SAUTI YA VIJANA WASAMARIA.
Program hii inatekelezwa na Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na dawati la vijana (Africa Youth Service -United Bible Society).
Madhumuni ya programu ni kuwasaidia, kuandaa, na kuwajengea vijana wadogo miaka 9-24 uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa ajili yao na kwa ajili ya maendeleo ya jamii, tukilenga kwenye masuala ya usawa na unyanyasaji wa kijinsia, ushiriki wa watu wenye ulemavu, elimu ya afya ya uzazi na ngono, mitandao ya kijamii, itikadi kali, na utunzaji wa mazingira.
Shughuli kubwa ya programu hii ni kutoa mafunzo kwa vijana wadogo, kupitia warsha shirikishi kwenye jamii yao kwa kushirikiana na makanisa pamoja na wadau wengine.
Walengwa wa mpanguu ni makanisa, shule, vikundi vya vijana, vituo vya watoto yatima,mashirika ya serikali,pamoja na wazazi/walezi.
Wadau wa Mradi
Majadiliano
Pia program hii inalenga.
Kuwapa taarifa sahihi vijana wadogo kuhusu mabadiliko ya kubalehe na afya ya uzazi, ujinsia,
usawa wa kijinsia, watu wenye ulemavu, urafiki na kujithamini, mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa
- Kuhimiza vijana kufanya maamuzi yenye afya na kuepuka ushawishi mbaya kutoka kwa marafiki, vyombo vya habari vya habari & mitandao na makundi yenye itikadi kali
- Kuwaandaa wadau wa program hii kuweza kutimiza wajibu wao wa kusaidia na kuchangia maendeleo chanya na shirikishi kwa vijana.
Kulingana na nyenzo na shughuli zilizopangwa, malengo yafuatayo yatatumika:
- Kuwaandaa wazazi/walezi kuhimiza na kuwezesha maendeleo chanya na shirikishi kwa vijana.
- Kutoa mafunzo ya stadi za maisha kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu
- Kutoa maarifa ya kimsingi kuhusu VVU
- Kujenga ufahamu na kutetea haki za watoto, ikiwa ni pamoja na hatari ya unyanyasaji wa kingono
- Kuwapa wazazi na walezi ujuzi wa kufuatilia na kuwalinda watoto.