01 AUGUST 2019, CHARITY NEWSLETTERS /BARUA YA UPENDO YA KILA MWEZI

01 AUGUST 2019, CHARITY NEWSLETTERS /BARUA YA UPENDO YA KILA MWEZI

Newsletter Header

Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha hata atakapo kuwa mzee. [Mithali 22:6]

Wapendwa Taifa la Mungu na wakristo wa Tanzania, malezi ni uangalizi wa karibu wa wazazi kwa mtoto wao kiroho, kiafya, kiakili, kitabia ili tuwe na Taifa imara na watu wanaomcha Mungu. Mungu alipomuumba Adamu na Hawa akasema “zaeni mkaongezeke…………[Mwanzo 1:28.]”

Ni wajibu wa wazazi katika familia na kanisani kuwahimiza watoto kulisoma na kulipenda Neno la Mungu yaani Biblia. Katika [Rum. 8:28] tunasoma: “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema……” Hii ni pamoja na kazi ya kulea watoto; Mungu hufanya kazi hiyo pamoja na sisi.

Katika [Zab. 127:3] Biblia inasema “Tazama wana ndio urithi wa BWANA uzao wa tumbo ni thawabu.” Mungu hatupi watoto ili tuwahifadhi kwa matumizi yetu wenyewe. Yeye anatupa watoto ili tuwalee kwa utukufu wake. Watoto wetu ni wa Mungu. Mungu amelithibitisha agano lake pamoja nasi, Katika [Kumb. 28:4] anasema “Utabarikiwa uzao wa tumbo lako” Pia katika [Isaya. 8:18] inasema “Angalieni, mimi na watoto hawa niliyopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israel……” Kwa sababu hii Mungu anataka watoto wetu wajifunze Neno lake na kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Mungu anatazamia wazazi wawaelekeze watoto kwake, kwa njia ya Neno lake yaani Maandiko Matakatifu (Biblia).

Walinde watoto wako na vishawishi viovu.

Ujue nia ya shetani siku zote ni kutaka kuwaangamiza watoto, iwe kiroho au hata kimwili kwa kuwavuta katika mambo ya ulimwengu. Kuna mambo kadha wa kadha ambayo watoto wanakutana nayo maishani na haya yanaweza kusababisha au kuwaondoa kabisa wasimfuate Mungu sawasawa. Neno la Mungu linasema “Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia… na dunia inapita pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”. [1Yoh. 2:15-17].
Marafiki wabaya na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yameangamiza familia nyingi na kuwapoteza watoto na vijana katika kiwango cha kutisha [Mithali 13:20] Neno la Mungu linasema “… Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.” [Zab. 1:1] inasema: “Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani
pa wenye mizaha.”

Nawasihi na kuwaomba Wakristo wa Tanzania kusimama na Chama chenu cha Biblia kuwaridhisha watoto wetu Neno la uzima, hivyo wapatie watoto Biblia katika maisha yao. Simama na huduma ya Chama cha Biblia cha Tanzania kuwapatia watoto na vijana.

Neno la Mungu kama zawadi na baraka kutoka kwa Mungu maishani mwao.
Amani na Neema ya Mungu iwe juu yako.
Mtumishi wenu katika Kristo

Alfred Kimonge.
Katibu Mkuu

JITIHADA ZINAZOFANYWA NA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA ILI KUHAKIKISHA VIONGOZI WA MAKANISA MBALI MBALI NCHINI WANAFIKIWA NA MPANGO HUU MADHUBUTI.

1

Pichani toka kulia: Baba Askofu Mkuu Dr. Shoo wa Kanisa la KKKT, Msaidizi wa
Askofu wa Kanisa hilo, Dayosisi ya Kaskazini Mch. Saria, Baba Askofu Amos Muhagachi Balozi wa CBT na Mjumbe wa Bodi, na Eng. Ekaeli Manase mjumbe
wa Bodi ya CBT; wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea bahasha
10,000 kwa ajili ya kuchangia huduma ya Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT).

3 1

Pichani: Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania ndugu Alfred
Kimonge (kushoto) na Fr. Sosthenes wa Kanisa Katoliki Dodoma baada
kikao cha pamoja kilichomteua kuwa mmoja wa wawakilishi wa Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT).

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2

Pichani: Baba Askofu Amos Muhagachi (wa tano toka kulia waliokaa) Balozi wa
CBT na Mjumbe wa Bodi, akiwa na Mapadre wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Dodoma, baada ya Mkutano wa pamoja uliofanyika mjini Dodoma.

5 2

Pichani: Mtume na Nabii Josephat Mwingira (katikati ) wa Huduma ya Efatha
na mkewe (kushoto) wakipokea zawadi ya Biblia kutoka kwa Baba Askofu
Amos Muhagachi (kulia) Balozi wa Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT) na mjumbe wa Bodi, alipomtembelea na kufanya mazungumzo naye kuhusu mkakati wa CBT wa kuhamasisha Makanisa kuchangia upatikanaji wa
Maandiko Matakatifu kwa ajili ya watoto, vijana na wafungwa hapa Tanzania.

4

Pichani: Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT) ndugu Alfred Kimonge (kushoto), Fr. Chesco P. Msaga (katikati) wa Kanisa Katoliki
Dodoma na Baba Askofu Amos Muhagachi (kulia), Balozi wa CBT na mjumbe wa Bodi, wakiwa studio za Redio Mwangaza Dodoma akizungumza juu ya mkakati wa Chama wa kuhamasisha Makanisa na Wakristo wote kuchangia
upatikanaji wa Maandiko Matakatifu kwa ajili ya watoto, vijana na
wafungwa hapa Tanzania.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Unaweza usibadilishe dunia yote na kuifanya iwe ya kumpenda Mungu, lakini kwa sadaka yako ya upendo kwa Chama cha Biblia cha Tanzania ya Tsh 5000 tu! na kuendelelea unaweza kumbadilisha milele mtoto, kijana au hata mfungwa mmoja.
Tuma sadaka yako ya upendo kupitia namba ya M-PESA ya Chama: 890890 kisha tuma ujumbe wa kuchangia katika namba hizi: 0762998819, 0754383636 na 0754479789. 
Pia unaweza kuchangia kupitia akaunti za Benki za DTB na NBC zilizoonyeshwa hapa chini  Changia kupitia benki ya DTB: Namba ya Akaunti: 0901969001 SWIFT OR WIRING CODE DTKETZTZ na Changia kupitia benki ya NBC: Namba ya Akaunti: 029103000362 na Mungu akubariki sana.

Na Mungu akubariki sana

Askofu Amos Muhagachi

Mhariri

Mawasiliano yatumwe kwa: Katibu Mkuu Chama cha Biblia cha Tanzania, P.0. Box 175, Dodoma, Tanzania. Email: aekimonge@yahoo.com T: +255262324661 Fax: +255262324058.

BARUA YA UPENDO YA KILA MWEZI YA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA

BARUA YA UPENDO YA KILA MWEZI YA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA

BLOGO TransparentCHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA

N0: 01 July 2019, NEWSLETTERS /BARUA YA UPENDO YA KILA MWEZI

16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area, P.O Box 175, Dodoma Tanzania. || T: +255 (026)-2324661 F: +255 (026)-2324058 || Email: info@biblesociety-tanzania.org || Site: www.biblesociety-tanzania.org

KWA WANACHAMA  WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA NA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA.

Umoja wetu katika Kristo! 

“Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.  Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi”.  (Yohana 17:21-23).

Umoja wa Kanisa ndiyo ishara ya mwili wa Kristo katika Ulimwengu. Kanisa ni familia ya Mungu katika ulimwengu huu, ni jumuiya ya watu wa Mungu wamwaminio Yesu Kristo katika maisha yao wakimsifu na kumshangilia Mungu katika ushuhuda na kuwaleta wengine ili wamjue Mungu wa kweli katika maisha yao. Chama cha Biblia cha Tanzania kimeendelea kwa uaminifu wote kulihudumia kanisa la nchi yetu kwa umoja wake kwa kuwapatia Maandiko Matakatifu [Biblia] ili kuliwezesha kanisa kuwa na Biblia katika mifumo na tafsiri mbali mbali kwa ajili ya uinjilisti na utume wake.
Kwa unyenyekevu mkuu nawaalika Wakristo wa madhehebu yote katika nchi yetu kushiriki katika huduma hii.Nakuomba ukiombee na kukichangia Chama cha Biblia cha Tanzania ili kipate fedha kwa ajili ya kutafiti, kuchapisha na kusambaza neno la Mungu kwa watu wote. Ni maombi yangu kwamba asiwepo Mtanzania hata mmoja anayetamani kulisoma neno la Mungu akalikosa kwa sababu ya gharama kubwa.  Mwaka huu tuna lengo la kuwapatia watoto, vijana na wafungwa Biblia. Kwa ushirikiano wa kanisa la Mungu hapa nchini, tunaweza kuwafikia watoto, vijana na wafungwa ili kujenga Taifa la wacha Mungu. Kwa sadaka yako na matoleo yako ya upendo utakuwa baraka kwa kumpatia mtoto, kijana na mfungwa kule gerezani neno la uzima.
Nakutumia barua hii ya upendo kukualika na kukukaribisha ili ushiriki pamoja nasi kulijenga Taifa letu kiroho ili liwe  taifa lenye kumhofu na  kumcha Mungu. Ombea  Taifa letu ili watu wake walipende na kulisoma Neno la Mungu.
Ni kiu yangu kwamba kila mtoto, kijana na mfungwa awe na Biblia yake mkononi.
Neema na Amani ya Kristo iwe pamoja nawe.

Alfred E. Kimonge
Katibu Mkuu

HAMASA YA KUFUNGUA MATAWI MIKOANI

Tawi la UDOM

Hawa ni Wanachama wa Tawi la Kitivo cha Sayansi ya Jamii moja ya matawi matatu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.

Tunamshukuru Mungu kwa kuanza mwaka huu kwa baraka zake na uamsho mpya wa Makanisa na Wakristo kujiunga kwa wingi kuwa wanachama wa Chama cha Biblia cha Tanzania. Hadi sasa tumefanikiwa kufungua matawi kama ifuatavyo;
1. Dodoma – Chuo Kikuu cha Dodoma [UDOM ] i. Tawi la  Kitivo cha Elimu – Wanachama 120
ii. Tawi la Kitivo cha Biashara na Utawala – Wanachama 78
iii. Tawi la Kitivo cha Sayansi ya Elimu ya Jamii – Wanachama 110
2. EAGT Buhemba Tarime – Wanachama 210
4. Umoja wa makanisa – Kilimanjaro
5. Marangu-Kilimanjaro
6. Umoja wa makanisa – jiji la Mwanza
Na bado hamasa inaendelea katika maeneo mengine likiwamo jiji la Dar es Salaam na Tabora.

1 min

Viongozi wa Makanisa ya Moshi ambao ni waanzilishi wa Tawi la Chama katika Mkoa wa Kilimanjaro

Mwenyekiti wa Tawi la Chama cha Biblia Tarime akikabithi Mchango wake Askofu Muhagachi Balozi wa Chama cha Biblia cha Tanzania

Mwenyekiti wa Tawi la EAGT Buhemba Tarime akimkabidhi mchango wake Askofu Muhagachi Balozi wa Chama cha Biblia cha Tanzania.

 

 

 

 

 

 

 

 

Tunakuomba ushiriki katika huduma hii kwa maombi yako,unaweza kuchangia kila mwezi Tsh 2000,______ Tsh 5000,______Tsh 10,000,_______au kuchangia kwa mwaka Tsh 25,000, ____Tsh  50,000,_____Tsh 100,000 au zaidi.  Kwa sadaka yako ya upendo unaweza kumfanya/kumgusa mtoto, kijana na mfungwa kumjua na kumfuata Kristo.
Nakualika kushiriki pamoja na Wakristo wengine waaminifu kwa kuchangia na kutuma mchango wako kwa akaunti ya M-PESA ya Chama cha Biblia cha Tanzania namba 890890 kisha tuma ujumbe wa kuchangia katika namba hizi: 0762998819,  0754383636 na 0754479789.

Pia unaweza kuchangia kupitia akaunti za Benki za DTB na NBC zilizoonyeshwa hapa chini.
Kwa DTB Akaunti Namba: 0901969001; SWIFT OR WIRING CODE DTKETZTZ
Kwa NBC Akaunti Namba: 029103000362

DTB

Akaunti Namba: 0901969001; SWIFT OR WIRING CODE DTKETZTZ

nbc

Akaunti Namba: 029103000362

 

 

 

 

 

 

Mungu na akubariki.
Askofu Amos Muhagachi
Mhariri.

 Mawasiliano yatumwe kwa: Katibu Mkuu Chama cha Biblia cha Tanzania, P.0. Box 175, Dodoma, Tanzania. Email: aekimonge@yahoo.com T: +255262324661 Mob: +255754383636
CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA CHAWAFIKIA WATOTO YATIMA NA WALIOKO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU WILAYANI MBARALI.

CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA CHAWAFIKIA WATOTO YATIMA NA WALIOKO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU WILAYANI MBARALI.

Na. Rose Mrema

Chama cha Biblia cha Tanzania ni taasisi ya Kikristo inayojishughulisha na kutafsiri, kuchapisha na kueneza Maandiko Matakatifu yaani Biblia kwa niaba ya makanisa yote ya Tanzania. Pia Chama cha Biblia kinaendesha program mbalimbali kwenye jamii lengo likiwa ni kuihudumia jamii kiroo na kimwili (Holistic Ministry) Kupitia Program ya “Je yuko wapi Msamaria mwema Leo? inayojishughulisha na mapambano dhidi ya UKIMWI ikilenga kupunguza unyanyapa hasa makanisani, kuhamasisha watu kupima kwa hiari, watu kubadilisha tabia kwa kutumia neno la Mungu na kuleta muungamaniko wa makanisa/misikiti katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI. Chama cha Biblia kupitia program hii kimeweza kuwafikia watoto walioachwa yatima baada ya wazazi wao kufariki kwa ugonjwa wa UKIMWI, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, wenye maambukizi na watoto wenye ulemavu.

DSC08065 min

Mtumishi wa Chama cha Biblia cha Tanzania (Mrs. Rose Mrema) akifundisha washiriki wa mafunzo ya watoto kutoka Ibohora.

Mpango huu wa watoto unatekelezwa katika kata ya Ubaruku,Wilaya ya Mbarali kwa kushirikiana na taasis za kidini, wadau wengine wanaohudumia watoto (KIWAUTA na SHIDEPHA) pamoja na viongozi wa serekali, na jamii kwa ujumla. Lengo ni kuwawezesha watoto hao kuishi maisha yaliyo kamilika kama walivyo watoto wengine, kuhamasishana kuikumbusha jamii wajibu wake juu ya watoto hao na  kumjengea mtoto uwezo wa maisha kwa ujumla.

DSC05993 min

Waalimu wa Sunday school, madrasa, shule za secondary na primari waliopata mafunzo ya watoto toka kata ya Ubaruku wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo.

22 min

Watoto wakiwa kwenye majadiliano ya makundi wakati wa mafunzo.

Mafanikio.

Baadhi ya mafanikio ya program.

  1. Mpango huu umepokelewa vizuri na Viongozi wa Serekali, dini, jamii pamoja na wadau wengine wanaojishughulisha na kuwahudumia watoto yatima na walioko kwenye mazingira magumu.
  • Tumeweza kukutana na viongozi wa serekali, dini na wadau wengine
  • Kufanya mafunzo na waalimu wa sunday school,madrasa, Waalimu wa malezi kutoka shule za msingi, na Sekondari zilizopo kata ya Ubaruku,na wahudumu wa watoto majumbani kutoka shirika la KIWAUTA .
  • Kuwafikia watoto zaidi ya 500 yatima na walioko kwenye mazingira magumu.
  • Kugawa vifaa vya kufundishia kwa washiriki waliopata mafunzo (Vitabu,Mwongozo na flip chart.)
  1. Baadhi ya washiriki waliopata mafunzo waliweza kuendeleza mafunzo waliyopata kwa kuwafundisha wazazi wenzao,watoto makanisani, na mashuleni kwenye vipindi vya dini.
    3 min

    Wazazi wa watoto wakiwa katika majadiliano.

  2. Vitendo vya unyanyasaji wa watoto majumbani vimepungua kwa kiasi kikubwa,,upendo umeongezeka ndani ya jamii, na kwa watoto wenyewe kwa wenyewe.
  3. Baadhi ya watoto waliopata mafunzo wamebadilika tabia ,wamekuwa wasafi,anasaidia kazi za nyumbani,wameacha udokozi,wizi,kutukana na kupigana.
  4. Washiriki wametambua wajibu wa kuwahudumia watoto hao ni jukumu la jamii nzima, wengi wao wameanzisha vikundi kwa lengo la kuwahudumia watoto na kutoa elimu kwa jamii.

Changamoto.

  • Washiriki wengi waliopata mafunzo hawajui kusoma na kuandika.

14 min

Mambo tuliyojifunza

  • Vijijini wapo watoto wengi ambao wameachwa na kusahaulika kutokana na hali duni ya maisha.
  • Miradi mingi ya kuwasaidia watoto hawa ipo mijini.
  • Wazazi/walezi wa watoto wanaishi kwenye mazingira magumu na hawana mtu anayewasaidia kuwalea watoto.Jambo hili linawafanya watoto kukosa mahitaji yao muhimu ya kila siku.
  • Ukosefu wa vitendea kazi kwa watoto walemavu.mf Baiskeli ili waweze kupata haki yao ya kwenda shule.
  • Elimu bado inahitajika kwenye jamii jinsi ya kuwahudumia watoto hawa hasa walemavu wengi wao wameachwa majumbani pasipo kupata elimu,matibabu na huduma nyingine muhimu.

 

 

Wafungwa na Mahabusu wa Gereza la Kiomboi wapata Biblia.

Wafungwa na Mahabusu wa Gereza la Kiomboi wapata Biblia.

Na: Canon Mwanamtwa:

Hawa ni Askari wa Gereza la Kiomboi wakipokea Biblia kwa niaba ya Wafungwa na Mahabusu wa Gereza la Kiomboi

Askari wa Gereza la Kiomboi wakipokea Biblia kwa niaba ya Wafungwa na Mahabusu wa Gereza la Kiomboi , Mkoa wa Singida wilaya ya Iramba.

Hawa ni Askari wa Gereza la Kiomboi wakipokea Biblia kwa niaba ya Wafungwa na Mahabusu wa Gereza la Kiomboi lililopa katika Mkoa wa Singida wilaya ya Iramba. Baada ya kupokea nilipata nafasi ya kuongea na Wafungwa na Mahabusu pamoja na Askari kutoa maelezo juu ya Chama Cha Biblia Tanzania kutoa Biblia hizo kwao, Wafungwa wawili walishukuru kwa niaba ya wenzao na kusema

” Tunamshukuru kwa Chama Cha Biblia kutukumbuka na kututhamini kwa kutuletea Biblia hizi na kwamba tutasoma Neno la Mungu na litatusaidia katika maisha yetu hata katika mazingira haya, asante sana”

MKUTANO WA VIONGOZI WA MAKANISA YA KANDA YA KASKAZINI NA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA ULIOFANYIKA WILAYANI MOSHI MKOANI KILIMANJARO. (TAREHE 04/06/2019).

MKUTANO WA VIONGOZI WA MAKANISA YA KANDA YA KASKAZINI NA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA ULIOFANYIKA WILAYANI MOSHI MKOANI KILIMANJARO. (TAREHE 04/06/2019).

Na: Felix Rwebandiza Jones.
Kitengo cha Tehama.

Mwenyekiti wa Kikao ambaye pia ni Baba Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kirutheri la Kiinjiri Jimbo la Moshi

Mwenyekiti wa Kikao ambaye pia ni Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania – Jimbo la Moshi, akifungua kikao

Wajumbe.
Waliohudhuria walikuwa 36 kama inavyooneshwa hapa chini.
1. Wakurugenzi Chama cha Biblia cha Tanzania (Rev. Askofu Amosi Muhagachi ambaye ni Balozi wa Chama cha Biblia cha Tanzania na Eng. Ekael Manase ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Chama cha Biblia cha Tanzania).
2. Maafisa wa Chama cha Biblia cha Tanzania (Rev. Ipyana Mwangota amabaye ni Meneja Tafrisi na Felix Jones ambaye ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA).
3. Wachungaji na Mapadre.
4. Mwangalizi wa Jimbo Katoliki la Moshi.
5. Wenyeviti wasaidizi wa Maaskofu.
Agenda kuu ya Kikao ilikuwa ni:
• Uhamasishaji wa Chama cha Biblia cha Tanzania,
• Uanachama na faida zake na
• Tafsiri ya Biblia kwa ujumla wake.
Baada ya ufunguzi wa kikao mwenyekiti aliruhusu watumishi kijitambulisha
Mmoja wa wajumbe akijiambulisha

Mmoja wa wajumbe akijitambulisha wakati wa Mkutano huo

na baada ya hapo alimkaribisha Rev. Askofu Amosi Muhagachi kueleza ujumbe wake kutoka Chama cha Biblia Cha Tanzania. Askofu Muhagachi alianza kwa kuelezea historia yake, kabla ya kuanza kufanya kazi na Chama cha Biblia cha Tanzania, ambapo akiwa mwanafunzi na mwanachama aliweza kuwa muhamasishaji katika shule ya Sekondary ya Mirambo Tabora na aliweza kuwahamasisha wanafunzi wenzake wachangie Chama cha Biblia cha Tanzania ili kipate fedha za kuchapisha Biblia nyingi ili wanafunzi wenzao wapate Neno la Mungu kama wao. Alifanya hivyo katika kipindi chote cha masomo yake “nilikuwa nikihamasisha wanafunzi wenzangu tuchangie Chama cha Biblia cha Tanzania, ili Chama cha Biblia cha Tanzania kiweze kuchapisha Biblia nyingi ili sisi na vijana wenzetu tupate Biblia” alisema Rev. Askofu Amosi Muhagachi.
Rev. Askofu Muhagachi akizungumza wakati wa Kikao

Rev. Askofu Muhagachi akizungumza wakati wa Kikao

Baba Askofu Amosi Muhagachi baada kuhitimu masomo yake alipata barua ya kuitwa kwenye usaili na baada ya hapo aliweza kuajiriwa kuwa Afisa Uhusiano na Makanisa na Uhamasishaji wa Chama cha Biblia cha Tanzania ambapo alikaa kwa miaka saba kabla ya kuwa Askofu wa kanisa la Mennonite Tanzania na baadaye kwenda masomoni nchini Marekani, ambako bado anaendelea na masomo yake.
Baba Askofu Amosi Muhagachi alieleza mikakati ya Chama cha Biblia cha Tanzania ambayo ni;
i. Kuyaomba makanisa kutenga juma moja kuombea Chama cha Biblia cha Tanzania na watendaji wake.
ii. Kuomba watu kujitolea kuchangia Chama cha Biblia cha Tanzania ili kipate pesa za kutosha za kutafiti, kuchapisha na kusambaza Neno la Mungu kwa lugha mbali mbali hapa Tanzania.
iii. Kuomba viongozi wa makanisa wakubali kuchangia mpango mkakati wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa kupeleka Neno la Mungu kwa wafungwa, vijana na watoto.
iv. Kuwaomba viongozi wa Makanisa kuendesha mpango wa kuwepo mashindano ya kukariri mistari ya Biblia kwa vijana na watoto katika Shule, Makanisa na Vyuoni.
v. Kuhamasisha utumiaji wa Biblia (Hard copy) makanisani na viongozi wahakikishe zimeandikwa au zina nembo ya Chama cha Biblia cha Tanzania kama njia ya kuepukana na watu wanaogushi/kuchakachua Neno la Mungu.
Baada ya kumaliza hotuba yake alimuomba Mwenyekiti wa kikao amkaribishe Eng. Ekael Manase alielezea juu ya Uanachama, wa Chama cha Biblia cha Tanzania.
Eng. Ekael Manase alianza kwa kumshukuru sana Baba Askofu Amosi Muhagachi kwa jinsi alivyoeleza vizuri kuhusu kuwahamasisha watu kukichangia Chama cha Biblia cha Tanzania.
Pia aliendelea kwa kuwaomba sana na kuwasihi watumishi wa Mungu wote waliohudhulia kuwa wanatakiwa kuwahimiza waumini wao na kufufua ari ya kusoma Neno la Mungu ikiwa ni pamoja na kuanzisha mashindano ya kusoma na kukariri mistari ya Biblia kwa vijana na watoto, kwa lengo la kuwaandaa ili waweze kukua wakilishika Neno la Mungu. Lakini pia aliwaomba sana wachungaji na mapadre kuwahimiza sana waumini wao kutumia Biblia (hard copy) na kuacha kutumia Biblia zilizowekwa kwenye simu za mikononi (soft copy). Kwani wanaweza wakasoma Neno lililopotoshwa na watu wenye nia ovu kwa Ukristo.
Eng. Ekael Manase aliendelea kueleza kuwa hayo yote hayawezi kufanikiwa kama vijana wetu na watoto wetu hawatakuwa na Biblia zao; kwa hivyo basi ili jambo hili liweze kufanikiwa tunahitaji tuwe na Biblia za kutosha na kwa bei wanayoimudu. Biblia za bei nafuu zinaweza kupatikana tu; endapo kama sisi sote tutajitoa kukichangia Chama cha Biblia cha Tanzania. “Maana kama Biblia zingeuzwa kwa bei yake halisi ingekuwa ghali sana, lakini michango inayotolewa kwa CBT inafanya Biblia iweze kuuzwa kwa bei rahisi” alisema Eng. Ekael Manase.
Pamoja na melezo mazuri ya kuwahamisha watumishi wa Mungu kuhusu kuchangia Biblia na kuwa himiza watoto na vijana kusoma Biblia, pia Eng. Ekael Manase aliwaeleza wajumbe waliohudhuria aina za uanachama; kuwa kuna uanachama wa aina tatu;
i. Uanachama wa maisha
• Uanachama wa Maisha Mme na Mke shilingi 15,000= na ahadi isiyopungua shilingi 15,000=kwa mwaka.
• Uanachama wa Maisha mtu mmoja shilingi 10,000= na ahadi isiyopungua shilingi 10,000= kwa mwaka.
ii. Uanachama wa Bidii
• Uanachama wa kawaida (bidii ) shilingi 5,000=kwa mwaka.
• Uanachama wa kawaida kwa Wanafunzi wa Sekondari na Vyuo shilingi 2,000= au zaidi kwa mwaka.
• Uanachama wa kawaida wa kushirikishwa kwa watoto na wanafunzi wa shule za Msingi shilingi 1,000= au zaidi kwa mwaka.
• Mwanachama wa Biblia Moja kwa Mwezi (Bible a Month Club) 5,000=, 10,000=, 15,000=, 20,000= au zaidi kwa mwezi.
iii. Uanachama wa Mashirika
• Uanachama wa Mashirika shilingi 50,000= na mchango usiopungua shilingi 50,000= kwa mwaka.
Mwisho Eng. Ekael Manase alimalizia kwa kusema kuwa hii itakuwa ni njia nzuri Zaidi ya kuwakusanya vijana na kupenda kusoma Neno la Mungu, na pia itasaidia sana kupanda mbegu ya Neno la Mungu ndani yao na kuwa na Taifa lenye kumcha Mungu na lenye maadili mema.
Kwa upande wake Meneja wa Tafsiri wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mch. Ipyana Mwangota alipopewa nafasi ya kuzungumza mbele ya wajumbe wote; alielezea kazi za Tafsiri anazozifanya ndani ya Chama cha Biblia cha Tanzania akiwa kama Meneja wa Tafsiri. Alifafanua kuwa wanafanya kazi ya kutafsiri Biblia kwa lugha mbali mbali ikiwa njia mojawapo ya kulisaida Kanisa kufanya kazi ya umisheni.
Mch. Ipyana Mwangota akitoa ukizungumzia juu ya Tafsiri

Meneja tafsiri, Mch. Ipyana Mwangota akitoa ukizungumzia juu ya Tafsiri

Alifafanua Zaidi juu ya kazi ya Tafsiri na kutaja Tafsiri zinazofanyika upande wa kanda ya Kasikazini ambazo ni Tafsiri ya Kivunjo, Kidatooga, Kimashame na Kimochi. Alinukuriwa akisema Pia Chama cha Biblia cha Tanzania kinakamilisha uchapaji wa Biblia ya Kisukuma. Kazi hii imepelekwa kule Korea kwa ajili ya uchapishaji. Ni tarajio letu kuwa kazi ya uchapishaji na uzinduzi itakamilika mwishoni mwa mwaka huu 2019. “Chama cha Biblia cha Tanzania kimepokea maombi ya Tafsiri na sasa kinaendelea kufanya pia Tafsiri ya lugha mbalimbali kubwa kama Igikuria, Kiha, Kinyiramba, Kirimi, Chikaguru na kihehe. Aidha CBT tumepokea maombi ya Kanisa katika maeneo ya Ufipa, Unyamwezi, Unyiha, na Upare ili kiweze kusaidia kutafsiri Biblia kwa Lugha ya Kifipa, Kinyamwezi, Kinyiha na Kipare na kukubali; na sas Chama cha Biblia cha Tanzania kipo katika mchakato wa kutafuta fedha ili kuianza kazi hii kwa ushirikiano na Makanisa mwaka 2020 Januari.
Baadhi ya Wajumbe wakisikiliza kwa Makini

Baadhi ya Wajumbe wakisikiliza kwa Makini.

Pia alieleza kuwa zipo Biblia ambazo zimetafsiriwa, kuchapishwa na zinatumika katika makabila lengwa kama vile Biblia ya Kinyakyusa (Mkoa wa Mbeya), Biblia ya Luhaya (Mkoa wa Kagera), Biblia ya Cigogo (Mkoa wa Dodoma), Biblia ya Kimasai (Mkoa wa Arusha), na Biblia ya Kihiraqw (Mkoa wa Manyara).
Pia alieleza kuwa Chama cha Biblia kimefanya tafsiri za Agano Jipya na sehemu za Biblia nyingi tu na zinatumika maeneo tofauti tofauti ili kukidhi haja ya watumiaji wa lugha husika kuendana na sera ya Vyama vya Biblia Duniani.
Kuhusu mchakato wa kazi ya tafsiri; Meneja Tafsiri alieleza kuwa ofisi yake, hutumia vifaa vya kisasa. Kwa lengo la kufanikisha kazi hii kubwa. Alionyesha Program ya Paratext kwa wajumbe wa mkutano kama mfano wa vifaa hivyo ili waone jinsi kazi hii inavyotendeka. Wajumbe walipongeza kazi hii kubwa na waliahidi kuiombea.
Pia alieleza kuwa Chama kwa sasa kinatia mkazo uwepo wa Biblia za Watoto, na hivyo kimekuwa kikiandaa Biblia za watoto ili kuhakikisha Makanisa hayakosi Biblia kwa watoto wadogo, wa kati na wale wanaoelekea umri wa utu uzima.
Mwisho alitoa wito kwa viongozi wa Makanisa kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Chama cha Biblia cha Tanzania katika kuhakikisha Maandiko Matakatifu yanapatikana kikamilifu kwa kuchangia na kuombea juhudi hizi.