HATIMAYE WAVUNJO WAPATA BIBLIA KAMILI

HATIMAYE WAVUNJO WAPATA BIBLIA KAMILI

Baada ya miaka mingi, Wachaga wa Wavunjo, wapata Biblia katika lugha yao ya Kivunjo. Katika Sherehe  na Ibaada ya uzinduzi wa Biblia kwa Lugha ya Kivunjo zimefanyika katika Usharika wa Samanga, Jimbo la Kilimanjaro Mashariki la Kanisa la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini, Ibaada hii imefanyika  September 27, 2020.

Kanisa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini usharika wa Samanga ambako uzinduzi huo ulifanyikia.

Sherehe hizo ziliudhuliwa na Maaskofu wa Makanisa Mbalimbali, Viongozi wa chama cha Biblia cha Tanzania, (akiwepo: Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Chama cha Biblia cha Tanzania, Baba Askofu Mark W. Malekana wa Kanisa la SDA Tanzania), viongozi wa serikali na vyama vya siasa.

IMG 8356
Viongozi wa Vyama vya Siasa na Serikali wakitambulishwa wakati wa hafla hiyo.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Mhashamu Baba Askofu Fredrick Onael Shoo ndiye aliyekuwa mgeni rasmi na ndiye aliyeongoza uzinduzi huu. Pia aliambatana na Maaskofu wengine wa Kanisa lake na Mhashamu Baba Askofu Amosi Muhagachi wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Jimbo la Kaskazini wakati wa Ibada hiyo.

Askofu Muhagachi akijitambulisha
Mhashamu Baba Askofu Fredrick Onael Shoo akimtambulisha mgeni wake Mhashamu Baba Askofu Amosi Muhagachi wa Kanisa la Mennonite Tanzania Jimbo la Kaskazini wakati wa Ibada hiyo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania akinazungumza kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha Biblia cha Tanzania ambao wanawakilisha Madhehebu na Makanisa yote yaliyopo hapa nchini. Alisema mengi akiusio Chama chake na Kazi mbali za Chama na hasa tafsiri mbali zilizofanyika na zinazofanyika kwa kushirikiana na Makanisa na wadau wengine.

Dr. Alfred Kimonge Kivunjo
Katibu Mkuu Dr. Alfred E. Kimonge wa Chama cha Biblia cha Tanzania wakati wa ibada ya Uzinduzi wa Biblia ya Kivunjo.

Kwanza alisema Chama cha Biblia cha Tanzania ni mwanachama kamili katika Muungano wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni (United Bible Societies-UBS). Kusudi la Muungano huu Ulimwenguni kote ni kutafsiri, kuchapisha na kueneza Neno la Mungu (Biblia) kwa Lugha ambayo mtu anayoweza kuilewa vizuri. Chama cha Biblia ni cha Makanisa yote na Kinajitegemea, lakini kinaheshimu mapatano na malengo ya Muungano wa vyama vya Biblia ulimwenguni. Vile vile kinazingatia malengo ya Kanisa katika  Uinjilishaji.Ni vyema Kanisa lijihusishe katika kukibeba, kukiombea, kuchangia Chama Cha Biblia  njia ya sadaka maalumu na vile vile kuhimiza uenezaji na usomaji wa Maandiko Matakatifu (Biblia).

Umoja wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni unatambua na kuheshimu tofauti zilizopo baina ya makundi ya watu. Hivyo pale watu wanapofikishiwa Neno la Mungu na ikadhihirika kuna udhaifu wa kulisoma, basi hatua zinachukuliwa ili kulihimiza Kanisa liwawekee watu misingi ya kujua kuisoma na kuiandika lugha yao. Matokeo ni kwamba watu hujua Lugha yao na mwisho huweza  kulisoma Neno la Mungu. Hivyo kwa kushirikiana na Kanisa, tafsiri mpya za Biblia zinaambatana na juhudi za kuwafundisha watu wazima kwa wadogo, kuisoma Biblia yao. Juhudi hii imefanyika kwa Wasukuma, Wamaasai, Wanyakyusa, Wairaqw, Wagogo  na Wachagga. Mikakati ipo kwa Wakaguru, Wahehe, Wadatooga na penginepo ambapo juhudi ya kutafsiri Biblia inaendelea.

Kwa makundi haya Chama cha Biblia kinachukua juhudi zote kuandaa na kuwafikishia watu Biblia iliyoandaliwa katika mifumo tofauti. Kwa mfano, Neno lililochapishwa –(“Printed Format”), Neno lililowekwa katika kanda-naswa – (Magnetic au digital cassette), Neno lililoingizwa kwa njia simulizi – (Audio-Aural-Visual Scriptures), Neno katika mifumo maalumu kama vile Braille kwa Wasioona, New Reader Scriptures kwa wasomaji wa awali, Neno katika mfumo wa Maandishi Makubwa kwa ajili ya Wazee na wengine wenye udhaifu wa macho, Neno katika matoleo ya watoto, Neno kwa njia ya Scripture Literacy Promotion, Neno katika Digital Bible Library.

Mwisho Katibu Mkuu alisema “Kazi bado ni kubwa, Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na Kanisa, kinayo mikakati ya kuwafikishia Neno la Mungu makundi/makabila yaliyobaki. Rai yetu kwa Kanisa tunaomba Biblia hii itumike katika ibada ili kazi hii iliyofanyika kwa miaka mingi na kwa gharama kubwa isiwe ya bure.

Leo tumekamilisha jitihada katika lugha ya Kivunjo kwa kuwakamilishia Biblia: Mungu anena na Wavunjo katika ukamilifu wa Biblia ya Kivunjo. Ni matumaini yetu kwamba Injili ya Wokovu katika Yesu Kristo itawafikia katika lugha yao ya moyoni na kusema sasa nimetambua Mungu anasema nami kwa lugha yangu.

Kwa njia ya tafsiri hii ya Biblia, Wavunjo nao watamsikia Bwana Yesu kwa ukaribu wa moyoni ili wapate fursa ya kushiriki katika halaiki ya mwisho”  “ Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha (Kivunjo)…” (Ufu. 7: 9-12).

Ili kufanya uzinduzi wa Biblia ni lazima Translation Consultant (TC) amthibitishie Katibu Mkuu kuwa kazi aliyokabidhiwa ni bora na inafaa kwa kuzinduliwa kwa ajili ya kuwapelekea watu na Kanisa. Akisoma risala kwa niaba ya Professor Aloo Osotsi Mojola, Askofu Julius Nyange alielezea changamoto na mafanikio waliyokutana tangu walipoanza tafsiri hadi Biblia hii ya kivunjo inapozinduliwa.

“Kutafsiri Biblia nzima katika msemo wa Kivunjo kulianzishwa mwaka wa 1991 na Chama cha Biblia cha Tanzania chini ya uongozi wa Marehemu Mchungaji Albert Mongi, pamoja na mimi nilikuwa mshauri wa Tafsiri, kutoka United Bible Societies. Agano Jipya la kwanza katika msemo wa Kivunjo lilichapishwa na kutolewa, pale Marangu mnamo Novemba 6, 1999. Na Siku ya leo, Septemba 27, 2020,  Biblia Takatifu katika lahaja ya Kivunjo inazinduliwa na kuwekwa wakfu. Jina la Bwana libarikiwe na kupewa sifa”.

Askofu Nyange akikabithi Biblia kwa Katibu Mkuu
Askofu Julius Nyange, ambaye alimwakilisha Professor Aloo Osotsi Mojola akimkabidhi Katibu Mkuu wa Chama Cha Biblia cha Tanzania Biblia ya Kivunjo.

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Baba Askofu Mark W. Malekana, alipokuwa akizungumza na Kanisa la Mungu, yeye  alifafanua umuhimu wa kulisoma Neno la Mungu (Biblia) na kuweka mipango endelevu ya kulisisha kwa vizazi, vijavyo.

Askofu Malekana
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Baba Askofu Mark W. Malekana akitoa hotuba yake fupi wakati wa uzinduzi wa Biblia ya Kivunjo.

Na mwisho alitoa shukurani kwa Mungu na Kanisa kwa kukiwezesha Chama cha Biblia cha Tanzania, Alisema kuwa Kanisa limejitoa sadaka ili kazi ya chama cha Biblia kiweze kufanikisha kazi hii kubwa kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Kisha Baba Askofu Fredrick Onael Shoo Mkuu wa KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini baada ya kukabithiwa Biblia hiyo na Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia Alichukua jukumu lake la Kuiweka WAKFU Biblia hii na alisema:

IMG 8386
Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania akimkabidhi Biblia ya Kivunjo Askofu Mkuu wa KKKT and Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Mhashamu Baba Askofu Fredrick Onael Shoo.

Baada ya kukabidhiwa Biblia hiyo na kuipokea kwa niaba ya Kanisa la Wavunjo, Baba Askofu aliiweka wakfu kwa maneno yafuatayo:-

“Ninaiweka wakfu tafsiri hii ya Biblia kwa lugha ya Kivunjo katika Jina la Mungu Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. AMEN.”

Kuweka wakfu Kivunjo Bible
Mhashamu Baba Askofu Fredrick Onael Shoo Mkuu wa KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini akiiweka wakfu Biblia ya Kivunjo.

Ni dhahiri kwamba tunachokiweka wakfu leo ni kitabu na makaratasi yake. Kile kilichoandikwa humo tayari ni wakfu. Maandiko yanazidi kusema katika Injili ya Yohana 6: 63, “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima”.

Biblia ina uzima: ina utakaso. Ameni.

Baada ya uzinduzi kufanyika. Waenezaji walianza kufanya kazi yao ya uzinduzi na kazi hii ilienda vizuri sana. Karibu Biblia 1,000 zilinunuliwa siku ile. Unaweza kuangalia katika picha Mbalimbali hapo chini.

20200927 142545
Wavunjo wakiangalia Biblia yao kwa Bashasha baada ya kuinunua kwa Bei ya punguzo ya siku hiyo ya 15,000/=.

Meneja wa Tafsiri wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Rev. Ipyana Mwangota, aliwahoji baadhi ya watu mbalimbali waliokuwa wakinunua na kusoma Biblia; Watu hawa walikuwa wenye furaha na wakimshukuru Mungu sana kwa kupata Biblia yao kwa Lugha ya Kivunjo.

DSC02098
DSC02165
20200927 123109
20200927 140601

Tunapenda kukushukuru na kukutakia Baraka za Bwana, unapoendelea kukiombea na kukichangia Chama cha Biblia cha Tanzania ili kiweze kufikisha Neno la Mungu kwa Watu na makundi mbalimbali hapa Tanzania.

Ameni.

MAHAFALI YA WAHITIMU WA CHIBWEDA MAGUBIKE TAREHE 19/09/2020.

MAHAFALI YA WAHITIMU WA CHIBWEDA MAGUBIKE TAREHE 19/09/2020.

MAHAFALI YA WAHITIMU WA CHIBWEDA MAGUBIKE TAREHE 19/09/2020.

LWA Kikagulu wahitimu 248 waliomaliza na kufaulu mafunzo ya kusoma na kuandika katika awamu ya pili ya mahafali ambayo yalikuwa yafanyike tarehe 21/03/2020 lakini yakahirishwa kutokana na covid -19. Sasa yalifanyika tarehe 19/09/2020 katika Kanisa la Anglikana huko Magubike.

 

Wahitimu mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa katika picha ya pamoja
Mratibu wa mpango huu Mwl. Frank Makalla wa kwanza kushoto kwa waliokaa mbele akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu waliosimama nyuma wenye vyeti pamoja na mgeni rasmi Canon Elias Lucas Chamwenye wa tatu kutoka kushoto na wageni wengine walioalikwa kwenye mahafari hayo.

Awamu ya kwanza waliohitimu ni jumla ya watu 69 ambapo wanawake ni 56 na wanaume ni 13 kutoka vijiji 5 Gairo ambavyo ni Gairo, Mogohigwa, Tabuhoteli, Mtumbatu pamoja na Kibedya.

Awamu ya pili waliohitimu jumla ni 248 ambapo wanawake ni 214 na wanaume ni 34; kutoka kwenye vijiji 13 ambavyo ni Magubike, Nguyami, Berega, Chakwale, Ibindo, Mwandi, Mamboya, Mbili, Dumbaalume, Maguha, Magela, Kiegeya Pamoja Na Mabula.

Waliojiandikisha ni 423 kati yao waliohitimu ni 317 na ambao hawajahitimu ni 106 kutokana na changamoto mbalimbali kama vile kuhama, shughuli za mashamba ,na matatizo mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza jana baada ya kukabidhi vyeti  kwa awamu ya pili ya wahitimu hao, Mratibu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mwl.Frank Makalla alisema wahitimu hao ni wa awamu ya pili ya programu iliyolenga kuwajengea uwezo wa kusoma na kuandika watu wazima wanaoanzia miaka 14 na kuendelea.

Magubike Mzee Makalla
Mh Makalla akiwa anazungumza na wahitimu katika mahafali

Mratibu wa Chama cha Biblia Tanzania, Mwl.Frank Makalla akizungumza na wahitimu wa awamu ya pili katika mahafali hayo huku akiwasisitiza wasiache kufanya yale waliyofundishwa pia wahakikishe kuwa kupitia wao watu wengi zaidi walijue neno la Mungu.

Mratibu wa mpango wa elimu kwa watu wazima kutoka Chama Cha Biblia Cha Tanzania akiongea jambo katika mahafali ya awamu ya pili iliyofanyika Magubike. Alisema kuwa mahafali hayo ni mwendelezo wa mahafali  ya awamu ya kwanza ya program hiyo iliyoanza mwaka 2017, ambapo watu 120 walijiandikisha huku watu 97 walihitimu mafunzo hayo ambayo pamoja na kuwafundisha kwa kutumia lugha ya chikagulu kufundishia, mafunzo hayo yanafanywa pia kuweza kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili.

Programu hiyo inafadhiliwa na Chama cha Biblia cha Finland, Chama cha Biblia cha Tanzania pamoja na Summer Institute of linguistics (SIL) ambao wanatoa utaalamu wa waalimu pamoja na mwongozo wa kuandaa vitabu vya kufundishia.  Programu hiyo inalenga zaidi kuwainua wanawake kujifunza kusoma na kuandika ingawa na wanaume wanakaribishwa kushiriki.

Wahitimu wakiwa wanaimba nyimbo katika mahafali yao
Wahitimu wa CHIBWEDA wakiwa katika picha ya pamoja katika mahafali yao iliyofanyika mnamo tarehe 19/09/2020 huko Magubike siku ya Jumamosi.

Mratibu wa mpango huu Mwl. Makalla alisema kati ya watu wazima 248 waliohitimu, wanawake ni 214 na wanaume ni 34 katika awamu hii ya pili ambao walishindwa kufanya hivyo mwezi wa Machi 2020 kutokana na ugonjwa wa corona ulioikumba Dunia nzima wakati huo. Akizungumzia sababu ya baadhi ya watu waliojiandikisha kushindwa kumaliza, Mwl. Makallla alisema kwa wale walioacha masomo, hao wamepewe nafasi ya kujiunga na darasa la awamu ya tatu ambalo limeanza tayari wakiendelea na mafunzo. Aidha, Mwl. Makalla aliomba ushirikiano na serikali katika mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwafanya wananchi waliokosa fursa ya kusoma na kuandika kujiunga na kuendelea kupata elimu hiyo.

“Katika programu yetu hii tumekuwa tukichukua wale wenye umri wa kuanzia miaka 14 na kuendelea, hivyo wale wenye miaka 14 hadi 17, serikali inaweza kuwatambua na kuwaingiza katika mfumo wa MEMKWA katika shule za msingi kama ambavyo Serikali inaelekeza kupitia wizara ya Elimu ili wakajifunze zaidi kwa sababu sisi hapa tunawafundisha kusoma na kuandika tu huko watajifunza masomo mengine pia kama Hesabu, Sayansi, Jiografia Historia na kadhalika.

Mgeni rasmi kabla ya kutoa vyeti kwa kundi la pili la wahitimu wa Chibweda ‘Furaha’ Canon Elias Lucas Chamwenye ambae alimwakilisha Askofu Godfrey Sehaba wa dayosisi ya Morogoro Kanisa la Anglikana aliwataka wahitimu hao kutumia maarifa hayo kujiendeleza kiuchumi na kushiriki katika uchumi wa taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kutumia haki yao ya kimsingi ya kupiga kura kuwachagua viongozi wa nchi Raisi, Wabunge, na Madiwani ifikapo tarehe 28/10/2020.

Ndg mgeni rasmi Canon Elias Lucas akiongea na wahitimu
Ndg. mgeni rasmi Canon Elias akitoa wosia kwa wahitimu

Mgeni rasmi; Canon Elias Lucas Chamwenye akiwa anazungumza na wahitimu wa awamu ya pili katika mahafali hayo.

Naye Meneja wa Miradi na utunishaji mfuko wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mch. Samwueli Mshana ambaye pia alimwakilisha Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania Ndg. Alfred Elias Kimonge, alisema lengo la Chama cha Biblia ni kutafsiri Biblia kwa lugha za asili,  kukuza na kutunza lugha ya asili  lakini pia kusaidia jamii husika kusoma na  kuelewa Neno la Mungu.  

Mch. Mshana akiendelea kuongea na wahitimu
Mch. Mshana akiwa anatoa pongezi na wosia kwa wahitimu

Meneja wa miradi na utunishaji mfuko wa Chama cha Biblia cha Tanzania Mch. Samwueli Mshana akiwapongeza wahitimu wa mahafali ya pili.

 Katibu wa idara ya mamaendeleo ya Akina Mama UMAKI Josephine Semwenda katika Dayosisi ya Morogoro ambaye alialikwa kuwatia moyo wahitimu hao aliwasisitizia wahitimu kutokuogopa kuitangaza lugha ya Chikagulu kila mahali katika eneo lao la ukaguruni na kuwahimiza kuwa mabalozi wema katika kuilinda lugha yao isipotee, alitumia nafasi hiyo pia kuwapongeza. wahitimu wote na kuwatakia kila lakheri katika kutekeleza majukumu ya kijamii na Kanisa.

Mwenyekiti wa UMAKI akiongea na wahitimu
Mh. Josephine akizungumza na wahitimu

Katibu wa UMAKI Ndg. Josephine Semwenda akitoa wosia wake kwa wahitimu kuzidi kutia juhudi katika kuwafundisha wengine hususani neno la Mungu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nguyami Mh.Gilbert Ngiga ambaye alitembea umbali mrefu kuja kushuhudia mahafali hayo alisema wao katika kijiji chao tayari wameshamchukua moja kati ya wahitimu hawa anayeitwa Rehema Penford na kumuweka katika kamati ya maendeleo ya kijiji, na wataendelea kufanya hivyo ili kuwahamasisha wengine kujiunga na mpango huu mzuri.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nguyani Mh. Gilbert akitoa wosia kwa wahitimu
Mwenyekiti huyo wa kijiji cha Nguyani Mh. Gilbert Ngiga alitoa shukurani zake nyingi kwa Chama cha Biblia chaTanzania kwa juhudi wanazozifanya kuwafikia watu mbalimbaliu.

Katika mahafali hiyo kulikuwa na vikundi mbalimbali vya nyimbo, ngonjera, mashairi, maigizo, na kusoma hadithi kutoka katika kitabu cha Chibweda mbele ya mgeni rasmi.

Wahitimu kwa pamoja wakiimba nyiombo
Kikundi cha nyimbo na ngoma.
Wahitimu wakiwa wanasoma ngonjera
Kikundi cha wahitimu wakisoma risala.
igizo magubike CHIBWEDA
Pichani, ni wahitimu wa awamu ya pili, katika igizo lao wakionyesha madhara ya kutokujua kusoma na kuandika ambapo tunaona mtoto aliyelala hapo chini alipoteza maisha baada ya mama yake kumpa dawa kinyume na maelekezo aliyopewa na daktari. Hii ni kwa sababu mama yake alipopewa taarifa na wenzake kwenda kujiunga na darasa la CHIBWEDA hakuwa tayari kujiunga na elimu ya watu wazima ambayo hutolewa bure na Chama cha Biblia cha Tanzania na kusababisha kifo cha mwanae kwa uzembe.

Katika mahafari hayo yaliyofanyika kanisani  Anglikana Magubike na mwenyeji wetu Kasisi Elkana Chogohe wa kanisa hilo. Alitoa shukurani zake kwa wahitimu na waanzilishi wa mafunzo kutoka Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kwa watu wazima waeneo hili la wakagulu.

Kasisi Elkana Mch wa kanisa la Anglikana akiwapongeza wahitimu wa awamu ya pili
Kasisi Elkana Chogohe  wa kanisa la Anglikana Magubike akitoa shukurani zake kwa wahitimu na waanzilishi wa mafunzo kutoka Chama cha Biblia cha Tanzaniakwa kwa watu wazima waeneo hili la wakagulu.
Wafungwa, Mahabusu Dar wakabidhiwa Biblia Takatifu

Wafungwa, Mahabusu Dar wakabidhiwa Biblia Takatifu

IMG 20200831 WA0009Na Dalphina Rubyema

WAKATI Chama cha Biblia cha Tanzania kikiwa kimetoa msaada wa Biblia Takatifu kwa wafungwa na mahabusu ya Magereza ya Segerea, Ukonga na Keko yote ya jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Gereza la Segerea, SSP. Daniel Mwakyoma amesema ukosefu wa uzio na upungufu wa nyumba za watumishi ni miongoni mwa changamoto zinazolikabili gereza hilo.

IMG 20200829 WA0013

Makabidhiano ya msaada huo upande wa Gereza la Segerea yamefanyika mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Arch. Ng’wilabuzu Ludigija na Maafisa Waandamizi wa gereza hilo, huku upande wa Chama cha Biblia kikiwakilishwa na wajumbe mbalimbali akiwemo Katibu wa Chama hicho, Mch. Alfred Kimonge, Meneja wa Mahusiano ya Makanisa na Utunishaji wa mfuko wa chama hicho, Mch.Samwel Mshana huku Kanisa Katoliki likiwakilishwa na Mjumbe wa Bodi wa Chama hicho hicho, Padri Chesco Msaga, CPP.S ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo ulioenda sambamba na utoaji wa mahitaji ya kimwili kwa wafungwa na mahabusu hao, unaojumuisha sabauni na dawa ya meno, Katibu wa Chama hicho, Mch. Kimonge amesema, lengo ni kuwapa wahusika fursa ya kusoma Neno la Mungu, linalobadilisha, na kutia faraja, msaada uliopokelewa kwa furaha na wahusika.

“Chama cha Biblia Tanzania ambacho kinajumuisha wanachama kutoka madehebu ya Waprotestanti, Wasabato, Wapentekoste na Wakatoliki, kinaguswa na maisha ya makundi mbalimbali wakiwemo mahabusu na wafungwa kama nyie, hivyo Biblia hizi tunazokabidhi kwenu tunaomba ziwasaidie kufanyie rejea yale mnayohubiriwa…zinafaa hata kwa wale wasiokuwa Wakristo,” amesisitiza.

IMG 20200829 WA0015

Msaada huo umeenda sambamba na ziara maalum ya Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala, Arch, Ng’wilabuzu Ludigija kutembela magereza yaliyopo wilayani kwake ya Segerea na Ukonga, kama sehehemu ya kujitambulisha.

Katika ziara hiyo Mkuu huyo wa Wilaya na wajumbe wa Chama cha Biblia, walipata fursa na kuzungumza na uongozi wa gereza hilo pamoja na kukutana na mahabusu na wafungwa, wakiwemo wanawake na wanaume ambapo waliwasilisha changamoto zao.

Upande wake SSP Mwakoyoma amesema ngome (gereza), haijazungushiwa uzio, hali inayosababisha hali ya usalama kuwa hatarini, hali inayoenda sambamba na ukosefu wa nyumba za watumishi kiasi cha kusababisha asilimi 90 kuishi uraiani nje ya kituo chao cha kazi.

Changamoto nyingine kama zilivyobainishwa na Mkuu huyo wa Gereza ni ukosefu wa huduma ya usafiri kwa mahabusu pindi wanapotakiwa kupelekwa mahakamani kusikiliza kesi zao, uhaba wa maji na kutokuwa na jenereta (standby generator) pindi umeme unapokatika, jambo ambalo ni hatari kwa jumuiya yenye msongamano wa watu kwani pia kuna mlundikano wa mahabusu.

Akitoa kero zinazowakabili wafungwa na mahabusu wanawake, nyampala wa kundi hilo, (jina tunalihifadhi) amesema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni baadhi ya watuhumiwa kuchanganyikiwa kiakili, hali inayosababishwa na masuala mbalimbali likiwemo la kesi zao kutokusikilizwa kwa wakati, jambo ambalo amesema ni hatari kwa wafungwa na mahabusu wengine.

IMG 20200829 WA0012

“Kuathirika kisaikolojia… anapiga mahabusu wenzake na anaweza hata kuwafanyia vitendo vingine vya kikatili zaidi, hivyo tunaomba hili liangaliwe na kufikishwa kunakostahili ili ikiwezekana hata wafanyiwe vipimo vya kitaalam zaidi na ikibainika ni shida, basi wapelekwe kwenye magereza yaliyotengwa kwa watu wa namna hii,” amesema.

Changamoto nyingine kwa wanawake ni uhaba wa magodoro hali inayowalazimu baadhi yao kulala chini kwenye sakafu, uhaba wa sare kwa wale ambao tayari wameshahukumiwa, lishe duni kwa watoto wanaoishi na mama zao gerezani pamoja na uhaba wa maji na vifaa vya usafi vya kutosha hali inayosababisha wengi kupata ugonjwa wa UTI.IMG 20200829 WA0016

Asia Mhamed ambaye ni mahabusu Na.125/2016 yeye amesema changamoto zaidi ipo kwa watuhumiwa wa kesi za mauaji, utakatishaji pesa na dawa za kulevya, ambapo amedai zimekuwa hazikilizwi kwa kile wanachoambiwa na mahakimu na majaji wanaosikiliza kesi hizo kuwa wanaendelea na upepelezi na hata wakati mwingine kudai kwamba kesi hizo uendeshaji wake unahitaji hela ambayo lazima iwe imetengwa kwenye bajeti ya serikali.

Upande wa mahabusu na wafungwa wanaume, mwakilishi wa kundi hilo, Florian Apolynal yeye amesema licha ya baadhi ya watuhumiwa wakiwemo wale wanaokabiliwa na kesi za Uhujumu Uchumi kutekeleza agizo la Rais, la kuandika barua na kutaka kufanyike maelewano (bargaining), lakini hawajui kinachoendelea baada ya kutekeleza hilo.

Pia wamedai kuwa kuna changamoto ya kubambikiziwa kesi zikiwemo za mauaji “… wakishakukamata wanakupa adhabu kali zenye mateso ili wakubadilishia kosa ambalo haujafanya… hivyo wengi humu tuna machungu kwani unakamatwa na kosa la wizi (robbery), lakini kwenye faili unaandikiwa mauji,” amesema mahabusu Charles Raphael Mkanya.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amesema kero hizo amezipelekea na atazifikisha ofisini kwake ajadiliane na wataalam na kile kitakachoshindikana atakipeleka ngazi za juu zaidi ili zipatiwe ufumbuzi.

Watu wazima 317 wajifunza kusoma, kuandika

Watu wazima 317 wajifunza kusoma, kuandika

 Na Anastazia Anyimike, Gairo – Morogoro

Pokea cheti Bibi Ongera

 Watu wazima 317 kati ya 423 kutoka vijiji 20 wameitimu mafunzo ya kusoma na kuandika kwa lugha ya Chikagulu.

Akizungumza jana baada ya kukabidhi vyeti 89 kwa awamu ya kwanza ya wahitimu hao, Mratibu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Frank Makalla alisema wahitimu hao ni wa awamu ya pili ya programu iliyolenga kuwajenga uwezo wa kusoma na kuandika watu wazima wanaoanzia miaka 15 na kuendelea.

Mratibu wa mpango wa elimu kwa watu wazima kutoka Chama Cha Biblia Cha Tanzania akiongea jambo katika mahafali ya awamu ya pili iliyofanyika Gairo

Mratibu wa Mradi Mwl. Frank Makalla

Mratibu wa mpango wa elimu kwa watu wazima kutoka Chama Cha Biblia Cha Tanzania akiongea jambo katika mahafali ya awamu ya pili iliyofanyika GairoAwamu ya kwanza ya programu hiyo iliyoanza mwaka 2017, watu 120 walijiandikisha huku watu 97 walihitimu mafunzo hayo ambayo pamoja na kuwafundisha kwa lugha ya Chikagulu, mafunzo hayo yanafanywa pia kuweza kusoma na kuandika kwa Kiswahili.

Programu hiyo inafadhiliwa na Chama cha Biblia cha Tanzania, Chama cha Biblia cha Finland na Taasisi ya Lugha ya Kenya, pia unalenga zaidi kuwainua wanawake ingawa na wanaume wanaruhusiwa kushiriki.

Makallla alisema kati ya watu wazima 317 waliohitimu, wanawake ni 270 na wanaume ni 47.

Akizungumzia sababu ya baadhi ya watu waliojiandikisha kushindwa kumaliza, Makallla alisema kwa wale walioacha masomo, hao wamepewe nafasi ya kuingia darasa la awamu ya tatu linalotarajia kuanzia Mei 15, mwaka huu ikiwa ni baada ya walimu kupewa mafunzo ya kujengewa uwezo.

Aidha, Makalla aliomba ushirikiano na serikali katika mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwafanya wananchi waliokosa fursa ya kusoma na kuandika.

“Katika programu yetu tumekuwa tunachukua wale wenye umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea, hivyo wale wenye miaka 15 hadi 17, serikali inaweza kuwatambua na kuwaingiza katika mfumo wa MEMKWA ili wakajifunze Zaidi kwa sababu sisi hapa tunawafundisha kusoma na kuandika tu, ” alieleza.

47

Mgeni rasmi Dk. Jackson Nyanda (Makamu Mwenyekiti Chama cha Biblia cha Tanzania)

Kabla ya kutoa vyeti kwa kundi la kwanza la wahitimu wa 89 wa Chibweda ‘Furaha’ Dk Jackson Nyanda aliwataka wahitimu hao kutumia maarifa hayo kujiendeleza kiuchumi na kushiriki katika uchumi wa taifa kwa ujumla.

38

Meneja Miradi na Uhusiano wa Makanisa Mch. Samwueli Mshana

Naye Meneja wa Miradi na utunishaji mfuko wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Samwueli Mshana ambaye pia alimwakilisha Katibu wa chama hicho, alisema lengo la chama chake ni kutafsiri Biblia kwa lugha za asili,  kukuza na kutunza lugha ya asili  lakini pia kusaidia jamii husika kuelewa Neno la Mungu.

Wanakisomo wa Elimu ya watu wazima katika msemo wa Kikaguru

Wanakisomo wa Elimu ya watu wazima katika msemo wa Kikaguru

Na. Ndugu Frank Makalla (Msimamizi Mkuu wa Mradi-CBT).

Chama Cha Biblia Cha Tanzania kilianzisha kisomo cha elimu ya watu wazima kwa kushirikiana na Chama Cha Biblia Cha Finland na SIL (Summer Institute of linguistic) mnamo mwaka 2017 na mwaka huo ulikuwa ni mwaka wa kuandaa vitabu kwa ajili ya wanakisomo wa elimu ya watu wazima katika msemo wa Kikagulu na kanisa katika eneo hilo lilishiriki kikamilifu kwa kutoa watafsiri na waandishi. Ndipo mradi ukaanza 2018 ukiwa na walimu 20 (ishirini). Walimu hao walianza na wanafunzi mia ishirini ambavyo wanafunzi 97 walihitimu na kupewa vyeti mwezi machi 2019.

Na baada ya hapo Madarasa ya kujifunza kusoma na kuandika yalianza mwezi wa nane 2019 katika vijiji 20 (ishirini) vingine na kila kijiji kina darasa moja na kila darasa lina walimu wawili 2 (wawili) na jumla ya wanafunzi ni 423 kwa vijiji vyote.

Madarasa hayo ishirini yanaendelea vizuri katika kiwango cha 97% (asilimia tisini na saba) wanaweza kusoma na kuandika. Tunatarajia watahitimu mwisho wa mwezi huu wa February 2020 na mahafali yatakuwa mwezi wa tatu  kuanzia tarehe 14/03/2020 (kumi na nne), 21/03/2020 (ishirini na moja) na 28/03/2020  (ishirini na nane) kwa maana yamegawanywa kwenye vituo vitatu ambavyo ni Gairo, Nguyami na Magubike.

IMG 20200124 WA0011

Darasa la Chibweda kijiji cha Kibedya

Mwalimu Devotha Madihi wa darasa la Chibweda kijiji cha Kibedya akifundisha darasani. Darasa hili lina mama mmoja mwenye watoto mapacha wanaonekana hapo chini na amekuwa akihudhulia vizuri sana darasani.

IMG 20200124 WA0012

Darasa la Chibweda Kijiji cha Berega

Wanakisomo wa darasa la Kikagulu katika Kijiji cha Berega wanajifunza kusoma na kuandika kwa kutumia lugha ya Kikaguru wakifundishwa na waalimu wao Rose Chitemo mwenye kilemba na Sofia Muhumba.

IMG 20200124 WA0016

Darasa la Chibweda Kijiji cha Berega

Mwanafunzi Merina Malali wa Darasa la Chibweda Berega akiwa anaandika kufuatia maelekezo ya waalimu.

IMG 20200124 WA0023

Darasa la Chibweda Kijiji cha Kiegea

Darasa la Kiegea wanafatilia mafundisho ya mwalimu ubaoni.

IMG 20200124 WA0025

Darasa la Chibweda Kijiji cha Tabuhoteri

Darasa la kijiji cha Tabuhoteli lina wakina mama wenye umri mkubwa na wana bidii sana katika kujifunza kusoma na kuandika.

IMG 20200124 WA0027

Darasa la Chibweda Kijiji cha Ibindo

Wanakisomo katika kijiji cha Ibindo wakipata maelekezo kutoka kwa walimu wao kuhusu kusoma na kuandika.

IMG 20200124 WA0016

Kujifunza kuandika

Mwanafunzi Merina Malali wa Darasa la Chibweda (mwenye kilemba cha pink) katika kijiji cha Berega akiwa anaandika kufuatia maelekezo ya waalimu.

Wanakisomo awa, wapo katika marudio wakisubiri kupewa mitihani yao ya mwisho ili hatimaye kukabidhiwa vyeti kwa wale watakaofaulu na kuhitimu masomo yao vizuri.

CHANGAMOTO:

Kwa kuwa hawa ni watu wazima zipo changamoto mbali mbali zinazoathiri mahudhurio darasani kama vile:- kazi za shamba, misiba kijijini na nje ya kijiji, kuumwa, kuuguliwa, mito kujaa na kuwatenganisha kwa muda, kutomaliza silabasi yao kwa wakati kwa kuwa wapo wenye kujifunza kwa polepole kulingana na umri wao na kusababisha waalimu kuwa fuatilia na kuwaelekeza kwa muda zaidi.  n.k.

Changamoto katika kuwafikia

Wakati mwingine kuna changamoto ya kuwafikia wanakisomo kwa sababu ya ubovu wa miundombinu hasa barabara kama picha inavyoonesha hapa chini.

IMG 20200124 WA0022

Kunasua gari

Wakati mwingine kipindi cha mvua changamoto kubwa ni barabara, mfano picha hiyo hapo Gari lilikwama kwenye matope kutokana ubovu wa barabara wakati tunakwenda kuona darasa la Mtumbatu na tulisaidiwa na wanakijiji kulinasua gari kwenye matope (Ndugu Frank Makalla akieleza).