijana, vituo vya watoto yatima,mashirika ya serikali,pamoja na wazazi/walezi.

IMG 3985 scaled

Wadau wa Mradi

IMG 4979 scaled

Majadiliano

IMG 5102 scaled

Pia program hii inalenga.

Kuwapa taarifa sahihi vijana wadogo kuhusu mabadiliko ya kubalehe na afya ya uzazi, ujinsia,

usawa wa kijinsia, watu wenye ulemavu, urafiki na kujithamini, mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa

  1. Kuhimiza vijana kufanya maamuzi yenye afya na kuepuka ushawishi mbaya kutoka kwa marafiki, vyombo vya habari vya habari & mitandao na makundi yenye itikadi kali
  2. Kuwaandaa wadau wa program hii kuweza kutimiza wajibu wao wa kusaidia na kuchangia maendeleo chanya na shirikishi kwa vijana.

    Kulingana na nyenzo na shughuli zilizopangwa, malengo yafuatayo yatatumika:

    1. Kuwaandaa wazazi/walezi kuhimiza na kuwezesha maendeleo chanya na shirikishi kwa vijana.
    2. Kutoa mafunzo ya stadi za maisha kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu
    3. Kutoa maarifa ya kimsingi kuhusu VVU
    4. Kujenga ufahamu na kutetea haki za watoto, ikiwa ni pamoja na hatari ya unyanyasaji wa kingono
    5. Kuwapa wazazi na walezi ujuzi wa kufuatilia na kuwalinda watoto.
    IMG 4979 scaled
    MAHAFALI YA SITA YA LWA KIKAGURU

    MAHAFALI YA SITA YA LWA KIKAGURU

    LITERACY FOR WOMEN IN AFRICA PROJECT.

    TAARIFA FUPI YA MPANGO & MAHAFALI YA SITA YA MPANGO HUU

    Mahafali ya sita ya mpango huu yalifanyika tarehe 17.2.2024 katika Ukumbi wa Nazarethi, Gairo mjini ambapo wanakisomo 421 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu Kisomo cha watu wazima na Mkuu wa (w) ya Gairo. Mh. Jabiri Shekimweri.  Sherehe hizi zilihudhuriwa na wageni wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Dkt. Alfred E. Kimonge, Bodi ya wakurugenzi wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wafanyakazi na viongozi wa makanisa na jamii kutoka wilaya ya Gairo na Kilosa.

    Mpango huu umeendelea kutekelezwa na Chama cha Biblia cha Tanzania katika (w) ya Gairo na Kilosa. Lengo kuu ni kuwasaidia wanawake na wasichana hawakuweza kwenda shule  na hawajui Kusoma na Kuandika.

    26 scaled

    Mmoja wa wanakisomo akipokea cheti cha kuitimu elfu hiyo.

    23 scaled
    13 scaled
    12 scaled
    beauty esthetician 43

    SHUGHULI ZA UTEKELEZAJI

    Katika kipindi cha mwaka 2023, Chama cha Biblia kupitia mpango huu kiliweza kutekeleza shughuli zifuatavyo;

    • Kufanya uhamasishaji na kuandikisha wanakisomo 450 (Me 379 & Ke 71) kabla ya madarasa kuanza.
    • Mpango huu umelenga zaidi wanawake na wasichana, ila wapo pia wanaume ambao wamejiunga na madarasa na wamekuwa wanufaika wazuri. Takwimu zinaonyesha kuna idadi kubwa ya wanaume wasiojua kusoma na kuandika na mpango huu unawakaribisha.
    • Kufanya mafunzo kwa waalimu 30 wanaofundisha kwenye madarasa ya watu wazima. Mafunzo haya yalifanyika Dodoma kwa wiki mbili yakiongozwa na wakufunzi kutoka SIL Nairobi, Kenya.
    • Kuchapisha na kuwagawa vitabu 450 vya kujisome kwa wanakisomo wote waliojiandikisha.
    • Kuhamasisha na kuanzisha vikundi (improving literacy groups) vya kujisome vitabu vya hadithi. Vikundi hivi ni kwa ajili ya wahitimu ili kuweza kuendeleza ujuzi na kupata uzoefu zaidi katika kujua kusoma na kuandika. Hapa wananapata nafasi ya kujisomea vitabu vya aina mbalimbali, majarida, magazeti, Biblia pamoja na makala nyingine nyingi.

    Wawezeshe Kusoma

    MAFANIKIO.

    • Kuongezeka kwa wanajamii wanaojua kusoma /kuandika kila mwaka kwenye eneo la mpango.
    • Wanawake kupata na kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwenye jamii yao kutokana na uwezo wao.
    • Kumekuwa na jamii inayojiamini zaidi na yenye uelewa juu ya masuala mbali mbali.mfano Afya, kilimo, mazingira kuanzia kwenye ngazi ya familia.
    • Kumewasaidia kusoma Neno la Mungu pamoja na hii imeongeza ukuaji wa kiroho.
    beauty esthetician 38
    14 scaled
    28 scaled
    9 scaled
    22 scaled
    6 scaled
    4 scaled
    21 scaled
    17 scaled

    Blog

    Product Updates & Sales

    Biblia kwa Wafungwa Kanda ya Kaskazini

    Biblia kwa Wafungwa Kanda ya Kaskazini

    Biblia kwa Wafungwa Kanda ya Kaskazini

    Habari Kamili.

    Chama cha Biblia cha Tanzania kimeendelea na huduma yake ya kugawa Biblia kwa baadhi ya magereza hapa nchini.

    Chama kimeendelea kutoa huduma hiyo kutokanana  sadaka na michango ya  wanachama wake, wadau mbali mbali na watu binafsi wenye mapenzi na neema ya kufanya kazi ya Mungu walioko ndani na nje ya nchi.

    Picha zinaonesha baadhi ya magereza yaliyoko katika kanda ya Kaskazini waliofikiwa na kugawiwa Biblia kutoka katika Chama cha Biblia chanTanzania.

    Tunamshukuru Mungu kwa neema hii. Tunaamini kupitia Biblia hizi watu watafikiwa na Neno la Mungu ambalo litabadilisha maisha yao, watazidi kumjua Mungu na kumtumikia. Tunaomba Mungu awabariki na aendelee kuwatumia ili kuwafikia walengwa wengi zaidi na kazi ya Mungu izidi kusonga mbele kwa ushindi mkuu.

    Wapare

    Ugawaji wa Maandiko Matakatifu (Biblia)kwa wafungwa wa Gereza (W) Same Kilimanjaro

    Hata Katesh wafungwa wanalitaja jjina la Yesu

    Ugawaji wa Maandiko Matakatifu (Biblia)kwa wafungwa wa Kateshi

    Kazi njema Magereza ya kaskazini imeanzia Babati Yesu asifiwe

    Ugawaji wa Maandiko Matakatifu (Biblia)kwa wafungwa wa Gereza la Manyara Babati

    Wafungwa wa Arusha Mjini

    Ugawaji wa Maandiko Matakatifu (Biblia)kwa wafungwa wa Gereza Arusha mjini

    Wafungwa wa Mbulu wanamtukuza Mungu pia
    BST IMAGE

    Sign up for the Bible Society of Tanzania mailing list

    MPANGO WA KISOMO CHA WATU WAZIMA – LITERACY FOR WOMEN IN AFRICA.

    MPANGO WA KISOMO CHA WATU WAZIMA – LITERACY FOR WOMEN IN AFRICA.

    MPANGO WA KISOMO CHA WATU WAZIMA – LITERACY FOR WOMEN IN AFRICA.

    Habari Kamili.

    Chama cha Biblia cha Tanzania kinaendelea kutekeleza mpango wa Kisomo cha elimu ya watu wazima katika wilaya ya Kilosa na Gairo kwenye vijiji 15 vilivyochaguliwa wakati wa kuanzishwa kwa mpango huu. Mpango wa Kisomo cha elimu ya watu wazima umeweza kuwafikia wanaume na wanawake 1500. Wanakisomo waliofikiwa na mpango huu wanajua kusoma na kuandika, maisha yao yamebadilika na wanaishi maisha ya kawaida kama walivyo watu wengine waliosoma. Pia ushirikishwaji wao katika masuala ya kijamii umeongezeka, wengine wamepata nafasi za uongozi kwenye jamii na Kanisa limeweza kuwa na washirika wanaoweza kusoma na kulielewa Neno la Mungu pia kufanya majukumu yao ya utumishi kwa weledi zaidi kulinganisha na ilivyokuwa kabla ya kujua kusoma na kuandika.

    Waalimu wa Chikagulu wakiwa kwenye mafunzo scaled

    Waalimu wa Chikagulu wakiwa kwenye mafunzo

    Ili kufanikisha mpango huu Chama cha Biblia kwa kushirikiana na SIL Nairobi walifanya mafunzo ya kuwajengea uwezo waalimu 30 wa Chikagulu. Mafunzo  hayo yalifanyika Dodoma kwa wiki mbili ambapo  waalimu waliweza kufundishwa  mada tofauti tofauti kulingana na mfumo wa mpango ulivyo, baadhi ya mada walizofundishwa ni mifumo ya literacy, sifa za mwalimu bora, sifa za mwanakisomo, majukumu ya mwalimu kabla  na akiwa ndani ya darasa.

    Kwa kipindi cha mwaka huu 2023, Chama cha Biblia cha Tanzania kimeweza kuandikisha wanakisomo 450. Wanakisomo waliojiandikisha  hawawezi kusoma, hawajawai kwenda shule na hawajawahi kukutana na jarida/ gazeti, kitabu chochote na hawajui kuandika. Madarasa yataanza mwezi June,2023 kwa kipindi cha miezi saba.

    Waalimu wa waalimu wa Chikagulu wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo scaled

    Waalimu wa waalimu wa Chikagulu wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo

    Askofu huyo aliwakumbusha washiriki wa mkutano huokumwomba Mungu zaidi kwa kuwa wanahubiri injili katika kizazi kinachobadilika lakini wao wanahubiri neno la Mungu lisilobadilika, jambo linaloibua changamoto mbalimbali ikiwemo lugha.
    Alitoa mfano kuwa wakati wao kama chama wanajitahidi kuhubiri injili kwa lugha ya
    Kiswahili inayosikika kwa watu wengi, lakini Kiswahili chenyewe kinabadilikabadilika.

    BST IMAGE

    Sign up for the Bible Society of Tanzania mailing list