Adult villagers in Gairo given another chance to learn how to read, write.

Adult villagers in Gairo given another chance to learn how to read, write.

Under Literacy Women in Africa Program (LWA) Adult Villagers in Berega Gairo Morogoro Tanzania given another chance to learn how to read and write.

1 Berega

CONGRATULATION: Photo that include the graduates, the guest of honor and the General Secretary of the Bible Society of Tanzania and other guests that were invited.

ADULT villagers in Gairo District in Morogoro Region who missed the formal primary education have another chance to learn how to read and write, thanks to the Bible Society of Tanzania. The society in collaboration with the Bible Society of Finland has initiated a programme to enable the villagers, especially women, to learn to read and write in their own language in Kaguru.

9 Berega

Graduate students playing and dancing with great joyful during their graduation.

Reading out a statement on behalf of fellow students, Buitisi Lirni thanked the Bible Society for the efforts that have made them achieve the goal.

8 Berega 1

Bi. Buitisi Lirni, Reading out a statement on behalf of fellow students.

She said now they can easily read the bible and other literature in Kaguru language and Kiswahili. “We missed this opportunity at early stages in life due to various but we can now read and write through the support of the Bible Society of Tanzania” she said.

She said through the programme they can now read the bible and other publications, noting that the programme has helped expand their horizon.

Speaking at the meeting the General Secretary of the Bible Society of Tanzania, Mr. Alfred Kimonge the programme undertaken through cooperation with Bible Society of Finland was to help women, especially those in the villages to read and write.

3 Berega 1

The General Secretary of the Bible Society of Tanzania, Mr. Alfred Kimonge (Standing) speaking during the Graduation.

He said women have shown great strength in fostering cooperation in any society and helped bring the desired changes, thus it was prudent to empower them to read the bible and other literatures.

Mr. Kimonge also observed that the church has a role to play in transforming the society, adding the program is in line with the government’s efforts to provide basic education to all Tanzanians. The General Secretary stated that Tanzania is among the five countries (Tanzania, Kenya, Malawi, Ethiopia and Namibia) globally that benefit from the program aimed at providing basic Learning skills using the respective people’s mother tongue.

“I am impressed by what I have seen here, now that you are able to write and read out your own statement, this is a clear indication the program has opened opportunity for to read more” he said.

He said bible translation in Kaguru language will be out soon, thus they will be able to read the word of God by themselves in their own language.

Also, Mr. Frank Makalla he said, these teachers are expected to start training new students on April 8, 2019 in those particular villages.

But also there will be training for other new twenty teachers, from ten other villages. From there they will start to register a new illiterate people (Women) and those students will begin their training on June 2019 at Berega Village.

4 Berega

Mr. Frank Makalla (Right) who is program coordinator speaking during the Graduation ceremony.

Guest of honor at the event, Canon Isaac Mgego noted that it was great honor to have people learn in their native language, that they understand most

5 Berega

Canon Isaac Mgego speaking during the graduation.

He said through the program, Kaguru tribe that was at the verge of extinction will now have its rightful honor once again. ”Please public more books in Kaguru language to help maintain our heritage as well as helping young generation to learn the language” he said.

However, he cautioned that using mother tongue should be used to help foster development instead of causing discrimination and division among them.

6 Berega

One of the graduates receiving certificate from the guest of honor.

Masomo ya uponyaji wa vidonda vya nafsi.

Masomo ya uponyaji wa vidonda vya nafsi.

trauma

Tunashukuru Sana kwa jinsi Chama Cha Biblia cha Tanzania kinavyojali na kuwahudumia watu mbalimbali. Pichani ni sehemu ya wakristo wa Parish ya Iringa Road KKKT. Ambao wanafundishwa masomo ya uponyaji wa vidonda vya nafsi.Masomo haya ni kwa faida yao nabaadae wawe viongozi wa wenzao katika kuanzisha na kuendeleza vikundi hivi vya uponyaji wa nafsi.

SEMINA YA UPONYAJI YA VIDONDA VYA NAFSI (TRAUMA HEALING) ILIYOFANYIKA WILAYANI MAGU MKOANI MWANZA

SEMINA YA UPONYAJI YA VIDONDA VYA NAFSI (TRAUMA HEALING) ILIYOFANYIKA WILAYANI MAGU MKOANI MWANZA

Picha hizi zinaonyesha jinsi Wawezeshaji wa Uponyaji wa vidonda vya Nafsi wa kutoka Mkoa wa Mara walivyokuwa na Furaha kubwa, mara baada ya kumaliza semina yao ya kutiwa moyo juu ya kazi yao ngumu ya uponyaji wa vidonda vya nafsi.Semina hii ilifanyika huko Magu Mkoani Mwanza kati ya tarehe 03/12/2018 na tarehe 06/12/2018.

2

Picha ya pamoja ya washiriki wa semina ya Uponyaji wa vidonda vya nafsi(TRAUMA HEALING) iliyofanyika wilayani Magu Mkoani Mwanza

6Washiriki wakiwa katika semina ya Uponyaji wa vidonda vya nafsi(TRAUMA HEALING)

5

Mchungaji Laulence Oiso akiongoza moja mosomo ya uponyaji wa nafsi  kwa washiriki wa semina hiyo.

 

Kifahamu Chama Cha Biblia cha Tanzania (CBT).

Kifahamu Chama Cha Biblia cha Tanzania (CBT).

CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA

Mzee Daudi reading

KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MAANDIKO MATAKATIFU KATIKA LUGHA INAYOELEWEKA VIZURI NA KWA BEI WANAYOIMUDU

1.Chama cha Biblia cha Tanzania ni nini?IMG 20181026 163614

Chama cha Biblia cha Tanzania ni Shirika la Kikristo lisilo la Kidhehebu lililoandikishwa mwaka 1965  chini ya Sheria ya Udhamini wa Vyama.

Chama cha Biblia cha Tanzania ni Mshiriki wa Muungano wa Vyama vya Biblia ulimwenguni ( United Bible Societies –UBS ) ambao kazi yake kubwa ni uenezaji wa Neno la Mungu kwa wingi na uhakika kama ifuatavyo:

–       Kueneza Neno la Mungu katika Lugha na Mawasiliano yanayokidhi mahitaji ya watu wengi Ulimwenguni.

–       Kueneza Neno la Mungu katika Tafsiri sahihi bila kupoteza uhalisi wa Maandiko Matakatifu.

–       Kuyauza Maandiko kwa bei wanayoimudi ili waweze kulifahamu Neno la Mungu.

  1. Kaziya Chama cha Biblia  ilianza lini Tanzania?

 20160917 160152( i ) Wamisionari wa kwanza kabisa nchini Tanganyika ndio walioanzisha kazi ya Chama kwenye karne ya 19.

 ( ii ) Kazi ya  kueneza  Biblia  iliendelea kukua na mwaka 1982 Chama kilifikia ngazi ya kuwa Mshiriki wa Muungano wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni na mwaka 1988 Chama kilipata uanachama kamili wa Muunganohuu.

3.Je kazi za Chama cha Biblia cha Tanzania ni zipi?

Chama cha Biblia cha Tanzania ni chombo cha Kanisa kinachotumika katika kutekeleza utume wa Kanisa  wa kuihubiri Injili kwa kila mtu.  Chama cha Biblia kinafanya yafuatayo:

a ) Kutafsiri Biblia katika Lugha mbalimbali za kienyeji.

Watafsiri wa Kikagulu b ) Kuchapisha katika Mitindo mbalimbali:

      – Biblia nzima.

      – Maagano na

      – Sehemu zake kwa wasomaji wapya.

 c )Kueneza Biblia,Maagano na sehemu zake kwa watu wote kwa kushirikiana na :

      – Makanisa na Mashirika yake.

      – Maduka ya Vitabu.

      – Watu binafsi pamoja na wakereketwa wa kujitolea.

 d )Kushirikiana na Vyama vingine katika kuhakikisha Biblia inasomwa kwa lugha zote za hapa Tanzania ili kila mtu auonje uzuri wa Yesu Kristo na kupata maisha mapya.

  1. Je, hadi sasa Chama cha Biblia cha Tanzania kimetafsiri Biblia katika Lugha zipi za kienyeji ?

medium 1 Chama hadi sasa kimemudu kutafsiri Biblia nzima katika Lugha  za:  Kiiraqw, Kihaya, Kinyakyusa, Kisukuma, Kijaluo, Kimasai na Kigogo. Pia kimeweza kutafsiri Agano Jipya katika Lugha za Kibena, Kimashami, Kivunjo, Kimochi, Kichasu( Kipare ), Kijita, Kidatooga, Igikuria, Kishambala, Kizaramo, Kinyiramba na Kirimi ( Kinyaturu )     Miradi ya Tafsiri inayoendelea ni ya Lugha za Kihehe, Kikaguru, Kiha na Kisukuma cha kisasa. Mbali na kuchapisha  Biblia, pia Chama kinachapisha matoleo yafuatayo:

–       Sehemu za Biblia.

–       Sehemu za Biblia kwa wasomaji wapya wanaojifunza Biblia kwa Kiingereza, Kiswahili na Lugha za Kienyeji.

–       Vipeperushi maalum vya vifungu vya Biblia kwa matukio mbalimbali k.m kuzaliwa kwa Yesu,kifo cha Yesu,wagonjwa waliolazwa,na matukio mbalimbali k.m Uhuru, Rushwa nk.

–       Kanda naswa za Neno la Mungu.

–       Neno la Mungu katika Braille kwa wasomaji wasioona.

–       Neno la Mungu kwa maandishi makubwa kwa wenye udhaifu wa macho.

    Kwa kawaida tafsiri inafanywa  kutoka katika Lugha za asili za Kiyunani na Kiebrania,na hivyo kazi ya Tafsiri ni ngumu, inahitaji uangalifu wa hali ya juu na

    inachukua miaka kati ya  8 hadi 10  kutoa toleo moja, kama kuna watafsiri walioajiriwa kwenye mradi kwa wakati wote na kuna wachambuzi 10-15.

  1. Je Chama cha Biblia kinapata  wapi fedha za kukiendesha?

    Chama cha Biblia cha Tanzania kinaendeshwa kwa michango ya

–       Makanisa.

–       Taasisi mbalimbali za Makanisa.

–       Watu binafsi ambao ni wanachama.

–       Marafiki wa Chama.

–       Muungano wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni ambao unatoa misaada ya Maandiko Matakatifu kutoka nje ambayo Chama kinayauza na kutumia sehemu ya mapato kuendesha huduma.

  1. Je Chama cha Biblia cha Tanzania kina mahitaji gani?

    Ili kutekeleza kazi zake za Kutafsiri, Kuchapisha na Kueneza Maandiko Matakatifu Chama cha Biblia chaTanzania kinahitaji kiasi kisichopungua  Dola Milioni moja za Marekani kwa mwaka.  Kama Kanisa na Wakristo binafsi watakuwa wanachangia kila mwaka  kwa uaminifu Chama kinaweza kuendesha kazi zake vizuri.

  1. Je, unawezaje kusaidia kazi za Chama cha Biblia ?

  DSC 6345 1  Kuna njia nyingi za kukisaidia Chama cha Biblia katika kazi zake na kinamualika kila Mkristo kushiriki yafuatayo:-

  ( i )Kujiunga na kuwa Mwanachama na kuchangia

      – Uanachama wa Maisha Mme na Mke shilingi 15,000= na ahadi isiyopungua shilingi 15,000=kwa mwaka.

      – Uanachama wa Maisha mtu mmoja shilingi 10,000= na ahadi isiyopungua shilingi 10,000= kwa mwaka.

      – Uanachama wa kawaida (bidii ) shilingi 5,000=kwa mwaka.

      – Uanachama wa kawaida kwa Wanafunzi wa Sekondari na Vyuo shilingi 2,000= au zaidi kwa mwaka.

      – Uanachama wa kawaida wa kushirikishwa kwa watoto na wanafunzi wa shule za Msingi shilingi 1,000= au zaidi kwa mwaka.

      – Uanachama wa Mashirika shilingi 50,000= na mchango usiopungua shilingi 50,000= kwa mwaka.

      – Mwanachama wa Biblia Moja kwa Mwezi ( Bible a Month Club) 5,000=, 10,000=, 15,000=, 20,000= au zaidi kwa mwezi.

 (ii )Tafsiri.

      Unaweza kusaidia Chama kwa :

–  Kuchangia Miradi ya Tafsiri kwa kutoa fedha taslimu.

–  Kuchangia Miradi ya Tafsiri kwa kuwapata Watafsiri wenye uwezo na Wachambuzi wenye mzigo na kazi hii.

– Kuchangia Miradi ya Tafsiri kwa kupitia Miswada ya Tafsiri.

(iii ) Uhamasishaji.

      -Kutoa sadaka au michango kila mara kwa Chama.

      – Kuhamasisha Makanisani juu ya Wiki ya Biblia ambayo ni kila wiki ya kwanza ya  Mwezi Novemba kila mwaka.

      – Kuanzisha Vikundi vya Biblia Moja kwa Mwezi ( Bible a Month Club-BAMC ) kwenye Makanisa na maeneo ya kazi.

      – Kusaidia kueneza Biblia kwa njia ya kuuza kwa kujitolea.

      – Kutoa njia mbadala au mawazo ya jinsi ya kutunisha Mfuko wa Chama ukishrikiana na Chama au kwa niaba ya Chama.

(iv ) Maombi.

     Ungana nasi katika kukiombea Chama.

( v ) Kujitolea.

     Unaweza kukisaidia Chama kwa kutoa muda wako na ujuzi wako wakati wowote kukisaidia Chama katika azma ya Kutafsiri, Kuchapisha, Kueneza na  katika kuhamasisha watu kutoa  kumfidia msomsji apate Biblia kwa bei nafuu.

  1. Kwanini Chama cha Biblia cha Tanzania kinatoa Maandiko Matakatifu bure kwa baadhi ya watu au vikundi ?

  18 2 Chama kinatoa Maandiko Matakatifu bure kwa baadhi ya watu wasio na uwezo wa kifedha kumudu kujinunulia,na vile vile ili kukidhi uhitaji wa Maandiko kwa

   Watanzania  walio wengi kinalazimika kuyauza kwa bei nafuu wanayoimudu ambayo iko chini ya ilyopangwa kuuzia.

  1. Wito wa Chama kwa Wakristo

    Chama kinatoa wito kwa Wakristo wote mmoja mmoja na Makanisa yote kujiunga na kuwa mwanachama wa Chama cha Biblia na kuchangia Chama

    fedha ,mawazo  nguvukazi na maombi ili kukiwezesha  kuendesha kazi zake za Kutafsiri,Kuchapisha na Kueneza Maandiko Matakatifu kwa watu wote

   Tanzania.