MRADI WA TALKING BIBLE
Mradi huu wa Talking Bible umepokelewa vizuri kwenye makanisa ya kigoma, na idadi ya makundi tuliyonayo ni 142. Pia mradi huu unaendelea vizuri na umeleta mabadiriko makubwa kwenye makanisa na kwenye jamii.
Ripoti toka mkoa wa Kigoma, Mkoa huu hadi sasa tuna vikundi 142 watu wanapenda sana huduma hii.
Zifuatazo ni shuhuda za watu wawili walio badirishwa na mpango huu. Ushuhuda wa Dada Recho Samsoni yeye alikuwa hapendi kufika kwenye vipindi Kanisani, lakini baada ya kauanzisha mpango huu sasa anafika Kanisani na pia anasema alikuwa halali nyumbani makazi yake makuu ni kwenye madanguro ya kujiuza sasa ameachana nayo ameamua kumfuata Yesu.
Ushuhuda wa ndugu Kurwa Ndabigenda amefurahia sana kujiunga na kipindi hiki
kabla hajajiunga na kipindi hiki amekuwa akinywa pombe sasa ameamua kuachana na kunywa pombe.
NB: Mpango huu Makanisa ya Kigoma yameupokea vizuri sana na wachungaji wameahidi kutoa ushirikiano.
Coverage
Viongozi wa kikundi cha mshikamano talking Bible Kigoma
Kaka Kurwa ni Mwenyekiti wa Kikudi cha Talking Bible (Biblia Inayoongea) na Dada Rachel ni Katibu wake. Wamekuwa ngozo muhimu sasa katika jamii.
Addresses
16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area.
P.O BOX 175, Dodoma -Tanzania.
Phone
+255 (0) 765 530 892
info@biblesociety-tanzania.org