Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.
Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”
Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.
MADARASA YA ELIMU YA WATU WAZIMA KWA LUGHA YA KIKAGULU {CHIBWEDA} AWAMU YA PILI GAIRO MKOANI MOROGORO.
MADARASA YA ELIMU YA WATU WAZIMA KWA LUGHA YA KIKAGULU {CHIBWEDA} AWAMU YA PILI GAIRO MKOANI MOROGORO. Mafundisho Moja ya juhudi zinazofanywa na waalimu katika madarasa ya Lwakikagulu. Maelekezo Mmoja wa waalimu wa Lwakikagulu akimuelekeza mwanafunzi kusoma na...
01 AUGUST 2019, CHARITY NEWSLETTERS /BARUA YA UPENDO YA KILA MWEZI
Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha hata atakapo kuwa mzee. [Mithali 22:6] Wapendwa Taifa la Mungu na wakristo wa Tanzania, malezi ni uangalizi wa karibu wa wazazi kwa mtoto wao kiroho, kiafya, kiakili, kitabia ili tuwe na Taifa imara na watu wanaomcha...
BARUA YA UPENDO YA KILA MWEZI YA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA
CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA N0: 01 July 2019, NEWSLETTERS /BARUA YA UPENDO YA KILA MWEZI 16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area, P.O Box 175, Dodoma Tanzania. || T: +255 (026)-2324661 F: +255 (026)-2324058 || Email: info@biblesociety-tanzania.org || Site:...
CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA CHAWAFIKIA WATOTO YATIMA NA WALIOKO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU WILAYANI MBARALI.
Na. Rose Mrema Chama cha Biblia cha Tanzania ni taasisi ya Kikristo inayojishughulisha na kutafsiri, kuchapisha na kueneza Maandiko Matakatifu yaani Biblia kwa niaba ya makanisa yote ya Tanzania. Pia Chama cha Biblia kinaendesha program mbalimbali kwenye jamii lengo...
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.
Donate Today or Get Involved