Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.
Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”
Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.
SEMINA YA UPONYAJI YA VIDONDA VYA NAFSI (TRAUMA HEALING) ILIYOFANYIKA WILAYANI MAGU MKOANI MWANZA
Picha hizi zinaonyesha jinsi Wawezeshaji wa Uponyaji wa vidonda vya Nafsi wa kutoka Mkoa wa Mara walivyokuwa na Furaha kubwa, mara baada ya kumaliza semina yao ya kutiwa moyo juu ya kazi yao ngumu ya uponyaji wa vidonda vya nafsi.Semina hii ilifanyika huko Magu Mkoani...
Kifahamu Chama Cha Biblia cha Tanzania (CBT).
CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MAANDIKO MATAKATIFU KATIKA LUGHA INAYOELEWEKA VIZURI NA KWA BEI WANAYOIMUDU 1.Chama cha Biblia cha Tanzania ni nini? Chama cha Biblia cha Tanzania ni Shirika la Kikristo lisilo la Kidhehebu...
CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA NA PROGRAMU YA BIBLIA MAGEREZANI
ZIARA KATIKA MAGEREZA YA MSALATO NA KONGWA DODOMA Moja kati ya wajibu muhimu kwa Chama cha Biblia cha Tanzania ni kuhakikisha kuwa watu wote wanapata fursa ya kupata maandiko matakatifu. Kutokana na jukukumu hilo tarehe 27/11/2018 watumishi wa Idara ya Mahusiano na...
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.
Donate Today or Get Involved