Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.
Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”
Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.
Hotuba ya Mch. Canon Prof. Aloo Osotsi Mojola. Mtaalamu wa Tafsiri Mstaafu wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni katika Uzinduzi wa Biblia ya Kwanza katika lahaja ya Kivunjo cha Kichagga Tarehe 27 Septemba, 2020.
Kama ilivyosomwa kwetu katika Ibada hiyo ya Uzinduzi na Askofu Julius Nyange Meneja Mstaafu wa Tafsri katika Chama cha Biblia cha Tanzania. Waheshimiwa Maaskofu, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia Cha Tanzania, Katibu Mkuu wa Chama Cha Biblia cha Tanzania,...
HOTUBA YA DR. ALFRED E. KIMONGE KATIBU MKUU WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA: KWENYE IBADA NA SHEREHE YA UZINDUZI WA BIBLIA YA KIVUNJO TAREHE 27 SEPTEMBA 2020.
HOTUBA YA DR. ALFRED E. KIMONGEKATIBU MKUU WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA:KWENYE IBADA NA SHEREHE YA UZINDUZI WA BIBLIA YA KIVUNJOTAREHE 27 SEPTEMBA 2020 Nawasalimu wote katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, na kipekee ninamsalimu Baba Askofu Fredrick Onael Shoo na...
HATIMAYE WAVUNJO WAPATA BIBLIA KAMILI
Baada ya miaka mingi, Wachaga wa Wavunjo, wapata Biblia katika lugha yao ya Kivunjo. Katika Sherehe na Ibaada ya uzinduzi wa Biblia kwa Lugha ya Kivunjo zimefanyika katika Usharika wa Samanga, Jimbo la Kilimanjaro Mashariki la Kanisa la Kilutheri Tanzania, Dayosisi...
MAHAFALI YA WAHITIMU WA CHIBWEDA MAGUBIKE TAREHE 19/09/2020.
MAHAFALI YA WAHITIMU WA CHIBWEDA MAGUBIKE TAREHE 19/09/2020.LWA Kikagulu wahitimu 248 waliomaliza na kufaulu mafunzo ya kusoma na kuandika katika awamu ya pili ya mahafali ambayo yalikuwa yafanyike tarehe 21/03/2020 lakini yakahirishwa kutokana na covid -19. Sasa...
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.
Donate Today or Get Involved