CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA CHASHEREHEKEA MAHAFALI YA WANAKISOMO GAIRO – MOROGORO

Gairo, Morogoro | 05 Januari 2026

Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT) kimefanya mahafali ya nane ya wanakisomo wa mradi wa Literacy for Women in Africa katika Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro, tarehe 05 Januari 2026. Sherehe hiyo ilihusisha wahitimu wa elimu ya watu wazima waliopata mafunzo ya kusoma na kuandika kupitia mradi huo unaolenga kuwawezesha wanawake na wasichana ambao hawakupata fursa ya elimu rasmi.

IMG 5131 scaled

Sherehe hiyo ilifunguliwa rasmi kwa risala iliyosomwa mbele ya mgeni rasmi, Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, ambaye aliwakilishwa na Diwani wa eneo hilo, pamoja na viongozi wa dini, viongozi wa vijiji vilivyofikiwa na mradi, na Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania aliyewakilishwa na Meneja wa Shughuli, Mchungaji John Mnong’one.

IMG 5061 scaled
IMG 5085 scaled

“Awali sikuweza kusoma wala kuandika. Kupitia mpango huu nimejifunza, na sasa naweza kusoma na kuandika kwa kujiamini. Hata nilipokwenda kupiga kura, nilijichagulia mwenyewe tofauti na zamani nilipolazimika kuchaguliwa na wengine.”

IMG 5035 scaled
IMG 5124 scaled
IMG 5153 scaled
IMG 5168 scaled

Akizungumza kupitia risala hiyo, CBT ilieleza kuwa mradi wa Literacy for Women in Africa ulianza kutekelezwa mwaka 2018 kwa kushirikiana na makanisa na wadau mbalimbali, wakiwemo Serikali za Wilaya za Gairo na Kilosa. Lengo kuu la mradi ni kuwasaidia wanawake na wasichana waliokosa elimu ya msingi kupata ujuzi wa kusoma na kuandika ili kuboresha maisha yao binafsi, kifamilia na kijamii.

Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi huo, CBT imewafikia wanakisomo 3,200 wakiwemo wanawake wengi na wanaume wachache. Kutokana na uhitaji mkubwa uliojitokeza kwa wanaume wasiojua kusoma na kuandika, mradi ulipanua wigo wake na kuanza kuandikisha wanaume waliokuwa tayari kujiunga na madarasa ya elimu ya watu wazima (CHIBWEDA).

IMG 5049 scaled

Kwa mwaka 2025 pekee, mradi uliweza kufanya uhamasishaji na kuandikisha wanakisomo 595 (wanaume 145 na wanawake 450), kuanzisha madarasa mapya katika vijiji vya Mkalama, Masenge, Kinyolisi, Kisitwi, Nyangala na Luhwaji, pamoja na kutoa mafunzo kwa waalimu 30 wa elimu ya watu wazima yaliyofanyika Dodoma kwa muda wa wiki mbili. Aidha, vitabu vya kujifunzia (Primer books) vilichapishwa na kugawiwa kwa wanakisomo wote waliosajiliwa, na vitabu 300 vya hadithi (story books) vilitolewa kwa wahitimu kwa matumizi baada ya kuhitimu.

Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 366 walikabidhiwa vyeti, ikiwa ni ishara ya mafanikio ya mradi katika kuongeza idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika kwenye jamii.

IMG 5054 scaled

Mradi huo umeleta matokeo chanya makubwa, yakiwemo kuongezeka kwa ujasiri wa wanawake kushiriki katika uongozi wa jamii, ushiriki wao katika shughuli za maendeleo, siasa na Kanisa, pamoja na kuimarika kwa uelewa wa jamii katika masuala ya afya, kilimo, ufugaji, mazingira na haki za kiraia. Wanufaika pia wameeleza kuwa mradi umewasaidia kusoma na kuelewa Neno la Mungu, kujiamini zaidi na kuimarisha mahusiano ndani ya familia na jamii kwa ujumla.

Rose Mrema

Literacy for Women coordinator, The Bible Society of Tanzania

Hata hivyo, CBT ilibainisha changamoto kadhaa, ikiwemo wanakisomo 185 kuacha masomo kati ya waliojiandikisha, uhitaji mkubwa wa mradi katika mikoa mingine nchini, upungufu wa fedha za kuendesha shughuli za mradi, pamoja na changamoto za miundombinu ya usafiri katika baadhi ya maeneo.

IMG 5155 scaled
IMG 5163 scaled
16
IMG 4950 scaled
IMG 5172 scaled
IMG 5031 scaled
IMG 5041 scaled
IMG 5009 scaled