Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.

Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni

“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”


Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.


Biblia kwa Wafungwa Kanda ya Kaskazini
Biblia kwa Wafungwa Kanda ya KaskaziniHabari Kamili.Chama cha Biblia cha Tanzania kimeendelea na huduma yake ya kugawa Biblia kwa baadhi ya magereza hapa nchini. Chama kimeendelea kutoa huduma hiyo kutokanana sadaka na michango ya wanachama wake, wadau mbali mbali...

MPANGO WA KISOMO CHA WATU WAZIMA – LITERACY FOR WOMEN IN AFRICA.
MPANGO WA KISOMO CHA WATU WAZIMA - LITERACY FOR WOMEN IN AFRICA.Habari Kamili.Chama cha Biblia cha Tanzania kinaendelea kutekeleza mpango wa Kisomo cha elimu ya watu wazima katika wilaya ya Kilosa na Gairo kwenye vijiji 15 vilivyochaguliwa wakati wa kuanzishwa kwa...

MKUTANO MKUU WA 37 WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA
MKUTANO MKUU WA 37 WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIAHabari Kamili. Mwenyekiti wa Bodi ya Chamacha Biblia Tanzania, Askofu Mkuu Mark Walwa Malekana amesema chama hicho kitajitahidi kuendelea kuchapisha na kusambaza neno la Mungu ili liweze kumfikia kwa kila mtu na...

Uenezaji wa Maandiko kwa 2022
Taasisi yetu kwa mwaka uliopita uliambatana na Baraka zake. Muungano wetu wa vyama vya Biblia ulimwenguni ulituweka katika mpango wa kuwafikia watu milioni moja ulimwenguni walio katika mazingira magumu au walengwa ambao hawana uwezo wa kununua Biblia. Tanzania...
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.

Donate Today or Get Involved