Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.
Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”
Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.
Wafungwa, Mahabusu Dar wakabidhiwa Biblia Takatifu
Na Dalphina RubyemaWAKATI Chama cha Biblia cha Tanzania kikiwa kimetoa msaada wa Biblia Takatifu kwa wafungwa na mahabusu ya Magereza ya Segerea, Ukonga na Keko yote ya jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Gereza la Segerea, SSP. Daniel Mwakyoma amesema ukosefu wa uzio na...
Watu wazima 317 wajifunza kusoma, kuandika
Na Anastazia Anyimike, Gairo - Morogoro Watu wazima 317 kati ya 423 kutoka vijiji 20 wameitimu mafunzo ya kusoma na kuandika kwa lugha ya Chikagulu.Akizungumza jana baada ya kukabidhi vyeti 89 kwa awamu ya kwanza ya wahitimu hao, Mratibu wa Chama cha Biblia cha...
Wanakisomo wa Elimu ya watu wazima katika msemo wa Kikaguru
Na. Ndugu Frank Makalla (Msimamizi Mkuu wa Mradi-CBT).Chama Cha Biblia Cha Tanzania kilianzisha kisomo cha elimu ya watu wazima kwa kushirikiana na Chama Cha Biblia Cha Finland na SIL (Summer Institute of linguistic) mnamo mwaka 2017 na mwaka huo ulikuwa ni mwaka wa...
TAFSIRI YA BIBLIA KWA LUGHA YA KIRIMI YAFIKIA PAZURI
Kwa Ufupi:Kutokana na kikao cha mapitio ya maendeleo ya mradi wa tafsiri ya Biblia kwa Lugha ya Kirimi November 04-09, 2019, Mkoani Singida, Tafsri bingwa Dr.Samy Tioye kutoka UBS athibitisha mradi huu kuendelea vizuri na umefikia hatua nzuri zaidi kwa hali hiyo...
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.
Donate Today or Get Involved