MAHAFALI YA WAHITIMU WA CHIBWEDA MAGUBIKE TAREHE 19/09/2020.

LWA Kikagulu wahitimu 248 waliomaliza na kufaulu mafunzo ya kusoma na kuandika katika awamu ya pili ya mahafali ambayo yalikuwa yafanyike tarehe 21/03/2020 lakini yakahirishwa kutokana na covid -19. Sasa yalifanyika tarehe 19/09/2020 katika Kanisa la Anglikana huko Magubike.

 

Wahitimu mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa katika picha ya pamoja
Mratibu wa mpango huu Mwl. Frank Makalla wa kwanza kushoto kwa waliokaa mbele akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu waliosimama nyuma wenye vyeti pamoja na mgeni rasmi Canon Elias Lucas Chamwenye wa tatu kutoka kushoto na wageni wengine walioalikwa kwenye mahafari hayo.

Awamu ya kwanza waliohitimu ni jumla ya watu 69 ambapo wanawake ni 56 na wanaume ni 13 kutoka vijiji 5 Gairo ambavyo ni Gairo, Mogohigwa, Tabuhoteli, Mtumbatu pamoja na Kibedya.

Awamu ya pili waliohitimu jumla ni 248 ambapo wanawake ni 214 na wanaume ni 34; kutoka kwenye vijiji 13 ambavyo ni Magubike, Nguyami, Berega, Chakwale, Ibindo, Mwandi, Mamboya, Mbili, Dumbaalume, Maguha, Magela, Kiegeya Pamoja Na Mabula.

Waliojiandikisha ni 423 kati yao waliohitimu ni 317 na ambao hawajahitimu ni 106 kutokana na changamoto mbalimbali kama vile kuhama, shughuli za mashamba ,na matatizo mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza jana baada ya kukabidhi vyeti  kwa awamu ya pili ya wahitimu hao, Mratibu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mwl.Frank Makalla alisema wahitimu hao ni wa awamu ya pili ya programu iliyolenga kuwajengea uwezo wa kusoma na kuandika watu wazima wanaoanzia miaka 14 na kuendelea.

Magubike Mzee Makalla
Mh Makalla akiwa anazungumza na wahitimu katika mahafali

Mratibu wa Chama cha Biblia Tanzania, Mwl.Frank Makalla akizungumza na wahitimu wa awamu ya pili katika mahafali hayo huku akiwasisitiza wasiache kufanya yale waliyofundishwa pia wahakikishe kuwa kupitia wao watu wengi zaidi walijue neno la Mungu.

Mratibu wa mpango wa elimu kwa watu wazima kutoka Chama Cha Biblia Cha Tanzania akiongea jambo katika mahafali ya awamu ya pili iliyofanyika Magubike. Alisema kuwa mahafali hayo ni mwendelezo wa mahafali  ya awamu ya kwanza ya program hiyo iliyoanza mwaka 2017, ambapo watu 120 walijiandikisha huku watu 97 walihitimu mafunzo hayo ambayo pamoja na kuwafundisha kwa kutumia lugha ya chikagulu kufundishia, mafunzo hayo yanafanywa pia kuweza kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili.

Programu hiyo inafadhiliwa na Chama cha Biblia cha Finland, Chama cha Biblia cha Tanzania pamoja na Summer Institute of linguistics (SIL) ambao wanatoa utaalamu wa waalimu pamoja na mwongozo wa kuandaa vitabu vya kufundishia.  Programu hiyo inalenga zaidi kuwainua wanawake kujifunza kusoma na kuandika ingawa na wanaume wanakaribishwa kushiriki.

Wahitimu wakiwa wanaimba nyimbo katika mahafali yao
Wahitimu wa CHIBWEDA wakiwa katika picha ya pamoja katika mahafali yao iliyofanyika mnamo tarehe 19/09/2020 huko Magubike siku ya Jumamosi.

Mratibu wa mpango huu Mwl. Makalla alisema kati ya watu wazima 248 waliohitimu, wanawake ni 214 na wanaume ni 34 katika awamu hii ya pili ambao walishindwa kufanya hivyo mwezi wa Machi 2020 kutokana na ugonjwa wa corona ulioikumba Dunia nzima wakati huo. Akizungumzia sababu ya baadhi ya watu waliojiandikisha kushindwa kumaliza, Mwl. Makallla alisema kwa wale walioacha masomo, hao wamepewe nafasi ya kujiunga na darasa la awamu ya tatu ambalo limeanza tayari wakiendelea na mafunzo. Aidha, Mwl. Makalla aliomba ushirikiano na serikali katika mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwafanya wananchi waliokosa fursa ya kusoma na kuandika kujiunga na kuendelea kupata elimu hiyo.

“Katika programu yetu hii tumekuwa tukichukua wale wenye umri wa kuanzia miaka 14 na kuendelea, hivyo wale wenye miaka 14 hadi 17, serikali inaweza kuwatambua na kuwaingiza katika mfumo wa MEMKWA katika shule za msingi kama ambavyo Serikali inaelekeza kupitia wizara ya Elimu ili wakajifunze zaidi kwa sababu sisi hapa tunawafundisha kusoma na kuandika tu huko watajifunza masomo mengine pia kama Hesabu, Sayansi, Jiografia Historia na kadhalika.

Mgeni rasmi kabla ya kutoa vyeti kwa kundi la pili la wahitimu wa Chibweda ‘Furaha’ Canon Elias Lucas Chamwenye ambae alimwakilisha Askofu Godfrey Sehaba wa dayosisi ya Morogoro Kanisa la Anglikana aliwataka wahitimu hao kutumia maarifa hayo kujiendeleza kiuchumi na kushiriki katika uchumi wa taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kutumia haki yao ya kimsingi ya kupiga kura kuwachagua viongozi wa nchi Raisi, Wabunge, na Madiwani ifikapo tarehe 28/10/2020.

Ndg mgeni rasmi Canon Elias Lucas akiongea na wahitimu
Ndg. mgeni rasmi Canon Elias akitoa wosia kwa wahitimu

Mgeni rasmi; Canon Elias Lucas Chamwenye akiwa anazungumza na wahitimu wa awamu ya pili katika mahafali hayo.

Naye Meneja wa Miradi na utunishaji mfuko wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mch. Samwueli Mshana ambaye pia alimwakilisha Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania Ndg. Alfred Elias Kimonge, alisema lengo la Chama cha Biblia ni kutafsiri Biblia kwa lugha za asili,  kukuza na kutunza lugha ya asili  lakini pia kusaidia jamii husika kusoma na  kuelewa Neno la Mungu.  

Mch. Mshana akiendelea kuongea na wahitimu
Mch. Mshana akiwa anatoa pongezi na wosia kwa wahitimu

Meneja wa miradi na utunishaji mfuko wa Chama cha Biblia cha Tanzania Mch. Samwueli Mshana akiwapongeza wahitimu wa mahafali ya pili.

 Katibu wa idara ya mamaendeleo ya Akina Mama UMAKI Josephine Semwenda katika Dayosisi ya Morogoro ambaye alialikwa kuwatia moyo wahitimu hao aliwasisitizia wahitimu kutokuogopa kuitangaza lugha ya Chikagulu kila mahali katika eneo lao la ukaguruni na kuwahimiza kuwa mabalozi wema katika kuilinda lugha yao isipotee, alitumia nafasi hiyo pia kuwapongeza. wahitimu wote na kuwatakia kila lakheri katika kutekeleza majukumu ya kijamii na Kanisa.

Mwenyekiti wa UMAKI akiongea na wahitimu
Mh. Josephine akizungumza na wahitimu

Katibu wa UMAKI Ndg. Josephine Semwenda akitoa wosia wake kwa wahitimu kuzidi kutia juhudi katika kuwafundisha wengine hususani neno la Mungu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nguyami Mh.Gilbert Ngiga ambaye alitembea umbali mrefu kuja kushuhudia mahafali hayo alisema wao katika kijiji chao tayari wameshamchukua moja kati ya wahitimu hawa anayeitwa Rehema Penford na kumuweka katika kamati ya maendeleo ya kijiji, na wataendelea kufanya hivyo ili kuwahamasisha wengine kujiunga na mpango huu mzuri.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nguyani Mh. Gilbert akitoa wosia kwa wahitimu
Mwenyekiti huyo wa kijiji cha Nguyani Mh. Gilbert Ngiga alitoa shukurani zake nyingi kwa Chama cha Biblia chaTanzania kwa juhudi wanazozifanya kuwafikia watu mbalimbaliu.

Katika mahafali hiyo kulikuwa na vikundi mbalimbali vya nyimbo, ngonjera, mashairi, maigizo, na kusoma hadithi kutoka katika kitabu cha Chibweda mbele ya mgeni rasmi.

Wahitimu kwa pamoja wakiimba nyiombo
Kikundi cha nyimbo na ngoma.
Wahitimu wakiwa wanasoma ngonjera
Kikundi cha wahitimu wakisoma risala.
igizo magubike CHIBWEDA
Pichani, ni wahitimu wa awamu ya pili, katika igizo lao wakionyesha madhara ya kutokujua kusoma na kuandika ambapo tunaona mtoto aliyelala hapo chini alipoteza maisha baada ya mama yake kumpa dawa kinyume na maelekezo aliyopewa na daktari. Hii ni kwa sababu mama yake alipopewa taarifa na wenzake kwenda kujiunga na darasa la CHIBWEDA hakuwa tayari kujiunga na elimu ya watu wazima ambayo hutolewa bure na Chama cha Biblia cha Tanzania na kusababisha kifo cha mwanae kwa uzembe.

Katika mahafari hayo yaliyofanyika kanisani  Anglikana Magubike na mwenyeji wetu Kasisi Elkana Chogohe wa kanisa hilo. Alitoa shukurani zake kwa wahitimu na waanzilishi wa mafunzo kutoka Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kwa watu wazima waeneo hili la wakagulu.

Kasisi Elkana Mch wa kanisa la Anglikana akiwapongeza wahitimu wa awamu ya pili
Kasisi Elkana Chogohe  wa kanisa la Anglikana Magubike akitoa shukurani zake kwa wahitimu na waanzilishi wa mafunzo kutoka Chama cha Biblia cha Tanzaniakwa kwa watu wazima waeneo hili la wakagulu.
× How can I help you?