
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia Tanzania, Askofu Dkt. Mark Malekana amesema katika ulimwengu huu ambao jamii inalalamika kuhusu kuporomoka kwa maadili kutokana na mambo ya ajabu yanayotokea, nguvu inayoweza kusadia jamii inayoathirika ni Neno la Mungu pekee.
Amesema hayo alipofungua Mkutano Mkuu wa 39 wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa Mwaka 2024 uliofanyika juzi Ijumaa Mei 30, 2025 katika ukumbi wa kanisa la KKKT jijini Dodoma.
Dkt. Malekana alisema Biblia ni maandiko matakatifu yatakayoweza kuibadilisha jamii kutoka kwenye kuwa ‘jamii ovu’ na kuwa jamii ‘inayompendeza Mungu’, hivyo ametoa wito kwa Biblia kupelekwa kwa wahitaji.
“Wito wangu mkubwa, ambao pia ni wito wa mkutano huu siku ya leo ni wito wa kupeleka Biblia kwa vijana, kupeleka Biblia kwa watoto, kupeleka Biblia magerezani, kupeleka Biblia kwa kila mtu kwa maana Biblia ndio italiponya taifa letu,” alisema Dkt. Malekana na kuongeza:
“Tunashukuru katika kuendesha mambo yake kwa muda mrefu lakini tunashukuru kuona kwamba makusanyo ya Watanzania wenye kutoka madhehebu mbalimbali na watu binafsi yameongezeka, sisi Watanzania tunaweza kutegemeza chama chetu cha Biblia kwa michango yenu kama wanachama, kwa michango yetu kama kanisa sambamba na michango kutoka kwa waumini mbalimbali wa madhehebu yote, Mungu akusaidie.”

“Unaposaidia Chama cha Biblia cha Tanzania, unaokoa kanisa na unaokoa Taifa la Tanzania, Mungu akubariki unaposaidia Chama cha Biblia cha Tanzania. Hivyo, mimi kama Mwenyekiti nawashukuru sana wajumbe waliohudhuria, nawashukuru kwa mwitikio wenu.”

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Dkt. Alfred Kimonge akisoma Mukhtasari wa Mkutano Mkuu wa chama kwa Mwaka 2023, alisema chama kimeendelea kushirikiana na shirika la ‘Talking Bible International’ kwa kuendelea kuwa kituo cha kupokea, kuandaa na kusambaza Biblia inayoongea kwa wahitaji katika nchi za Mashariki,Kati, Kaskazini na Magharibi mwa Afrika.
Alisema mwaka 2023 jumla ya nakala 1,404 za Biblia zinazoongea zilisambazwa katika nchi za Kenya,Uganda, Zambia, Eritrea na Niger.

Dkt. Kimonge alisema nchini Tanzania jumla ya nakala 1,800 zilisambazwa ambapo kupitia mradi huo wa makundi ya watu wasioona na wasiojua kusoma, yameweza kufikiwa kwa kushirikiana na makanisa, taasisi za dini na watu binafsi wa kujitolea (volunteers).
Aidha, Dkt. Kimonge alisema mradi wa Kamusi ya Biblia kutoka Kiebrania/Kiyunani _Kiswahili (Scholarly Dictionary) ambao unahusu kuundaa Kamusi ya Kiebrania/Kiyunani kwenda Kiswahili (Hebrew/Greek-Shwahili ) ilikamilika Septemba 2023.
Alisema mradi wa Elimu kwa Wanawake (Literacy for Women in Africa), Chama cha Biblia Tanzania kimeendelea kuutekeleza katika Halmashauri ya Wilaya ya Gairo na Kilosa. Lengo la mradi huo ni kuwasadia wanawake na wasichana ambao hawajui kusoma na kuandika kutokana na mazingira tofauti mbalimbali.

Dkt. Kimonge aliyataja mazingira hayo kuwa pamoja na tamaduni ambazo jamii iliamini mtoto wa kike hatakiwi kupelekwa shule, hasa vijijini.
Alisema tamaduni hizo zilisababisha jamii kutoona umuhimu wa elimu na kujishughulisha na shughuli nyingine kama kilimo na ufugaji.

Naye Mhazina wa Chama cha Biblia Tanzania, Fadha Chesco Msaga akisoma taarifa ya ya fedha kwa mwaka ulioishia Desemba 31, 2024 alisema: “Tunashukuru Mungu kwa mwamko ulionyeshwa na makanisa kwa kipindi cha mwaka 2024 katika kuchangia Biblia kwa watoto, vijana na wafungwa”.
















Related Articles
UZINDUZI WA BIBLIA YA KIKAGULU
UZINDUZI WA BIBLIA YA KIKAGULU – WILAYA YA GAIRO, MKOA WA MOROGORO.Tarehe: 8 Juni 2025Mahali:Gairo, Morogoro Uzinduzi wa Biblia ya Kikagulu Unasisitiza Uthamini wa Lugha za AsiliDr. Alfred Elias Kimonge akikabidhi Biblia kwa ajili ya kuzinduliwa.Ibada na kubariki wa...
Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) 2024
info@biblesociety-tanzania.org(+255) 784-683 1209th Road /14 Hatibu, Madukani Area
Maafali ya Saba ya Mradi wa Literacy for Women in Africa
Maafali ya Saba ya Mradi wa Literacy for Women in Africa.Mahali: ukumbi wa Nazareti, wilayani Gairo, mkoani Morogoro.Hafla hii ilihudhuriwa na viongozi wa dini na serikali wakiwemo wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa (W) ya Gairo pamoja na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji...