Kwa Ufupi:

Kutokana na kikao cha mapitio ya maendeleo ya mradi wa tafsiri ya Biblia kwa Lugha ya Kirimi November 04-09, 2019, Mkoani Singida, Tafsri bingwa Dr.Samy Tioye  kutoka UBS athibitisha mradi huu kuendelea vizuri na umefikia hatua nzuri zaidi kwa hali hiyo Biblia ya Lugha ya Kirimi tunaitegemea iwe imekamilika 2020 December.

Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na Kanisa tunafanya kazi ya kutafsiri Biblia kwa Lugha ya Kirimi. Kazi hii inafanyika kwa ustadi mkubwa na kuzingatia kanuni na utalaam wa tafsiri ya Biblia kutoka muungano wa vyama vya Biblia Ulimwenguni (UBS).

Kwa mantiki hiyo hapa chini katika picha tunaona Dr.Samy Tioye mmoja wa watafsiri Bingwa wa Lugha kutoka UBS akiwa na watafsiri wa Lugha ya Kirimi katika kuangalia usahihi wa kazi hii muhimu.

jifuze na hili

Kirimi team, Singida, Tanzania

Mshauri bingwa wa Tafsiri za Biblia Dr.Samy Tioye akiwa anawaonyesha aina mbalimbali za tafsiri za Biblia na namna zinavyoweza kutumika kusaidia tafsiri ya Biblia kwa Lugha ya Kirimi, Katika ofisi ya tafsiri ya Biblia kwa Lugha Kirimi Mkoani Singida.

maelekezo

Maelekezo

Mshauri bingwa wa Tafsiri za Biblia Dr.Samy Tioye akiwa anaelezea jambo kwa watafsiri wa Biblia kwa Lugha ya Kirimi, Katika ofisi ya tafsiri ya Biblia kwa Lugha Kirimi Mkoani Singida.

umakini

Umakini

Watafsiri wa Biblia kwa Lugha ya Kirimi (Mch. Elia Mande na Mch. Simoni Kusina) wakipitia na kufanya masahihisho ya kitabu cha Kumbukumbu la torati.

kusaiisha

kusaiisha

Mrs. Joyce Shisha, Katibu muhutasi wa mradi wa Kirimi akiingiza masahihisho ya kitabu cha Kumbukumbu ya tarati kwenye Programu maalumu ya Tafsiri za Biblia iitwayo Paratext.

pamoja

Pamoja

Picha ya pamoja kati ya Meneja wa Tafsiri, mtafsiri Bingwa pamoja na watafsiri wa Biblia kwa Lugha ya Kirimi.

× How can I help you?