by The Bible Society of Tanzania | Apr 24, 2019 | News
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Biblia wa mwaka 2018 uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa kuu la Kiinjili la Kirutheli Dayosisi ya Dodoma tarehe 12/4/2019.
MATUKIO KATIKA PICHA.

Viongozi wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania wakijadiliana mambo mbalimbali kabla ya kuingia kwenye mkutano.

Watumishi wa Chama Cha Biblia Ndugu Choyo Sabanja(katikati)na Neema Mathayo (Kushoto) wakiandikisha wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka 2018.

Jaji mkuu Mstaafu wa Tanzania Mh.Augustino Ramadhani(katikati),Rev.Martina Kabisama(kulia) na Rev.Victoria Ntenga ambao ni wajumbe wa Bodi ya Chama Cha Biblia Cha Tanzania wakipitia Ajenda za Mkutano mkuu wa Chama.

Wajumbe wa Bodi ya Chama Cha Biblia Cha Tanzania Prof. Godfrey Majule (Kushoto), Prof. Godson Maanga na Askofu Amos Muagachi wakipitia kwa makini agenda za mkutano mkuu wa Chama Cha Biblia uliofanyika tarehe 12/4/2019 Dodoma.

Mjumbe wa Mkutano mkuu kutoka Mwanza Muinjilisti Sifaeli Mgema akichangia mada kwenye mkutano mkuu wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania.

Mjumbe wa Mkutano mkuu kutoka Kigoma Fidelis Mbiha akichangia mada kwenye mkutano mkuu wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania

Viongozi wakuu wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania Mwenyekiti wa Bodi Rt Rev. Mark Marekana(wa pili kutoka kulia),Makamu Mwenyekiti Rev.Dr.Jackson Nyanda,Katibu mkuu Alfred E.Kimonge (wa pili kushoto)na Mhazini Fr.Chesco P.Msaga wakijibu hoja za wajumbe kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka 2018 uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa kuu la Kiinjili la Kirutheli jijini Dodoma.

Mhazini mkuu wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania Fr. Chesco P. Msaga akisoma taarifa ya fedha kwenye mkutano mkuu wa mwaka 2018.

Mchungaji Salum Isaka kutoka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu akielezea jinsi Mradi wa Uponyaji wa Vidonda vya nafsi unavyowanufaisha wakimbizi kukabiliana na vidonda vya nafsi. Katika Mkutano Mkuu huo wa Mwaka 2018.

Askofu Amos Muagachi akielezea taarifa ya uhamasishaji wa wanachama wapya wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania kwenye mkutano mkuu wa mwaka 2018 uliofanyika terehe 12/4/2019.

Wanawake wa Kikagulu kutoka Gairo wakisoma kitabu cha CHIBWEDA kilichoandikwa kwa Lugha ya Kikagulu. Wakati Mkutano Mkuu wa Mwaka 2018.

Wanawake wa Kigagulu kutoka Gairo wakisoma kitabu cha CHIBWEDA kilichoandikwa kwa Lugha yao wakiwa pamoja na Mratibu wa mpango wa wanawake kusoma na kuandika(LITERACY FOR WOMEN IN AFRICA) Ndugu Frank makala(kushoto). Wakati Mkutano Mkuu wa Mwaka 2018.

Meneja Shughuli Mchungaji John Mnong’one (kushoto) na mratibu wa miradi ya LITERACY na TRAUMA HEALING Ndugu Frank Makalla (katikati) wakifutilia yanayoendelea kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka 2018.

Picha ya pamoja ya viongozi wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma waliojiandikisha kuwa wanachama wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania.

Picha ya pamoja ya wakurugenzi wa Bodi na Menejimenti ya Chama Cha Biblia Cha Tanzania.

Picha ya pamoja ya watumishi na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Biblia wa mwaka 2018 uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa kuu la Kiinjili la Kirutheli Dayosisi ya Dodoma tarehe 12/4/2019.
by The Bible Society of Tanzania | Apr 2, 2019 | News, UpComingEvent
Chama cha Biblia cha Tanzania kupitia uongozi wake, kinawatangazia na kuwakaribisha wanachama wake wote wakiwemo wakurugenzi wa Bodi wa chama, wafanyakazi, na wadhamini wake kuhudhuria mkutano mkuu wa mwaka 2018 wa kupokea taarifa ya mwaka uliopita na kupanga mipango ya mwaka huu. Mkutano utafanyika tarehe 12/4/2019 katika ukumbi wa Kanisa la Lutheran Dodoma mjini kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Wanachama wote wanakaribishwa kushiriki ili kufanikisha malengo ya mkutano wetu.
(more…)
by The Bible Society of Tanzania | Apr 2, 2019 | Literacy News, News

ONGERA: Wakakugulu kwa kuhitimu Mafunzo ya kusoma na kuandika.
Chama cha Biblia cha Tanzania, kimeanzisha utekelezaji wa mradi wa kujifunza kusoma na kuandika kwa watu wazima kwa lugha ya kikagulu na kiswahili waliokosa fursa hiyo kutokana na sababu mbalimbali, katika vijiji 30 vya wilaya ya Gairo mkoni Morogoro ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za serikali kupambana na adui ujinga.
Akizungumza kwenye mahafali ya kwanza yaliyojumuisha wahitimu 97 wa elimu ya watu wazima yaliyofanyika katika kijiji cha Berega wilyanai hapa

Mratibu wa Mradi, Mwl. Frank Makala (Kulia) akitoa taarifa fupi ya mradi mbele ya katibu mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania.
Mratibu wa mradi huo Frank Makala, alisema kuwa lengo ni kuwasaidia kujua kusoma na kuandika wote waliokosa fursa hiyo hapo awali.
Alisema kuwa wahitimu hao 97, ni sehemu ya 120 ambao ndiyo wajiiandkisha kujiunga na elimu ya watu wazima ya kusoma na kuanadika mwezi Septemba mwaka jana ambao wachache kati yao walishindwa kufika mwisho kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo hali ya kiuchumi.
“Hawa wahitimu wanaomaliza leo ni kutoka katika vijiji 10, ambavyo ndivyo tulianza navyo katika mradi kama awamu ya kwanza na leo 97 wameza kuhitimu na wote wanajua kusoma na kuandika wengine wachache wamekosa kufika siku ya leo kutokana na hali za kiuchumi kwani wengine walilazimika kwenda kwenye shughuli zao za kilimo ili kujitafuatia riziki”alisema Makala.
Makala aliongeza kuwa mradi huo wa kusoma na kuandika unatoa mafunzo kwa kutumia lugha na kiswahili na kikagulu ili kuweza kuwawezesha wanafunzi kuelewa kwa wepesi.
“Tunatumia lugha mama ya kikagulu na kiswahili katika kufundisha na hii imetusaidia sana kuweza kuwafundisha wanafunzi hawa ambao ni watu waziama na wengi wao walikuja hawajui lolote kwenye upande wa kusoma, lakini kwa kipindi cha miezi sita kila mmoja anajua kusona na kuandika kwa lugha yake ya kuzaliwa ambayo ni kikagulu lakini pia wakati huohuo na kiswahili”alisema.
Alifafnua kuwa madarasa mengine katika awamu ya pili yanatarajia kuanza mwezi Aprili mwaka huu ambapo vijiji vingine 10 vitahusishwa na baadaye mwezi mei vijiji vingine 10 na watarajia hadi ifikapo Novemba 2019 kuwa na jumla ya vijiji 30, ambavyo vimefikiwa na mradi huo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Askofu wa kanisa Agrikan Tanzania Dayosisi ya Morogoro, Canon Isack Mgego akizungumza katika mahafali hayo alisema wao kama kanisa wanajisikia faraja kuwa sehemu ya kuwawezesha watanzania katika kupambana na adui ujinga.

Mgeni Rasmi Canon Isaac Mgego akihutubia wakati wa sherehe hiyo
“Adui ujinga ni moja kati ya maadui ambao taifa letu linapambana nao na sisi kama kanisa tunayofuraha leo kuwezesha watu kujua kusoma na kuandika ili waweze kuondokana na umaskini ambao umekuwa ukiwakabili”alisema Mgego
.Naye mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo Saraha Robert, alisema kuwa anashikuru mradi huo kutoka Chama cha Biblia Tanzania kutokana na kumwezesha kujua kusoma na kuanadika na atoa rai kwa wengine kujitokeza katika kushiriki katika madarasa yanayofuata.
“Mimi nilikuwa sijui kabisa kusoma lakini kufunshishwa kusoma na kuandika kwa kutumia lugha yangu mama kuniwezesha kujua kwa haraka zaidi, na sasa nitaweza kusoma magazate,vipimo vya afya lakini pia matumizi ya dawa ninayoandikiwa hospitalini” alisema.
Matukio katika Picha

Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia akicheza na wanakisomo wakati wa mapokezi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Canon Boniface Mkami, Mwl. Ngobei, Mzee wa Kanisa, Mratibu wa Mradi Mwl. Frank Makalla kutoka Chama cha Biblia cha Tanzani. Wakisalimia

Utambulisho: Diwani wa Kata ya Berega Gairo Morogoro

Wahitimu wakishangilia kwa Furaha

Wanakisomo wakisoma Risala Mbele ya Mgeni rasmi

Katibu Mkuu wa CBT, akitoa maelezo mafupi kuhusu mradi wa Elimu ya watu wazima kwa wakina mama wa Kikaguru.

Mmoja wa wahitimu akipokea cheti wakati wa sherehe hiyo.
by The Bible Society of Tanzania | Mar 29, 2019 | Literacy News, News
Under Literacy Women in Africa Program (LWA) Adult Villagers in Berega Gairo Morogoro Tanzania given another chance to learn how to read and write.

CONGRATULATION: Photo that include the graduates, the guest of honor and the General Secretary of the Bible Society of Tanzania and other guests that were invited.
ADULT villagers in Gairo District in Morogoro Region who missed the formal primary education have another chance to learn how to read and write, thanks to the Bible Society of Tanzania. The society in collaboration with the Bible Society of Finland has initiated a programme to enable the villagers, especially women, to learn to read and write in their own language in Kaguru.

Graduate students playing and dancing with great joyful during their graduation.
Reading out a statement on behalf of fellow students, Buitisi Lirni thanked the Bible Society for the efforts that have made them achieve the goal.

Bi. Buitisi Lirni, Reading out a statement on behalf of fellow students.
She said now they can easily read the bible and other literature in Kaguru language and Kiswahili. “We missed this opportunity at early stages in life due to various but we can now read and write through the support of the Bible Society of Tanzania” she said.
She said through the programme they can now read the bible and other publications, noting that the programme has helped expand their horizon.
Speaking at the meeting the General Secretary of the Bible Society of Tanzania, Mr. Alfred Kimonge the programme undertaken through cooperation with Bible Society of Finland was to help women, especially those in the villages to read and write.

The General Secretary of the Bible Society of Tanzania, Mr. Alfred Kimonge (Standing) speaking during the Graduation.
He said women have shown great strength in fostering cooperation in any society and helped bring the desired changes, thus it was prudent to empower them to read the bible and other literatures.
Mr. Kimonge also observed that the church has a role to play in transforming the society, adding the program is in line with the government’s efforts to provide basic education to all Tanzanians. The General Secretary stated that Tanzania is among the five countries (Tanzania, Kenya, Malawi, Ethiopia and Namibia) globally that benefit from the program aimed at providing basic Learning skills using the respective people’s mother tongue.
“I am impressed by what I have seen here, now that you are able to write and read out your own statement, this is a clear indication the program has opened opportunity for to read more” he said.
He said bible translation in Kaguru language will be out soon, thus they will be able to read the word of God by themselves in their own language.
Also, Mr. Frank Makalla he said, these teachers are expected to start training new students on April 8, 2019 in those particular villages.
But also there will be training for other new twenty teachers, from ten other villages. From there they will start to register a new illiterate people (Women) and those students will begin their training on June 2019 at Berega Village.

Mr. Frank Makalla (Right) who is program coordinator speaking during the Graduation ceremony.
Guest of honor at the event, Canon Isaac Mgego noted that it was great honor to have people learn in their native language, that they understand most

Canon Isaac Mgego speaking during the graduation.
He said through the program, Kaguru tribe that was at the verge of extinction will now have its rightful honor once again. ”Please public more books in Kaguru language to help maintain our heritage as well as helping young generation to learn the language” he said.
However, he cautioned that using mother tongue should be used to help foster development instead of causing discrimination and division among them.

One of the graduates receiving certificate from the guest of honor.
by The Bible Society of Tanzania | Mar 22, 2019 | News, UpComingEvent

On Saturday, March 23rd, 2019 at Berega Morogoro, will be the graduates of literacy training and the training supervisor is Mwl. Frank Makalla and the guest will be the General Secretary of the Bible Society of Tanzania who is Ndg. Alfred Kimonge. We welcome you all.