Mkuu wa KKKT ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Shoo, amewataka Wakristo kuitunza na kuindeleza lugha zao za asili kwani ndio msingi na urithi walio nao.

Askofu Dkt. Shoo aliyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Biblia ya lugha ya Kimochi (Kichagga cha Old Moshi), iliyofanyika katika Usharika wa Bethel Msaranga, iliyoambatana na kuweka wakfu eneo la ujenzi wa Kanisa la Mtaa huo.

Askofu Dkt. Shoo alisema watu wengi wamekuwa wakipuuzia lugha zao na kusema ni vyema kujifunza na kuziendeleza lugha zao za asili. Katika Uzinduzi huo wa Biblia, Katibu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Dkt. Alfred Kimonge alisema mbali na Uzinduzi wa Biblia hiyo bado wanakabiliwa na changamoto ikiwemo wenye lugha zao kutotilia maanani na kutozipa kipaumbele.

“wengine wameshajiwekea kuwa kuwasiliana kwa lugha za asili ni udhaifu, wapendwa si kweli kwamba lugha za asili ni udhaifu. Lugha ya asili ndio inajenga moyo wa mtu na ndio lugha mama kwa wote wanaoishi,” alisema.

Addresses

16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area.
P.O BOX 175, Dodoma -Tanzania.

Phone

+255 (0) 765 530 892

Email

info@biblesociety-tanzania.org

× How can I help you?