UZINDUZI WA SEHEMU YA BIBLIA KWA LUGHA YA KINYIHA WAFANYIKA KANISA LA MORAVIAN, MBOZI

Jimbo la Mbozi, Kanisa la Moravian Ushirika wa Igamba – 27 Oktoba 2024

IMG 9844 scaled

Tukio la kihistoria la uzinduzi wa vitabu vya Biblia vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kinyiha vitabu vya Ruthu, 1 Samweli, 1 Wafalme, na Yona limefanyika leo katika Kanisa la Moravian Ushirika wa Igamba, Jimbo la Mbozi. Uzinduzi huu umefanywa na Katibu Mkuu wa Jimbo la Mbozi, Mchungaji Rayson Kibona, huku ukiongozwa na Mch. Lastone Chalotela Mwamlima ambaye ni mratibu wa mradi pia mwenyekiti wa wilaya na Mchungaji Wiliadi Zewanga mchungaji wa ushirika wa Igamba Moravian.

Tukio hilo muhimu limeandaliwa na Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na makanisa ya Kikristo kutoka Mkoa wa Songwe, hasa Wilaya ya Mbozi ambako lugha ya Kinyiha huzungumzwa kwa wingi.

20241027 094333 scaled
IMG 9764 scaled
IMG 9753 scaled

Katika hafla hiyo, viongozi mbalimbali walihudhuria na kutoa hotuba kuhusu umuhimu wa tukio hili. Madam Leah Kiloba, Meneja wa Tafsiri kutoka Chama cha Biblia cha Tanzania, aliwasilisha ujumbe wa Chama hicho na Umoja wa Vyama vya Biblia Duniani, akieleza majukumu makuu ya Chama kuwa ni kutafsiri, kuchapisha, na kusambaza Biblia kwa gharama nafuu ili kuwafikia watu wote. Kiloba alisisitiza umuhimu wa mradi huu kwa jamii ya Wanyiha na kuwashukuru washiriki wote waliotoa mchango katika tafsiri. Pia aliwaomba jamii ya wanyiha baada ya kupokea vitabu hivyo wavisome kisha kama kuna makosa wayalete ili yalekebishwe mapema kabla ya Biblia kamili kukamilika.

Watafsiri na Wahakiki wa Tafsiri
Kazi ya kutafsiri vitabu hivi imefanywa kwa bidii na ushirikiano wa wataalamu wa lugha, viongozi wa makanisa, na wahakiki wa tafsiri. Baadhi ya watafsiri wakuu ni:
– Mch. Lastone Chalotela Mwamlima (mratibu)
– Mch. Justus Vhalondeghe Sinkonde
– Mch. Philimon Partson Balanga
– Dada Christina Chares Singogo

IMG 9821 scaled
IMG 9816 scaled

Wahakiki wa tafsiri walioshiriki ni pamoja na:
– Mch. Sila Mwamwezi
– Mch. Sostini Mwansenga
– Mch. Wilhelm Mwakavanga
– Mch. Selemani Nkota
– Mch. Lameck Nzowa
– Mch. Nichorous Shonza
– Dada Martha Mwashiuya
– Dada Upendo Mwashilindi
Pia, Dkt. Chris Pekka Wilde alitajwa kwa mchango wake muhimu wa kiufundi kama mshauri wa mradi huu.

IMG 9835
IMG 9828 scaled

Viongozi wa Makanisa Mbalimbali Wajumuika

Uzinduzi huu ulihudhuriwa na wachungaji na viongozi wa makanisa kutoka madhehebu tofauti, wakiwemo wawakilishi kutoka makanisa ya Last Church, Kanisa Katoliki, TAG, na KKKT. Viongozi hawa walipongeza hatua hii kama ishara ya kuendelea kwa kasi kwa mradi huu, ambao unalenga kuongeza upatikanaji wa Biblia kwa lugha ya Kinyiha kwa ufasaha.

IMG 9754 scaled
IMG 9771 scaled

Mafanikio na Matumaini ya Mradi wa Tafsiri kwa Lugha ya Kinyiha

Tukio hili limeibua matumaini makubwa na linaashiria mwanzo mzuri kwa jamii ya Wanyiha kupata Biblia kwa lugha yao wenyewe, hatua ambayo itaimarisha zaidi imani na kueneza Neno la Mungu kwa undani zaidi katika eneo hilo.

IMG 9764 scaled

0 Comments

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

× How can I help you?