Heri ya Siku ya Wanawake Duniani (IWD)
Watoto katika kituo cha SAAFAD Membe.
Kituo hiki kiko Kijiji cha Membe, Kata ya Membe na Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma.

Katika kusherekea sikukuu ya wanawake Duniani, wanawake wa Chama cha Biblia cha Tanzania, wadau na Chama cha Biblia cha Tanzania wamejumuika leo tarehe 08/03/2022 kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wanaolelewa kwenye kituo cha SAAFAD Membe.
Katika siku hiyo wanawake wa Chama cha Biblia wamepata fursa ya kukutana na watoto zaidi ya 100 wanaolelewa kwenye kituo hiko ambao ni yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ilikuwa ni ya furaha kwa wanawake, watoto wenyewe pamoja na wageni wengine walioshiriki kwenye sherehe hiyo.
Wanawake hao walipata mda wa kuzungumza na watoto hao kuhusu mada mbali mbali zikiwemo athari za mimba utotoni, umuhimu wa kujitunza na jinsi kuepukana na vishawishi wanavyokutana navyo katika makuzi yao na kuliishi Neno la Mungu wanalofundishwa na walezi wao kituoni hapo.
Watoto walipata muda wa kushirikisha story za maisha yao. Huyo binti anashuhudia namna mama yake alivyomkataa na wadogo zake mara tu baba alipofariki na mama kuolewa na mwanaume mwingine. Wote wanalelewa kwenye kituo cha SAAFAD.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni

“Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.”


Baadhi ya watoto walifanya matembezi wakiongozwa na Mch.Samweli Mshana wa Chama cha Biblia Tanzania.


Uzinduzi wa Biblia ya Kihehe
Biblia kwa Lugha ya Kihehe Yazinduliwa Rasmi Iringa – Miaka 30 ya Kazi Yafikia TamatiNa Mwandishi Wetu, Iringa 29 Juni 2025Dr. Alfred Elias Kimonge akikabidhi Biblia kwa ajili ya kuzinduliwa.Mgeni rasmi. Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

UZINDUZI WA BIBLIA YA KIKAGULU
UZINDUZI WA BIBLIA YA KIKAGULU – WILAYA YA GAIRO, MKOA WA MOROGORO.Tarehe: 8 Juni 2025Mahali:Gairo, Morogoro Uzinduzi wa Biblia ya Kikagulu Unasisitiza Uthamini wa Lugha za AsiliDr. Alfred Elias Kimonge akikabidhi Biblia kwa ajili ya kuzinduliwa.Ibada na kubariki wa...

Mkutano Mkuu wa 39 wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa Mwaka 2024
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia Tanzania, Askofu Dkt. Mark Malekana amesema katika ulimwengu huu ambao jamii inalalamika kuhusu kuporomoka kwa maadili kutokana na mambo ya ajabu yanayotokea, nguvu inayoweza kusadia jamii inayoathirika ni Neno la Mungu pekee....

Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) 2024
info@biblesociety-tanzania.org(+255) 784-683 1209th Road /14 Hatibu, Madukani Area
Get Involved
We have Bibles in different Tanzanians languages that you can read online. You can also download Bible reading plans to guide you through the Bible.

Donate Today or Get Involved