CHAMA CHA BIBLIA CHA TANZANIA KIMEWAFIKIA WATU WENYE ULEMAVU.

DSC02466

Miongoni mwa malengo ya Chama Chama Biblia cha Tanzania ni pamoja na kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na neno la Mungu. Kupitia programu ama miradi mbalimbali inayofanywa na Chama Cha Biblia, hufanikiwa kuyafikia makundi mbalimbali ya watu katika jamii na miongoni mwa makundi hayo ni pamoja na walemavu ambapo ndani ya kundi la walemavu lipo kundi la vipofu yaani wasiokuwa na uwezo wa kuona. Ili kufikia azma yake ya kuhakikisha kila mtu anafikiwa na neno la Mungu watu wenye ulemavu wa macho ni kati ya kundi ambalo linatakiwa kufikiwa na huduma za Chama Cha Biblia.

Katika kulitilimiliza lengo hilo, Chama Cha Biblia cha Tanzania kupitia programu ya Biblia kwa vipofu (Braille Bible) kimefanikiwa kuwafikia watu 34 wenye ulemavu wa macho kutoka katika Kata 3 za Wilaya ya Kongwa ili kuandaa mpango wa pamoja kwa lengo la kuwapatia Braille Bible na Audio Bible ili waweze kukua kiroho.

Lakini pia walihamasishwa kuanzisha vikundi vya ‘Imani huja kwa kusikia’ kama sehemu ya wao kukutana na kujadili neno la Mungu kwa pamoja.

DSC02285Elisha Letema

Kimsingi walifurahi sana kutembelewa kwani Elisha Letema alisema “watu wenye ulemavu ni watu wanaotengwa sana na jamii kutokana na jinsi walivyo” lakini kwa kutembelewa na Chama Cha Biblia nao walijiona ni sehemu ya jamii na kusikia kupendwa mno na Mungu ambapo aliongezea kwamba mradi huu wa kuwapatia Biblia utawanufaisha sana kwani yeye anaamini hata wanadamu wakimtenga, Mungu haweza mtenga,, kwa hiyo kwa kupata Biblia itawasaidia kumjua zaidi Mungu na kumtegemea,, kumtumainia yeye daima.

DSC02331Judith Pembamoto

Lakini pia Judith Pembamoto aliongezea kwa kusema kuwa yeye hakuwa na ufahamu mkubwa sana juu ya elimu ya Mungu kwa sababu ya kukosa nyenzo ama vitabu vya dini ambapo akasema programu hii ya Braille Bible itamsaidia kumjua Mungu aliyeumba Mbingu na Dunia (Nchi)

Kitendo cha kuwatembelea na kuwafikia kiliwafanya wafurahi sana na kukishukuru Chama Cha Biblia cha Tanzania kwa kuwatembelea na kuwakumbuka kiasi cha kufungua mioyo yao na kuwa na utayari wa kushirikiana nao kwenye huduma zitolewazo na CHAMA CHA BIBLIA.

× How can I help you?