Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.
Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”
Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.
Wafungwa na Mahabusu wa Gereza la Kiomboi wapata Biblia.
Na: Canon Mwanamtwa: Hawa ni Askari wa Gereza la Kiomboi wakipokea Biblia kwa niaba ya Wafungwa na Mahabusu wa Gereza la Kiomboi lililopa katika Mkoa wa Singida wilaya ya Iramba. Baada ya kupokea nilipata nafasi ya kuongea na Wafungwa na Mahabusu pamoja na Askari...
MKUTANO WA VIONGOZI WA MAKANISA YA KANDA YA KASKAZINI NA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA ULIOFANYIKA WILAYANI MOSHI MKOANI KILIMANJARO. (TAREHE 04/06/2019).
Na: Felix Rwebandiza Jones. Kitengo cha Tehama. Wajumbe. Waliohudhuria walikuwa 36 kama inavyooneshwa hapa chini. 1. Wakurugenzi Chama cha Biblia cha Tanzania (Rev. Askofu Amosi Muhagachi ambaye ni Balozi wa Chama cha Biblia cha Tanzania na Eng. Ekael Manase ambaye ni...
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania (CBT) 2018.
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Biblia wa mwaka 2018 uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa kuu la Kiinjili la Kirutheli Dayosisi ya Dodoma tarehe 12/4/2019. MATUKIO KATIKA PICHA. ...
Tangazo Muhimu! Announcement!
Chama cha Biblia cha Tanzania kupitia uongozi wake, kinawatangazia na kuwakaribisha wanachama wake wote wakiwemo wakurugenzi wa Bodi wa chama, wafanyakazi, na wadhamini wake kuhudhuria mkutano mkuu wa mwaka 2018 wa kupokea taarifa ya mwaka uliopita na kupanga...
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.
Donate Today or Get Involved