Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.

Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni

“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”


Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.


Yaliyojiri Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) 2023
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 2023 (AGM) wa Jumuiya ya Biblia Tanzania ulikuwa tukio muhimu sana, uliwaleta pamoja wanachama na wadau ili kujadili mustakabali wa shirika. Mkutano huo uliofanyika mjini Dodoma Mei 17, 2024 ulilenga mipango ya kimkakati na jitihada za...

Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) 2023
Mark your calendars for an important gathering of the Bible Society of Tanzania members on May 17, 2024, starting at 9 AM at ELCT-Dodoma Conference Hall.May 17, 2024The Bible Society of Tanzania invites all active members to attend the Annual General Meeting (AGM)...

SAUTI YA VIJANA WASAMARIA.
SAUTI YA VIJANA WASAMARIA.Program hii inatekelezwa na Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na dawati la vijana (Africa Youth Service -United Bible Society). Madhumuni ya programu ni kuwasaidia, kuandaa, na kuwajengea vijana wadogo miaka 9-24 uwezo wa kufanya...

MAHAFALI YA SITA YA LWA KIKAGURU
LITERACY FOR WOMEN IN AFRICA PROJECT.TAARIFA FUPI YA MPANGO & MAHAFALI YA SITA YA MPANGO HUUMahafali ya sita ya mpango huu yalifanyika tarehe 17.2.2024 katika Ukumbi wa Nazarethi, Gairo mjini ambapo wanakisomo 421 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu Kisomo cha watu...
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.

Donate Today or Get Involved