Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha hata atakapo kuwa mzee. [Mithali 22:6]
Wapendwa Taifa la Mungu na wakristo wa Tanzania, malezi ni uangalizi wa karibu wa wazazi kwa mtoto wao kiroho, kiafya, kiakili, kitabia ili tuwe na Taifa imara na watu wanaomcha Mungu. Mungu alipomuumba Adamu na Hawa akasema “zaeni mkaongezeke…………[Mwanzo 1:28.]”
Ni wajibu wa wazazi katika familia na kanisani kuwahimiza watoto kulisoma na kulipenda Neno la Mungu yaani Biblia. Katika [Rum. 8:28] tunasoma: “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema……” Hii ni pamoja na kazi ya kulea watoto; Mungu hufanya kazi hiyo pamoja na sisi.
Katika [Zab. 127:3] Biblia inasema “Tazama wana ndio urithi wa BWANA uzao wa tumbo ni thawabu.” Mungu hatupi watoto ili tuwahifadhi kwa matumizi yetu wenyewe. Yeye anatupa watoto ili tuwalee kwa utukufu wake. Watoto wetu ni wa Mungu. Mungu amelithibitisha agano lake pamoja nasi, Katika [Kumb. 28:4] anasema “Utabarikiwa uzao wa tumbo lako” Pia katika [Isaya. 8:18] inasema “Angalieni, mimi na watoto hawa niliyopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israel……” Kwa sababu hii Mungu anataka watoto wetu wajifunze Neno lake na kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Mungu anatazamia wazazi wawaelekeze watoto kwake, kwa njia ya Neno lake yaani Maandiko Matakatifu (Biblia).
Walinde watoto wako na vishawishi viovu.
Ujue nia ya shetani siku zote ni kutaka kuwaangamiza watoto, iwe kiroho au hata kimwili kwa kuwavuta katika mambo ya ulimwengu. Kuna mambo kadha wa kadha ambayo watoto wanakutana nayo maishani na haya yanaweza kusababisha au kuwaondoa kabisa wasimfuate Mungu sawasawa. Neno la Mungu linasema “Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia… na dunia inapita pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”. [1Yoh. 2:15-17].
Marafiki wabaya na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yameangamiza familia nyingi na kuwapoteza watoto na vijana katika kiwango cha kutisha [Mithali 13:20] Neno la Mungu linasema “… Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.” [Zab. 1:1] inasema: “Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani
pa wenye mizaha.”
Nawasihi na kuwaomba Wakristo wa Tanzania kusimama na Chama chenu cha Biblia kuwaridhisha watoto wetu Neno la uzima, hivyo wapatie watoto Biblia katika maisha yao. Simama na huduma ya Chama cha Biblia cha Tanzania kuwapatia watoto na vijana.
Neno la Mungu kama zawadi na baraka kutoka kwa Mungu maishani mwao.
Amani na Neema ya Mungu iwe juu yako.
Mtumishi wenu katika Kristo
Alfred Kimonge.
Katibu Mkuu
JITIHADA ZINAZOFANYWA NA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA ILI KUHAKIKISHA VIONGOZI WA MAKANISA MBALI MBALI NCHINI WANAFIKIWA NA MPANGO HUU MADHUBUTI.
Unaweza usibadilishe dunia yote na kuifanya iwe ya kumpenda Mungu, lakini kwa sadaka yako ya upendo kwa Chama cha Biblia cha Tanzania ya Tsh 5000 tu! na kuendelelea unaweza kumbadilisha milele mtoto, kijana au hata mfungwa mmoja.
Tuma sadaka yako ya upendo kupitia namba ya M-PESA ya Chama: 890890 kisha tuma ujumbe wa kuchangia katika namba hizi: 0762998819, 0754383636 na 0754479789.
Pia unaweza kuchangia kupitia akaunti za Benki za DTB na NBC zilizoonyeshwa hapa chini Changia kupitia benki ya DTB: Namba ya Akaunti: 0901969001 SWIFT OR WIRING CODE DTKETZTZ na Changia kupitia benki ya NBC: Namba ya Akaunti: 029103000362 na Mungu akubariki sana.
Na Mungu akubariki sana
Askofu Amos Muhagachi
Mhariri
Mawasiliano yatumwe kwa: Katibu Mkuu Chama cha Biblia cha Tanzania, P.0. Box 175, Dodoma, Tanzania. Email: aekimonge@yahoo.com T: +255262324661 Fax: +255262324058.