Tunakualika Karibu Ushiriki nasi katika
Uzinduzi wa Biblia ya Kisukuma
Jumapili, Juni 27, 2021
Mahali: KANISA LA AIC MISSION MAKONGOLO – MWANZA
Saa 08:00 Mchana – 12:00 Jioni
Tukio la bure kabisa
Imetafsiriwa na Chama cha Biblia cha Tanzania
Jinunulie Biblia yako katika lugha yako ya mama
Pia kinawakaribisha wanachama wote wa Chama cha Biblia walioko mkoa wa Mwanza kwenye uzinduzi wa Biblia ya Kisukuma.
Uzinduzi huo utafanyika katika kanisa la AIC Makongoro, Jumapili tar.27.6.2021 kuanzia saa 8 mchana hadi 12 jioni.
Muda huu utawapa nafasi waumini kutoka madhehebu mbali mbali kuweza kushiriki tukio hili, baada ya kumaliza ibada za Jumapili ndani ya makanisa yao.
Wanachama wote mnakaribishwa kushiriki tukio hili muhimu na la kihistoria kwa Chama cha Biblia, Kanisa na jamii nzima ya Kisukuma.
Upatapo taarifa hii mkaribishe na mwenzako, Wakristo kutoka madhehebu yote mnakaribishwa.
Tuunge mkono kwa kushiriki kikamilifu katika uzinduzi wa Biblia hii.
Tukutane AIC Makongoro kwenye uzinduzi wa Biblia ya Kisukuma Jumapili.
Karibuni 🙏🙏🙏
BIBLIA hiyo itakuwa inauzwa kwa bei ya punguzo.
Jiandae upate nakala yako pia.
Mungu ataongea na wewe kwa lugha yako ya Kisukuma.