Biblia kwa Wafungwa Kanda ya Kaskazini
Habari Kamili.
Chama cha Biblia cha Tanzania kimeendelea na huduma yake ya kugawa Biblia kwa baadhi ya magereza hapa nchini.
Chama kimeendelea kutoa huduma hiyo kutokanana sadaka na michango ya wanachama wake, wadau mbali mbali na watu binafsi wenye mapenzi na neema ya kufanya kazi ya Mungu walioko ndani na nje ya nchi.
Picha zinaonesha baadhi ya magereza yaliyoko katika kanda ya Kaskazini waliofikiwa na kugawiwa Biblia kutoka katika Chama cha Biblia chanTanzania.
Tunamshukuru Mungu kwa neema hii. Tunaamini kupitia Biblia hizi watu watafikiwa na Neno la Mungu ambalo litabadilisha maisha yao, watazidi kumjua Mungu na kumtumikia. Tunaomba Mungu awabariki na aendelee kuwatumia ili kuwafikia walengwa wengi zaidi na kazi ya Mungu izidi kusonga mbele kwa ushindi mkuu.
Ugawaji wa Maandiko Matakatifu (Biblia)kwa wafungwa wa Gereza (W) Same Kilimanjaro
Ugawaji wa Maandiko Matakatifu (Biblia)kwa wafungwa wa Kateshi
Ugawaji wa Maandiko Matakatifu (Biblia)kwa wafungwa wa Gereza la Manyara Babati
Ugawaji wa Maandiko Matakatifu (Biblia)kwa wafungwa wa Gereza Arusha mjini