KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA BIBLIA MKOANI DODOMA

KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA BIBLIA MKOANI DODOMA

KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA BIBLIA MKOANI DODOMA

11
20241103 155004 scaled

Dodoma, 03 Novemba 2024 – Maadhimisho ya kilele cha Juma la Biblia mwaka huu yamefanyika kwa mafanikio makubwa mkoani Dodoma, katika Uwanja wa Mashujaa. Maadhimisho hayo yaliyoanza na maandamano ya amani kutoka makao makuu ya Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT) hadi viwanja vya zamani vya Mashujaa, yalivutia umati wa wanachama na wadau mbalimbali. Maandamano hayo yalipambwa na bendi ya tarumbeta na kwaya ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), huku wanachama wakivalia tisheti zilizo na nembo ya CBT na kauli mbiu ya mwaka huu: “Neno la Mungu, Maadili Yetu.”

Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Askofu Amos Muhagachi, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CBT, akiwa ameambatana na viongozi wengine wakuu wa Chama akiwemo Katibu Mkuu wa CBT, Dkt. Alfred Elias Kimonge, na Mkurugenzi wa CBT, Dkt. Anna Solo. Pia, sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi wa makanisa, wanachama wa CBT, na wanafunzi wa UDOM.

1
4
20241103 174033

Katika hotuba yake mgeni rasmi Askofu Amos Muhagachi alisoma Neno la Mungu kutoka Zaburi 119:105, “Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu,” akisisitiza umuhimu wa Neno la Mungu kama msingi wa maadili. Alisema, “Biblia ni kitabu kinachotuunganisha sisi Wakristo na kinatuonyesha maisha ya mwanadamu, ukombozi, na umilele wake.” Pia alihimiza mpango mkubwa wa maadhimisho mwaka ujao, kwa kushirikiana zaidi ili kufikia wadau wengi.

Askofu MuhagachiGS Maandamano

Katika hotuba yake, Katibu Mkuu Dkt. Kimonge aliwashukuru wanachama na wadau wote waliojitolea kushiriki Juma la Biblia lililoanza tarehe 28 Oktoba na kumalizika leo 03 Novemba. Dkt. Kimonge alieleza kwamba lengo kuu la CBT ni kutafsiri, kuchapisha, na kusambaza Biblia kwa watu wote, wakiwemo Wakristo na wasio Wakristo. Alihimiza umoja katika kuchangia kazi hii muhimu, hasa kwa makundi yasiyo na uwezo wa kununua Biblia, kama vile wafungwa na vijana.

20241103 162244 scaled
6

Katika kuelezea historia ya CBT, Dkt. Kimonge alitaja hadithi ya binti Maria Jones, mwenye umri wa miaka kumi na tano, aliyekuwa mkulima wa Wales. Kiu yake ya kumiliki Biblia ilichochea harakati za kuanzisha vyama vya Biblia, ambavyo leo vinafanya kazi katika nchi zaidi ya 160, kusambaza mamilioni ya Biblia na maandiko mengine katika lugha zaidi ya 15,000.

20241103 161423 scaled
20241103 161436 scaled

Maadhimisho hayo yamehitimishwa kwa maneno ya shukrani kutoka kwa Meneja wa Mahusiano na Makanisa, Mch. Samweli Mshana, aliyewapongeza viongozi wote kwa kufanikisha Juma la Biblia kwa ufanisi. “Shukrani kwa viongozi wetu na wanachama wote wa CBT kwa kazi kubwa mliyofanya. Mungu awabariki sana,” alisema Mch. Mshana.

20241103 154856 scaled
3

Maadhimisho ya Juma la Biblia yanaendelea kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha ushirikiano kati ya waumini, wadau, na jamii kwa ujumla kupitia Neno la Mungu, na CBT inaahidi kuendelea na jitihada hizi kwa ustawi wa kiroho wa Watanzania.

2

Comments

UZINDUZI WA SEHEMU YA BIBLIA KWA LUGHA YA KINYIHA WAFANYIKA KANISA LA MORAVIAN, MBOZI

UZINDUZI WA SEHEMU YA BIBLIA KWA LUGHA YA KINYIHA WAFANYIKA KANISA LA MORAVIAN, MBOZI

UZINDUZI WA SEHEMU YA BIBLIA KWA LUGHA YA KINYIHA WAFANYIKA KANISA LA MORAVIAN, MBOZI

Jimbo la Mbozi, Kanisa la Moravian Ushirika wa Igamba – 27 Oktoba 2024

IMG 9844 scaled

Tukio la kihistoria la uzinduzi wa vitabu vya Biblia vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kinyiha vitabu vya Ruthu, 1 Samweli, 1 Wafalme, na Yona limefanyika leo katika Kanisa la Moravian Ushirika wa Igamba, Jimbo la Mbozi. Uzinduzi huu umefanywa na Katibu Mkuu wa Jimbo la Mbozi, Mchungaji Rayson Kibona, huku ukiongozwa na Mch. Lastone Chalotela Mwamlima ambaye ni mratibu wa mradi pia mwenyekiti wa wilaya na Mchungaji Wiliadi Zewanga mchungaji wa ushirika wa Igamba Moravian.

Tukio hilo muhimu limeandaliwa na Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na makanisa ya Kikristo kutoka Mkoa wa Songwe, hasa Wilaya ya Mbozi ambako lugha ya Kinyiha huzungumzwa kwa wingi.

20241027 094333 scaled
IMG 9764 scaled
IMG 9753 scaled

Katika hafla hiyo, viongozi mbalimbali walihudhuria na kutoa hotuba kuhusu umuhimu wa tukio hili. Madam Leah Kiloba, Meneja wa Tafsiri kutoka Chama cha Biblia cha Tanzania, aliwasilisha ujumbe wa Chama hicho na Umoja wa Vyama vya Biblia Duniani, akieleza majukumu makuu ya Chama kuwa ni kutafsiri, kuchapisha, na kusambaza Biblia kwa gharama nafuu ili kuwafikia watu wote. Kiloba alisisitiza umuhimu wa mradi huu kwa jamii ya Wanyiha na kuwashukuru washiriki wote waliotoa mchango katika tafsiri. Pia aliwaomba jamii ya wanyiha baada ya kupokea vitabu hivyo wavisome kisha kama kuna makosa wayalete ili yalekebishwe mapema kabla ya Biblia kamili kukamilika.

Watafsiri na Wahakiki wa Tafsiri
Kazi ya kutafsiri vitabu hivi imefanywa kwa bidii na ushirikiano wa wataalamu wa lugha, viongozi wa makanisa, na wahakiki wa tafsiri. Baadhi ya watafsiri wakuu ni:
– Mch. Lastone Chalotela Mwamlima (mratibu)
– Mch. Justus Vhalondeghe Sinkonde
– Mch. Philimon Partson Balanga
– Dada Christina Chares Singogo

IMG 9821 scaled
IMG 9816 scaled

Wahakiki wa tafsiri walioshiriki ni pamoja na:
– Mch. Sila Mwamwezi
– Mch. Sostini Mwansenga
– Mch. Wilhelm Mwakavanga
– Mch. Selemani Nkota
– Mch. Lameck Nzowa
– Mch. Nichorous Shonza
– Dada Martha Mwashiuya
– Dada Upendo Mwashilindi
Pia, Dkt. Chris Pekka Wilde alitajwa kwa mchango wake muhimu wa kiufundi kama mshauri wa mradi huu.

IMG 9835
IMG 9828 scaled

Viongozi wa Makanisa Mbalimbali Wajumuika

Uzinduzi huu ulihudhuriwa na wachungaji na viongozi wa makanisa kutoka madhehebu tofauti, wakiwemo wawakilishi kutoka makanisa ya Last Church, Kanisa Katoliki, TAG, na KKKT. Viongozi hawa walipongeza hatua hii kama ishara ya kuendelea kwa kasi kwa mradi huu, ambao unalenga kuongeza upatikanaji wa Biblia kwa lugha ya Kinyiha kwa ufasaha.

IMG 9754 scaled
IMG 9771 scaled

Mafanikio na Matumaini ya Mradi wa Tafsiri kwa Lugha ya Kinyiha

Tukio hili limeibua matumaini makubwa na linaashiria mwanzo mzuri kwa jamii ya Wanyiha kupata Biblia kwa lugha yao wenyewe, hatua ambayo itaimarisha zaidi imani na kueneza Neno la Mungu kwa undani zaidi katika eneo hilo.

IMG 9764 scaled

Comments

UZINDUZI WA KITABU CHA KWANZA NA CHA PILI CHA SAMWELI KWA LUGHA YA CHASU

UZINDUZI WA KITABU CHA KWANZA NA CHA PILI CHA SAMWELI KWA LUGHA YA CHASU

UZINDUZI WA KITABU CHA KWANZA NA CHA PILI CHA SAMWELI KWA LUGHA YA CHASU

Kanisa la KKKT Usharika wa Hedalu, Dayosisi ya Pare – 20 Oktoba 2024

20241020 100910 scaled

Wapendwa waalikwa walikusanyika leo kwa tukio la kihistoria la uzinduzi wa kitabu cha Kwanza na cha Pili cha Samweli vilivyotafsiriwa kwa Lugha ya Chasu (Kipare). Uzinduzi huo uliandaliwa na Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na makanisa ya Kikristo yaliyoko katika wilaya za Mwanga na Same Mkoa wa Kilimanjaro, na kuongozwa na Mratibu wa Mradi, Mchungaji Elineema Mndeme.

Mchungaji Mndeme aliwashukuru wageni wote walioshiriki kwenye tukio la uzinduzi, wakiwemo Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Mwanga, Mchungaji Timothy Msangi, na Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Pare, Mchungaji Ibrahim Ndekia. Pia aliwapongeza wawakilishi kutoka Chama cha Biblia cha Tanzania, akiwemo Katibu Mkuu, Dkt. Alfred Kimonge, kwa kuwezesha kazi kubwa ya kutafsiri Biblia kwa lugha ya Chasu.

Rev. Elineema Mndeme
IMG 9613 scaled

Kazi ya tafsiri imefanywa kwa ushirikiano wa wataalamu wa lugha, viongozi wa makanisa, na wahakiki wa tafsiri. Mchango mkubwa ulitolewa na Meneja wa Tafsiri, Dada Leah Kiloba, na washirika wake katika Chama cha Biblia cha Tanzania, pamoja na wataalamu wa teknolojia ya taarifa Felix na Charles, ambao waliweka mifumo ya tafsiri katika kompyuta.

Kwa upande wa usimamizi wa tafsiri, Dkt. Chris Pekka Wilde, mshauri wa mradi, ametajwa kwa mchango wake wa kiufundi na ushauri thabiti katika kuhakikisha tafsiri zinafuata viwango vya juu.
Mradi wa kutafsiri Biblia kwa lugha ya Chasu unahusisha watafsiri wanne: Mchungaji Elineema Mndeme (Mratibu), Mchungaji Joasi Mpinda, Mchungaji Msifuni Msuya, na Mchungaji Imani Chediel Mgonja. Wahakiki wa tafsiri wamejumuisha wachungaji na wainjilisti na wajumbe raia kutoka maeneo mbalimbali ya jamii ya Chasu.

IMG 9603 scaled
IMG 9551 scaled
IMG 9555 scaled

Mpaka sasa, nusu ya vitabu vya Agano la Kale vimetafsiriwa. Kazi ya tafsiri inapitia hatua nne: kwanza, mtafsiri anatafsiri kitabu chake; pili, watafsiri wote wanakipitia; tatu, wahakiki wa jamii wanakikagua; na mwisho, mshauri wa kitaalamu anakihakiki.

Vitabu vilivyokamilika mpaka ngazi ya mshauri ni Ruthi, Yona, Yoshua, Waamuzi, Kitabu cha Nyakati 1 na Nyakati 2, Kitabu cha Wafalme 1 na Wafalme 2, Esta, Mwanzo, pamoja na Kitabu cha Kwanza na cha Pili cha Samweli ambavyo vimezinduliwa leo rasmi.

20241020 100712 scaled
20241020 100729 scaled

Aidha, Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kiko kwenye ngazi ya uhakiki, na kinatarajiwa kufika kwa mshauri mwezi Novemba. Kitabu cha Hesabu kiko katika hatua ya kuratibu, huku vitabu vya Kutoka, Mambo ya Walawi, Nehemia, na Ezra vikiwa katika hatua ya awali ya tafsiri.

Mchungaji Samweli Mshana kutoka Chama cha Biblia cha Tanzania alitoa hotuba fupi akieleza majukumu makuu ya Chama hicho, ambayo ni kutafsiri, kuchapisha, kusambaza Biblia, na kutafuta rasilimali fedha ili kupunguza gharama za shughuli hizo kwa njia ya uchangishaji fedha (fundraising).

Aliwasihi Wakristo kujiunga na Chama cha Biblia cha Tanzania ili kusaidia kupunguza bei za maandiko, hususani kwa ajili ya wafungwa na jamii zinazoishi katika hali ngumu.

20241020 101040
IMG 9601 scaled
IMG 9559 scaled

Pia katika Ibada hiyo alikabidhi redio 60 zenye Biblia kwa lugha ya Chasu, zinazojulikana kama mpiga mbiu (proclaimer), na kuomba viongozi wa Kanisa waziweke wakfu kwa matumizi ya kanisa. Pia aliwahimiza kusimamia mradi wa “Imani Huja kwa Kusikia” kwa kuanzisha vikundi vya kusikiliza, na akawakumbusha kutuma ripoti za maendeleo ya vikundi hivyo.

Mchungaji Mshana pia aliwaomba viongozi wa makanisa kuzindua kitabu cha kwanza na cha pili cha Samweli vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Chasu kama ishara ya hatua kubwa iliyofikiwa katika mradi huo.

IMG 9598 scaled

Tukio hili limekuwa la mafanikio makubwa na linaashiria mwanzo mzuri wa upatikanaji wa Biblia kwa Lugha ya Chasu, jambo ambalo litasaidia sana kueneza Neno la Mungu kwa ufasaha katika jamii hiyo.

Comments

Join

Work With Me

Uzinduzi wa sehemu ya Biblia za vitabu vya 2 Samweli, Ruthi, na Yona kwa lugha ya Kinyamwezi.

Uzinduzi wa sehemu ya Biblia za vitabu vya 2 Samweli, Ruthi, na Yona kwa lugha ya Kinyamwezi.

Uzinduzi wa Tafsiri ya Biblia

Uzinduzi wa tafsiri ya Biblia za vitabu vya 2 Samweli, Ruthi, na Yona kwa lugha ya Kinyamwezi umefanyika katika kanisa la Moraviani, Parishi ya Ipole, wilayani Skonge, mkoa wa Tabora. Tukio hili limeongozwa na Katibu wa Kanisa wa Wilaya ya Skonge, Mchungaji Jackson Mkombo, mbele ya waumini wa Parishi ya Ipole, chini ya Mchungaji Charles Kavula.
Kwa upande wa Chama cha Biblia cha Tanzania, walihudhuria wawakilishi kadhaa akiwemo Meneja wa Tafsiri wa Chama hicho, Dada Leah Kiloba, pamoja na Mchungaji Samweli Mshana, ambaye ni Meneja wa Mahusiano na Makanisa. Pia, Mwinjiristi Choyo Sabanja alihudhuria kama mwakilishi wa meneja wa Uenezi na Masoko. Watafsiri wa Biblia walioshiriki katika kazi ya kutafsiri vitabu hivi walikuwepo pia katika hafla hiyo.

Hafla ya Uzinduzi

29 Septemba 2024

20240929 120154 scaled

Hafla ya uzinduzi wa tafsiri ya vitabu vya Biblia kwa lugha ya Kinyamwezi ilifanyika katika kanisa la Moraviani, Parishi ya Ipole. Tukio hili lilihudhuriwa na viongozi wa kanisa, wawakilishi wa Chama cha Biblia cha Tanzania, na watafsiri wa Biblia.

HABARI KAMILI

IMG 8635 scaled

Chama cha Biblia cha Tanzania kimefanya uzinduzi wa sehemu ya Biblia za vitabu vya 2 Samweli, Ruthi, na Yona kwa lugha ya Kinyamwezi. Uzinduzi huo umefanyika katika kanisa la Moraviani, Parishi ya Ipole, wilayani Skonge, mkoa wa Tabora. Tukio hili limeongozwa na Katibu wa Kanisa wa Wilaya ya Skonge, Mchungaji Jackson Mkombo, mbele ya waumini wa Parishi ya Ipole, chini ya Mchungaji Charles Kavula.

Kwa upande wa Chama cha Biblia cha Tanzania, walihudhuria wawakilishi kadhaa akiwemo Meneja wa Tafsiri wa Chama hicho, Dada Leah Kiloba, pamoja na Mchungaji Samweli Mshana, ambaye ni Meneja wa Mahusiano na Makanisa. Pia, Mwinjiristi Choyo Sabanja alihudhuria kama mwakilishi wa meneja wa Uenezi na Masoko.

MG 8728 scaled
MG 8699 scaled

Watafsiri wa Biblia walioshiriki katika kazi ya kutafsiri vitabu hivi walikuwepo pia katika hafla hiyo. Wakiwa wameongozwa na Mratibu wao, Mchungaji Christe Katuma wa Kanisa la Moravian Tabora mjini, walihusisha Mchungaji Elack Kadubula wa Kanisa la TAG Ipuli, Tabora, Mchungaji Ellen Mpasi wa Kanisa la Moraviani Skonge Mission, na Mchungaji George Ruvula wa Kanisa la Moraviani Tabora mjini. Mwakilishi wa wahakiki, Mchungaji Festo Karangu wa Kanisa la Pentekoste Ipole, Skonge, Tabora, naye pia alishiriki.

Tafsiri ya Biblia kwa lugha ya Kinyamwezi ilianza mwezi Machi mwaka 2020, na hadi sasa, watafsiri wamefanikiwa kukamilisha vitabu vinne, ambavyo ni 1 Samweli, 2 Samweli, Ruthi, na Yona. Uzinduzi wa vitabu hivi umechochea zaidi jitihada za kuendelea na mchakato wa kutafsiri Biblia nzima kwa lugha ya Kinyamwezi.

MG 8712 scaled
MG 8707 scaled

Meneja Tafsiri wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Dada Leah Kiloba, alitoa ombi kwa kanisa kuendelea kupitia vitabu vilivyozinduliwa ili kama kuna makosa yoyote, yarekebishwe kabla ya Biblia nzima kukamilika. Lengo ni kuhakikisha kuwa Biblia inatolewa bila makosa yoyote ambayo yanaweza kupotosha maana ya Neno la Mungu.

Mchungaji Samweli Mshana, Meneja wa Mahusiano na Makanisa wa Chama cha Biblia cha Tanzania, aliomba ushirikiano wa kanisa katika kuiunga mkono kazi za Chama cha Biblia kwa michango, maombi, na kuwa wanachama wa Chama cha Biblia. Pia alikumbushia umuhimu wa kuadhimisha Juma la Biblia ili kusaidia kuhakikisha Neno la Mungu linafikia watu wote nchini Tanzania.

MG 8731 scaled
MG 8739 scaled

Katika hafla hiyo, Mchungaji Mshana aligawa pia Biblia za Mpiga Mbiu (Proclaimer), ambazo ni Biblia zinazoongea kwa lugha ya Kinyamwezi na Kiswahili. Biblia hizi ni muhimu kwa watu wasiojua kusoma na kuandika, au wenye changamoto mbalimbali, ili waweze kusikia na kufahamu Neno la Mungu kwa urahisi zaidi.

HABARI KATIKA PICHA

Ungana Nasi Katika Kazi ya Mungu

Uzinduzi wa Mpango wa kuwafikia wanafunzi kupitia Biblia Inayoongea

Uzinduzi wa Mpango wa kuwafikia wanafunzi kupitia Biblia Inayoongea

Scripture Union Lunch scaled

Umoja wa Kujisomea Biblia Tanzania (Scripture Union Tanzania), kwa kushirikiana na Chama cha Biblia cha Tanzania na Talking Bible International, wamezindua rasmi mpango wa kuwafikia watoto mashuleni kwa kupitia Biblia Inayoongea. Uzinduzi huu ulifanyika tarehe 07 Septemba 2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Edmund Rice Sinon, jijini Arusha, chini ya uongozi wa Askofu Abel Mollel wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati.

Lengo kuu la mpango huu ni kuyafikia mashule yote nchini Tanzania, kwa lengo la kurejesha maadili mema katika jamii na taifa kupitia mafundisho ya Neno la Mungu. Kwa sasa, mradi huu utaanza kutekelezwa katika mikoa ya Arusha na Manyara kabla ya kuenea nchi nzima.

Katika hafla ya uzinduzi, viongozi na wageni mashuhuri walihudhuria, wakiwemo:

– Askofu Paul Akyoo, Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Meru na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Umoja wa Kujisomea Biblia Tanzania.

– Dkt. Alfred Elias Kimonge, Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania.

– Dada Rhoda, Mwakilishi kutoka Chama cha Biblia cha Marekani.

– Dada Stella Mtui, Katibu wa Umoja wa Kujisomea Biblia Tanzania.

– Dkt. Nancy Kahuthia, Mwakilishi wa Umoja wa Kujisomea Biblia duniani.

– Kaka Paul Lindberg, Mkurugenzi wa Talking Bible International kwa eneo la Afrika.

– Kaka Teddy Tewodres, Mwakilishi kutoka taasisi ya Talking Bible International eneo la Afrika Mashariki.

Uzinduzi huu unatoa matumaini ya kuleta mabadiliko chanya kwa kizazi kipya kupitia mafundisho ya Biblia na kuimarisha misingi ya maadili katika jamii ya Watanzania.

JCO9752 scaled
JCO9776 scaled
JCO9632 scaled
JCO9722 scaled
JCO9716 scaled
JCO9827 scaled
JCO9810 scaled

Kuhusu Umoja wa Kujisomea Biblia Tanzania

Umoja wa Kujisomea Biblia Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali linalolenga kueneza mafundisho ya Neno la Mungu kwa watoto na vijana mashuleni. Kupitia mpango wa Biblia Inayoongea, tunalenga kurejesha maadili mema katika jamii na taifa kwa ujumla.
Mpango wa Biblia Inayoongea unalenga kufikia mashule yote nchini Tanzania, kwa kuanzia na mikoa ya Arusha na Manyara. Lengo kuu ni kuimarisha misingi ya maadili kwa kizazi kipya kupitia mafundisho ya Biblia.

Uzinduzi wa Mpango wa Biblia Inayoongea

07 Septemba 2024

JCO9583 scaled

Uzinduzi wa mpango wa Biblia Inayoongea ulifanyika tarehe 07 Septemba 2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Edmund Rice Sinon, jijini Arusha. Hafla hii ilihudhuriwa na viongozi na wageni mashuhuri wakiwemo Askofu Abel Mollel wa KKKT, Dkt. Alfred Elias Kimonge, Dada Rhoda, Dada Stella Mtui, Dkt. Nancy Kahuthia, Kaka Paul Lindberg, na Kaka Teddy Tewodres.

Viongozi na Wageni Mashuhuri

Hafla ya uzinduzi wa mpango wa Biblia Inayoongea ilihudhuriwa na viongozi na wageni mashuhuri kutoka taasisi mbalimbali, wakionesha umoja na mshikamano katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii ya Watanzania.

Askofu Paul Akyoo
Askofu Paul Akyoo

Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Meru na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini

Dkt. Alfred Elias Kimonge
Dkt. Alfred Elias Kimonge

Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania

Dada Rhoda

Mwakilishi kutoka Chama cha Biblia cha Marekani

Dada Stella Mtui
Dada Stella Mtui

Katibu wa Umoja wa Kujisomea Biblia Tanzania

JCO9804 scaled

Vipengele Muhimu vya Mpango

Biblia Inayoongea

Mpango huu unalenga kuwafikia watoto mashuleni kwa kutumia Biblia inayosikika, ili kuwasaidia kuelewa na kuishi mafundisho ya Neno la Mungu.

Kuimarisha Maadili

Kupitia mafundisho ya Biblia, mpango huu unalenga kurejesha maadili mema katika jamii na taifa kwa ujumla.

Kufikia Mashule Yote

Mpango huu utaanza kutekelezwa katika mikoa ya Arusha na Manyara, na baadaye kuenea nchi nzima, kuhakikisha kila mtoto anapata fursa ya kusikia Neno la Mungu.

Maoni na Ushuhuda

“Mpango wa Biblia Inayoongea ni muhimu sana kwa kizazi kipya. Unaleta matumaini ya mabadiliko chanya katika jamii yetu.” – Askofu Abel Mollel
“Ninaamini kwamba kupitia mpango huu, watoto wengi wataweza kuelewa na kuishi mafundisho ya Biblia, na hivyo kuimarisha maadili yao.” – Dkt. Nancy Kahuthia
“Uzinduzi wa mpango huu ni hatua kubwa katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii yetu. Tunatarajia kuona matokeo mazuri.” – Kaka Paul Lindberg

Changia Mpango wa Biblia Inayoongea

Mkutano Mkuu (AGM) 2023

Mkutano Mkuu (AGM) 2023

Kupambana na Upotoshaji Kuhusu Neno la Mungu

Soma Biblia yenye Nembo ya Chama cha Biblia Tanzania

Katika zama ambazo habari potofu kuhusu Neno la Mungu zimeenea, ni muhimu kusoma Biblia zenye nembo ya Chama cha  Biblia cha Tanzania. Hii inahakikisha uhalisi na ufuasi wa mafundisho ya kweli ya Biblia.

Uzima Tele Bible 1
BST IMAGE

Ushauri wa Askofu Mark Malekana

Wakati wa mkutano huo uliofanyika Mei 17, 2024, Askofu Mark Malekana, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia cha Tanzania, alisisitiza umuhimu wa kusoma Biblia zenye nembo ya Chama cha Biblia. Uku akiangazia suala linalokuwa la habari potofu kuhusu Neno la Mungu, haswa kwenye mitandao ya kijamii.

Askofu Malekana aliwataka Wakristo na jamii ya Watanzania kuwa makini na kuhakikisha wanasoma Biblia halisi. Alisisitiza kuwa nembo ya Chama cha Biblia Tanzania ni alama ya uaminifu na uhalisi, hivyo kuwasaidia waumini kuepukana na mitego ya mafundisho potofu.

MG 0890 scaled
MG 1695 scaled

Katika Mkutano huo Mahubiri yaliongozwa na Askofu Dastani Banji Mhadhiri Chuo Kikuu cha St.John ambapo aliwaasa kufanya Kazi kwa pamoja kwa sababu tunapofanya Kazi kwa pamoja watu wa MUNGU tunajengana.

“Kufanya kazi pamoja ni kitu cha msingi ambacho Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe ametuachia kielelezo Kwa timu ambayo inafanya kazi pamoja nae na hata alipoondoka kazi inaendelea na sisi leo kama timu pia tunaendeleza kazi hiyo” amesema
Aidha amesema kuwa kazi inayofanywa na Chama cha Biblia cha Tanzania inaendeleza kazi ya Kristo katika kuujenga mwili wa Kristo, katika kutafsri,  kuhifadhi, kuandika, na kueneza. “Majukumu haya ni majukumu ya pamoja tunawezeshana katika safari hii na watu wanaofanya kazi katika timu wana nia moja ya kuinua Chama cha Biblia cha Tanzania ili Biblia imfikie mtu wa MUNGU” amesema

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania Dkt.Alfred Kimonge akisoma Taarifa ya Chama hicho ya kuanzia Januari 1, hadi Disemba 31 Mwaka 2023 amesema waliungana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwafariji wananchi wa katesh mkoani Manyara waliopatwa madhila yaliyotokana na maporomoko ya udongo yaliyosababisha maafa makubwa yakiwemo Vifo vya Ndugu zetu, Makazi,Mifugo,chakula na mali.

MG 0935 scaled
MG 0926 scaled

Dkt. Kimonge ametaja baadhi ya misaada hiyo kuwa ni pamoja na Biblia UV05 pisi 100 zenye thamani ya shilingi 2,700,000,Tenzi za rohoni pisi 120 zenye thamani ya shilingi 360,000
Pia ameongeza kuwa walitoa maneno ya Hekima 300 yenye thamani ya shilingi 1,500,000 na bati G 30 mita 3 pisi 304 zenye thamani ya shilingi 6,042,000

Katika Salamu zilizotolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Kilimanjaro Dkt.Stanley Hotay katika Mkutano huo amewasihi wanachama wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania kufanya Kazi ya kueneza ujumbe wa Chama Cha Biblia kupitia makanisani, katika maeneo ya Mikoa, Wilaya, kata, Mitaa na Vitongojini.

MG 1983 1 scaled

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama Cha Biblia Cha Tanzania Mhe.Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza katika Mkutano huo wa mwaka wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania uliofanyika Mei 17,2024 katika Ukumbi wa Kanisa la KKKT jijini Dodoma 

WAZIRI MKUU MSTAAFU JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA AMEAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA

MG 1771 scaled

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama Cha Biblia Cha Tanzania Mhe.Joseph Butiku akitoa salaam zake katika Mkutano huo wa mwaka wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania uliofanyika Mei 17,2024 katika Ukumbi wa Kanisa la KKKT jijini Dodoma 

MG 1915 scaled

Mhazini wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania Fr.Chesco Msaga akiwasilisha Muhtasari wa taarifa ya Mhazini kwa mwaka ulioisha 31 Desemba 2023 kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania uliofanyika Mei 17,2024.

MG 1923 scaled

Mch. John Mnong’one Meneja Shughuli fedha na Utawala akiwasilisha ripoti ya fedha ya mwaka 2023.

16 scaled

Askofu wa Jimbo la Dodoma kanisa la Full Gospel Bible Fellow ship Neema Mduma akitoa salaam zake katika Mkutano huo wa mwaka wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania uliofanyika Mei 17,2024 katika Ukumbi wa Kanisa la KKKT Jijini Dodoma.

13 1 scaled

Makamu mwenyeki wa Chama Askofu Amos Muhagachi akimvisha Beji Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mhe. Jaji Joseph Sinde Walioba na kumkabidhi Biblia.

MG 1730 scaled

Katika salam zake Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Kilimanjaro Dkt.Stanley Hotay katika Mkutano huo amewasihi wanachama wa Chama Cha Biblia Cha Tanzania kufanya Kazi ya kueneza ujumbe wa Chama Cha Biblia makanisani na kila mahali.

Gundua Mkusanyiko Wetu wa Biblia

Chama cha Biblia cha Tanzania na baadhi ya Picha Biblia

BIBLIA SUV
Biblia ya Zip
Copy of Biblia ya button
HOLY BIBLE
AWALI
Biblia ya button
SEHEMU BIBLIA
Uzima Tele Bible
SUKUMA
MAFUNZO

Tunza Ukweli: Nunua Biblia Yako Leo