Na Felix Jones

Wakagulu wapatao 756 wanawake wakiwa 550 na wanaume wakiwa 206 waliojiunga na mpango wa kujifunza kusoma na kuandika (LWA Kikagulu) mnamo tarehe 15/06/2020 hadi tarehe 30/11/2020 hatimaye walihitmu mafunzo hayo huku wakiwa na furaha kwa kujua kusoma na kuandika. Wakizungumzia furaha yao wameonekana wakiwa na bashasha na furaha sana kwa kupata elimu hii muhimu kwa maisha yao.

“Sasa ninaweza kusoma na kuandika na hata nikiumwa nikiandikiwa dawa sina haja ya mtu kunisomea na pia naweza kushiriki kikamilifu katika huduma za kijamii kama kupiga kura na mengine mengi katika dunia ya sasa” mama moja alisikika akisema maneno hayo kwa furaha.

Sherehe hizo zilifanyika tarehe 27/02/2021 katika Ukumbi wa Nazareth huko Gairo.

Gairo wahitimu
Mratibu wa mpango huu Mwl. Frank Makalla wa kwanza kushoto kwa waliokaa mbele akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu waliosimama nyuma wenye vyeti pamoja na mgeni rasmi Baba Askofu Paulo Jacob Mameo wa Kanisa KKKT Jimbo la Morogoro wa pili kutoka kushoto na wageni wengine walioalikwa kwenye mahafali hayo.

Christina Musa
IMG 0067

Baadhi ya wakinamama wenye umri mkubwa walioweza kushiriki na kupata vyeti vyao.

Kabla ya kugawa vyeti kulitanguliwa na hotuba na nasaa mbalimbali kutoka kwa Mgeni rasmi na viongozi mbalimbali walioalikwa kwenye mahafali haya ya tatu tangu kuanzishwa kwa mpango wa LWA Chikagulu katika mkoa wa Morogoro wilaya za Kilosa na Gairo

Canon Mstaafu Bonifas Mkami wa Kanisa Anglikani Jimbo la Morogoro

Canoni Mstaafu Bonifasi Mkami ni mmoja wa wachambuzi wa Biblia ya lugha ya Chikagulu inayoendelea kutafsiriwa katika lugha hiyo pia ni mmoja wa watu walioshiriki katika uandishi wa kitabu cha Chibweda. Akizungumza baada kupewa nafasi ya kuongoza ibada ya ufunguzi wa  maafali alisema

“Mpango huu wa akina mama kujifunza kusoma na kuandika kwa lugha yao wenyewe kupitia Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama kikaona kianzie kwetu sisi wakagulu. Baada ya hapo tukaanza uandishi wa vitabu.

Kwanza cha Mwalimu, pili cha mwanafunzi kwa neema ya Mungu, mimi nilikuwa mmojawapo. Jina la Kitabu cha Mwanafunzi na Mwalimu tulikiita “CHIBWEDA” kwa maana ya FURAHA na kuweka picha zinazotoa taswira ya Kikagulu”.

Bonifasi Mkami
Canon Mstaafu Bonifas Mkami wa Kanisa Anglikani Jimbo la Morogoro

Pia aliongeza kusema “Baada ya kukamilisha kuandika vitabu hivyo ikawa ni kazi ya kuwatafuta walimu wanaojua kuzungumza Kikagulu kwa ufasaha ili wapewe mafunzo ya kufundisha madarasa ya wanakisomo watakaojifunza kusoma na kuandika kwa kutumia lugha yao ya Kikagulu kwa kuwa ndiyo wanayoilewa Zaidi na baadae wanaweza kusoma na kuandika kwa Kiswahili na lugha zingine bila shida yoyote na baada ya hapo yakaanzishwa madarasa 10 ya kwanza na waalimu 20 katika awamu hii ya kwanza.”

Nasaha na shukrani za Canon Bonifasi Mkami

Kujua kwenu kusoma na Kuandika kutasaidia sana baada ya Biblia yetu sisi wakagulu tunayoiandaa kwa sasa na iko hatua za mwisho. Itakuwa rahisi ninyi kuisoma bila shida kwa hiyo tunatoa shukrani nyingi kwa Chama cha Biblia cha Finland na Chama cha Biblia cha Tanzania kuwezesha mpango huu katika mkoa wetu katika wilaya zetu za Kilosa na Gairo katika lugha hii ya Chikagulu Mwenyezi Mungu na awabariki sana.

Na zaidi tunawashukuru sana Mwalimu Frank Makalla mratibu wa mpango huu, Ndugu Timothy Kamau, Dr Suzan Nyaga na Ruth Munguth wa SIL Kenya.

Nawaombeni ninyi mliofaidika na mpango huu, muwe mawakili wema na waminifu katika kutunza lugha yetu.

Mratibu wa mpango huu wa LWA Chikagulu Mwalimu Frank Makalla

Akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti kwa awamu ya tatu ya wahitimu hao, Mratibu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mwl.Frank Makalla alisema

“wahitimu hao ni wa awamu ya tatu ya programu hii iliyolenga kuwajengea uwezo wanawake kusoma na kuandika ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kwenda shule wakati walipostahili kwenda shule, hii ni fursa kwao wakiwa watu wazima kuanzia aka 14 na kuendelea ingawa na wanaume wanaruhusiwa kushiriki japo si kwa kiwango kikubwa maana mpango unawalenga wanawake ambao hawakupata nafasi hiyo ya kusoma na kuandika kutokana na sababu mbali mbali.”

Mwl. Makalla
Mratibu wa mpango wa kusoma na kuandika wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Mwl.Frank Makalla akizungumza na wahitimu wa awamu ya tatu katika mahafali hayo huku akiwasisitiza wasiache kufanya yale waliyofundishwa pia wahakikishe kuwa kupitia wao watu wengi zaidi walijue Neno la Mungu.

Awamu ya kwanza waliohitimu ni jumla ya watu 97 ambapo wanawake ni 83 na wanaume ni 14 kutoka vijiji 10 vya Gairo na Kilosa ambavyo ni Gairo, Mtumbatu, Chakwale,  Mamboya, Maguha, Berega, Mwandi,Magela, Mabula, pamoja na Italagwe.

Awamu ya pili waliohitimu jumla ni 248 ambapo wanawake ni 214 na wanaume ni 34; kutoka kwenye vijiji 10 vingine ambavyo ni Mogohigwa, Kibedya, Tabuhotel, Magubike, Nguyami, Ibindo, Ntembo, Mbili, Dumbaalume, pamoja na Kiegeya.

Waliojiandikisha ni 423 kati yao waliohitimu ni 317 na ambao hawajahitimu ni 106 kutokana na changamoto mbalimbali kama vile kuhama, shughuli za mashamba, na matatizo mbalimbali ya kijamii.

Aliendelea kusema kuwa mahafali hayo ni mwendelezo wa mahafali ya awamu ya kwanza ya program hiyo iliyoanza mwaka 2017, ambapo watu 120 walijiandikisha huku watu 97 walihitimu mafunzo hayo ambayo pamoja na kuwafundisha kwa kutumia lugha ya chikagulu kama lugha ya kufundishia kwa urahisi wa kuelewa kwa lugha yao lakini kadiri wanvyoendelea kujifunza kusoma na kuandika hatimaye wanaweza kusoma na kuandka katika lugha ya Kiswahili na lugha zingine.

Alieza pia kuwa programu hiyo inafadhiliwa na Chama cha Biblia cha Finland na Chama cha Biblia cha Tanzania kikitoa usimamizi wa mpango na uratibu uku Summer Institute of linguistics (SIL) hawa wanatoa utaalamu wa waalimu pamoja na mwongozo wa kuandaa vitabu vya kufundishia.  Programu hiyo inalenga zaidi kuwainua wanawake kujifunza kusoma na kuandika ingawa na wanaume wanakaribishwa kushiriki.

DSC09837
Wahitimu wa CHIBWEDA wakiwa katika kufuatilia hotuba na nasaha za viongozi wakati wa mahafali yao iliyofanyika mnamo tarehe 27/02/2021 huko Gairo siku ya Jumamosi.

Mratibu wa mpango huu Mwl. Makalla alisema kati ya watu wazima 395 waliohitimu, wanawake ni 337 na wanaume ni 58 katika awamu hii ya tatu  

Aidha, Mwl. Makalla aliomba ushirikiano na serikali katika mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwafanya wananchi waliokosa fursa ya kusoma na kuandika kujiunga na kuendelea kupata elimu hiyo.

“Katika programu yetu hii tumekuwa tukichukua wale wenye umri wa kuanzia miaka 14 na kuendelea, hivyo wale wenye miaka 14 hadi 17, serikali inaweza kuwatambua na kuwaingiza katika mfumo wa MEMKWA katika shule za msingi kama ambavyo Serikali inaelekeza kupitia wizara ya Elimu ili wakajifunze zaidi kwa sababu sisi hapa tunawafundisha kusoma na kuandika tu huko watajifunza masomo mengine pia kama Hesabu, Sayansi, Jiografia Historia na kadhalika.

IMG 9994

Changamoto ya kwa nini wanaanza wengi na kuhitimu wachache?

Sababu zilizotajwa ni kwamba jamii ya wakagulu ni wakulima na wafugaji kwa hiyo wakati wa masika wakulima wanahamia mbali na vijiji ambako ardhi ina rutuba zaidi kwa kilimo cheye kuleta tija, pili wafugaji wanahamia maeneo mengine kutafuta malisho na maji kwa ajili ya mifugo yao  na matatizo mbalimbali ya kijamii.

Katibu wa UMAKI Ndg. Josephine Semwenda

Katibu wa idara ya maendeleo ya akina Mama UMAKI Josephine Semwenda katika Dayosisi ya Morogoro ambaye alialikwa kuwatia moyo wahitimu hao aliwasisitizia wahitimu kutokuogopa kuitangaza lugha ya Chikagulu kila mahali katika eneo lao la ukaguluni na kwingineko kwa kuwahimiza kuwa mabalozi wema katika kuilinda lugha yao isipotee, alitumia nafasi hiyo pia kuwapongeza. Wahitimu wote na kuwatakia kila lakheri katika kutekeleza majukumu ya kijamii na Kanisa.

Na hapa aliendelea kueleza zaidi kuwa

“Kwa Neema ya Mungu mmemaliza, Mungu aendelee kuwa karibu sana aendelee kuachia nguvu ya kuendelea kujifunza zaidi hata katika masomo mengine pia natamani kuona wengine hata mufike secondary kwasababu mmeshajua kusoma na baadae mtafika mbali Bwana Yesu asifiwe.  Bila shaka kujua kusoma kwenu kutawasaidia sasa kuendeleza kusoma Neno la Mungu lakini pia kuweza kusoma vitabu mbalimbali na kufahamu mambo mengi ambayo usipojua kusoma na kuandika unakuwa kama kipofu na mambo mengi yanakupita.”

Mratibu wa Umaki

Sisi Idara ya UMAKI tunashukuru kwa ajili ya neema hii. Mana ninyi wahitimu mtakuwa nguzo muhimu kwenye madarasa yetu ya UMAKI kwa kuwafundisha na kuwaongoza wanawake kwenye madarasa yetu ya umaki na kufanya mambo mbalimbali kwa ajili ya idala ya kina mama ambao wengi wao hawajajua kusoma na kuandika. Maana wengine wanapoombwa kutoa Neno au labda kufundisha jambo fulani wengine huwa hawawezi kwa sababu hawajui kusoma na kuandika sasa wale wa madarasa ya umaki mtakuwa msaada mkubwa kwao.

Mwisho kabisa niendelee kupongeza tena na tena kwa juhudi ambazo mmezichukua hata kufikia siku ya leo Mungu awabariki lakini msiishie hapo muendelee kujiendeleza ili muweze kupata mambo makubwa zaidi na Jina la Bwana litaendelea kuhimidiwa kama sasa hivi unaweza kusoma masomo ya Biblia na muweze kusoma kwingine hata katika taifa letu pia Mungu awabariki muendelee kutimiza ahadi aliyo wapatia Bwana Yesu. Amina.

Diwani wa Kata ya Gairo na katibu wa Mbunge jimbo la Gairo Ndugu Danstan Mwegoha

Diwani Danstan Mwegoha aliwashukuru sana Chama cha Biblia cha Tanzania na wote waliotia mkono katika mpango huu kwa kutambua umuhimu wa wananchi wetu wakristo wetu kuendesha mafunzo ya elimu ya watu wazima na hasa kwa kuwalenga wakinamama ni msaada mkubwa kwao, sisi tunasema wakina mama ni jeshi kubwa kwa sababu wakina mama ndiyo wenye majukumu makubwa na akina mama ndiyo wenye malezi mazuri kwa watoto. Na pia wakina mama ndiyo wanaowatunza wakina baba.

Diwani
Diwani Danstan Mwegoha akihutubia wahitmu

Na pia aliendelea kusema, Kwenye utaratibu wetu wa kutoa mikopo mara nyingi huwezi kukuta wakina baba wakiwa kwenye vikundi hivyo bali utakuta wakinamama, vijana, na walemavu, kwa hiyo wakinamama pamoja na vipato vyao vidogo wanaweza kuunganisha nguvu kwa kukopa na kulipa vizuri kuliko wakina baba.

Zamani ilikuwa ni vigumu sana kusomesha watoto wa kike kwa sababu wakina baba walikuwa wanahitaji kupokea mahali kwa kunufaika zaidi sasa bila kuangalia maisha ya binti zao kwa wakati ujao. Ninaishukuru sana serikali yetu inaonekana kuwajali na kuwalinda watoto wa kike katika kupata elimu.

Jukumu letu sisi kama serikali na Chama hiki kinacho endesha mafunzo haya tuombe sana kuwa na ushirikiano wa kutosha. Sisi kwa heshima yetu ya uongozi kwa mujibu wa nafasi yangu katika uongozi msisitizo na mkazo wa mtu kuchaguliwa na kupigiwa kura katika ngazi yoyote kuna vipengele vimeandikwa kwamba ni lazima mtu ajue kusoma na kuandika ndipo aruhusiwe kugombea nafasi na si vinginevyo kwahiyo unaweza kupata nafasi ya kuwa kiongozi kama diwani, mbunge, Rais n.k, kwa kuwa sasa mnajua kusoma na kuandika. Nawatakia Baraka za Mungu katika kuendelea mbele. Mungu awabariki sana.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nguyami.

Ndugu Mgeni rasmi, katika Kijiji changu sisi tumejiona fahari sana kwa kuwepo mpango huu na wengi waliohitimu katika mafunzo haya wamekuwa Baraka sana kwa kijiji chetu kwa maana miongoni mwao tulipata mama mmoja ambaye sasa ni mwekahazina anayeitwa Rehema Penford wa kijiji chetu. Kabla ya kupatiwa elimu hii haikuwa hivyo.

Na wananchi wengi wanawaamini watu wanaopitia elimu hii kwa kuwa wameonekana kuwa na ufahamu mkubwa na maadili mema katika Jamii yetu. Sisi kama serikali tunatafuta mpango mzuri wa kuwasaidia Chama cha Biblia cha Tanzania ili kiweze kuwafikia wengi zaidi katika Kijiji chetu.

DSC09878
Mwenyekiti wa Kijiji wa Kijiji cha Nguyami Mh. Gilbert Ngiga

Ushauri wangu kwenu wahitimu wa CHIBWEDA nawaomba sana, huu uwe mwanzo wa kutaka kujiendeleza zaidi na zaidi ili mfikie ndoto zenu. Na nyinyi pia ni rahisi serikali kuwasaidia mikopo katika kujiendeleza kwenu kwa maana kumuelimisha mwanamke umeielimisha jamii yote.

Zaidi nawapongeza tena Chama cha Biblia kwa kuwezesha mpango huu na mimi naahidi kujiunga na Chama hiki ili nami nitoe mchango wangu hata kwa pesa kidogo na Mwenyezi Mungu na awabariki sana.

Meneja wa miradi na utunishaji wa mfuko wa CBT Mchungaji Samwel Mshana.

 Mch. Samweli Mshana ambaye pia alimwakilisha Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania alisema

Mgeni rasmi, Baba Askofu Paulo Jacob Momeo, Mheshimiwa mratibu wa UMAKI, Mheshimiwa mratibu wa mpango, Mheshimiwa Canon mstahafu, mheshimiwa Mwenyekiti wa kijiji cha Nguyami, waandishi wa habari, mheshimiwa mratibu wa Chibweda, walimu na wahitimu wote, Bwana wetu Yesu Kristo asifiwe.

Kwanza, nianze kumshukuru Baba Askofu lakini pili nimshukuru sana mheshimiwa Diwani kwasababu kweli mara ya kwanza lakini kwa sababu mimi ni Meneja wa miradi hii ni mara ya kwanza kuwa na viongozi wa serikali. Mheshimiwa Diwani tunakushukuru karibu sana lakini sitaacha kushukuru pia mwenyekiti wa kijiji cha Nguyami umetoa ushuhuda chanya unao onyesha faida ya mradi huu wa CHIBWEDA na pia tuwashukuru waalimu kwa jinsi ambavyo mmekuwa mkijitoa kwa jinsi ambavyo mme onyesha juhudi sio jambo rahisi kwa kiufupi umfundisha mwanafunzi mpaka afikie hatua ya kusoma na kuandika kama ambo tumeshuhudia mama yule alivyo soma risala Mungu awabariki sana.

Rev. Mshana
Mchungaji Mshana akiongea na wahitimu wa awamu ya tatu wa Chibweda wakati mahafali hayo huko Gairo.

Wahitimu wa leo kwa niaba ya Katibu Mkuu napenda kuwapongeza.

Najua kwamba mmevumilia mambo mengi wakati wakusoma wengine mlipata changamoto za hapa na pale lakini kwa neema ya MUNGU mmeweza kuvumilia yote hayo na mmefika hatua ya mwisho.

Mimi nasema hongeleni sana na Chama cha Biblia kinaona fahari sana kwaajili yenu, mme tufanya kumtukuza Mungu kila tunapo waona hasa katika juhudi zenu na jinsi ambavyo mmefikia hatua hiyo kwakweli sisi mmejawa furaha na mmetufanya tumtukuze MUNGU kwaajili yenu na mimi kama Meneja wa miradi na muakilishi wa Katibu Mkuu sito acha kusema elimu na bidii kama  ambavyo mmesikia viongozi wanavyo sema ukisoma

Wakolosai 1 : 10 “mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;

Kwahiyo matunda ya elimu hiyo muyafanye na baadhi yenu kule kijijini hata ajira za vijiji sasa mnaachiwa maana mwazoni ilikuwa sio rahisi, na kwa sababu ya elimu muliyo ipata  imewasaidia sana na sasa mnaweza kuajirika.

Mgeni rasmi Baba Askofu Paulo Jacob Mameo

Mgeni rasmi kabla ya kutoa vyeti kwa kundi la tatu la wahitimu wa Chibweda ‘Furaha’ Baba Askofu Momeo wa KKKT aliwataka wahitimu hao kutumia maarifa hayo kujiendeleza kiuchumi na kushiriki katika uchumi wa taifa kwa ujumla.

DSC09889
Mgeni rasmi; Baba Askofu Paulo Jacob Mameo akiwa anazungumza na wahitimu wa awamu ya tatu katika mahafali hayo katika ukumbi wa Nazareth Gairo.

Baba Askofu Memo aliendelea kuwatia moyo na kuwahimiza kuendeleza kuenzi lugha yao ya Kikagulu na uku wakitumia maarifa hayo waliyoyapata kusaidia kueneza injili kwa watu wengine kwa maana sasa wanaweza kusoma na kuandika na kuwasaidia wengine uko vijijini wasiojua bado kusoma Biblia.

Mwisho nichukue nafasi hii kwa niaba yangu na Kanisa kuwashukuruni Chama cha Biblia cha Tanzania kwa jitihada nzuri ya kufuta ujinga kwa kusoma na kuandika kwa kuanzisha elimu ya watu wazima hasa kupitia kusoma Biblia. Mradi huu ni kitu kizuri sana sio tu kwa kufuta ujinga bali pia kwa kueneza maandiko matakatifu ya Neno la Mungu, Mungu aendelee kuwabariki ili habari njema iendelee kuenea kwa mbinu kama hii ya kufuta ujinga wa kutokusoma na kuandika. Mungu aendelee kuwapa maono zaidi ili huduma hii iendelee. Amina!

Katika mahali hayo burudani ilikuwa sehemu ya sherehe hizo, ambapo wahitimu hao pamoja na walimu wao walionesha michezo na nyimbo mbali mbali za kusifu na kushukuru wadau mbali mbali waliofanikisha wao kupata elimu hii.

Na hapa ni vikundi mbalimbali vya wahitimu wakitoa shukurani zao kupitia njia mbalimbali zikiwemo vile nyimbo, ngonjera pamoja na usomaji wa risala mbele ya mgeni rasmi.

Kikundi cha Ngoma
Wahitimu wa awamu ya tatu ‘CHIBWEDA’ wakiimba wimbo maalumu wa kukishukuru Chama cha Biblia cha Finland na Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kuwaletea mpango huu wa kujifunza kusoma na kuandika.
Wahitimu Chibweda 2021wakisoma Risala 1
Pichani, ni wahitimu wa awamu ya tatu Chibweda, wakisoma Risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa sherehe hiyo.
× How can I help you?