LITERACY FOR WOMEN IN AFRICA PROJECT.
TAARIFA FUPI YA MPANGO & MAHAFALI YA SITA YA MPANGO HUU
Mahafali ya sita ya mpango huu yalifanyika tarehe 17.2.2024 katika Ukumbi wa Nazarethi, Gairo mjini ambapo wanakisomo 421 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu Kisomo cha watu wazima na Mkuu wa (w) ya Gairo. Mh. Jabiri Shekimweri. Sherehe hizi zilihudhuriwa na wageni wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Dkt. Alfred E. Kimonge, Bodi ya wakurugenzi wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wafanyakazi na viongozi wa makanisa na jamii kutoka wilaya ya Gairo na Kilosa.
Mpango huu umeendelea kutekelezwa na Chama cha Biblia cha Tanzania katika (w) ya Gairo na Kilosa. Lengo kuu ni kuwasaidia wanawake na wasichana hawakuweza kwenda shule na hawajui Kusoma na Kuandika.
Mmoja wa wanakisomo akipokea cheti cha kuitimu elfu hiyo.
SHUGHULI ZA UTEKELEZAJI
Katika kipindi cha mwaka 2023, Chama cha Biblia kupitia mpango huu kiliweza kutekeleza shughuli zifuatavyo;
- Kufanya uhamasishaji na kuandikisha wanakisomo 450 (Me 379 & Ke 71) kabla ya madarasa kuanza.
- Mpango huu umelenga zaidi wanawake na wasichana, ila wapo pia wanaume ambao wamejiunga na madarasa na wamekuwa wanufaika wazuri. Takwimu zinaonyesha kuna idadi kubwa ya wanaume wasiojua kusoma na kuandika na mpango huu unawakaribisha.
- Kufanya mafunzo kwa waalimu 30 wanaofundisha kwenye madarasa ya watu wazima. Mafunzo haya yalifanyika Dodoma kwa wiki mbili yakiongozwa na wakufunzi kutoka SIL Nairobi, Kenya.
- Kuchapisha na kuwagawa vitabu 450 vya kujisome kwa wanakisomo wote waliojiandikisha.
- Kuhamasisha na kuanzisha vikundi (improving literacy groups) vya kujisome vitabu vya hadithi. Vikundi hivi ni kwa ajili ya wahitimu ili kuweza kuendeleza ujuzi na kupata uzoefu zaidi katika kujua kusoma na kuandika. Hapa wananapata nafasi ya kujisomea vitabu vya aina mbalimbali, majarida, magazeti, Biblia pamoja na makala nyingine nyingi.
Wawezeshe Kusoma
MAFANIKIO.
- Kuongezeka kwa wanajamii wanaojua kusoma /kuandika kila mwaka kwenye eneo la mpango.
- Wanawake kupata na kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwenye jamii yao kutokana na uwezo wao.
- Kumekuwa na jamii inayojiamini zaidi na yenye uelewa juu ya masuala mbali mbali.mfano Afya, kilimo, mazingira kuanzia kwenye ngazi ya familia.
- Kumewasaidia kusoma Neno la Mungu pamoja na hii imeongeza ukuaji wa kiroho.
Blog
Product Updates & Sales
Uzinduzi wa sehemu ya Biblia (portion) kwa lugha ya Kiha.
Uzinduzi wa sehemu ya Biblia (portion) kwa lugha ya Kiha.Mahali: Kijiji cha Nyakimwe, Wilaya ya Buhigwe Dhehebu: Kanisa la Anglican Maelezo ya Meneja wa Tafsiri, Leah Kiloba Leah Kiloba alielezea maendeleo ya mradi huu, akisisitiza kuwa Chama cha Biblia kinaendelea...
KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA BIBLIA MKOANI DODOMA
KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA BIBLIA MKOANI DODOMADodoma, 03 Novemba 2024 – Maadhimisho ya kilele cha Juma la Biblia mwaka huu yamefanyika kwa mafanikio makubwa mkoani Dodoma, katika Uwanja wa Mashujaa. Maadhimisho hayo yaliyoanza na maandamano ya amani kutoka...
UZINDUZI WA SEHEMU YA BIBLIA KWA LUGHA YA KINYIHA WAFANYIKA KANISA LA MORAVIAN, MBOZI
UZINDUZI WA SEHEMU YA BIBLIA KWA LUGHA YA KINYIHA WAFANYIKA KANISA LA MORAVIAN, MBOZIJimbo la Mbozi, Kanisa la Moravian Ushirika wa Igamba – 27 Oktoba 2024Tukio la kihistoria la uzinduzi wa vitabu vya Biblia vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kinyiha vitabu vya Ruthu, 1...