Mkutano Mkuu wa 39 wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa Mwaka 2024

Mkutano Mkuu wa 39 wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa Mwaka 2024

Mkutano Mkuu wa 39 wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa Mwaka 2024
Comments
5

Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia Tanzania, Askofu Dkt. Mark Malekana amesema katika ulimwengu huu ambao jamii inal­alamika kuhusu kuporomoka kwa maadili kutokana na mambo ya aja­bu yanayotokea, nguvu inayoweza kusadia jamii inayoathirika ni Neno la Mungu pekee.

Amesema hayo alipofungua Mku­tano Mkuu wa 39 wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa Mwaka 2024 uliofanyika juzi Iju­maa Mei 30, 2025 katika ukumbi wa kanisa la KKKT jijini Dodoma.

Dkt. Malekana alisema Biblia ni maandiko matakatifu yatakayoweza kuibadilisha jamii kutoka kwenye kuwa ‘jamii ovu’ na kuwa jamii ‘in­ayompendeza Mungu’, hivyo am­etoa wito kwa Biblia kupelekwa kwa wahitaji.

“Wito wangu mkubwa, ambao pia ni wito wa mkutano huu siku ya leo ni wito wa kupeleka Biblia kwa vija­na, kupeleka Biblia kwa watoto, ku­peleka Biblia magerezani, kupeleka Biblia kwa kila mtu kwa maana Bib­lia ndio italiponya taifa letu,” alisema Dkt. Malekana na kuongeza:

“Tunashukuru katika kuendesha mambo yake kwa muda mrefu lakini tunashukuru kuona kwamba maku­sanyo ya Watanzania wenye kutoka madhehebu mbalimbali na watu binafsi yameongezeka, sisi Watan­zania tunaweza kutegemeza chama chetu cha Biblia kwa michango yenu kama wanachama, kwa michango yetu kama kanisa sambamba na michango kutoka kwa waumini mbalimbali wa madhehebu yote, Mungu akusaidie.”

7

“Unaposaidia Chama cha Biblia cha Tanzania, unaokoa kanisa na unaokoa Taifa la Tanzania, Mun­gu akubariki unaposaidia Chama cha Biblia cha Tanzania. Hivyo, mimi kama Mwenyekiti nawashukuru sana wajumbe waliohudhuria, na­washukuru kwa mwitikio wenu.”

3

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Dkt. Alfred Kimonge akisoma Mukhtasari wa Mkutano Mkuu wa chama kwa Mwaka 2023, alisema chama kimeendelea kushirikiana na shirika la ‘Talking Bible Internation­al’ kwa kuendelea kuwa kituo cha kupokea, kuandaa na kusambaza Biblia inayoongea kwa wahitaji ka­tika nchi za Mashariki,Kati, Kaska­zini na Magharibi mwa Afrika.

Alisema mwaka 2023 jumla ya nakala 1,404 za Biblia zinazoon­gea zilisambazwa katika nchi za Kenya,Uganda, Zambia, Eritrea na Niger.

MG 5069 scaled

Dkt. Kimonge alisema nchini Tanzania jumla ya nakala 1,800 zilisambazwa ambapo kupitia mradi huo wa makundi ya watu wasioona na wasiojua kusoma, ya­meweza kufikiwa kwa kushirikiana na makanisa, taasisi za dini na watu binafsi wa kujitolea (volunteers).

Aidha, Dkt. Kimonge alisema mradi wa Kamusi ya Biblia kutoka Kiebrania/Kiyunani _Kiswahili (Scholarly Dictionary) ambao una­husu kuundaa Kamusi ya Kiebra­nia/Kiyunani kwenda Kiswahili (Hebrew/Greek-Shwahili ) ilikami­lika Septemba 2023.

Alisema mradi wa Elimu kwa Wanawake (Literacy for Women in Africa), Chama cha Biblia Tanzania kimeendelea kuutekeleza katika Halmashauri ya Wilaya ya Gairo na Kilosa. Lengo la mradi huo ni ku­wasadia wanawake na wasichana ambao hawajui kusoma na kuan­dika kutokana na mazingira tofauti mbalimbali.

MG 4908 scaled

Dkt. Kimonge aliyataja mazingira hayo kuwa pamoja na tamaduni ambazo jamii iliamini mtoto wa kike hatakiwi kupele­kwa shule, hasa vijijini.

Alisema tamaduni hizo zilisababisha jamii kutoona umuhimu wa elimu na kujishu­ghulisha na shughuli nyingine kama kilimo na ufugaji.

24

Naye Mhazina wa Chama cha Biblia Tanzania, Fadha Chesco Msaga akisoma taarifa ya ya fedha kwa mwaka ulioishia Desemba 31, 2024 alisema: “Tunashukuru Mun­gu kwa mwamko ulionyeshwa na makanisa kwa kipindi cha mwaka 2024 katika kuchangia Biblia kwa watoto, vijana na wafungwa”.

13
33
23
21
35
34
20
39
32
25
9
8
MG 4465 scaled
MG 4780 scaled
MG 4658 scaled
MG 4876 scaled
MG 4883 scaled
MG 4884 scaled
MG 4793 scaled

Related Articles

UZINDUZI WA BIBLIA YA KIKAGULU

UZINDUZI WA BIBLIA YA KIKAGULU

UZINDUZI WA BIBLIA YA KIKAGULU – WILAYA YA GAIRO, MKOA WA MOROGORO.Tarehe: 8 Juni 2025Mahali:Gairo, Morogoro Uzinduzi wa Biblia ya Kikagulu Unasisitiza Uthamini wa Lugha za AsiliDr. Alfred Elias Kimonge akikabidhi Biblia kwa ajili ya kuzinduliwa.Ibada na kubariki wa...

Mkutano Mkuu wa 39 wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa Mwaka 2024

Mkutano Mkuu wa 39 wa Chama cha Biblia cha Tanzania wa Mwaka 2024

Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia Tanzania, Askofu Dkt. Mark Malekana amesema katika ulimwengu huu ambao jamii inal­alamika kuhusu kuporomoka kwa maadili kutokana na mambo ya aja­bu yanayotokea, nguvu inayoweza kusadia jamii inayoathirika ni Neno la Mungu pekee....

Maafali ya Saba ya Mradi wa Literacy for Women in Africa

Maafali ya Saba ya Mradi wa Literacy for Women in Africa

Maafali ya Saba ya Mradi wa Literacy for Women in Africa.

Mahali: ukumbi wa Nazareti, wilayani Gairo, mkoani Morogoro.

Picture5

Hafla hii ilihudhuriwa na viongozi wa dini na serikali wakiwemo wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa (W) ya Gairo pamoja na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji pia Afisa mipango na Afisa maendeleo ya jamii ambapo waliwapongeza sana wahitimu kwa juhudi zao kubwa na kusisitiza umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii.

Chama cha Biblia, kupitia mradi wake wa Literacy for Women in Africa, kimefanikisha hatua muhimu katika kuimarisha elimu ya wanawake nchini. Mahafali ya saba ya mradi huu yaliyofanyika tarehe 23 Januari 2025 katika ukumbi wa Nazareti, wilayani Gairo, mkoani Morogoro, yaliwahitimu wanawake 353 katika ngazi ya A ya kusoma na kuandika.

Picture6
Picture4

Mradi wa Literacy for Women in Africa umeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya wanawake hawa. Wengi wao sasa wanaweza kusoma Biblia, kuendesha biashara ndogo ndogo, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii zao.

“Shuhuda kutoka kwa mmoja wa wahitimu: “Kabla ya kuanza kusoma, nilikuwa tegemezi sana. Sasa naweza kusoma na kufuatilia habari, na hata kuandika barua ya maombi ya kazi na kushiriki na mambo mbalimbali ya kijamii kama kupiga kura na kuchagua viongozi na hata kugombea nafasi za kiuongozi kama uenyekiti wa mtaa. Maisha yangu yamebadilika kabisa!”

Picture Mzee
Meza kuu wakifurahia jambo wakati wa maafali

Mahafali haya yamekuwa ushahidi tosha wa kwamba elimu ni nguvu. Chama cha Biblia kinaendelea kujizatiti kuhakikisha kuwa wanawake wengi zaidi wanapata fursa ya kujifunza na kukuza uwezo wao. Tunawashukuru sana wadau wote kwa ushirikiano wenu katika kufanikisha mradi huu.

Wahitimu
Picture ya Pamoja
2
Picture3
7

Matukio katika Picha

Comments

Uzinduzi wa sehemu ya Biblia (portion) kwa lugha ya Kiha.

Uzinduzi wa sehemu ya Biblia (portion) kwa lugha ya Kiha.

Uzinduzi wa sehemu ya Biblia (portion) kwa lugha ya Kiha.

Mahali: Kijiji cha Nyakimwe, Wilaya ya Buhigwe 

Dhehebu: Kanisa la Anglican 

IMG 0263 scaled

Maelezo ya Meneja wa Tafsiri, Leah Kiloba

Leah Kiloba alielezea maendeleo ya mradi huu, akisisitiza kuwa Chama cha Biblia kinaendelea kujitahidi kuhakikisha upatikanaji wa Biblia kwa watu wote wa madhehebu mbalimbali bila ubaguzi. Alifafanua kuwa mradi huu unalenga kumjumuisha kila Mkristo kwa kutoa nafasi sawa ya kusoma Neno la Mungu katika lugha yao wenyewe. 

Sherehe ya uzinduzi wa tafsiri ya Biblia ya Position ya Kiha (kitabu cha Yeremia) ilifanyika katika Kanisa la Anglican kijijini Nyakimwe, wilaya ya Buhigwe. Tukio hili lilihudhuriwa na waumini kati ya 400 na 700 kutoka madhehebu mbalimbali, pamoja na makanisa ya Anglican, Roman Catholic, Pentecostal, na Sabato, ambayo yalialikwa rasmi kushiriki.

IMG 0131 scaled
IMG 0066 scaled

Historia ya Mradi kutoka kwa Mchungaji Ntakije

Mchungaji Ntakije aliwasilisha historia ya mradi huu wa kutafsiri Biblia kwa lugha ya Kiha, akielezea hatua zilizochukuliwa kufanikisha kazi hii muhimu na changamoto zilizokabiliwa. Alielezea jinsi jamii imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono mradi huu.

Kusoma Maandiko na Baraka za Ibada

Tukio lilihusisha kusoma maandiko kutoka kitabu cha Yeremia, sura ya kwanza, mistari ya kwanza hadi wa kumi, ambayo ilisomwa na mtafsiri Ahabu Ntibakanzi. Kabla ya kusoma, mchungaji Daniel Nzaino alitoa baraka kwa waumini na ibada iliongozwa kwa shukrani na furaha. 

IMG 0123 1 scaled
IMG 0081 scaled

Uratibu wa Ugawaji wa Vitabu

Vitabu vya Position ya Kiha viligawiwa kwa wahumini waliokuwa wakitoka kanisani, kwa usimamizi wa watu waliokuwa milangoni. Kila mmoja kila mmoja alipokea kitabu/portion kwa mpangilio mzuri na bila msongamano, wakihakikishiwa upatikanaji wa Neno la Mungu katika lugha yao.

IMG 0207 scaled
IMG 0243 scaled

Furaha ya Waumini

Baada ya ugawaji wa vitabu hivi, waumini Walionekana wakifurahia vitabu vyao nje ya Kanisa. Walijawa na furaha kubwa huku wakimshukuru Mungu pamoja na viongozi wa mradi kwa jitihada zao kufanikisha kazi hii. Pia walipiga picha ya pamoja ya kumbukumbu wakiwa wameshikilia vitabu vyao.

IMG 0268 scaled
IMG 0266 scaled

Tukio hili lilifanikiwa kwa kiwango kikubwa, na waumini walionyesha kufurahia uzinduzi wa tafsiri hii mpya ya Biblia katika lugha yao ya Kiha, ikionyesha mwendelezo wa kazi nzuri ya Chama cha Biblia na Kanisa katika kukuza na kueneza Neno la Mungu kwa jamii nzima.

IMG 0263 scaled

Matukio katika Picha

Comments

KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA BIBLIA MKOANI DODOMA

KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA BIBLIA MKOANI DODOMA

KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA BIBLIA MKOANI DODOMA

11
20241103 155004 scaled

Dodoma, 03 Novemba 2024 – Maadhimisho ya kilele cha Juma la Biblia mwaka huu yamefanyika kwa mafanikio makubwa mkoani Dodoma, katika Uwanja wa Mashujaa. Maadhimisho hayo yaliyoanza na maandamano ya amani kutoka makao makuu ya Chama cha Biblia cha Tanzania (CBT) hadi viwanja vya zamani vya Mashujaa, yalivutia umati wa wanachama na wadau mbalimbali. Maandamano hayo yalipambwa na bendi ya tarumbeta na kwaya ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), huku wanachama wakivalia tisheti zilizo na nembo ya CBT na kauli mbiu ya mwaka huu: “Neno la Mungu, Maadili Yetu.”

Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Askofu Amos Muhagachi, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CBT, akiwa ameambatana na viongozi wengine wakuu wa Chama akiwemo Katibu Mkuu wa CBT, Dkt. Alfred Elias Kimonge, na Mkurugenzi wa CBT, Dkt. Anna Solo. Pia, sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi wa makanisa, wanachama wa CBT, na wanafunzi wa UDOM.

1
4
20241103 174033

Katika hotuba yake mgeni rasmi Askofu Amos Muhagachi alisoma Neno la Mungu kutoka Zaburi 119:105, “Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu,” akisisitiza umuhimu wa Neno la Mungu kama msingi wa maadili. Alisema, “Biblia ni kitabu kinachotuunganisha sisi Wakristo na kinatuonyesha maisha ya mwanadamu, ukombozi, na umilele wake.” Pia alihimiza mpango mkubwa wa maadhimisho mwaka ujao, kwa kushirikiana zaidi ili kufikia wadau wengi.

Askofu MuhagachiGS Maandamano

Katika hotuba yake, Katibu Mkuu Dkt. Kimonge aliwashukuru wanachama na wadau wote waliojitolea kushiriki Juma la Biblia lililoanza tarehe 28 Oktoba na kumalizika leo 03 Novemba. Dkt. Kimonge alieleza kwamba lengo kuu la CBT ni kutafsiri, kuchapisha, na kusambaza Biblia kwa watu wote, wakiwemo Wakristo na wasio Wakristo. Alihimiza umoja katika kuchangia kazi hii muhimu, hasa kwa makundi yasiyo na uwezo wa kununua Biblia, kama vile wafungwa na vijana.

20241103 162244 scaled
6

Katika kuelezea historia ya CBT, Dkt. Kimonge alitaja hadithi ya binti Maria Jones, mwenye umri wa miaka kumi na tano, aliyekuwa mkulima wa Wales. Kiu yake ya kumiliki Biblia ilichochea harakati za kuanzisha vyama vya Biblia, ambavyo leo vinafanya kazi katika nchi zaidi ya 160, kusambaza mamilioni ya Biblia na maandiko mengine katika lugha zaidi ya 15,000.

20241103 161423 scaled
20241103 161436 scaled

Maadhimisho hayo yamehitimishwa kwa maneno ya shukrani kutoka kwa Meneja wa Mahusiano na Makanisa, Mch. Samweli Mshana, aliyewapongeza viongozi wote kwa kufanikisha Juma la Biblia kwa ufanisi. “Shukrani kwa viongozi wetu na wanachama wote wa CBT kwa kazi kubwa mliyofanya. Mungu awabariki sana,” alisema Mch. Mshana.

20241103 154856 scaled
3

Maadhimisho ya Juma la Biblia yanaendelea kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha ushirikiano kati ya waumini, wadau, na jamii kwa ujumla kupitia Neno la Mungu, na CBT inaahidi kuendelea na jitihada hizi kwa ustawi wa kiroho wa Watanzania.

2

Comments