Na. Rose Mrema

Chama cha Biblia cha Tanzania ni taasisi ya Kikristo inayojishughulisha na kutafsiri, kuchapisha na kueneza Maandiko Matakatifu yaani Biblia kwa niaba ya makanisa yote ya Tanzania. Pia Chama cha Biblia kinaendesha program mbalimbali kwenye jamii lengo likiwa ni kuihudumia jamii kiroo na kimwili (Holistic Ministry) Kupitia Program ya “Je yuko wapi Msamaria mwema Leo? inayojishughulisha na mapambano dhidi ya UKIMWI ikilenga kupunguza unyanyapa hasa makanisani, kuhamasisha watu kupima kwa hiari, watu kubadilisha tabia kwa kutumia neno la Mungu na kuleta muungamaniko wa makanisa/misikiti katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI. Chama cha Biblia kupitia program hii kimeweza kuwafikia watoto walioachwa yatima baada ya wazazi wao kufariki kwa ugonjwa wa UKIMWI, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, wenye maambukizi na watoto wenye ulemavu.

DSC08065 min

Mtumishi wa Chama cha Biblia cha Tanzania (Mrs. Rose Mrema) akifundisha washiriki wa mafunzo ya watoto kutoka Ibohora.

Mpango huu wa watoto unatekelezwa katika kata ya Ubaruku,Wilaya ya Mbarali kwa kushirikiana na taasis za kidini, wadau wengine wanaohudumia watoto (KIWAUTA na SHIDEPHA) pamoja na viongozi wa serekali, na jamii kwa ujumla. Lengo ni kuwawezesha watoto hao kuishi maisha yaliyo kamilika kama walivyo watoto wengine, kuhamasishana kuikumbusha jamii wajibu wake juu ya watoto hao na  kumjengea mtoto uwezo wa maisha kwa ujumla.

DSC05993 min

Waalimu wa Sunday school, madrasa, shule za secondary na primari waliopata mafunzo ya watoto toka kata ya Ubaruku wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo.

22 min

Watoto wakiwa kwenye majadiliano ya makundi wakati wa mafunzo.

Mafanikio.

Baadhi ya mafanikio ya program.

  1. Mpango huu umepokelewa vizuri na Viongozi wa Serekali, dini, jamii pamoja na wadau wengine wanaojishughulisha na kuwahudumia watoto yatima na walioko kwenye mazingira magumu.
  • Tumeweza kukutana na viongozi wa serekali, dini na wadau wengine
  • Kufanya mafunzo na waalimu wa sunday school,madrasa, Waalimu wa malezi kutoka shule za msingi, na Sekondari zilizopo kata ya Ubaruku,na wahudumu wa watoto majumbani kutoka shirika la KIWAUTA .
  • Kuwafikia watoto zaidi ya 500 yatima na walioko kwenye mazingira magumu.
  • Kugawa vifaa vya kufundishia kwa washiriki waliopata mafunzo (Vitabu,Mwongozo na flip chart.)
  1. Baadhi ya washiriki waliopata mafunzo waliweza kuendeleza mafunzo waliyopata kwa kuwafundisha wazazi wenzao,watoto makanisani, na mashuleni kwenye vipindi vya dini.
    3 min

    Wazazi wa watoto wakiwa katika majadiliano.

  2. Vitendo vya unyanyasaji wa watoto majumbani vimepungua kwa kiasi kikubwa,,upendo umeongezeka ndani ya jamii, na kwa watoto wenyewe kwa wenyewe.
  3. Baadhi ya watoto waliopata mafunzo wamebadilika tabia ,wamekuwa wasafi,anasaidia kazi za nyumbani,wameacha udokozi,wizi,kutukana na kupigana.
  4. Washiriki wametambua wajibu wa kuwahudumia watoto hao ni jukumu la jamii nzima, wengi wao wameanzisha vikundi kwa lengo la kuwahudumia watoto na kutoa elimu kwa jamii.

Changamoto.

  • Washiriki wengi waliopata mafunzo hawajui kusoma na kuandika.

14 min

Mambo tuliyojifunza

  • Vijijini wapo watoto wengi ambao wameachwa na kusahaulika kutokana na hali duni ya maisha.
  • Miradi mingi ya kuwasaidia watoto hawa ipo mijini.
  • Wazazi/walezi wa watoto wanaishi kwenye mazingira magumu na hawana mtu anayewasaidia kuwalea watoto.Jambo hili linawafanya watoto kukosa mahitaji yao muhimu ya kila siku.
  • Ukosefu wa vitendea kazi kwa watoto walemavu.mf Baiskeli ili waweze kupata haki yao ya kwenda shule.
  • Elimu bado inahitajika kwenye jamii jinsi ya kuwahudumia watoto hawa hasa walemavu wengi wao wameachwa majumbani pasipo kupata elimu,matibabu na huduma nyingine muhimu.

 

 

× How can I help you?