Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.
Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”
Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.
Adult villagers in Gairo given another chance to learn how to read, write.
Under Literacy Women in Africa Program (LWA) Adult Villagers in Berega Gairo Morogoro Tanzania given another chance to learn how to read and write. ADULT villagers in Gairo District in Morogoro Region who missed the formal primary education have another chance to...
Kagulu Literacy Class Graduation
On Saturday, March 23rd, 2019 at Berega Morogoro, will be the graduates of literacy training and the training supervisor is Mwl. Frank Makalla and the guest will be the General Secretary of the Bible Society of Tanzania who is Ndg. Alfred Kimonge. We welcome you...
Masomo ya uponyaji wa vidonda vya nafsi.
Tunashukuru Sana kwa jinsi Chama Cha Biblia cha Tanzania kinavyojali na kuwahudumia watu mbalimbali. Pichani ni sehemu ya wakristo wa Parish ya Iringa Road KKKT. Ambao wanafundishwa masomo ya uponyaji wa vidonda vya nafsi.Masomo haya ni kwa faida yao nabaadae wawe...
SEMINA YA UPONYAJI YA VIDONDA VYA NAFSI (TRAUMA HEALING) ILIYOFANYIKA WILAYANI MAGU MKOANI MWANZA
Picha hizi zinaonyesha jinsi Wawezeshaji wa Uponyaji wa vidonda vya Nafsi wa kutoka Mkoa wa Mara walivyokuwa na Furaha kubwa, mara baada ya kumaliza semina yao ya kutiwa moyo juu ya kazi yao ngumu ya uponyaji wa vidonda vya nafsi.Semina hii ilifanyika huko Magu Mkoani...
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.
Donate Today or Get Involved