Chama cha Biblia cha Tanzania, kimeanzisha utekelezaji wa mradi wa kujifunza kusoma na kuandika kwa watu wazima kwa lugha ya kikagulu na kiswahili waliokosa fursa hiyo kutokana na sababu mbalimbali, katika vijiji 30 vya wilaya ya Gairo mkoni Morogoro ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za serikali kupambana na adui ujinga.
Akizungumza kwenye mahafali ya kwanza yaliyojumuisha wahitimu 97 wa elimu ya watu wazima yaliyofanyika katika kijiji cha Berega wilyanai hapa
Mratibu wa mradi huo Frank Makala, alisema kuwa lengo ni kuwasaidia kujua kusoma na kuandika wote waliokosa fursa hiyo hapo awali.
Alisema kuwa wahitimu hao 97, ni sehemu ya 120 ambao ndiyo wajiiandkisha kujiunga na elimu ya watu wazima ya kusoma na kuanadika mwezi Septemba mwaka jana ambao wachache kati yao walishindwa kufika mwisho kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo hali ya kiuchumi.
“Hawa wahitimu wanaomaliza leo ni kutoka katika vijiji 10, ambavyo ndivyo tulianza navyo katika mradi kama awamu ya kwanza na leo 97 wameza kuhitimu na wote wanajua kusoma na kuandika wengine wachache wamekosa kufika siku ya leo kutokana na hali za kiuchumi kwani wengine walilazimika kwenda kwenye shughuli zao za kilimo ili kujitafuatia riziki”alisema Makala.
Makala aliongeza kuwa mradi huo wa kusoma na kuandika unatoa mafunzo kwa kutumia lugha na kiswahili na kikagulu ili kuweza kuwawezesha wanafunzi kuelewa kwa wepesi.
“Tunatumia lugha mama ya kikagulu na kiswahili katika kufundisha na hii imetusaidia sana kuweza kuwafundisha wanafunzi hawa ambao ni watu waziama na wengi wao walikuja hawajui lolote kwenye upande wa kusoma, lakini kwa kipindi cha miezi sita kila mmoja anajua kusona na kuandika kwa lugha yake ya kuzaliwa ambayo ni kikagulu lakini pia wakati huohuo na kiswahili”alisema.
Alifafnua kuwa madarasa mengine katika awamu ya pili yanatarajia kuanza mwezi Aprili mwaka huu ambapo vijiji vingine 10 vitahusishwa na baadaye mwezi mei vijiji vingine 10 na watarajia hadi ifikapo Novemba 2019 kuwa na jumla ya vijiji 30, ambavyo vimefikiwa na mradi huo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Askofu wa kanisa Agrikan Tanzania Dayosisi ya Morogoro, Canon Isack Mgego akizungumza katika mahafali hayo alisema wao kama kanisa wanajisikia faraja kuwa sehemu ya kuwawezesha watanzania katika kupambana na adui ujinga.
“Adui ujinga ni moja kati ya maadui ambao taifa letu linapambana nao na sisi kama kanisa tunayofuraha leo kuwezesha watu kujua kusoma na kuandika ili waweze kuondokana na umaskini ambao umekuwa ukiwakabili”alisema Mgego
.Naye mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo Saraha Robert, alisema kuwa anashikuru mradi huo kutoka Chama cha Biblia Tanzania kutokana na kumwezesha kujua kusoma na kuanadika na atoa rai kwa wengine kujitokeza katika kushiriki katika madarasa yanayofuata.
“Mimi nilikuwa sijui kabisa kusoma lakini kufunshishwa kusoma na kuandika kwa kutumia lugha yangu mama kuniwezesha kujua kwa haraka zaidi, na sasa nitaweza kusoma magazate,vipimo vya afya lakini pia matumizi ya dawa ninayoandikiwa hospitalini” alisema.
Matukio katika Picha