Taasisi yetu kwa mwaka uliopita uliambatana na Baraka zake. Muungano wetu wa vyama vya Biblia ulimwenguni ulituweka katika mpango wa kuwafikia watu milioni moja ulimwenguni walio katika mazingira magumu au walengwa ambao hawana uwezo wa kununua Biblia. Tanzania tulipewa nakala 50,000 za Biblia. Biblia hizo tulizigawa katika mashule na magereza.


Mch. John Mnong’one akimkabidhi SSP Nelson Kanyungu askari anayehudumia Ibada katika gereza la Kigoma. Picha ya Pili akikabidhi viongozi wa Makanisa yaliyomo katika Kambi ya wakimbizi Nyarugusu Kasulu



Watoto wa shule ya Mshingi Suguta Kongwa wakifurahia kupata Biblia.
Uenezaji wetu Mwaka huu ulikuwa kama ifuatavyo.
Biblia 500, 0000
Agano Jipya 59,000
Sehemu za Bibia portion 1,800

Akina mama hawa wa Kabila la Kibarbaig walisikiliza mpango wa FCBH walihitimu kupewa Biblia bure. Walikataa kupokea Biblia ya bure wakalipia Biblia zao kwa furaha.
Tulipowambia kuwa wana stahili,
walisema heri kutoa kuliko kupokaea
BIBLIA INAYOONGEA.
Tunamshukuru Mungu kwa taasisi yetu kuingia mkataba na Shirika la Talking Bible International kuwa Chama cha Biblia cha Tanzania tumekuwa kituo cha kuandaa na kugawa Biblia TB inayoongea kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Mpaka sasa tumeandaa na kugawa nakala 450 za TB kwa nchi za Kenya, Uganda na Zambia.

Hapa watumishi wa Chama cha Biblia wakiandaa TB katika lugha ya Kibemba na Kitonga tayari kwa kuzipeleka Zambia
Mwaka huu CBT kiliendesha semina kwa wasioona 18 na kuwafundisha kusikiliza Agano Jipya .

Give Today
Children
Prison
Membership
Youth
Blind
Other