Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.
Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”
Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.
MPANGO WA MSAMARIA MWEMA.
Katika kipindi cha mwaka 2020 kupitia mpango wa Msamaria mwema Chama cha Biblia kiliweza kupata fedha kidogo kutoka UBS fedha iliyotuwezesha kutoa mafunzo ya UKIMWI kwa jamii kwa kushirikiana na makanisa, misikiti na wadau wengine walioko katika mapambano ya ugonjwa...
MAHAFALI YA WAHITIMU WA CHIBWEDA AWAMU YA TATU GAIRO TAREHE 27/02/2021.
Na Felix JonesWakagulu wapatao 756 wanawake wakiwa 550 na wanaume wakiwa 206 waliojiunga na mpango wa kujifunza kusoma na kuandika (LWA Kikagulu) mnamo tarehe 15/06/2020 hadi tarehe 30/11/2020 hatimaye walihitmu mafunzo hayo huku wakiwa na furaha kwa kujua kusoma na...
Uzinduzi wa Agano Jipya la Kiha
Tunakualika katika: Uzinduzi wa Agano Jipya la Kiha (INSEZERANO NSHASHA) Karibu Ushiriki nasi Jumapili, Novemba 22, 2020 Imetafsiriwa na Chama cha Biblia cha Tanzania Mahali: Kanisa Katoliki Kasulu Mjini – Kigoma Saa 03:00 Asubuhi – 08:00 Mchana Tukio la bure...
HOTUBA YA DR. ALFRED E. KIMONGE KATIBU MKUU WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA: KWENYE IBADA NA SHEREHE YA UZINDUZI WA BIBLIA YA KIDATOOGA TAREHE 04 OKTOBA 2020.
Nawasalimu wote katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, na kipekee ninamsalimu Baba Askofu Nicholaus Nsanganzelu na wote waliongozana naye. Bwana Yesu apewe sifa. Ninazungumza kwa ridhaa ya Baraza la Wakurugenzi wa Chama cha Biblia cha Tanzania ambao wanawakilisha...
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.
Donate Today or Get Involved