MKUTANO MKUU WA 37 WA CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA
Habari Kamili.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama
cha Biblia Tanzania, Askofu Mkuu Mark Walwa Malekana amesema chama hicho kitajitahidi kuendelea kuchapisha na kusambaza neno la Mungu ili liweze kumfikia kwa kila mtu na injili izidi kuhubiriwa.
Alisema hayo katika Mkutano
Mkuu wa Mwaka 2022 wa chama
hicho uliofanyika katika ukumbi
wa mikutano wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT) jijini Dodoma, Ijumaa wiki hii.
Malekana, ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato alisema kuwa mafanikio ya kidunia yanataka juhudi na akili zako za mtu, lakini bila Mungu juhudi na akili hizo haziwezi kumfikisha popote.
Akinukuu maandiko kutoka katika kitabu cha Kutoka 33:15, mwenyekiti huyo wa bodi aliwakumbusha washiriki wa mkutano huo na jamii kwa ujumla, kuishi kwa kumwomba Mungu.
“Katika maisha yako omba Mungu awe pamoja nawe, iwe ni biashara unafanya au utumishi popote pale. Yesu alisema pasipo mimi hamuwezi kufanya neno lolote, na sisi kama Chama cha Biblia tunamwomba Mungu awe pamoja nasi katika majukumu ya chama katika kutafsiri Biblia, kuchapisha, sambamba na kutawanya maandiko matakatifu”.
“Kizazi hiki kinatakiwa watu warudi kwenye Neno la Mungu na kumtazama Kristo, na kwa upande wetu Chama cha Biblia tunajitaidi kuchapisha na kusambaza Neno la Mungu kwa kila mtu, wakiwemo watoto, wafungwa..na vijana ni kipaumbele cha Chama cha Biblia cha Tanzania
Picha kutoka kushoto ni Dkt. Alfred E. Kimonge katibu Mkuu Chama cha Biblia cha Tanzania, wa pili kutoka kushoto ni Askofu Mkuu Mark Walwa Malekana, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia cha Tanzania, wa tatu kutoka kushoto ni Askofu Christian Ndossa wa Kanisa la Kilutheli la Kiinjili Tanzania Dayosisi ya Dodoma na Mwisho Askofu Amos Muhagachi, Makamu Mwenyekiti wa Bodi.
Askofu Christian Ndossa wa Kanisa la Kilutheli la Kiinjili Tanzania Dayosisi ya Dodoma akihudumu wakati wa mkutano huo.
Askofu Mkuu Mark Walwa Malekana, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia cha Tanzania akionesha riport ya taarifa ya fedha
Dkt. Alfred E. Kimonge katibu Mkuu Chama cha Biblia cha Tanzania, akiwasilisha taarifa ya utendaji na fedha kwa mwaka wa 2022.
Katika maisha yako omba Mungu awe pamoja nawe, iwe ni biashara unafanya au utumishi popote pale. Yesu alisema pasipo mimi hamuwezi kufanya neno lolote, na sisi kama Chama cha Biblia cha Tanzania tunamwomba Mungu awe pamoja nasi katika majukumu ya chama
katika kutafsiri Biblia, kuchapisha, sambamba na kutawanya maandiko matakatifu”.
Naye Askofu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma, Christian Ndossa alisema neno la Mungu ndio msingi na taa za miguu ya chama hicho.
Askofu Ndossa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo alisema kuwa, chama hicho kinaweza kuwa na vitabu vingi pamoja na mipango mbalimbali, lakini bila neno la Mungu kitakosa kitu cha kukisaidia.
“Tunaweza kuwa na mipango mbalimbali, tukawa na vitabu vingi, tukasoma maandiko ya wataalamu lakini tukakosa kitu
cha kutusaidia kama tutakosa neno la Mungu ambalo ndio taa ya miguu yetu na mwanga katika maisha yetu sisi tulio wanachama wa Chama cha Biblia Tanzania,”
alisema.
Askofu huyo aliwakumbusha washiriki wa mkutano huokumwomba Mungu zaidi kwa kuwa wanahubiri injili katika kizazi kinachobadilika lakini wao wanahubiri neno la Mungu lisilobadilika, jambo linaloibua changamoto mbalimbali ikiwemo lugha.
Alitoa mfano kuwa wakati wao kama chama wanajitahidi kuhubiri injili kwa lugha ya
Kiswahili inayosikika kwa watu wengi, lakini Kiswahili chenyewe kinabadilikabadilika.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Alfred Kimonge alisema wanayo
kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa rehema na baraka zake kwa mwaka wa 2022.
“Hakika umekuwa mwaka wa baraka kwetu, umekuwa mwaka wa kuinuliwa na kuendelea kufanya kazi ya Mungu kwa ujasiri na bidii baada kipindi cha mpito ambacho dunia ilikubwa na ugonjwa wa hatari wa mlipuko wa Covid-19. Hakika Mungu ni mwaminifu sana kwetu,” alisema.