Na: Felix Rwebandiza Jones.
Kitengo cha Tehama.

Mwenyekiti wa Kikao ambaye pia ni Baba Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kirutheri la Kiinjiri Jimbo la Moshi

Mwenyekiti wa Kikao ambaye pia ni Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania – Jimbo la Moshi, akifungua kikao

Wajumbe.
Waliohudhuria walikuwa 36 kama inavyooneshwa hapa chini.
1. Wakurugenzi Chama cha Biblia cha Tanzania (Rev. Askofu Amosi Muhagachi ambaye ni Balozi wa Chama cha Biblia cha Tanzania na Eng. Ekael Manase ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Chama cha Biblia cha Tanzania).
2. Maafisa wa Chama cha Biblia cha Tanzania (Rev. Ipyana Mwangota amabaye ni Meneja Tafrisi na Felix Jones ambaye ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA).
3. Wachungaji na Mapadre.
4. Mwangalizi wa Jimbo Katoliki la Moshi.
5. Wenyeviti wasaidizi wa Maaskofu.
Agenda kuu ya Kikao ilikuwa ni:
• Uhamasishaji wa Chama cha Biblia cha Tanzania,
• Uanachama na faida zake na
• Tafsiri ya Biblia kwa ujumla wake.
Baada ya ufunguzi wa kikao mwenyekiti aliruhusu watumishi kijitambulisha
Mmoja wa wajumbe akijiambulisha

Mmoja wa wajumbe akijitambulisha wakati wa Mkutano huo

na baada ya hapo alimkaribisha Rev. Askofu Amosi Muhagachi kueleza ujumbe wake kutoka Chama cha Biblia Cha Tanzania. Askofu Muhagachi alianza kwa kuelezea historia yake, kabla ya kuanza kufanya kazi na Chama cha Biblia cha Tanzania, ambapo akiwa mwanafunzi na mwanachama aliweza kuwa muhamasishaji katika shule ya Sekondary ya Mirambo Tabora na aliweza kuwahamasisha wanafunzi wenzake wachangie Chama cha Biblia cha Tanzania ili kipate fedha za kuchapisha Biblia nyingi ili wanafunzi wenzao wapate Neno la Mungu kama wao. Alifanya hivyo katika kipindi chote cha masomo yake “nilikuwa nikihamasisha wanafunzi wenzangu tuchangie Chama cha Biblia cha Tanzania, ili Chama cha Biblia cha Tanzania kiweze kuchapisha Biblia nyingi ili sisi na vijana wenzetu tupate Biblia” alisema Rev. Askofu Amosi Muhagachi.
Rev. Askofu Muhagachi akizungumza wakati wa Kikao

Rev. Askofu Muhagachi akizungumza wakati wa Kikao

Baba Askofu Amosi Muhagachi baada kuhitimu masomo yake alipata barua ya kuitwa kwenye usaili na baada ya hapo aliweza kuajiriwa kuwa Afisa Uhusiano na Makanisa na Uhamasishaji wa Chama cha Biblia cha Tanzania ambapo alikaa kwa miaka saba kabla ya kuwa Askofu wa kanisa la Mennonite Tanzania na baadaye kwenda masomoni nchini Marekani, ambako bado anaendelea na masomo yake.
Baba Askofu Amosi Muhagachi alieleza mikakati ya Chama cha Biblia cha Tanzania ambayo ni;
i. Kuyaomba makanisa kutenga juma moja kuombea Chama cha Biblia cha Tanzania na watendaji wake.
ii. Kuomba watu kujitolea kuchangia Chama cha Biblia cha Tanzania ili kipate pesa za kutosha za kutafiti, kuchapisha na kusambaza Neno la Mungu kwa lugha mbali mbali hapa Tanzania.
iii. Kuomba viongozi wa makanisa wakubali kuchangia mpango mkakati wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa kupeleka Neno la Mungu kwa wafungwa, vijana na watoto.
iv. Kuwaomba viongozi wa Makanisa kuendesha mpango wa kuwepo mashindano ya kukariri mistari ya Biblia kwa vijana na watoto katika Shule, Makanisa na Vyuoni.
v. Kuhamasisha utumiaji wa Biblia (Hard copy) makanisani na viongozi wahakikishe zimeandikwa au zina nembo ya Chama cha Biblia cha Tanzania kama njia ya kuepukana na watu wanaogushi/kuchakachua Neno la Mungu.
Baada ya kumaliza hotuba yake alimuomba Mwenyekiti wa kikao amkaribishe Eng. Ekael Manase alielezea juu ya Uanachama, wa Chama cha Biblia cha Tanzania.
Eng. Ekael Manase alianza kwa kumshukuru sana Baba Askofu Amosi Muhagachi kwa jinsi alivyoeleza vizuri kuhusu kuwahamasisha watu kukichangia Chama cha Biblia cha Tanzania.
Pia aliendelea kwa kuwaomba sana na kuwasihi watumishi wa Mungu wote waliohudhulia kuwa wanatakiwa kuwahimiza waumini wao na kufufua ari ya kusoma Neno la Mungu ikiwa ni pamoja na kuanzisha mashindano ya kusoma na kukariri mistari ya Biblia kwa vijana na watoto, kwa lengo la kuwaandaa ili waweze kukua wakilishika Neno la Mungu. Lakini pia aliwaomba sana wachungaji na mapadre kuwahimiza sana waumini wao kutumia Biblia (hard copy) na kuacha kutumia Biblia zilizowekwa kwenye simu za mikononi (soft copy). Kwani wanaweza wakasoma Neno lililopotoshwa na watu wenye nia ovu kwa Ukristo.
Eng. Ekael Manase aliendelea kueleza kuwa hayo yote hayawezi kufanikiwa kama vijana wetu na watoto wetu hawatakuwa na Biblia zao; kwa hivyo basi ili jambo hili liweze kufanikiwa tunahitaji tuwe na Biblia za kutosha na kwa bei wanayoimudu. Biblia za bei nafuu zinaweza kupatikana tu; endapo kama sisi sote tutajitoa kukichangia Chama cha Biblia cha Tanzania. “Maana kama Biblia zingeuzwa kwa bei yake halisi ingekuwa ghali sana, lakini michango inayotolewa kwa CBT inafanya Biblia iweze kuuzwa kwa bei rahisi” alisema Eng. Ekael Manase.
Pamoja na melezo mazuri ya kuwahamisha watumishi wa Mungu kuhusu kuchangia Biblia na kuwa himiza watoto na vijana kusoma Biblia, pia Eng. Ekael Manase aliwaeleza wajumbe waliohudhuria aina za uanachama; kuwa kuna uanachama wa aina tatu;
i. Uanachama wa maisha
• Uanachama wa Maisha Mme na Mke shilingi 15,000= na ahadi isiyopungua shilingi 15,000=kwa mwaka.
• Uanachama wa Maisha mtu mmoja shilingi 10,000= na ahadi isiyopungua shilingi 10,000= kwa mwaka.
ii. Uanachama wa Bidii
• Uanachama wa kawaida (bidii ) shilingi 5,000=kwa mwaka.
• Uanachama wa kawaida kwa Wanafunzi wa Sekondari na Vyuo shilingi 2,000= au zaidi kwa mwaka.
• Uanachama wa kawaida wa kushirikishwa kwa watoto na wanafunzi wa shule za Msingi shilingi 1,000= au zaidi kwa mwaka.
• Mwanachama wa Biblia Moja kwa Mwezi (Bible a Month Club) 5,000=, 10,000=, 15,000=, 20,000= au zaidi kwa mwezi.
iii. Uanachama wa Mashirika
• Uanachama wa Mashirika shilingi 50,000= na mchango usiopungua shilingi 50,000= kwa mwaka.
Mwisho Eng. Ekael Manase alimalizia kwa kusema kuwa hii itakuwa ni njia nzuri Zaidi ya kuwakusanya vijana na kupenda kusoma Neno la Mungu, na pia itasaidia sana kupanda mbegu ya Neno la Mungu ndani yao na kuwa na Taifa lenye kumcha Mungu na lenye maadili mema.
Kwa upande wake Meneja wa Tafsiri wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mch. Ipyana Mwangota alipopewa nafasi ya kuzungumza mbele ya wajumbe wote; alielezea kazi za Tafsiri anazozifanya ndani ya Chama cha Biblia cha Tanzania akiwa kama Meneja wa Tafsiri. Alifafanua kuwa wanafanya kazi ya kutafsiri Biblia kwa lugha mbali mbali ikiwa njia mojawapo ya kulisaida Kanisa kufanya kazi ya umisheni.
Mch. Ipyana Mwangota akitoa ukizungumzia juu ya Tafsiri

Meneja tafsiri, Mch. Ipyana Mwangota akitoa ukizungumzia juu ya Tafsiri

Alifafanua Zaidi juu ya kazi ya Tafsiri na kutaja Tafsiri zinazofanyika upande wa kanda ya Kasikazini ambazo ni Tafsiri ya Kivunjo, Kidatooga, Kimashame na Kimochi. Alinukuriwa akisema Pia Chama cha Biblia cha Tanzania kinakamilisha uchapaji wa Biblia ya Kisukuma. Kazi hii imepelekwa kule Korea kwa ajili ya uchapishaji. Ni tarajio letu kuwa kazi ya uchapishaji na uzinduzi itakamilika mwishoni mwa mwaka huu 2019. “Chama cha Biblia cha Tanzania kimepokea maombi ya Tafsiri na sasa kinaendelea kufanya pia Tafsiri ya lugha mbalimbali kubwa kama Igikuria, Kiha, Kinyiramba, Kirimi, Chikaguru na kihehe. Aidha CBT tumepokea maombi ya Kanisa katika maeneo ya Ufipa, Unyamwezi, Unyiha, na Upare ili kiweze kusaidia kutafsiri Biblia kwa Lugha ya Kifipa, Kinyamwezi, Kinyiha na Kipare na kukubali; na sas Chama cha Biblia cha Tanzania kipo katika mchakato wa kutafuta fedha ili kuianza kazi hii kwa ushirikiano na Makanisa mwaka 2020 Januari.
Baadhi ya Wajumbe wakisikiliza kwa Makini

Baadhi ya Wajumbe wakisikiliza kwa Makini.

Pia alieleza kuwa zipo Biblia ambazo zimetafsiriwa, kuchapishwa na zinatumika katika makabila lengwa kama vile Biblia ya Kinyakyusa (Mkoa wa Mbeya), Biblia ya Luhaya (Mkoa wa Kagera), Biblia ya Cigogo (Mkoa wa Dodoma), Biblia ya Kimasai (Mkoa wa Arusha), na Biblia ya Kihiraqw (Mkoa wa Manyara).
Pia alieleza kuwa Chama cha Biblia kimefanya tafsiri za Agano Jipya na sehemu za Biblia nyingi tu na zinatumika maeneo tofauti tofauti ili kukidhi haja ya watumiaji wa lugha husika kuendana na sera ya Vyama vya Biblia Duniani.
Kuhusu mchakato wa kazi ya tafsiri; Meneja Tafsiri alieleza kuwa ofisi yake, hutumia vifaa vya kisasa. Kwa lengo la kufanikisha kazi hii kubwa. Alionyesha Program ya Paratext kwa wajumbe wa mkutano kama mfano wa vifaa hivyo ili waone jinsi kazi hii inavyotendeka. Wajumbe walipongeza kazi hii kubwa na waliahidi kuiombea.
Pia alieleza kuwa Chama kwa sasa kinatia mkazo uwepo wa Biblia za Watoto, na hivyo kimekuwa kikiandaa Biblia za watoto ili kuhakikisha Makanisa hayakosi Biblia kwa watoto wadogo, wa kati na wale wanaoelekea umri wa utu uzima.
Mwisho alitoa wito kwa viongozi wa Makanisa kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Chama cha Biblia cha Tanzania katika kuhakikisha Maandiko Matakatifu yanapatikana kikamilifu kwa kuchangia na kuombea juhudi hizi.

× How can I help you?