Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.

Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni

“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”


Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.


CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA NA PROGRAMU YA BIBLIA MAGEREZANI
CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA NA PROGRAMU YA BIBLIA MAGEREZANI ZIARA KATIKA MAGEREZA YA MSALATO NA KONGWA DODOMA Moja kati ya wajibu muhimu kwa Chama cha Biblia cha Tanzania ni kuhakikisha kuwa watu wote wanapata fursa ya kupata maandiko matakatifu. Kutokana na...

Uzinduzi wa Biblia ya Kisukuma
Hatimaye Biblia ya Kisukuma yazinduliwa kwa kishindo mkoani Mwanza. Na Felix Jones Uzinduzi wa Biblia ya Kisukuma umefanyika katika Kanisa Kuu AIC Makongoro Mwanza na kuudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Umoja wa Makanisa mkoa wa Mwanza. Akizungumza katika hafla hiyo...

Uzinduzi wa Biblia ya Kisukuma
Tunakualika Karibu Ushiriki nasi katika Uzinduzi wa Biblia ya Kisukuma Jumapili, Juni 27, 2021 Mahali: KANISA LA AIC MISSION MAKONGOLO – MWANZA Saa 08:00 Mchana – 12:00 Jioni Tukio la bure kabisa Imetafsiriwa na Chama cha Biblia cha Tanzania Jinunulie Biblia yako...

Kuhamasisha Makanisa
Kazi ya kuamasisha makanisa na viongozi wa dini katika madhehebu mbali mbali ya Kikristo hapa nchini juu ya umuhimu wa kuwapatia watoto, vijana na wafungwa Neno la Mungu (Biblia), inaendelea katika Kanda ya kaskazini. Na leo wajumbe wa Bodi wa Chama cha Biblia cha...
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.

Donate Today or Get Involved