Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.

Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni

“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”


Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.


UZINDUZI WA KITABU CHA KWANZA NA CHA PILI CHA SAMWELI KWA LUGHA YA CHASU
UZINDUZI WA KITABU CHA KWANZA NA CHA PILI CHA SAMWELI KWA LUGHA YA CHASUKanisa la KKKT Usharika wa Hedalu, Dayosisi ya Pare - 20 Oktoba 2024Wapendwa waalikwa walikusanyika leo kwa tukio la kihistoria la uzinduzi wa kitabu cha Kwanza na cha Pili cha Samweli...

Uzinduzi wa sehemu ya Biblia za vitabu vya 2 Samweli, Ruthi, na Yona kwa lugha ya Kinyamwezi.
Uzinduzi wa tafsiri ya Biblia za vitabu vya 2 Samweli, Ruthi, na Yona kwa lugha ya Kinyamwezi umefanyika katika kanisa la Moraviani, Parishi ya Ipole, wilayani Skonge, mkoa wa Tabora. Tukio hili limeongozwa na Katibu wa Kanisa wa Wilaya ya Skonge, Mchungaji Jackson...

Uzinduzi wa Mpango wa kuwafikia wanafunzi kupitia Biblia Inayoongea
Umoja wa Kujisomea Biblia Tanzania (Scripture Union Tanzania), kwa kushirikiana na Chama cha Biblia cha Tanzania na Talking Bible International, wamezindua rasmi mpango wa kuwafikia watoto mashuleni kwa kupitia Biblia Inayoongea. Uzinduzi huu ulifanyika tarehe 07...

Mkutano Mkuu (AGM) 2023
Katika zama ambazo habari potofu kuhusu Neno la Mungu zimeenea, ni muhimu kusoma Biblia zenye nembo ya Chama cha Biblia cha Tanzania. Hii inahakikisha uhalisi na ufuasi wa mafundisho ya kweli ya Biblia.Wakati wa mkutano huo uliofanyika Mei 17, 2024, Askofu Mark...
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.

Donate Today or Get Involved