Uzinduzi wa Biblia ya lugha ya Kimochi

Uzinduzi wa Biblia ya lugha ya Kimochi

Mkuu wa KKKT ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Shoo, amewataka Wakristo kuitunza na kuindeleza lugha zao za asili kwani ndio msingi na urithi walio nao.

Askofu Dkt. Shoo aliyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Biblia ya lugha ya Kimochi (Kichagga cha Old Moshi), iliyofanyika katika Usharika wa Bethel Msaranga, iliyoambatana na kuweka wakfu eneo la ujenzi wa Kanisa la Mtaa huo.

Askofu Dkt. Shoo alisema watu wengi wamekuwa wakipuuzia lugha zao na kusema ni vyema kujifunza na kuziendeleza lugha zao za asili. Katika Uzinduzi huo wa Biblia, Katibu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Dkt. Alfred Kimonge alisema mbali na Uzinduzi wa Biblia hiyo bado wanakabiliwa na changamoto ikiwemo wenye lugha zao kutotilia maanani na kutozipa kipaumbele.

“wengine wameshajiwekea kuwa kuwasiliana kwa lugha za asili ni udhaifu, wapendwa si kweli kwamba lugha za asili ni udhaifu. Lugha ya asili ndio inajenga moyo wa mtu na ndio lugha mama kwa wote wanaoishi,” alisema.

Addresses

16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area.
P.O BOX 175, Dodoma -Tanzania.

Phone

+255 (0) 765 530 892

Email

info@biblesociety-tanzania.org

Bible Production

Bible Production

IMG 8386

We publish scriptures in various formats including print, audio, visual and braille in order to meet the needs of all kinds of people. Since the scriptures are mostly used on a daily basis, we make sure the quality is top. This therefore dictates where production is done. Most of our production is done abroad and this comes at a high cost.

HOTUBA YA DR. ALFRED E. KIMONGE KATIBU MKUU WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA: KWENYE IBADA NA SHEREHE YA UZINDUZI WA BIBLIA YA KIDATOOGA TAREHE 04 OKTOBA 2020.

HOTUBA YA DR. ALFRED E. KIMONGE KATIBU MKUU WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA: KWENYE IBADA NA SHEREHE YA UZINDUZI WA BIBLIA YA KIDATOOGA TAREHE 04 OKTOBA 2020.

Nawasalimu wote katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, na kipekee ninamsalimu Baba Askofu Nicholaus Nsanganzelu na wote waliongozana naye. Bwana Yesu apewe sifa.

Ninazungumza kwa ridhaa ya Baraza la Wakurugenzi wa Chama cha Biblia cha Tanzania ambao wanawakilisha Kanisa zima hapa nchini yaani madhehebu yote. Mwenyekiti wa Baraza hili kwa awamu hii ni Mhashamu Askofu Mark Walwa Malekana wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA).

Chama cha Biblia cha Tanzania ni mwanachama kamili katika Muungano wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni (United Bible Societies-UBS). Kusudi la Muungano huu Ulimwenguni kote ni kutafsiri, kuchapisha, kueneza Neno la Mungu (Biblia) kwa lugha anayoweza kuilewa vizuri msomaji na kwa bei anayoiweza. Chama kinajitegemea lakini kinaheshimu mapatano na malengo ya Muungano huo. Vile vile kinazingatia malengo ya Kanisa katika Umisionari na Uinjilishaji. Makusudi ni kwamba Kanisa lijihusishe katika kukibeba, kukiombea, kuchangia gharama kwa njia ya sadaka maalumu na vile vile kuhimiza uenezaji na usomaji wa Maandiko Matakatifu.

Malengo hayo yanatokana na utume wa Bwana Yesu asemapo, “Basi, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” (Math: 28: 19). Hivyo Chama kinafanya juhudi ya kuwapatia watu wote Neno la Mungu katika lugha zao bila nyongeza au kipunguzi katika maana, na kwa bei ambayo walengwa wataimudu.

Ili kutimiza lengo hili Chama cha Biblia, kinatafsiri Biblia au sehemu zake kutoka lugha za awali (Kieberania na Kiyunani) kwenda katika lugha lengwa na kisha kuchapisha na kueneza Neno kwa walengwa. Malengo haya yanafanyika kwa kushirikiana na Kanisa na vyombo vyake. Mara nyingi Kanisa ndilo linaona umuhimu wa kutafsiri na kukiomba Chama cha Biblia kifanye kazi hiyo ya kutafsiri. Kwa hiyo Chama cha Biblia ni mtumishi wa Kanisa. Ni nani anayestahili kupatiwa Neno la Mungu? Ingewezekana, kila mtu apatiwe Neno la Mungu katika lugha yake ili apate nafasi ya kuusikia ujumbe wa kwamba Yesu Kristo pekee ndiye njia, kweli na uzima: ndiye Mwokozi.

Binadamu wamegawanyika katika makundi mbalimbali na tofauti. Makundi hayo yanatambuliwa kama makabila yenye lugha maalum, mengine yana utaifa, mengine yanajitaja kwa njia ya koo, n.k. Ijapokuwa makundi hayo yanatambuliwa hivyo, kunakuwepo sababu nzuri kama za uzalendo zinazoyachukulia makundi hayo kwa pamoja kama ni kitu kimoja. Hata hivyo kama vile ukuta imara unavyotokana na matofali moja moja yaliyo imara, hivyo na watu wenye utambulisho wao wa pekee kwa pamoja wanajenga jamii/taifa imara. Watu wanaimarishwa na tofauti zao. “Katika tofauti zetu tunapata uimara” Katika Ufunuo wa Yesu Kristo (Ufu. 7:9-12) tunaona jinsi wakombolewa wote walivyo pamoja katika halaiki ya mwisho, ijapokuwa ziko tofauti dhahiri kati yao.

Umoja wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni unatambua na kuheshimu tofauti zilizopo baina ya makundi ya watu. Hivyo pale watu wanapofikishiwa Neno la Mungu na ikadhihirika kuna udhaifu wa kulisoma, basi hatua zinachukuliwa ili kulihimiza Kanisa liwawekee watu misingi ya kujua kuisoma na kuiandika lugha yao. Matokeo ni kwamba kwa kuijua lugha yake kwa kulisoma Neno la Mungu kunamuwezesha mtu kujifunza lugha nyingine. Hivyo kwa kushirikiana na Kanisa, tafsiri mpya za Biblia zinaambatana na juhudi za kuwafundisha watu wazima kwa wadogo, kuisoma Biblia yao. Juhudi hii imefanyika kwa Wasukuma, Wamaasai, Wanyakyusa, Wairaqw na Wachagga. Mikakati ipo kwa Wakaguru, Wagogo, Wahehe, Wadatooga na penginepo ambapo juhudi ya kutafsiri Biblia inaendelea.

Kwa makundi haya Chama cha Biblia kinachukua juhudi zote kuandaa na kuwafikishia watu Biblia iliyoandaliwa katika mifumo tofauti. Kwa mfano, Neno lililochapishwa –(“Printed Format”), Neno lililowekwa katika kanda-naswa – (Magnetic au digital cassette), Neno lililoingizwa kwa njia simulizi – (Audio-Aural-Visual Scriptures), Neno katika mifumo maalumu kama vile Braille kwa Wasioona, New Reader Scriptures kwa wasomaji wa awali, Neno katika mfumo wa Maandishi Makubwa kwa ajili ya Wazee na wengine wenye udhaifu wa macho, Neno katika Matoleo ya Watoto, Neno kwa njia ya Scripture Literacy Promotion, Neno katika Digital Bible Library.

Huduma hii ni kwa ajili ya Kanisa, ili liweze kutumia zana hizo katika kuyatunza makundi hayo yote ya watu walioko katika maeneo yao ya Umisheni.

Muungano wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni kutokana na tamko la pamoja imejiwekea Sera ya kutafsiri Biblia aidha kwa mara ya kwanza au kwa kuhariri upya iliyokuwapo, ili angalau ifikapo 2033 makundi au makabila yote;

  • Yanayofikia au kuzidi idadi ya watu 500,000 wapatiwe Biblia nzima.
  • Yanayofikia idadi ya watu 250,000 wapatiwe Agano Jipya.
  • Yanayofikia idadi ya watu 100,000 wapatiwe Kisehemu cha Biblia (Bible Portions).

Hapa Tanzania tumekamilisha tafsiri 43 kati ya lugha 132 kazi inaendelea.

Ieleweke kwamba tafsiri ikianza tu, lengo ni kuikamilisha Biblia nzima hata kama idadi ya wazungumzaji ni ndogo ili asiwepo mtu atakayesema “nimekosa nafasi katika ufalme wake Yesu Kristo kwa kuwa Neno lake halikupatikana katika lugha yangu”

Makanisa kwa kushirikiana ndiyo yanayoomba kuanzisha na hatimaye kukamilisha tafsiri ili kila mtu awe na Biblia yake katika lugha anayoichagua na kuielewa.

Hizi lugha ambazo ni kitambulisho cha kila mtu na lugha yake, zinakabiliwa na changamoto kadhaa, kwa mfano;

  • Kutotiliwa maanani na kupewa kipaumbele na baadhi ya mamlaka tawala na Makanisa.
  • Lugha ya utawala (kama vile Kiingereza, Kiswahili, n.k) inagandamiza lugha nyingine na kuashiria kuitoa.

Neno la Mungu linadumu milele. Kwa hiyo lugha ambayo inalizungumzia Neno la Mungu inadumishwa. Ni wajibu wa Kanisa kuhakikisha Biblia inayozinduliwa inatumika katika ibada zao.

Hapa Tanzania kuna makundi/makabila ya lugha hai 132. Hadi sasa kuanzia 1846 hadi 2020 Chama cha Biblia, kwa kushirikiana na Kanisa tumetafsiri Neno la Mungu katika makabila yafuatayo;

Sehemu Agano Jipya Biblia
1. Swahili Southern 1846
2. Swahili (SUV) 1952
3. Swahili (CL) 1996
4. Wajita 1920 1930
5. Wakuria 1969 1996
6. Wamasai 1905 1923 1992
7. Wadatooga 2002 2009 2020
8. WaIraqw 1957 1977 2003
9. Kivunjo 1966 1999 2020
10. Machame 1932 1999
11. Kimochi 1892 1999
12. Wanyakyusa 1895 1908 1996
11. Wahaya 1920 1930 2001
13. Wasukuma 1895 1925/2001 1960/2020
14. Wakuria 1969 1996
15. Wameru 1964
16. Chasu/Pare 1910 1922
17. Kihehe 1999
18. Kibena 1914
19. Cigogo 1886 1899 2002
20. Kidatooga 2009 2020
21. Kiluo 1953
22. Kinyamwanga 1982
23. Chiyao 1920
24. Kimambwe 1901
25. Kilungu 1901
26. Kishambala 1908
27. Kinyamwezi 1951
28. Kitaveta 1949
29. Kinyiha 1950
30. Kinyiramba 2010
31. Kirimi 2010
32. Kikerewe 1946
33. Kikinga 1961
34. Kizaramo 1975
35. Kifipa 1988
36. Kikaguru 2010
37. Kibondei 1887
38. Kingoni 1891
39. Kizigua 1906
40. Kimpoto 1913
41. Kizinza 1930
42. Kihangaza 1938
43. Kiha 1960
44. Kiwanji 1985
45. Kizanaki 1948

Kazi bado ni kubwa, Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na Kanisa, kinayo mikakati ya kuwafikishia Neno la Mungu makundi/makabila yaliyobaki. Rai yetu kwa Kanisa tunaomba Biblia hii itumike katika ibada ili kazi hii iliyofanyika kwa miaka mingi na kwa gharama kubwa isiwe ya bure.

Leo tumekamilisha jitihada katika lugha ya Kidatooga kwa kuwakamilishia Biblia: Mungu anena na Wadatooga katika ukamilifu wa Biblia ya Kidatooga. Ni matumaini yetu kwamba Injili ya Wokovu katika Yesu Kristo itawafikia katika lugha yao ya moyoni na kusema sasa nimetambua Mungu anasema nami kwa lugha yangu.

Kwa njia ya tafsiri hii ya Biblia, Wadatooga nao watamsikia Bwana Yesu kwa ukaribu wa moyoni ili wapate fursa ya kushiriki katika halaiki ya mwisho “ Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha (Kidatooga)…” (Ufu. 7: 9-12).

Bwana Yesu atubariki sisi sote.

Dr. Alfred E. Kimonge

KATIBU MKUU.

CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA.

04 Oktoba, 2020.

Hotuba ya Mch. Canon Prof. Aloo Osotsi Mojola. Mtaalamu wa Tafsiri Mstaafu wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni katika Uzinduzi wa Biblia ya Kidatooga Oktoba 4, 2020.

Hotuba ya Mch. Canon Prof. Aloo Osotsi Mojola. Mtaalamu wa Tafsiri Mstaafu wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni katika Uzinduzi wa Biblia ya Kidatooga Oktoba 4, 2020.

Kama ilivyosomwa kwetu katika Ibada hiyo ya Uzinduzi na Askofu Julius Nyange Meneja Mstaafu wa Tafsri katika Chama cha Biblia cha Tanzania.

Waheshimiwa Viongozi, Maaskofu, Mapadre, Wachungaji, Katibu Mkuu na Watumishi wote wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Watendakazi wa Kanisa na Watumishi wa Mungu, Wamishenari, Viongozi wa Serikali na hasa Wakristo na wasemaji wa lugha ya Kidatooga.  Ndugu waalikwa wote, Mabibi na Mabwana nawasalimu katika Jina kuu la Yesu Kristo Mwokozi wetu.

Ni furaha kubwa kushuhudia tukio hili kubwa la kihistoria, la Uzinduzi wa Biblia katika lugha ya Kidatooga. Nifuraha kubwa kwetu sote kushuhudia siku hii ya leo.

Wote tunaikumbuka siku kama hii, wakati wa Uzinduzi na kuwekwa wakfu  Agano Jipya la Kidatoga, iliyofanyika Oktoba 12, 2009 katika viwanja vya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli karibu na Ziwa Basotu, Mbulu. 

Tukio la leo ni kutimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Mradi wa kutafsiri Biblia kwa lugha ya Kidatoga.

Sasa jamii yote ya Kidatoga na wasemaji wa lugha yta Kidatoga wataweza kusoma na kumsikia Mungu akiongea nao kwa lugha yao ya moyoni.

Lugha ya Kidatoga ni tawi la familia ya kusini ya lugha ya Kinilotiki (Southern Nilotic language family). Lahaja saba za Kidatoga ni pamoja na – Bajuta, Gisamjaga, Barabaiga, Isimijega na Rotigenga, Buradiga na Bijanjida.

Barabaiga ndilo kundi kubwa zaidi katika familia hii. Wadatoga wakati mwingine hujulikana kama Wamang’ati hasa kwa mujibu wa Wamasai.  Mang’ati maana yake ni “adui” ingawa kwa sasa kwa ujumla halitumiki tena, na linasisitizwa lisitumike kabisa. Tunazungumzia Wadatoga.

Historia ya mradi wa Kidatoga imekuwa ndefu na ngumu sana. Lakini tunamshukuru Mungu kwa sababu ya siku hii maalum iliyosubiriwa kwa muda mrefu, sasa imefika. 

Mnamo mwaka 1987 shirika la SIL lilitambua uhitaji wa Biblia kwa jamii ya Kidatoga.

Jambo hili lilipelekea kanisa la KKKT Dayosisi ya Mbulu kuwaalika shirika la SIL kuanzisha mradi wa tafsiri ya Biblia kwa Kidatoga. Shirika la SIL likaandaa timu wa tafsiri ambayo iliongozwa na John  na Heidi McCauley. Baada ya kipindi kifupi karibu na mwishoni mwa mwaka 1989 John na Heidi McCauley wakabadilishwa na Ralph na Anette Schubert. Kutokana na mabadiliko haya SIL hawakupata msukumo wa kuendelea na mradi huu.

Baadaye, kanisa la KKKT Dayosisi ya Mbulu likakiomba Chama cha Biblia cha Tanzania kuwasaidia. Chama cha Biblia cha Tanzania hakikusita, kiliupokea mradi huu na kuusimamia.

Kwa msukumo na msimamo mkubwa wa aliyekuwa Katibu Mkuu wakati huo Hayati Mch. Albert Mongi alihakikisha kwamba jitihada hizi zinafanikiwa. Uzinduzi rasmi wa Mradi huu ulifanyika katika Hospitali ya Kilutheri ya Haydom, tarehe 14 Januari, 1990. 

Timu ya Watafsiri ilikuwa na watumishi wafuatao – Mch. Elikana Gayewi, Mch. Festo Basso na Mch. Joseph Maho. Badaye, Mch. Gayewi aliicha timu lakini Pamoja na changamoto nyingi za kazi hii ngumu, Mch. Maho na Mch. Basso walistahimili na kung’ang’ana kuifanya.  Hali kadhalika kwa jitihada za Dr. Isaac Malleyeck za kufanya kampeni kwa ajili ya mradi huu Pamoja na misaada mbali mbalimbali za aliyekuwa kiongozi wa Hospitali ya Haydom, Hayati Dr. Olson na familia yake ilikuwa muhimu sana kwa maendeleo ya mradi. Kwa msukumo mkubwa wa aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mbulu, Hayati Askofu Yoram Girgis aliyehimiza na kutamani kuona kwamba Wadatoga wanapata Biblia yao ilikuwa zana kubwa katika kusukuma mbele mafanikio ya mradi.

Tahajia (Arthography) ya lugha hii iliyoandaliwa kwa msaada wa Shirika la SIL iliweka msingi wa kazi liyoendelea. Hata hivyo, kabla ya kufikia mwisho wa kazi hii wafanyakazi wa Shirika la SIL  wakajitoa. Ndipo baadaye, ikabadilishwa, ikarekebishwa na kukubaliwa.

Haikanushiki kwamba Tahajia itahitaji kuboreshwa siku zijazo

Kwa kweli, ari ya kutafsiri Agano Jipya ilianza tangu mwaka 1998 na kuendelea. Mnamo 2002 Agano Jipya likawa limekamilika. Kazi ya Agano la Kale ikafuatia mara moja. Injili ya Marko  ilichapishwa kama Kitabu nakutolewa tayari kwa kusambazwa katika ibada ya uzinduzi iliyofanyika katika Kanisa la Kilutheri karibu na Ziwa Basotu tarehe 7 Julai, 2002. Nakala zote 2000 zilichapishwa na Chama cha Biblia cha Tanzania zilisambazwa mara moja.

Agano Jipya lilichapishwa mwaka 2009 na hatimaye kuwekwa wakf una kuzinduliwa  katika sherehe iliyofanyika katika Kanisa la KKKT karibu na Ziwa Basotu mahali palipo na ofisi za  Mradi.  

Sherehe ile ya vifijo na furaha iliongozwa na Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosis ya Kati Singida Mhasham Askofu E. Sima kwa niaba ya Askofu Zebedayo wa KKKT Dayosis ya Mbulu.

Chama cha Biblia cha Tanzania kiliwakilishwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wakati huo Mch. Drk Mkunga Mtingele, Pamoja na watumishi kadhaa wa Chama wakiwemo – Alfred Kimonge, John Mnong’one, Mch. (Askofu) Julius Nyange na wengine. Mtaalamu wa Tafsiri kutoka Ofisi  Vyama vya Biblia Ulimwenguni  Prof. Aloo Osotsi Mojola pia alikuwepo pamoja na wageni wengine kutoka Chama cha Biblia cha Marekani na Ujumbe wa Kilutheri wa Norway.

Tukio la leo, ni kilele cha jitihada zilizoanza miaka mingi iliyopita. Hakika, leo ni siku ya kipekee isiyo na kifani na ya kihistoria. Hii ndiyo siku ambayo wamisionari walioweka misingi ya Kanisa kati ya Wadatoga bila shaka waliiota na kutama kuiona. Sisi tunaishuhudia leo na kwa kweli ni siku ya ajabu nay a kupendeza machoni petu. Jina la BWANA litukuzwe. Mioyo yetu imeja sifa na shukrani nyinge kwa Mungu wetu aliyetuwezesha kuiona siku hii.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri hapa Mbulu na makanisa mengine yaliyoshiriki wanapaswa kusifiwa na kushukuriwa kwa kazi na jitihada uhudi zao za kuutangaza mradi hadi kufikia siku hii ya leo.

Watafsiri wa Kidatoga na hasa Mch. Joseph Maho, Mch. Festo Basso, Dr Isaack Malleyeck, familia ya Hayati Dr. Olson na Ujumbe wa Kilutheri wa Norway, Chama cha Biblia cha Tanzania Pamoja na watumishi wake, na hasa aliyekuwa Katibu Mkuu wakati huo Mch. Albert Mongi, Mch. Canon Dr. Mkunga Mtingele, Nd. Alfred Kimonge, Mch. (Askofu) Julius Nyange, Mch. Canon Prof. Aloo Osotsi Mojola, Pamoja na wote waliovujajsho kwa namna moja au nyingine kuona kwamba Biblia katika lugha ya Kidatoga – wanapongezwa sana kwa kazi ya upendo.

Sifa na Utukufu apewe Mungu wetu aliye Juu!

Imeandaliwa na Mch. Canon Prof. Aloo Osotsi Mojola. Mtaalamu wa Tafsiri Mstaafu wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni na ambaye kwa sasa ni Profesa wa Falsafa na Mitaala ya Tafsiri, Chuo Kikuu cha St. Paul, Limuru Kenya.

Hotuba ya Mch. Canon Prof. Aloo Osotsi Mojola. Mtaalamu wa Tafsiri Mstaafu wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni katika Uzinduzi wa Biblia ya Kwanza katika lahaja ya Kivunjo cha Kichagga Tarehe 27 Septemba, 2020.

Hotuba ya Mch. Canon Prof. Aloo Osotsi Mojola. Mtaalamu wa Tafsiri Mstaafu wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni katika Uzinduzi wa Biblia ya Kwanza katika lahaja ya Kivunjo cha Kichagga Tarehe 27 Septemba, 2020.

Kama ilivyosomwa kwetu katika Ibada hiyo ya Uzinduzi na Askofu Julius Nyange Meneja Mstaafu wa Tafsri katika Chama cha Biblia cha Tanzania.

Waheshimiwa Maaskofu, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia Cha Tanzania, Katibu Mkuu wa Chama Cha Biblia cha Tanzania, viongozi wa Makanisa na viongozi wa Serikali, waheshimiwa Mapadri, Makasisi na Wachungaji, akina baba na akina mama, ndugu wote katika Kristo Yesu na wageni wote waalikwa, mabibi na mabwana nawasalimu nyote katika jina tukufu la Yesu Kristo.

Leo ni siku ya shangwe, furaha, nderemo na vigelegele, kwa sababu ya tukio hili kubwa la kihistoria linalofanyika leo tarehe 27 Septemba, 2020. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kanisa hapa Kilimanjaro Biblia ya kwanza katika lahaja au msemo wa Kivunjo-Chagga inazinduliwa na kutolewa rasmi na Kanisa kwa wakristo wote wanaoongea na kuelewa msemo huu.

Wamisionari wa Kilutheri, kikundi cha Leipzig, waliofika kwa mara ya kwanza maeneo haya ya Kilimanjaro Tanzania, miaka ya 1890, wakianzia pale Old Moshi, na baadaye Nkwarungo, Mamba, Shira, Mwika, Masama, Uswaa na Marangu; wakiwemo Emil Muller, Gerhard Althaus, Robert Fassman, Albin Boeme na Theodore Passler, bila shaka tukio la leo lilikuwa ndoto yao. Mmoja wao, mmisionari mwanaisimu na mwana-anthropolojia, Bruno Gutmann, aliyepewa jina “Wasahuye a Wachaka” alilipa kipaumbele suala la kuitafsri Biblia katika lugha ya Kichagga. Juhudi za wamisionari Bruno Gutmann, R Fassman pamoja na wazee wenyeji zilizaa matunda kwa machapisho yafuatayo, mnamo mwaka 1905 kitabu cha Injili ya Yohana kilipochapishwa, mwaka 1908 Barua ya Paulo kwa Warumi, mwaka 1911 Injili ya Mariko, na hatimaye mwaka 1939 Agano Jipya la kwanza katika Kichagga ilichapishwa. Kitabu hiki cha Agano Jipya kilichapishwa na Chama cha Biblia cha Wurttemberg, kule Stuttgart, Ujerumani. Toleo la pili lilichapishwa na Chama Cha Biblia cha Tanzania, Dodoma, mnamo 1999.

Kutafsiri Biblia nzima katika msemo wa Kivunjo kulianzishwa mwaka wa 1991 na Chama cha Biblia cha Tanzania chini ya uongozi wa Marehemu Mchungaji Albert Mongi, pamoja na Mshauri wa Tafsiri, Professor Aloo Osotsi Mojola wa United Bible Societies. Agano Jipya la kwanza katika msemo wa Kivunjo lilichapishwa na kutolewa, pale Marangu mnamo Novemba 6, 1999.

Miradi mitatu ya kutafsiri Biblia ya Kimochi, Biblia ya Kimachame na Biblia hii ya Kivunjo yote ilianzishwa mwaka huo huo wa 1991. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa zote zimekamilika karibu wakati mmoja.

Biblia ya Kivunjo ndio ya kwanza kuchapishwa na kutolewa; zingine zitafuata karibuni. Ningependa kuwashukuru Mchungaji John Mlay na Mchungaji Professor Godson Maanga ambao walijitolea pakubwa kukamilisha Biblia hii ya Kivunjo.

Siku ya leo, Septemba 27, 2020 Biblia Takatifu katika lahaja ya Kivunjo inazinduliwa na kuwekwa wakfu. Jina la Mwenyezi Mungu libarikiwe na kupewa sifa.

Hatuna budi kuwashukuru wale wote ambao wamechangia kwa hali na mali kufanikisha kazi hii takatifu na tukufu, wakiwemo wafuatao:

  1. Marehemu Mchungaji Albert Mongi na viongozi wa Vunjo waliounga mkono juhudi hizi za kutafsiri Biblia katika msemo wa Kivunjo.
  2. Wale wote waliohusika katika kuhakiki na kuchambua tafsiri yote ya Biblia hii.
  3. Mtaalam wa kompyuta na mratibu wa kazi za kutafsiri pale Chama Cha Biblia cha Tanzania – Mchungaji (Askofu) Julius Nyange, pamoja na wafanyakazi wa Chama Cha Biblia, Dodoma ambao kwa njia moja au nyingine wamekuwa sehemu ya kazi hii kubwa.
  4. Wataalam na washauri wa tafsiri ya Biblia waliowashauri watafsiri wa Biblia ya Kivunjo katika kukamilisha kazi yao.
  5. Viongozi wa Makanisa walioombea kazi hii pamoja na kuwatembelea watafsiri na kuwatia moyo.

Mwisho, hatuwezi kuwasahau ninyi nyote – hasa walengwa wa Biblia hii, ambao mmefika hapa siku ya leo kushangilia na kupokea Biblia yenu.

Utukufu na sifa na ukuu kwa Mungu peke yake!

Asanteni sana.

(Imeandaliwa na Professor Aloo Osotsi Mojola, Professor of Philosophy and Translation Studies, Limuru, Kenya, Retired UBS Translation Consultant and former Africa Translation Coordinator, United Bible Societies. Worked with the Kivunjo translation team from 1991 till completion of project.)

HOTUBA YA DR. ALFRED E. KIMONGE KATIBU MKUU WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA: KWENYE IBADA NA SHEREHE YA UZINDUZI WA BIBLIA YA KIVUNJO TAREHE 27 SEPTEMBA 2020.

HOTUBA YA DR. ALFRED E. KIMONGE KATIBU MKUU WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA: KWENYE IBADA NA SHEREHE YA UZINDUZI WA BIBLIA YA KIVUNJO TAREHE 27 SEPTEMBA 2020.

HOTUBA YA DR. ALFRED E. KIMONGE

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA:

KWENYE IBADA NA SHEREHE YA UZINDUZI WA BIBLIA YA KIVUNJO

TAREHE 27 SEPTEMBA 2020

Nawasalimu wote katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, na kipekee ninamsalimu Baba Askofu Fredrick Onael Shoo na wote waliongozana naye. Bwana Yesu apewe sifa.

Ninazungumza kwa ridhaa ya Baraza la Wakurugenzi wa Chama cha Biblia cha Tanzania ambao wanawakilisha Kanisa zima hapa nchini yaani madhehebu yote. Mwenyekiti wa Baraza hili kwa awamu hii ni Mhashamu Askofu Mark Walwa Malekana wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA).

Chama cha Biblia cha Tanzania ni mwanachama kamili katika Muungano wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni (United Bible Societies-UBS). Kusudi la Muungano huu Ulimwenguni kote ni kutafsiri, kuchapisha, kueneza Neno la Mungu (Biblia) kwa lugha anayoweza kuilewa vizuri msomaji na kwa bei anayoiweza. Chama kinajitegemea lakini kinaheshimu mapatano na malengo ya Muungano huo. Vile vile kinazingatia malengo ya Kanisa katika Umisionari na Uinjilishaji. Makusudi ni kwamba Kanisa lijihusishe katika kukibeba, kukiombea, kuchangia gharama kwa njia ya sadaka maalumu na vile vile kuhimiza uenezaji na usomaji wa Maandiko Matakatifu.

Malengo hayo yanatokana na utume wa Bwana Yesu asemapo, “Basi, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” (Math: 28: 19). Hivyo Chama kinafanya juhudi ya kuwapatia watu wote Neno la Mungu katika lugha zao bila nyongeza au kipunguzi katika maana, na kwa bei ambayo walengwa wataimudu.

Ili kutimiza lengo hili Chama cha Biblia, kinatafsiri Biblia au sehemu zake kutoka lugha za awali (Kieberania na Kiyunani) kwenda katika lugha lengwa na kisha kuchapisha na kueneza Neno kwa walengwa. Malengo haya yanafanyika kwa kushirikiana na Kanisa na vyombo vyake. Mara nyingi Kanisa ndilo linaona umuhimu wa kutafsiri na kukiomba Chama cha Biblia kifanye kazi hiyo ya kutafsiri. Kwa hiyo Chama cha Biblia ni mtumishi wa Kanisa. Ni nani anayestahili kupatiwa Neno la Mungu? Ingewezekana, kila mtu apatiwe Neno la Mungu katika lugha yake ili apate nafasi ya kuusikia ujumbe wa kwamba Yesu Kristo pekee ndiye njia, kweli na uzima: ndiye Mwokozi.

Binadamu wamegawanyika katika makundi mbalimbali na tofauti. Makundi hayo yanatambuliwa kama makabila yenye lugha maalum, mengine yana utaifa, mengine yanajitaja kwa njia ya koo, n.k. Ijapokuwa makundi hayo yanatambuliwa hivyo, kunakuwepo sababu nzuri kama za uzalendo zinazoyachukulia makundi hayo kwa pamoja kama ni kitu kimoja. Hata hivyo kama vile ukuta imara unavyotokana na matofali moja moja yaliyo imara, hivyo na watu wenye utambulisho wao wa pekee kwa pamoja wanajenga jamii/taifa imara. Watu wanaimarishwa na tofauti zao. “Katika tofauti zetu tunapata uimara” Katika Ufunuo wa Yesu Kristo (Ufu. 7:9-12) tunaona jinsi wakombolewa wote walivyo pamoja katika halaiki ya mwisho, ijapokuwa ziko tofauti dhahiri kati yao.

Umoja wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni unatambua na kuheshimu tofauti zilizopo baina ya makundi ya watu. Hivyo pale watu wanapofikishiwa Neno la Mungu na ikadhihirika kuna udhaifu wa kulisoma, basi hatua zinachukuliwa ili kulihimiza Kanisa liwawekee watu misingi ya kujua kuisoma na kuiandika lugha yao. Matokeo ni kwamba kwa kuijua lugha yake kwa kulisoma Neno la Mungu kunamuwezesha mtu kujifunza lugha nyingine. Hivyo kwa kushirikiana na Kanisa, tafsiri mpya za Biblia zinaambatana na juhudi za kuwafundisha watu wazima kwa wadogo, kuisoma Biblia yao. Juhudi hii imefanyika kwa Wasukuma, Wamaasai, Wanyakyusa, Wairaqw na Wachagga. Mikakati ipo kwa Wakaguru, Wagogo, Wahehe, Wadatooga na penginepo ambapo juhudi ya kutafsiri Biblia inaendelea.

Kwa makundi haya Chama cha Biblia kinachukua juhudi zote kuandaa na kuwafikishia watu Biblia iliyoandaliwa katika mifumo tofauti. Kwa mfano, Neno lililochapishwa –(“Printed Format”), Neno lililowekwa katika kanda-naswa – (Magnetic au digital cassette), Neno lililoingizwa kwa njia simulizi – (Audio-Aural-Visual Scriptures), Neno katika mifumo maalumu kama vile Braille kwa Wasioona, New Reader Scriptures kwa wasomaji wa awali, Neno katika mfumo wa Maandishi Makubwa kwa ajili ya Wazee na wengine wenye udhaifu wa macho, Neno katika Matoleo ya Watoto, Neno kwa njia ya Scripture Literacy Promotion, Neno katika Digital Bible Library.

Huduma hii ni kwa ajili ya Kanisa, ili liweze kutumia zana hizo katika kuyatunza makundi hayo yote ya watu walioko katika maeneo yao ya Umisheni.

Muungano wa Vyama vya Biblia Ulimwenguni kutokana na tamko la pamoja imejiwekea Sera ya kutafsiri Biblia aidha kwa mara ya kwanza au kwa kuhariri upya iliyokuwapo, ili angalau ifikapo 2033 makundi au makabila yote;

  • Yanayofikia au kuzidi idadi ya watu 500,000 wapatiwe Biblia nzima.
  • Yanayofikia idadi ya watu 250,000 wapatiwe Agano Jipya.
  • Yanayofikia idadi ya watu 100,000 wapatiwe Kisehemu cha Biblia (Bible Portions).

Hapa Tanzania tumekamilisha tafsiri 43 kati ya lugha 132 kazi inaendelea.

Ieleweke kwamba tafsiri ikianza tu, lengo ni kuikamilisha Biblia nzima hata kama idadi ya wazungumzaji ni ndogo ili asiwepo mtu atakayesema “nimekosa nafasi katika ufalme wake Yesu Kristo kwa kuwa Neno lake halikupatikana katika lugha yangu”

Makanisa kwa kushirikiana ndiyo yanayoomba kuanzisha na hatimaye kukamilisha tafsiri ili kila mtu awe na Biblia yake katika lugha anayoichagua na kuielewa.

Hizi lugha ambazo ni kitambulisho cha kila mtu na lugha yake, zinakabiliwa na changamoto kadhaa, kwa mfano;

  • Kutotiliwa maanani na kupewa kipaumbele na baadhi ya mamlaka tawala na Makanisa.
  • Lugha ya utawala (kama vile Kiingereza, Kiswahili, n.k) inagandamiza lugha nyingine na kuashiria kuitoa.

Neno la Mungu linadumu milele. Kwa hiyo lugha ambayo inalizungumzia Neno la Mungu inadumishwa. Ni wajibu wa Kanisa kuhakikisha Biblia inayozinduliwa inatumika katika ibada zao.

Hapa Tanzania kuna makundi/makabila ya lugha hai 132. Hadi sasa kuanzia 1846 hadi 2020 Chama cha Biblia, kwa kushirikiana na Kanisa tumetafsiri Neno la Mungu katika makabila yafuatayo;

Sehemu

Agano Jipya

Biblia

1.

Swahili Southern

1846

2.

Swahili (SUV)

1952

3.

Swahili (CL)

1996

4.

Wajita

1920

1930

5.

Wakuria

1969

1996

6.

Wamasai

1905

1923

1992

7.

Wadatooga

2002

2009

2020

8.

WaIraqw

1957

1977

2003

9.

Kivunjo

1966

1999

2020

10.

Machame

1932

1999

11.

Kimochi

1892

1999

12.

Wanyakyusa

1895

1908

1996

11.

Wahaya

1920

1930

2001

13.

Wasukuma

1895

1925/2001

1960/2020

14.

Wakuria

1969

1996

15.

Wameru

1964

16.

Chasu/Pare

1910

1922

17.

Kihehe

1999

18.

Kibena

1914

19.

Cigogo

1886

1899

2002

20.

Kidatooga

2009

2020

21.

Kiluo

1953

22.

Kinyamwanga

1982

23.

Chiyao

1920

24.

Kimambwe

1901

25.

Kilungu

1901

26.

Kishambala

1908

27.

Kinyamwezi

1951

28.

Kitaveta

1949

29.

Kinyiha

1950

30.

Kinyiramba

2010

31.

Kirimi

2010

32.

Kikerewe

1946

33.

Kikinga

1961

34.

Kizaramo

1975

35.

Kifipa

1988

36.

Kikaguru

2010

37.

Kibondei

1887

38.

Kingoni

1891

39.

Kizigua

1906

40.

Kimpoto

1913

41.

Kizinza

1930

42.

Kihangaza

1938

43.

Kiha

1960

44.

Kiwanji

1985

45.

Kizanaki

1948

Kazi bado ni kubwa, Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na Kanisa, kinayo mikakati ya kuwafikishia Neno la Mungu makundi/makabila yaliyobaki. Rai yetu kwa Kanisa tunaomba Biblia hii itumike katika ibada ili kazi hii iliyofanyika kwa miaka mingi na kwa gharama kubwa isiwe ya bure.

Leo tumekamilisha jitihada katika lugha ya Kivunjo kwa kuwakamilishia Biblia: Mungu anena na Wavunjo katika ukamilifu wa Biblia ya Kivunjo. Ni matumaini yetu kwamba Injili ya Wokovu katika Yesu Kristo itawafikia katika lugha yao ya moyoni na kusema sasa nimetambua Mungu anasema nami kwa lugha yangu.

Kwa njia ya tafsiri hii ya Biblia, Wavunjo nao watamsikia Bwana Yesu kwa ukaribu wa moyoni ili wapate fursa ya kushiriki katika halaiki ya mwisho “ Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha (Kivunjo)…” (Ufu. 7: 9-12).

Bwana Yesu atubariki sisi sote.

Dr. Alfred E. Kimonge

KATIBU MKUU.

CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA.

27 SEPTEMBA, 2020.