Na. Ndugu Frank Makalla (Msimamizi Mkuu wa Mradi-CBT).
Chama Cha Biblia Cha Tanzania kilianzisha kisomo cha elimu ya watu wazima kwa kushirikiana na Chama Cha Biblia Cha Finland na SIL (Summer Institute of linguistic) mnamo mwaka 2017 na mwaka huo ulikuwa ni mwaka wa kuandaa vitabu kwa ajili ya wanakisomo wa elimu ya watu wazima katika msemo wa Kikagulu na kanisa katika eneo hilo lilishiriki kikamilifu kwa kutoa watafsiri na waandishi. Ndipo mradi ukaanza 2018 ukiwa na walimu 20 (ishirini). Walimu hao walianza na wanafunzi mia ishirini ambavyo wanafunzi 97 walihitimu na kupewa vyeti mwezi machi 2019.
Na baada ya hapo Madarasa ya kujifunza kusoma na kuandika yalianza mwezi wa nane 2019 katika vijiji 20 (ishirini) vingine na kila kijiji kina darasa moja na kila darasa lina walimu wawili 2 (wawili) na jumla ya wanafunzi ni 423 kwa vijiji vyote.
Madarasa hayo ishirini yanaendelea vizuri katika kiwango cha 97% (asilimia tisini na saba) wanaweza kusoma na kuandika. Tunatarajia watahitimu mwisho wa mwezi huu wa February 2020 na mahafali yatakuwa mwezi wa tatu kuanzia tarehe 14/03/2020 (kumi na nne), 21/03/2020 (ishirini na moja) na 28/03/2020 (ishirini na nane) kwa maana yamegawanywa kwenye vituo vitatu ambavyo ni Gairo, Nguyami na Magubike.
Darasa la Chibweda kijiji cha Kibedya
Mwalimu Devotha Madihi wa darasa la Chibweda kijiji cha Kibedya akifundisha darasani. Darasa hili lina mama mmoja mwenye watoto mapacha wanaonekana hapo chini na amekuwa akihudhulia vizuri sana darasani.
Darasa la Chibweda Kijiji cha Berega
Wanakisomo wa darasa la Kikagulu katika Kijiji cha Berega wanajifunza kusoma na kuandika kwa kutumia lugha ya Kikaguru wakifundishwa na waalimu wao Rose Chitemo mwenye kilemba na Sofia Muhumba.
Darasa la Chibweda Kijiji cha Berega
Mwanafunzi Merina Malali wa Darasa la Chibweda Berega akiwa anaandika kufuatia maelekezo ya waalimu.
Darasa la Chibweda Kijiji cha Kiegea
Darasa la Kiegea wanafatilia mafundisho ya mwalimu ubaoni.
Darasa la Chibweda Kijiji cha Tabuhoteri
Darasa la kijiji cha Tabuhoteli lina wakina mama wenye umri mkubwa na wana bidii sana katika kujifunza kusoma na kuandika.
Darasa la Chibweda Kijiji cha Ibindo
Wanakisomo katika kijiji cha Ibindo wakipata maelekezo kutoka kwa walimu wao kuhusu kusoma na kuandika.
Kujifunza kuandika
Mwanafunzi Merina Malali wa Darasa la Chibweda (mwenye kilemba cha pink) katika kijiji cha Berega akiwa anaandika kufuatia maelekezo ya waalimu.
Wanakisomo awa, wapo katika marudio wakisubiri kupewa mitihani yao ya mwisho ili hatimaye kukabidhiwa vyeti kwa wale watakaofaulu na kuhitimu masomo yao vizuri.
CHANGAMOTO:
Kwa kuwa hawa ni watu wazima zipo changamoto mbali mbali zinazoathiri mahudhurio darasani kama vile:- kazi za shamba, misiba kijijini na nje ya kijiji, kuumwa, kuuguliwa, mito kujaa na kuwatenganisha kwa muda, kutomaliza silabasi yao kwa wakati kwa kuwa wapo wenye kujifunza kwa polepole kulingana na umri wao na kusababisha waalimu kuwa fuatilia na kuwaelekeza kwa muda zaidi. n.k.
Changamoto katika kuwafikia
Wakati mwingine kuna changamoto ya kuwafikia wanakisomo kwa sababu ya ubovu wa miundombinu hasa barabara kama picha inavyoonesha hapa chini.
Kunasua gari
Wakati mwingine kipindi cha mvua changamoto kubwa ni barabara, mfano picha hiyo hapo Gari lilikwama kwenye matope kutokana ubovu wa barabara wakati tunakwenda kuona darasa la Mtumbatu na tulisaidiwa na wanakijiji kulinasua gari kwenye matope (Ndugu Frank Makalla akieleza).
Kutokana na kikao cha mapitio ya maendeleo ya mradi wa tafsiri ya Biblia kwa Lugha ya Kirimi November 04-09, 2019, Mkoani Singida, Tafsri bingwa Dr.Samy Tioye kutoka UBS athibitisha mradi huu kuendelea vizuri na umefikia hatua nzuri zaidi kwa hali hiyo Biblia ya Lugha ya Kirimi tunaitegemea iwe imekamilika 2020 December.
Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na Kanisa tunafanya kazi ya kutafsiri Biblia kwa Lugha ya Kirimi. Kazi hii inafanyika kwa ustadi mkubwa na kuzingatia kanuni na utalaam wa tafsiri ya Biblia kutoka muungano wa vyama vya Biblia Ulimwenguni (UBS).
Kwa mantiki hiyo hapa chini katika picha tunaona Dr.Samy Tioye mmoja wa watafsiri Bingwa wa Lugha kutoka UBS akiwa na watafsiri wa Lugha ya Kirimi katika kuangalia usahihi wa kazi hii muhimu.
Kirimi team, Singida, Tanzania
Mshauri bingwa wa Tafsiri za Biblia Dr.Samy Tioye akiwa anawaonyesha aina mbalimbali za tafsiri za Biblia na namna zinavyoweza kutumika kusaidia tafsiri ya Biblia kwa Lugha ya Kirimi, Katika ofisi ya tafsiri ya Biblia kwa Lugha Kirimi Mkoani Singida.
Maelekezo
Mshauri bingwa wa Tafsiri za Biblia Dr.Samy Tioye akiwa anaelezea jambo kwa watafsiri wa Biblia kwa Lugha ya Kirimi, Katika ofisi ya tafsiri ya Biblia kwa Lugha Kirimi Mkoani Singida.
Umakini
Watafsiri wa Biblia kwa Lugha ya Kirimi (Mch. Elia Mande na Mch. Simoni Kusina) wakipitia na kufanya masahihisho ya kitabu cha Kumbukumbu la torati.
kusaiisha
Mrs. Joyce Shisha, Katibu muhutasi wa mradi wa Kirimi akiingiza masahihisho ya kitabu cha Kumbukumbu ya tarati kwenye Programu maalumu ya Tafsiri za Biblia iitwayo Paratext.
Pamoja
Picha ya pamoja kati ya Meneja wa Tafsiri, mtafsiri Bingwa pamoja na watafsiri wa Biblia kwa Lugha ya Kirimi.
Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha hata atakapo kuwa mzee. [Mithali 22:6]
Wapendwa Taifa la Mungu na wakristo wa Tanzania, malezi ni uangalizi wa karibu wa wazazi kwa mtoto wao kiroho, kiafya, kiakili, kitabia ili tuwe na Taifa imara na watu wanaomcha Mungu. Mungu alipomuumba Adamu na Hawa akasema “zaeni mkaongezeke…………[Mwanzo 1:28.]”
Ni wajibu wa wazazi katika familia na kanisani kuwahimiza watoto kulisoma na kulipenda Neno la Mungu yaani Biblia. Katika [Rum. 8:28] tunasoma: “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema……” Hii ni pamoja na kazi ya kulea watoto; Mungu hufanya kazi hiyo pamoja na sisi.
Katika [Zab. 127:3] Biblia inasema “Tazama wana ndio urithi wa BWANA uzao wa tumbo ni thawabu.” Mungu hatupi watoto ili tuwahifadhi kwa matumizi yetu wenyewe. Yeye anatupa watoto ili tuwalee kwa utukufu wake. Watoto wetu ni wa Mungu. Mungu amelithibitisha agano lake pamoja nasi, Katika [Kumb. 28:4] anasema “Utabarikiwa uzao wa tumbo lako” Pia katika [Isaya. 8:18] inasema “Angalieni, mimi na watoto hawa niliyopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israel……” Kwa sababu hii Mungu anataka watoto wetu wajifunze Neno lake na kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Mungu anatazamia wazazi wawaelekeze watoto kwake, kwa njia ya Neno lake yaani Maandiko Matakatifu (Biblia).
Walinde watoto wako na vishawishi viovu.
Ujue nia ya shetani siku zote ni kutaka kuwaangamiza watoto, iwe kiroho au hata kimwili kwa kuwavuta katika mambo ya ulimwengu. Kuna mambo kadha wa kadha ambayo watoto wanakutana nayo maishani na haya yanaweza kusababisha au kuwaondoa kabisa wasimfuate Mungu sawasawa. Neno la Mungu linasema “Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia… na dunia inapita pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”. [1Yoh. 2:15-17].
Marafiki wabaya na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yameangamiza familia nyingi na kuwapoteza watoto na vijana katika kiwango cha kutisha [Mithali 13:20] Neno la Mungu linasema “… Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.” [Zab. 1:1] inasema: “Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.”
Nawasihi na kuwaomba Wakristo wa Tanzania kusimama na Chama chenu cha Biblia kuwaridhisha watoto wetu Neno la uzima, hivyo wapatie watoto Biblia katika maisha yao. Simama na huduma ya Chama cha Biblia cha Tanzania kuwapatia watoto na vijana.
Neno la Mungu kama zawadi na baraka kutoka kwa Mungu maishani mwao.
Amani na Neema ya Mungu iwe juu yako.
Mtumishi wenu katika Kristo
Alfred Kimonge.
Katibu Mkuu
JITIHADA ZINAZOFANYWA NA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA ILI KUHAKIKISHA VIONGOZI WA MAKANISA MBALI MBALI NCHINI WANAFIKIWA NA MPANGO HUU MADHUBUTI.
Pichani toka kulia: Baba Askofu Mkuu Dr. Shoo wa Kanisa la KKKT, Msaidizi wa Askofu wa Kanisa hilo, Dayosisi ya Kaskazini Mch. Saria, Baba Askofu Amos Muhagachi Balozi wa CBT na Mjumbe wa Bodi, na Eng. Ekaeli Manase mjumbe wa Bodi ya CBT; wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea bahasha 10,000 kwa ajili ya kuchangia huduma ya Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT).
Pichani: Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania ndugu Alfred Kimonge (kushoto) na Fr. Sosthenes wa Kanisa Katoliki Dodoma baada kikao cha pamoja kilichomteua kuwa mmoja wa wawakilishi wa Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT).
Pichani: Baba Askofu Amos Muhagachi (wa tano toka kulia waliokaa) Balozi wa CBT na Mjumbe wa Bodi, akiwa na Mapadre wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Dodoma, baada ya Mkutano wa pamoja uliofanyika mjini Dodoma.
Pichani: Mtume na Nabii Josephat Mwingira (katikati ) wa Huduma ya Efatha na mkewe (kushoto) wakipokea zawadi ya Biblia kutoka kwa Baba Askofu Amos Muhagachi (kulia) Balozi wa Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT) na mjumbe wa Bodi, alipomtembelea na kufanya mazungumzo naye kuhusu mkakati wa CBT wa kuhamasisha Makanisa kuchangia upatikanaji wa Maandiko Matakatifu kwa ajili ya watoto, vijana na wafungwa hapa Tanzania.
Pichani: Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT) ndugu Alfred Kimonge (kushoto), Fr. Chesco P. Msaga (katikati) wa Kanisa Katoliki Dodoma na Baba Askofu Amos Muhagachi (kulia), Balozi wa CBT na mjumbe wa Bodi, wakiwa studio za Redio Mwangaza Dodoma akizungumza juu ya mkakati wa Chama wa kuhamasisha Makanisa na Wakristo wote kuchangia upatikanaji wa Maandiko Matakatifu kwa ajili ya watoto, vijana na wafungwa hapa Tanzania.
Unaweza usibadilishe dunia yote na kuifanya iwe ya kumpenda Mungu, lakini kwa sadaka yako ya upendo kwa Chama cha Biblia cha Tanzania ya Tsh 5000 tu! na kuendelelea unaweza kumbadilisha milele mtoto, kijana au hata mfungwa mmoja.
Tuma sadaka yako ya upendo kupitia namba ya M-PESA ya Chama: 890890 kisha tuma ujumbe wa kuchangia katika namba hizi: 0762998819, 0754383636 na 0754479789.
Pia unaweza kuchangia kupitia akaunti za Benki za DTB na NBC zilizoonyeshwa hapa chini Changia kupitia benki ya DTB: Namba ya Akaunti: 0901969001 SWIFT OR WIRING CODE DTKETZTZ na Changia kupitia benki ya NBC: Namba ya Akaunti: 029103000362 na Mungu akubariki sana.
Na Mungu akubariki sana
Askofu Amos Muhagachi
Mhariri
Mawasiliano yatumwe kwa: Katibu Mkuu Chama cha Biblia cha Tanzania, P.0. Box 175, Dodoma, Tanzania. Email: aekimonge@yahoo.com T: +255262324661 Fax: +255262324058.
KWA WANACHAMA WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA NA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA.
Umoja wetu katika Kristo!
“Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi”. (Yohana 17:21-23).
Umoja wa Kanisa ndiyo ishara ya mwili wa Kristo katika Ulimwengu. Kanisa ni familia ya Mungu katika ulimwengu huu, ni jumuiya ya watu wa Mungu wamwaminio Yesu Kristo katika maisha yao wakimsifu na kumshangilia Mungu katika ushuhuda na kuwaleta wengine ili wamjue Mungu wa kweli katika maisha yao. Chama cha Biblia cha Tanzania kimeendelea kwa uaminifu wote kulihudumia kanisa la nchi yetu kwa umoja wake kwa kuwapatia Maandiko Matakatifu [Biblia] ili kuliwezesha kanisa kuwa na Biblia katika mifumo na tafsiri mbali mbali kwa ajili ya uinjilisti na utume wake.
Kwa unyenyekevu mkuu nawaalika Wakristo wa madhehebu yote katika nchi yetu kushiriki katika huduma hii.Nakuomba ukiombee na kukichangia Chama cha Biblia cha Tanzania ili kipate fedha kwa ajili ya kutafiti, kuchapisha na kusambaza neno la Mungu kwa watu wote. Ni maombi yangu kwamba asiwepo Mtanzania hata mmoja anayetamani kulisoma neno la Mungu akalikosa kwa sababu ya gharama kubwa. Mwaka huu tuna lengo la kuwapatia watoto, vijana na wafungwa Biblia. Kwa ushirikiano wa kanisa la Mungu hapa nchini, tunaweza kuwafikia watoto, vijana na wafungwa ili kujenga Taifa la wacha Mungu. Kwa sadaka yako na matoleo yako ya upendo utakuwa baraka kwa kumpatia mtoto, kijana na mfungwa kule gerezani neno la uzima.
Nakutumia barua hii ya upendo kukualika na kukukaribisha ili ushiriki pamoja nasi kulijenga Taifa letu kiroho ili liwe taifa lenye kumhofu na kumcha Mungu. Ombea Taifa letu ili watu wake walipende na kulisoma Neno la Mungu.
Ni kiu yangu kwamba kila mtoto, kijana na mfungwa awe na Biblia yake mkononi.
Neema na Amani ya Kristo iwe pamoja nawe.
Alfred E. Kimonge
Katibu Mkuu
HAMASA YA KUFUNGUA MATAWI MIKOANI
Hawa ni Wanachama wa Tawi la Kitivo cha Sayansi ya Jamii moja ya matawi matatu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Tunamshukuru Mungu kwa kuanza mwaka huu kwa baraka zake na uamsho mpya wa Makanisa na Wakristo kujiunga kwa wingi kuwa wanachama wa Chama cha Biblia cha Tanzania. Hadi sasa tumefanikiwa kufungua matawi kama ifuatavyo;
1. Dodoma – Chuo Kikuu cha Dodoma [UDOM ]
i. Tawi la Kitivo cha Elimu – Wanachama 120
ii. Tawi la Kitivo cha Biashara na Utawala – Wanachama 78
iii. Tawi la Kitivo cha Sayansi ya Elimu ya Jamii – Wanachama 110
2. EAGT Buhemba Tarime – Wanachama 210
4. Umoja wa makanisa – Kilimanjaro
5. Marangu-Kilimanjaro
6. Umoja wa makanisa – jiji la Mwanza
Na bado hamasa inaendelea katika maeneo mengine likiwamo jiji la Dar es Salaam na Tabora.
Viongozi wa Makanisa ya Moshi ambao ni waanzilishi wa Tawi la Chama katika Mkoa wa Kilimanjaro
Mwenyekiti wa Tawi la EAGT Buhemba Tarime akimkabidhi mchango wake Askofu Muhagachi Balozi wa Chama cha Biblia cha Tanzania.
Tunakuomba ushiriki katika huduma hii kwa maombi yako,unaweza kuchangia kila mwezi Tsh 2000,______ Tsh 5000,______Tsh 10,000,_______au kuchangia kwa mwaka Tsh 25,000, ____Tsh 50,000,_____Tsh 100,000 au zaidi. Kwa sadaka yako ya upendo unaweza kumfanya/kumgusa mtoto, kijana na mfungwa kumjua na kumfuata Kristo.
Nakualika kushiriki pamoja na Wakristo wengine waaminifu kwa kuchangia na kutuma mchango wako kwa akaunti ya M-PESA ya Chama cha Biblia cha Tanzania namba 890890 kisha tuma ujumbe wa kuchangia katika namba hizi: 0762998819, 0754383636 na 0754479789.
Pia unaweza kuchangia kupitia akaunti za Benki za DTB na NBC zilizoonyeshwa hapa chini. Kwa DTB Akaunti Namba: 0901969001; SWIFT OR WIRING CODE DTKETZTZ
Kwa NBC Akaunti Namba: 029103000362
Akaunti Namba: 0901969001; SWIFT OR WIRING CODE DTKETZTZ
Akaunti Namba: 029103000362
Mungu na akubariki. Askofu Amos Muhagachi Mhariri.
Mawasiliano yatumwe kwa: Katibu Mkuu Chama cha Biblia cha Tanzania, P.0. Box 175, Dodoma, Tanzania. Email: aekimonge@yahoo.com T: +255262324661 Mob: +255754383636