Na Anastazia Anyimike, Gairo – Morogoro

Pokea cheti Bibi Ongera

 Watu wazima 317 kati ya 423 kutoka vijiji 20 wameitimu mafunzo ya kusoma na kuandika kwa lugha ya Chikagulu.

Akizungumza jana baada ya kukabidhi vyeti 89 kwa awamu ya kwanza ya wahitimu hao, Mratibu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Frank Makalla alisema wahitimu hao ni wa awamu ya pili ya programu iliyolenga kuwajenga uwezo wa kusoma na kuandika watu wazima wanaoanzia miaka 15 na kuendelea.

Mratibu wa mpango wa elimu kwa watu wazima kutoka Chama Cha Biblia Cha Tanzania akiongea jambo katika mahafali ya awamu ya pili iliyofanyika Gairo

Mratibu wa Mradi Mwl. Frank Makalla

Mratibu wa mpango wa elimu kwa watu wazima kutoka Chama Cha Biblia Cha Tanzania akiongea jambo katika mahafali ya awamu ya pili iliyofanyika GairoAwamu ya kwanza ya programu hiyo iliyoanza mwaka 2017, watu 120 walijiandikisha huku watu 97 walihitimu mafunzo hayo ambayo pamoja na kuwafundisha kwa lugha ya Chikagulu, mafunzo hayo yanafanywa pia kuweza kusoma na kuandika kwa Kiswahili.

Programu hiyo inafadhiliwa na Chama cha Biblia cha Tanzania, Chama cha Biblia cha Finland na Taasisi ya Lugha ya Kenya, pia unalenga zaidi kuwainua wanawake ingawa na wanaume wanaruhusiwa kushiriki.

Makallla alisema kati ya watu wazima 317 waliohitimu, wanawake ni 270 na wanaume ni 47.

Akizungumzia sababu ya baadhi ya watu waliojiandikisha kushindwa kumaliza, Makallla alisema kwa wale walioacha masomo, hao wamepewe nafasi ya kuingia darasa la awamu ya tatu linalotarajia kuanzia Mei 15, mwaka huu ikiwa ni baada ya walimu kupewa mafunzo ya kujengewa uwezo.

Aidha, Makalla aliomba ushirikiano na serikali katika mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwafanya wananchi waliokosa fursa ya kusoma na kuandika.

“Katika programu yetu tumekuwa tunachukua wale wenye umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea, hivyo wale wenye miaka 15 hadi 17, serikali inaweza kuwatambua na kuwaingiza katika mfumo wa MEMKWA ili wakajifunze Zaidi kwa sababu sisi hapa tunawafundisha kusoma na kuandika tu, ” alieleza.

47

Mgeni rasmi Dk. Jackson Nyanda (Makamu Mwenyekiti Chama cha Biblia cha Tanzania)

Kabla ya kutoa vyeti kwa kundi la kwanza la wahitimu wa 89 wa Chibweda ‘Furaha’ Dk Jackson Nyanda aliwataka wahitimu hao kutumia maarifa hayo kujiendeleza kiuchumi na kushiriki katika uchumi wa taifa kwa ujumla.

38

Meneja Miradi na Uhusiano wa Makanisa Mch. Samwueli Mshana

Naye Meneja wa Miradi na utunishaji mfuko wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Samwueli Mshana ambaye pia alimwakilisha Katibu wa chama hicho, alisema lengo la chama chake ni kutafsiri Biblia kwa lugha za asili,  kukuza na kutunza lugha ya asili  lakini pia kusaidia jamii husika kuelewa Neno la Mungu.

× How can I help you?